Wasioona wawezeshwa kupiga kura ya maoni Zanzibar
Mwandishi wetu
Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), imeandaa kifaa maalum kitakachotumika kuwawezesha kupiga kura watu wenye ulemavu wa kuona kupiga kura ya maoni bila kusaidiwa na mtu mwingine.
Hayo yalielezwa na Afisa wa Mawasiliano wa Jumuiya ya Wakulima wa Chumvi (AZASPO), Othmani Bakari Shehe wakati akitoa mada ya kura ya maoni ya Zanzibar.
Alisema kifaa hicho, ambacho kitawekwa katika kila kituo cha kupigia kura, kitawawezesha watu wasiona kuchagua wanachokitaka.
Alisema watakaohusika kupiga kura hiyo ni wale tu waliopatiwa vitambulisha na ZEC na waliopawe vitambulisho na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Mungano.
Nao wananchi katika shehia mbali mbali wamehoji sababu za jambo hilo lipelekwe kwao kwa vile elimu juu ya uendeshaji
hawana badala ya kufanywa na baraza lao la wawakilishi ambao ni wawakilishi kutoka kila sehemu ya zanzibar





One Comment on "Wasioona wawezeshwa kupiga kura ya maoni Zanzibar"
Huo wizi mwengine mpya unakuja yaani kwali CCM wana mbinu 100 na Walikua wametumia 1 na zikabaki 99. Hivi hii tume (ZEC) kwa uwajibikaji gani ulionao mpaka wakawawezesha watu wasioona kupiga kura? Mbona watu tele wenye macho yao na masharti ya kupiga kura hawakuandikishwa kwa maksudi ili wasipige kura? Hapa tusidanganyane.