Habari

WAZANZIBAR LAZIMA TUPAMBANE KWELI KWELI

Moh’d Rajab.

Kwa hakika ya Zanzibar imefikia kule wakoloni (CCM ya BARA) walikotamani Zanzibar ifike. Na vibaraka kwa kweli wametumika vya kutosha katika kuwatumikia mabwana zao ili mradi wanajaza matumbo yao.

Usizungumze hali ya kiuchumi. Zanzibar imeshapotea katika ramani ya kisiasa licha ya nafasi muhimu nchi hii iliochaguliwa kukaa na Mungu. Huku akiwataka waja wake waishi katika pepo yao ya dunia lakini vibaraka wameshaifisidi.

Sasa ule usemi wa *makongwe ilikuwa yangu, wakauza nikaa vyangu* unasawiri mazingira na uhalisia wa hali ya sasa. Vibaraka wamewafanya Wazanzibari, kujiona wakosefu, wageni, wadhalili ndani ya ardhi yao ya uzawa kutoka kwa wakombozi na wapigania uhuru wa nchi yetu.

*Ama kwa hakika Mungu ulituahidi kutupatia mitihani. Naam. Kweli mtihani huu wa CCM uliouacha kwetu ni mkubwa na sio saizi yetu*
Mateso wanayopatiwa waja wako kutoka kwa vibaraka wa nchi yetu ni makubwa sana.

1) Suala la dhulma limeongezeka maradufu. Mazombi wamekuwa wakihaha mithili ya majibwa yenye kichaa kilichochanganyika na njaa. Wanapofika popote hupora mali za watu na kuharibu pia. Nadhani walipoambiwa eti wameongezewa mishahara ili kuja kuhakikisha wanadhulumu kama wanavyoagizwa na madhalimu walio juu yao.

2) Suala la kupigwa kwa watu wasio na hatia limekuwa jambo la holela na lililozagaa. Huenda wanatufunza ukomavu. Kama sio dalili za kuelekea kupaazwa. Maana laana ya Mungu sina shaka yoyote kwamba imeshawapata watumwa na watumaji.

3) Kuvunjiwa watu makazi na mali zao. Na huvunja ili wapate wapore. Wizi huu walianza wakubwa zao kwa kuwatumia wao (mazombi) ili mradi madhalimu na majehel wamekutana.

Msidhani mateso haya mnayowapa Wazanzibar yatawaacha salama. Mnaweza kututeka, kutupiga, kutuweka ndani, kutuvunja mifupa na hata kutuua. Mwisho mkatuchoma moto mili ya marehemu. Ivi lakini ni kweli mtatubadili dhamira na nia iliyo nyoyoni mwetu?

Tumekataa kwenye kura. Na sasa ni wakati wa kukataa kwa vitendo uonevu na udhalilishaji wa vibaraka.
Ombi langu ni moja tu.

*Mechi hii imejaa faul na mwamuzi anafurahishwa na faul hizo. Na anawasaidia wacheza faul ili washinde. Tusipojikaza na tukaendana na mchezo, watatuvunja sote*

*NI LAZIMA TUPAMBANE KWELI KWELI*

FB

Share: