Habari

wasiwasi wangu juu ya maoni

wazanzibari sisi ni watu ambao tunakuwa hamu na shauku ya kutaka mabadiliko juu ya muungano kupitia mchakato huu wa katiba wengi tumejenga tamaa ya asilimia  sitini huenda mfumo na muundo wa muungano ukabadilika

suali je kutokana na utowaji wa maoni wa wazanzibar kwa njia ya fomu za tume ya mabadiliko ya katiba unaweza kuwa ni mfumo salama juu ya maoni yao

sababu maoni haya yanachukuliwa lakini nani anae uhakika wa kuwa hayato chakachuliwa  maana yakipelekwa ofisi ya tume zanzibar  wahafidhina wanaweza kuyaingilia usiku kupitia idara ya usalama wa taifa au kupitia jeshi la polisi na jeshi la wananchi wa tanzania wakaingiza yale maoni ambato wanayataka waoo

nani mwenye uhakika na haya maoni sababu yanaweza kufikishwa ofisi ndogo ya tume hapo gofu lakini yakenda kufunguliwa machinjioni daresalam na kubadilishwa barua zote na kuweka vile wao wanavyo taka

wazanzibar kwa wale tunaotaka muungano wa mkataba basi hatuna budi kulazimisha kutowa maoni yalio wazi  maana kutowa maoni kwa njia ya baruwa ni sawa na mtu anaetaka mabadilio kisha yumo ndani ya chumba anapiga mayowe hali ya kuwa hasikilikani au hata akisikilikana chumba kimefungwa kwa kufuli hakuna ufunguo wala wakukifunguwa

isijekuwa barua ni mtego wa wahafidhina na maharamia wa zanzibar ili kufanya kile wanacho kitaka wao  wazanzibar wenzangu tuone mbali juu ya hizi fomuu  tusiwe kama kaa na ngisi kutegwa kwa uzio na kuingia tele au tukawa kama samaki aitwae barobaro hukamatwa kwa maji ya vyayo kwahivyo tuwe makini fomu za tume maana usalama wa taifa na vikosi vya ulinzi haviko huru na haki vinatumiwa na viko kwa ajili ya matumizi ya wahafidhina na maharamia

WAZANZIBAR TUAMKE  MFUMO WA FOMU ZA TUME UPO KIUJANJA UJANJA TUU

Share: