Habari

Wazalendo: Hivo TCU Inafanya Kazi na Ofisi Ya Utumishi Zbar?

Assalamu alaikhum Warahmatullah Wabarakatuhu Ndugu zangu Wazanzibari Wa ndani na Nje ya Visiwa Vyetu Adhimu. Na Habari Zenu Nduguzetu Wengine munaosoma Mtandao huu. Ndugu Wazanzibari makala hii inahusika na dhulma kubwa za wazi wazi tunazofanyiwa na Serikali ya Tanganyika. Ndio nimeona hakuna budi ila kuifikisha kadhia hii katika mitandao ya Jamii ili Tuweze kusaidiana Mawazo nini chakufanya kama Wananchi Wa Zanzibar tuliokuwa hatuna Mtetezi.

-TCU Watoa amri, Waajiriwa wote Zanzibar Wapeleke Vyeti Vyao Tanganyika.

-Usajili wa Vyeti ni kwa Wazanzibari Tuu, Watoto Wa Malaika Weusi na Miungu Isiojuwa hata kunawa mavi na kuoga Janaba wao huwa hawasajiliwi?

– Wizara ya Kilimo, Afya, Elimu ni Vyombo vya Muungano, Huyu Afisa Wa Utumishi Yeye ana Elimu gani hapo Utumishi?

1.TCU Watoa amri, Waajiriwa wote Zanzibar Wapeleke Vyeti Vyao Tanganyika
Nduguzangu Wazanzibari mimi leo nimepigwa na Mshangao mkubwa baada yakuona Mwanangu niliomsomesha kwa pesa yangu ya Kuvuja Jasho- Maanayake sikupewa (Mkopo kwa Fitna) na hata hakiba ya Sanda Sina. Alipomaliza masomo mwezi uliopita ametakiwa na Wizara ya SMZ (ATI) mshahara wake hauto-ongezwa wala kuajiriwa mpaka Cheti chake Hicho ambacho amesoma Katika Chuo cha Eldorate Nairobi. Akipeleke TCU kitambuliwe kama Chuo hicho Kimefikia Viwango vya Elimu ya Juu.

Mtoto wangu alichanganyikiwa kuona kwamba Wizara za SMZ au Ofisi ya Utumishi inatumika Kuwakandamiza Ndugu zao Wazanzibari kwa kisingizio kwamba Elimu yao Imetolewa Nje ya Tanzania. Mwanangu huyu hakusita ila akasubiri tulipopata vijipesa akaenda BARA kuwaona hao TCU . Alipofika aliambiwa kwamba Vyeti vyake Avikabidhishe Ofisa mmoja na akapewa risiti. Na kuombwa arudi baada ya Wiki- Emagine kuveryfied Vyeti Inachukuwa Wiki hii kweli inaingia akilini. Mtoto wangu alifanya hivo na aliporudi TCU baada ya ile wiki waliomtaka alikuta Vyeti havionekani na aliambiwa na Maaofisa hawa kwamba Huyu mtu aliemtaja wala hajulikani na wala hakuna mfanyakazi mwenye jina hilo… Alipoanza kuzozana nao na kutoa ushahidi wa jina na cheo cha huyo karani ndipo alipotupiwa maneno ya kejeli ” Nyinyi Wazanzibali muna matatizo sana nyinyi… enda zako ..”
Kesi hio pia nimemsikia msichana mmoja ambae amesoma chuo cha TMBI- Tanzania Commission of Univercity. Na chuo kimesajiliwa na Bord ya Vyuo vikuu vya Tanzania. Lakini Watoto wengi hasa wenye asili ya Kizanzibari wakimaliza Vyuo hawapati ajira. Na wametakiwa Vyeti Vyao Ati Wavipeleke TCU vifanyiwe Usajili kwamba ni Vyeti Halali.

MaSuali langu Ndugu Wazalendo na naomba munisaidie Jibu.
. Hivo Utasajilije Chuo halafu Vyeti vya Wanafunzi Useme Huvitambui? Huo Sio Ujinga na Unyanganyi wa Serikali ya Magufuli na Kundi lake la Wezi?
. Hivo Vyuo vya Egarton, Eldorate, Kenyata, Makerere vitakuwa Chini Kielimu kuliko Vyuo vyetu vya Tanganyika ambavyo Vina Uvyama na Ubaguzi.?

2. Usajili wa Vyeti ni kwa Wazanzibari Tuu, Watoto Wa Malaika Weusi na Miungu Isiojuwa hata kunawa mavi na kuoga Janaba wao huwa hawasajiliwi?
Nataka kuuliza tena kwamba Usajili Huu wa Vyeti Umeanza lini? Na kwanini TCU kama Wana Mashaka na Watahaniniwa Hawawaulizi Wakuu wa Vyuo hivo au Academic Secretary? Kwanini Wawasumbuwe wananchi Wanyonge ambao wamehangaika kutafuta Elimu ilio Bora kwa ajili yakuisaidia Nchi yao Sasa wanasumbuliwa?.

Hivo hawa Watoto wa Wafalme Weusi wa Kimalaika, na Miungu MYeusi wao Watoto Wao ( tunawajuwa wanasoma UK. Malasyia, China, UsA) Jee wao hutakiwa pia Vyeti vyao viende TCU vikachakachuliwe. Au ni Watoto wa Kizanzibari tuu ndio wanao fanyiwa Hivo?

Inasikitisha kuona kwamba Ofisa wa Utumishi wa SMZ ndio Vikwazo vikubwa vya Ajira za Wazanzibari waliosoma. Na Kule Wizara ya Afya na Kilimo Ndio Kumekuwa Kuna Waomi Wasiokuwa na Vission.

Wizara ya Kilimo Imepoteza Millioni ya Fedha kuwasomesha Wafanya kazi wao ambao ni tegemeo lakuendeleza Sector hio. Leo Wamemaliza Masomo Wanawataka Wapeleke Vyeti Vyao TCU ili Vipate Kuibiwa na kuuziwa Watu wengine.. Hivo kweli Zanzibar tutafika hivi.?

3. Wizara ya Kilimo, Afya, Elimu ni Vyombo vya Muungano, Huyu Afisa Wa Utumishi Yeye ana Elimu gani hapo Utumishi?

Naomba nipatiwe Jibu jengine kwasababu sasaivi nazidi kuchanganyikiwa, hivo Wizara ya Kilimo, Afya, Elimu ni vyombo vya Muungano?
Kwanini ajira katika wizara hizo hazitoki mpaka Watoto wetu Wapeleke vyeti vyao Bara? Hivo CC Wazanzibari hatuwezi kujitambua na Ku- Veryfy Vyeti vya Wananchi wetu Mpaka vipelekwe Tanganyika..

Tunataka kujuwa Amri hii yakuwataka Wazanzibari wanaorudi masomoni Nje ya Tanganyika wapeleke Vyeti Vyao TCU imetoka kwa Malaika Gani ?

WASIA:

Ningewaomba nduguzetu wa Kizanzibari kwamba wasifanye mchezo wakuchukuwa Vyeti Vyao nakuvipeleka TCU. Kwani Wizara hio kwanza ina upendeleo. Pili ni Wizi wa Kuuza Vyeti. Tatu ni Wizara ya Tanganyika na haihusiani hata kidogo na SMZ au Wizara ya Utumishi ya Zanzibar.

Hivo nakuombeni shikamamneni na muache mara moja kuchukuwa Vyeti vyenu kwenda Kuwagaia Walanguzi ambao Asili yao nikunyanganya Haki za Watu hasa Wazanzibari.

Huo Mtindo wakusikia Vyeti Tuvipeleke TCU tayari umeshawabana watu Wengi na kupoteza Shahada zao za Juu za masomo.. Kama kweli TCU kinafanya kazi kwa Kisheria hakina haja yakutaka Ku Veryfied Vyeti kwakutumia Watu kupeleka vyeti hivo. Kwasababu kwanza hawana uhakika huyu mpelekaji wa Cheti hicho cheti ni Chake.

Kwa Utaalamu wa Uchekiji Vyeti na So call Veryfication kuna Mitandao ya Vyuo Vikuu na TCU wanakuwa na Access yakuwasiliana na Vyuo hivo vya Kenya, Uganda, South Africa, Zimbabwe, Botwasana n.k. Kama kweli Wana nia yakutaka kuhakiki Vyeti kama ni halali ni lazima Wao TCU wawasiliane na Academics Secretary wa Vyuo hivo na Wapeleke Jina series number ya Mtu ambae cheti chake kinataka kuhakikiwa na wao Watapata Reselt. za Mtu huyu kama Cheti chake ni halali au laa.

Njia nyengine yoyote ile hii haikubaliki na nilazima Wazanzibari Tusimame Imara Kuupinga Utawala huu Wa Kidhalimu Unaotaka Kutuibia hata Shahada zetu za Masomo.

Wabilahi Tofiq

Share: