Wengine hao!!!
Wasikilize Watanganyika wengine hao:
111111111111111111111111111111111111111111111111111111111
Kinafuata nini kati ya TZ Bongoland na ZNZ?
Sijaelewa nami ninaomba somo. Ina maana nasi tunakuwa na Tanganyika yetu (Kilio cha Mtikila). Yaani kunakuwa na serikali 3 na ya muungano? Halafu tunakwenda Unguja na Pemba au ZNZ kwa passport? Hao waliohamia bara toka ZNZ kwa sasa na toka zama hizo wakifanya biashara inabidi wawe wawekezaji kama wale watokao UK, USA, China. Vivyo kwa waliokule kutoka bongoland. Watarudisha ardhi waliyonunua au kupewa na Wizara na kwenda TIC kujiandikisha uwekezaji huku bara? Kule ZNZ ka-nchi kadogo kuhamia sisi wengi na kujenga na kulima miaka mingi ilopita ilikuwa soo, ila wenzetu wamepeta mpaka Ulanga Kilombero na wapo mjini Dar wanauza maji kutoka boreholes na kuunganishia wateja kama Dawasa. Borehole with electrified pump, malory, daladala, taxi, vituo vya mafuta, mifugo; Ilala Sokoni hadi Bungoni, Mwananyamala, Bagamoyo, Mkuranga majumba na maduka ya Biashara; Temeke, Mbagala Kiburugwa na mwelekeo sasa ni Nyamisati Rufiji-Mikindani-Lindi/Mtwara. Hawa wote watarudi ZNZ au watabaki kuwa wageni wakae kwa Visa? Nasi kuishi kwa Visa ZNZ?
Na zile bili za umeme wa Tanesco,zitalipwa kwa faida kubwa? Nasi tukienda kule kufundisha vyuoni tunakuwa foreign lecturers na wakija huku ni vivyo? Tunaomba shule. Halafu vyama tena hakuna kuwa na CCM kule na huku CUF maana ni nchi tofauti kule inarudi ASP na kuwa na CUF au inakuwaje? Kutegemeana raslimali inakuwaje tuanze kuwahi maeneo watakayouza ili kurudisha ardhi warudi ZNZ? Jee hii imo? Maana kwa somo kunaliwa na kwa mwali pia kuliwe nasi tutavipataje vya nchi hiyo nyingine? Na uchaguzi wa viongozi wa CUF inakuwaje sasa huku bara? Mbona imeingia wakati mbaya? Sisi haki yetu inakuwa wapi wenye hili li-nchi kubwa linalovamiwa kila upande na wahamiaji toka nchi jirani na hii sasa imeongezeka ambapo wageni huwa na haki zaidi kwetu kuliko sisi kwao. Huku huvuna mikoko, misitu nchi kavu, kuvuna meno mpaka ya ngiri, kuvua na nyavu za chandarua cha Arusi na kuvua hadi katika Marine Parks. Tuelimishwe kabla hatujaona boti na jahazi zinaingia Ruvu Delta na Kisiju kupakua TV na marobota ya nguo yatokayo Uarabuni usiku wa manane tukasema ni wahamiaji haram tumevamiwa.
Jenga ufa usije ukatakiwa kuziba ukute. Tujuzane.
22222222222222222222222222222222222222222222222222222222222
Kwangu mimi, ni muumini mzuri wa Muungano, lakini kwa maono yangu ya mbele, naona wenzetu wanaanza kujitenga taratibu na Muungano..
Kwanza ni pale walipokubaliana kufanya serikali ya mseto, hapo inabidi tuweke alama za kuuliza, je walizungumza mambo gani baina ya Maalim Seif na Karume?
Pia swala la mafuta limeleta mtafaruku mkubwa katika muungano, wenzetu wanadai mbona wenyewe hawafaidiki na madini ya bara kuleta maendeleo ya Zanzibar?
Wameona mbali kuwa tunawanyonya ili hali wenyewe wanauwezo wa kujitegemea na kuleta maendeleo kuliko leo katika muungano..
Pia baada ya kupelekewa Mamlaka ya mapata TRA, Wazanzibar walinung’unika sana kua tunawanyonya kwa kodi zao kuletwa bara, ivo solution ni kujiondoa kwenye Muungano usiokua na manufaa…
Tumeshuhudia kazi imeanza kwa mabadiliko ya katiba ya Zanziba kutambulika kama nchi, na kunamengine mengi yanakuja…
Tuwaache wajitenge kwani itatusaidia hata sisi bara kuamka na kuona wenzetu znz maendeleo yatakavyokuja haraka na kutusuta sisi..
Nawasilisha..
333333333333333333333333333333333333333333333333333333333333
Tukiendelea kujiuliza maswali haya ni akika muda si mrefu Tanganyika itapata uhuru kutoka kwa wakolono Tanzania; na kwasababu Tanzania ni wajanja tu hawana nchi basi huo ndio utakuwa mwisho wao
kaza buti tunakaribia mwisho
444444444444444444444444444444444444444444444444
..Nadhani hatuna haja ya kuumiza vichwa juu ya Zanzibar! Zanzibar ilikuwa nchi, ni nchi na itabaki kuwa nchi..Ukweli ni kwamba tafsiri ya Katiba ya Zanzibar (Marekebisho) ya 2010 ndiyo muafaka kwa mazingira ya kisheria. Tatizo la kutuumiza vichwa hapa ni “Je, Tanganyika imekwenda wapi?” Nafikiri itakuwa busara kujaribu kutafakari juu ya Tanganyika kupoteza “sovereignty2 yake badala ya kuhangaika na Zanzibar ambayo tayari wameshajifagilia njia ya kujitambulisha kwenye “MUUNGANO”…Hakika ni kwamba, “kuna ZANZIBAR” ndani ya MUUNGANO ilhali hakuna “TANGANYIKA” ndani yake. Huu ni wakati wa kujadili na kupata majibu toshelezi.
55555555555555555555555555555555555555555555555555
Ninakuunga mkono.
Mimi nadhani tatizo ni kwamba Tanganyika kama mmojawapo wa wadau wa Muungano hana msemaji na mtetezi wake kwenye masuala ya Muungano. Na wakati Zanzibar wanalalamika kuhusu mambo fulani fulani kuhusu Muungano hakuna wa kujadiliana naye kwa sababu Tanganyika aliyeungana naye hayupo ili waweze kukaa chini wajaribu kutatua matatizo yao. Na Tanganyika hakuwahi kukasimu madaraka kwa “Tanzania Bara” kuzungumzia mambo ya muungano kwa niaba yake. Kumbuka Zanzibar haikuungana na Tanzania Bara kwani wakati wa muungano Tanzania Bara haikuwapo. Na hakuna popote ambapo Tanzanyika ilibadili jina lake rasmi na kuitwa Tanzania Bara. Sijui hili jina Tanzania Bara lilitokea wapi?
Ni mawazo yangu tu.
25 Comments on "Wengine hao!!!"
mtu akiwajibu hawa yatawafika au yataishia hapa mtandaoni MZALENDO?
una maana gani MTANGANYAKA
Hii “kijini” ya Kae ua?
Nimeelewa kuwa makala ya hapo juu yamechapishwa kwenye mtandao mwengine na hapa Mzalendo tumeletewa kopi tu. Suali langu ni: jee kumjibu mwandishi itamfika kwenye mtandao alotuma au itaishia hapa Mzalendoo?.
Samahani kwa usumbufu.
Nafikiria kama Watanganyika wanataka kujitoa kutoka kwenye muungano wanaweza kufanya hivyo kwani ni haki yao. Kama wangelihisi kama Zanzibar inawadhulumu basi nahisi wangelikwisha fanya hivyo zamani sana. Kuhusu kuwafukuza wazanzibari wanaoishi bara pia ni haki yao lakini itakuwa ni ujinga wa mwisho ambao wangeweza kuufanya katika historia yao. Nasema hivyo kwa sababu hao wazanzibari watakao wafukuza hapo Dar wengi wao ndio matajiri wanaolipa mapato kwa hiyo kama wataamua kurudi makwao tutawapoke kwa mikono miwili. Pili kama kweli watawafukuza Wazanzibari walioko Bongo hawatoishia hapo tu, watawafukuza Wahindi, watawafukuza wenye asili ya kiarabu. Wakiwamaliza wageni watasakamana wenyewe kwa wenyewe. Wataanza kwani mchaga awe na duka Dar, nae arudi kwao Arusha.
Nafikiria huo sio ustaarabu mzuri, Wazanzibari hawadai kuwafukuza Wabara, Wanadai maslahi ya nchi yao, na kilio hicho kipo kwa muda mrefu, lakini hakuna hata kiongozi mmoja wa Tanzania aliyekua tayari kusikiliza kilio hicho kwa njia ya majadiliano au kura za maoni, na Badala yake walizidi kuwakandamiza kwa kuingiza mambo kwenye mikataba ya muungano kiunyemela.
Nyinyi Watanganyika ndio wa kulaumiwa kwa hilo. Umekuwa kama ule muungano wa Wasovieti, Watu walikuwa na Nchi zao, lugha zao na utamaduni wao, lakini walikuwa hawaruhusiwi kuzungumza lugha zao, hawaruhusiwi kuendeleza utamaduni waowala dini zao. Ndio maana ulivunjika ingawa hakuna Jeshi lililokuwa na nguvu na likiogopewa ulimwenguni kama la Urusi.
Sisi tunataka Muungano kama wa Europe. Kila nchi ina mamlaka yake wanachangia tu katika huo muungano. Na kuna faida nyingi ambazo wanachama wake huzipata kwa mfano misaada ya kiuchumi. Lakini nyinyi mulikuwa na nadharia ya Kikommunisti yaani “Chako ni cha kwetu pamoja lakini changu ni cha kwangu tu” Raslimali zote za Zanzibar ni za muungano, lakini lakini raslimali za Tanganyika ni za kwao wenyewe na Wazanzibari haziwahusu
ninyi danganyikaz munahitajika mupate darasa la kutosha ili kuweza kujua,kuelewa na kufahamu siasa za zanzibar zilivyo lakini pia mupate darasa maalumu kuihusu zanzbar yenyewe kabla ya uhuru baada ya uhuhru,kabla ya mapinduzi na baada ya mapinduzi na kama vile haitoshi munatakiwa mupatiwe somo maalumu la ziada juu ya muungano [elimu hizi lazima muje muzipatie kwenye kitovu cha ustaarabu namaanisha zan zi baaar],mukishapata madarasa hayo mutapata ufahamu wa kutosha na kuanzia hapo hamutaleta pumba na takataka kama hizi ila mutakuwa na uwezo wa kujenga hoja makini.>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>nawasilisha.
@MTANGANYAKA
Hao watanganyika wengi wanasoma humu kwenye mzalendo. Hivyo usidhani majibu hayawafiki. Nimetembelea kwenye hiyo blog yao nimeona cut and paste kama hii iliyowekwa wao wamechukua kutoka mzalendo.
Hivyo wanaangalia na kujisomea kwa murwa. Chochote ukatakachoandika mategeo yangu watakipata.
@ashakh
Natowa shukran nyingi kwa kunielimisha. Muda kwa sasa umenipita lakini wataipata. Hivi nimeelewa kuwa twala sahani moja na ndio jambo jema hasa kwani wakitia bizari tutaweka tangawizi huku tukisubiri mchapuko utakavyowakolea. Kumbe hapa ndipo pakuwasomesha hassa.
Shukran
A/aleikum
Jamani jamani jamni halahala ujiti ncha ina hoho hili suala la mungano ni tete sana tuwe makini wakati wakuchangia tusikurupuke tuu tukasema tuvunje muungano , mimi ni zanzabari halissi lakini siungimkono hata kidogo kuvunjwa mungano, mungano huu wetu nitofauti sna na muingano mengine hilo tulijue wazi, sahivi tushaungana mapaka damu ukiachilia nchi , nazungumza na wenzagu hasa tulioshiba makuku yataa, manake sisi ndo wamwanzo kutoa maoni kuvunja muungano .
mimi maoni yangu kama tumechoka na muungano basi ipigwe kura na yamaoni kwa wale wazanzibar walioko bara tu , wao ndio wanao jua faida ya mungano na hasra zake kuliko sisi huku tulio shiba makuku ya taa na sema hivo kwakuwa tukivunja muungano wao ndio watakakua waathirika wakubwa na lolote lile litakalotokea kwa kule bara kuliko sisi tulioko nje nya zanziba na nadani ya znzibar
kwahiyo ndugu zangu wazanzibar tuwe makini sana suala hili tusiwe najazba wala hamaki tuwe na busra zaidi kuliko jazba
Hakuna lisilo zungumzika sisi sote nidugu mmoja damu moja hakuana haja ya kufarakiana na kuchukiana kwani hata SUBUHANA WATAALA halipedi hilo ta kutengana, km kuna matatizo basi tukae na tuyasuluhishe kwa aaamni naupendo INSHAAALA
Nakutakieni ramadhan njema
BANDA MWENYEWE
Salam.
@ Banda,mimi ni mmoja ya watu walioishi Dar kwa muda mrefu sasa na nilifaidika na mengi kutoka kule na nilibahatika kununua hata baadhi ya maeneo(ardhi) na hadi leo ninayamiliki maeneo yaho.
Pia nina nusu na robo ya familia yangu iko huko na hata nimeowa huko na nimezaa watoto na hadi sasa wanaishi huko,mimi kwa muda huu niko nje ya Tanzania ila jamaa(yani kaka,dada,wajomba mashangazi na mke na watoto wangu wako huko).
Sasa kwa hoja ya ya kuwauliza wahusika wanaoishi huko nina asilimia zaidi ya 70 kua wanaukataa muungano na wasio ukataa wanataka muundo wa serekali tatu.
Nakuishi au kuchanganya damu sio hoja ya kushika, huku ikituangamizia nchi yetu ,kwa sababu kama kuchangia damu hata ulaya ,arabuni na nje nyengine ziko damu za kizanzibari je, na hahuko tuungane?
Banda hayo ndio maoni yangu na ninaamini kua ndio ukweli.
AHSANTE.
.
A/ALEIKUM
@mkarafuu naona jibu unalo mwenyewe , nanukuu maneneo yako “mimi kwa muda huu niko nje ya tanzania ” ila hukumaanisha uko nje ya tanzania kivipi , kwamaana hiyo wewe huto athirika ila jamaa zako abao wako kule ndio watakaathirika zaidi.
Nahuko kwengine uliko changaya damu sio km tanganyika ujue hilo , huko sikwambii kungana hata ukaaazi kupewa tabu ,
@ Banda hata mimi nataka serikali tatu lkn si kwa sababu wazanzibar tutapata hasara tukivunja muungano bali ni kwa kuwasaidia hawa waislam watanganyika ambao wamebaguliwa ktk nchi yao na kufanywa daraja la mwisho kutokana na ulegevu wao na kuacha mafundisho ya allah. Hata mahakama ya kadhi imewashinda na waende wakasome mombasa.
Leo hii mzanzibari ukiwa tanganyika ni bora ukumbane na mkristo atakusaidia kuliko muislam wa tanganyika. Kuna haja ya kuwaelimisha la si hivyo tanganyika itakua hakuna muislam tena kwani leo hii waislam ndio walevi,ombaomba,makahaba, wezi nk. Na wakristo ndio mabosi ofisini.
Wazanzibar ambao nimehojiana nao wafika 50
ambao wako tanganyika lkn ni 2 ambao wanaishi huko kwa kupenda waliobakia wote wanaishi kwakua hawana la kufanya tu.
Nani mzanzibari atapenda kukaa tanganyika halafu watoto wake wafanye biashara ya kuuza na kununua utupu? Nani anaetamani wanawe wawe walevi? Nani anataka wanawe wawe majambazi? Utaishi vipi tanganyika uepukane na haya?
Wazanzibari tunajali zaidi heshima yetu kuliko mali. So magari,maduka,majumba nk sio lolote watachua watanganyika wauzie pombe.
Hawa watanganyika Nawajifunze kutoka africa ya kusini na kutoka zimbabwe, afrika ya kusini wao hawakuwafukuza wazungu kwani walijua ndio wenye uchumi na wakajua kua waafrica wao si wazalishaji. Ndio leo inaitwa half london. Lkn mugabe zimbabwe alikuja na mawazo ya kimapinduzi ya kuwanyan’ganya wazungu mashamba kama karume leo imekua ombaomba kuliko zanzibar nchi ambazo zamani zikitoa misaada hata kuipa hiyo s/africa.
@ Banda
Narudia maneno yangu athari siku zote, popote zinatokea. Tunacholinganisha ni athari na faida. Nimewahi kusema kitu kitakuwa kizuri ikiwa faida zake ni nyingi kuliko athari. Pia kinakuwa kibaya ikiwa athari zake ni nyingi kuliko faida. Mfano Chloroquin, nidawa ukizila nyingi utakufa.
Kuwa na jamaa au mali kule Bara haina sababu ya kusema kwamba muungano ni mzuri. Binafsi nina nyumba tatu ndani ya Dar pamoja na ndugu zangu wanaishi. Lakini niko tayari (nitashadidia) muungano uvunjike.
Tukumbuke walipokuwepo wakoloni hali ilikuwa vipikatika nchi yetu. Tukilinganisha na sasa hivi, utaona ni vyengine. Wazee wetu waliwaona wabaya, wanatunyonya, nk wakawaondosha. Leo jee si ndio mimi na wewe BANDA tunakimbilia kwenye manchi yao tunaishi. Na zaidi tunanunua hata hizo nyumba.
Kuvunjika kwa muungano sio sababu ya kufukuzuna au kigombana, tunachotaka ni kutambuana na kushirikiana vizuri zaidi.
A/ALEIKUM
Jamni narejea pale pale na maonai yangu muungano usivunjwee, hakuna lisilo wezekana wala lisilozungumzika.
@ bosco kama waislamu wa tanganyika wamekua walegevu wa mafundishi ya ALLHA SUBUHANA WA TAAALLA je unategemea nini hapo? fikra zako unafikiri kuwa na tanganyika au kuvunja muungao watakazana ? hiyo haiwezekani hata kama zitakuja tanganyika 20, kwa ni MUNGU lishasema kuwa “hatombadilisha mtu nafsi yake mpaka yeye mwenyewe kwanza abadilike “sasa ndugu yangu kama nafsi zetu ni chafu tutegemee dhabu kutoka kwa ALLHA
@ bosco. nafikiri unajua walio athirika pale zimbabw e ni nani je ni mugabe au wananchi wake , nahapa ndipo penye kilio changu kwa ndugu zangu wazanzibara walioko bara ndio watao athirika jamani , kuna baadhi ya ndugu zetu wakiarabu leo hii hawataki hata kuisikia zanzibra wakiyakumbua yalio wakuta mwaka 64, je munataka na ndugu zetu walioko bara yawakute haya ? naamini tuna viongozi wazuri tuu zanzibar wenye busara na hekma wakulitatu hili bila hata kufarikiana au kutenga , kwani umoja ni nguvu na utengano ni zaifu
@ashakh unanyumba tatu sawa lakini nafsi haipo pale , nasijui kwanini ulijenga pale na usijenge zanzibara ukitambua kuwa zanzibar ndio nyumbani,ndugu yangu unazungumza haya ukiwa nje ya nchi, na unataka mungano uvunjike kwakuwa unapo pakukimbilia
Kuna Mtanganyika mmoja alieleza maneno zuri ktk maoni yao hapo juu. Na ni dalili ya kuwa wanaenza kuelewa jnsi ya UTATA wa MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR: nanukuu maneno yao hapo chini
….”Na Tanganyika hakuwahi kukasimu madaraka kwa “Tanzania Bara” kuzungumzia mambo ya muungano kwa niaba yake. Kumbuka Zanzibar haikuungana na Tanzania Bara kwani wakati wa muungano Tanzania Bara haikuwapo. Na hakuna popote ambapo Tanzanyika ilibadili jina lake rasmi na kuitwa Tanzania Bara. Sijui hili jina Tanzania Bara lilitokea wapi?”
Majibu yangu kwao siokwamba Tanganyika haikuwahi (KUKASIMU MADARAKA KWA TANZANIA).Bali Julious Nyerere na Cabinet yake Aliitumia katiba ya Tanganyika na akaibatiza kua ndio katiba ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Nakuwataka mawaziri wote wanaoitumikia Serikali ya jamhuri ya tanganyika wabakie kuitumikia Jamhuri ya Mungano wa tanganyika na Zanzibar. Hiyo ilikua ni ilani ya tarehe 22.April.1964.
Baada ya Miezita (kumloby Abeid mani Karume na Mamber wa Mapinduzi), Watanganyika hawa waliopeleka barua kwa umoja wa Mataifa (UN).Uliyosema kwamba Watu wa Zanzibar na Watu wa Tanganyika wameungana na jina ni Tanzaia. Barua hiyo ilikua na muhuru a Tanzania (nembo ya Adamu na hawa). Lakina haina jina wala signature.
Sasa ndugu Watanganyika mujuwekma huu Muungano haukua na nia njema kwa Zanzibar wala Waanzibari. Na ndio maana wazanzbari miaka yote wakawa wanalalamika. na nyinyi muenyamaz kimya. Kwani nyinyi ndio munaopata faida yamisaada, mabalozi ya nje,nk.
Sasaikiwa wakati wa Muungano Tanzania bara haikuwapo na neno Tanzanyika halionekani popote. Jiulizeni weyewe… Where is Tanganyika? Na ilikuaje hii Tanzania ikawa ina mkoa nao ni Zanzibar? Hiyo Tnzania where does came from?
Lamwisho Watanganika wacheni ujinga wakusema mutawafukuza Wazanzibari waliokua wameinves Bara. Kwani kufanya hivyo nikudhoofisha uchumi wenu wa GDP. Nanyinyi asii yenu siowatu wakufanya biashara ila kazi zenu ni kuingia madukani wakati wa usiku na mukauwa watu au mukaiba…Namutakapo mfukuza Mpemba/ mzanzibari alieko bara, kama alivosema ndugu yangu (Wamtambwe) Hamutaishiahap mutaanza kulana wenyee kwa wenyewe mchaga na muhaya, msukuma na mgogo, myamwezi namuambuu n.k
Kama Zanzibar itajitenga nakuleta maendeleo yake wenyewe, kunaweza kuwafunua macho nyinyi (Watanganyika).Na mukadai uongozi bora ambao mutakua na state region zenu ambazo zinaunganisha Tanganyika nzima kama vile USA au Europe. kila Region wanajiendesha wenyewe na nirahisi ku-kantrol Curruption.
Nawazanzibari tutakua na jirani wazuri ambao tuataendelea kusare ideas, marage hata culture studying. kwa watakao taka kufanya hiyo.
@ Banda
Asalam Aleykum,
Mim nasema sioni kama Zanziba wanataka kuvunja Muungano lakini naona wanataka kuuimarisha. Muungano utaimarika ikiwa hakuna sehemu ya Muungano ambayo itajihisi inaonewa. Hata kama Tanganyika inajihisi iko sehemu ambayo Wazanzibari inawaonea, basi ni haki yao kukaa na kuirekebisha sehemu. Suala linakuja wanaposema Bongo kuna Wazanzibari wengi ambao wanapeta kwa hiyo watawafukuza. Mimi nasema kama kwao hilo ni kero basi wanahaki ya kulirekebisha lakini sifikri kama itakuwa jambo la busara. Nasema si Busara kwa sababu Wazanzibari hao wanachangia asilimia katika mapato ya Serikali ya Tanganyika kwa hiyo nafikiri kwao wangelifurahia kwamba wanao Wazanzibari kama hao. Namaanisha wakiwafukuza watahasirika hao Wazanzibari na Pia Serikali ya Tanganyika. Nasema ni ukweli kwamba wazanzibari wanauzoefu mkubwa kwenye mambo ya biashara ukilinganisha na wa Tanganyika kwa hiyo popote watakapoishi wataweza kuendesha biashara zao. Kwani hata wazanzibari wanaofanya biashara hapo Bongi hivi sasa wanauza nchi nyingi za jirani, na naamini wataweza kufanya hivyi kama itabidi warudi zanzibar na hiyo itakuwa ni faida kubwa kwa Zanzibar.
Nchi yoyote haiwezi kuendelea bila ya kuwa tajiri. Na hilo ndilo kosa kubwa tulilolifanya baada ya kupata uhuru wetu kuwafukuza matajiri na kunjanganya watu mali zao. Leo inelikuwa Mandela wangeliamua kuwafukuza Wazungu au kuwanyang’anya mali zao, basi ingelikwisha anguka chini kama Tanzania au Zaidi.
Sijidharau wala sitaki tujidharau lakini ni ukweli wa mambo kila kabila duniani wanauwezo fulani ambao kabila jengine haliwezi kuwafikia huo ni ukweli wa mambo kwa hiyo kila nchi ikiwa na mchnganyiko wa makabila mengi basi wanauwezo mkubwa wa kuweza kuendelea.Ingelikuwa Amerika hawakuweko Waafrika wangelikuwa Super power kwa silaha na Technologia nyengine lakini kwenye michezo wasingetamba.
Nataka kukueleza kitu kimoja najua mtacheka lakini umo ukweli kidogo ndani yake. Wezetu Wazungu wanaichukulia hii dunia kama kiwiliwili, kwa hiyo wameyagawa kila Bara kama kiungo fulani. Europe ni kichwa cha dunia, ndicho kinachofikiri, kutowa mawazo. Jee tujiulize Waafrika tumepewa Status gani? Status yetu ni “Sexual Organ” kazi yetu ni ngono na kuzalisha tu. Hainamaana ya kwamba hatuna wenye uwezo wowote, wako wenye uwezo kuliko hata hao wazungu wenyewe lakini majirity yetu tuko hivyo
@ashakh
sasa ndugu yangu unasema una nyumba 3 huko tanganyika at the sometime wewe ni unataka muungano uvunjwe .sasa kwanini hukujenga kule pemba badala yake umeenda pahala siku zote unawachukia watu wake pamoja na tabia zao.”hypocrite” mtu kwao bwana kwanini usijenga kwenu?
umesema sababu iliyokufanya uwepo huko uliko ni kwasababu ya tanganyika ,sasa nakuuliza jee muungano ukivunjwa na maalim seif tukijaaliwa atakuwa raisi wa zanzibar utafungasha virago na kurudi zanzibar?
nimegundua kwamba watu wengi wanaopiga kelele za kuvunjwa muungano wapo nje ya nchi tayari wanapo pa kukimbilia.mimi nasema kuvunja muungano sio solution ya matatizo ya znz.
serikali 3 ndio nahisi itakuwa suluhisho
muunguja: Wewe watu wanaposema maoni yao nakimbilia kusema ati nankuu….”nimegundua kwamba watu wengi wanaopiga kelele za kuvunjwa muungano wapo nje ya nchi tayari wanapo pa kukimbilia.mimi nasema kuvunja muungano sio solution ya matatizo ya znz.
serikali 3 ndio nahisi itakuwa suluhisho”
Suala langu kwani muungano kuvunjika lazima kuzuke vita? Hizi ndio fikra zenu nyinyi watu wenye asili ya Tanganyika. Shari tu ndio inayowapitikia kwenye nyoyo zenu. Wewe uko nje unaona TV za kila aina, umesikia ni nchi gani iliovunja muungano kwa mtutu wa bunduki?
Hivi karibuni Kosovo walijitangazia uhuru wao na WaSerbian, Rassian wakapinga. Lakini ilikua peacefull. Sasa nasisi kama mungano utavunjwa na Watanganyika sio wazanzibari kwani kuna wazanzibari wengi wanataka serikali tatu (haa mimi).basi kama itakua ni hivo (utavunjika)kuutakua kwa amani na sheria.
Tukumukeni Sisi wazanzibari tumerekebisha katiba iliokua ikileta Utata wa Zanzibar kua sisehemu ya Tanganyika. Bali ni nchi ilioungana na Tanganyika. Na mambo mengine yafuata kidogo kidogo kwa kisheria na kidemokrasia. Tena hapa neno pakukimbilia munapo linatokea wapi tena
Sasa unaanza kumshambilia Sh. Ashkh bure.Wacha fikra za kijinga na shari. Ishaalah Ramadhani hii (muunguja..ndugu yangu tutakua na serikali tatu kama wengi tunavotaka.Na hata hawa Watanganyika watakubali kwa hilo, hakuna mushkeli. Amen
Assalaam alykum
Mimi naomba ni changie kidogo, kwanza ndugu yetu @ Banda , hofu yako ni kuchanganya kwetu damu , kwani ni watu wa nchi ngapi ambazo wazanzibari wamechanganya damu nao . jee tumeungana na nchi hizo!ukenda karibu kila nchi duniani utawakuta wazanzibari wamefanya vitu vyao, hata wewe hapo ulipo naamini wapo Wazanzibari waliochanganya damu na wa hapo.
jengine lilonifanya nichangie ni pale uliposema “hakuna haja ya kuchukiana na kufarikiana kwani hata SUBUHANA WA TAALA halipendi hilo” , nikweli Subhaana wa taala ametuhiumiza kushirikiana lakini katika njia ya Mwenyezimungu, sio katika kudhulumiana , pia wakushirikiana (kumfanya rafiki) ni Muislam mwenzako katika masuala ya kheri ,sasa sisi tuungane na hawa katika njia gani !? wewe mwenyewe huoni kama hawa hawafai kuwa marafiki huu ukandamizaji wanaotufanyia huuoni na mwisho wanakwambia hata nchi huna wewe (Zanzibar) ni kijimkoa tu fulani , tena wanakwambia kwa jeuri na kibri
tunataka muungano wa wazanzibar sio mungano wa nyerere na karume
hapo ndipo tutaelewana.
@ZAMKO
katika maoni yangu mimi sikutaja vita ,sasa sijui nani kakwambia swala la vita.vile vile swali langu nimemuuliza ashakh ,sasa wewe ni ashakh?unless una nickname 2 hapa mzalendo moja ZAMKO na ASHAKH.
twende kwenye topic.niliposema ashakh and company wanapo pa kukimbilia sikuwa na maana kwamba vita vitatokea isipokuwa ile freedom of movement between one part to another itakuwa haipo tena kwasababu muungano utakuwa haupo tena.na vile vile utapewa choice either uwe raia au uwe treated as a foreigner sasa kama unaipenda znz inabidi urudi kwenu na uwe unakwenda tanganyika kama mgeni.
tunajua muungano una matatizo lakini kuuvunja si suluhisho ,hata huyo kiongozi wenu maalim seif yeye yuko infavour of serikali tatu which is i think ndio dawa ya kuondoa kero za muungano.
sasa nakuuliza wewe zamko AKA ashakh muungano ukivunjwa na maalim seif akijaaliwa kuongoza zanzibar ,jee utaondoka huko ulikojificha ughaibuni na kwenda kuishi zanzibar?nakuuliza hivyo kwasababu siku zote mnaamini kuvunja muungano na maalim seif kuongoza nchi ndio suluhisho ya matatizo ya zanzibar.
Muunguja
Nimejenga bara sikwa sababu ya kuishi bali ni kibiashara. Nadhani unafahamu masuala ya biashara watu wanafika uchina kununua suruali tu. Ndio namimi nimejenga kwa ajili ya kupata kijio.
Huko Pemba pia ninazo nyumba mbili, ndio za mwanzo kujenga. Ahsante kwa kunikumbusha, “Nyumbani ni nyumbani hata iwe juu ya jabali”. Kuna nyimbo wameimba Les Wanyika inasema “Nyumbani ni nyumbani” itafute.
Kilicho nileta huku, Muunguja, kuna mambo nimeyakosa huko nyumbani. Na Inshaallah kwa vile nimeyapata basi usiwe na wasiwasi mimi nitarudi. Kwani huku vilevile kuna mambo nayakosa, na kuyapa lazima nirudi nyumbani. Ndio ukaambiwa maisha ni mzungumko.
Maalim Seif akiingia ikulu, na Muunguja akiingia bungeni tunamatumaini mambo yatakuwa murwa. Sasa kipi cha kuendelea kukaa huku na kula makuku mabovu, haidhuru ndio yaliyo tunenepesha na kuingia hali baada ya njaa kali tuliyokuwa nayo.
Muunguja mara zote unazotembela Zanzibar naona huja fanya utafiti. Nakupa gerentii kuna watu wengi sana muungano hawautaki. Wanataka uvunjike leo. Sikatai wako wenye maoni ya kutaka serikali tatu,lakini ni wachache.
Muunguja,
Kwanza fahamu Maalim Seif hawezi kuvunja muungano. Tutakao vunja muungano ni sisi wananchi. Najuwa unapenda kumtaja Maalim Seif. Yeye tayari ameshakwambia sera zake juu ya muungano. Hivyo hapana haja ya kumuingiza hapa.
Muunguja, sikujificha ughaibuni na ndio hata wewe ukawa unanijuwa nami nakujuwa = tunajuwana, tunaonana, nk. Ingekuwa niko mafichoni basi tusingeonana.
Muunguja, mawazo yako ni ya nadharia ya kisayansi na siyo ya kivitendo (practical). Practical sayansi hata siku moja haikwambii kuna efficiency of 100%. Sasa unaposema Maalim Seif ndio ataweza kuondao matatizo, nitakuuliza yapi?
Kwa chuki zako unaweza kumfananisha na kiumbe chengine, lakini kwa ufahamu wangu nitamfananisha na binaadam kama walivyo wengine. Hivyo kwa matatizo ya muungano naamini Maalim Seif anaweza kuyatatua. Kuwaletea wanachi maendeleo anaweza. Kuwapeleka Wazanzibar kwenye Mars hilo hawezi. Kuwaingiza Wazanzibar peponi, pia nalo hawezi, nk.
Suluhisho la matatizo ya Zanzibar wa kuyatatua ni Maalim Seif akishirikiana na Mzanzibar mwenye. Haya kuyajuwa yataka wenye akili na muona, nasio kina eheeee.
@ashakh
mimi simchukii maalim lakini nachukia some of his political views.sasa kutofautiana ideology haina mana kwamba mimi namchukua maalim seif.outside politics naamini yeye ni mtu mzuri tuu.kuna baadhi ya mambo mimi nakubaliana nae kwamfano hilo la serikali 3.
watu wanafikiria kuvunja muungano kutaleta big changes in znz kiuchumi na kimaendeleo.ok muungano una matatizo lakini ndugu yangu na sisi wenyewe wazanzibar tuna matatizo tena wala si madogo.mafisadi wanatafuna pesa watu wana njaa alafu viongozi wanafanya watu wa bara as a scapegoat.sijasikia hata siku moja znz viongozi wanafukzwa kazi kwa sababu ya ufisadi au uzembe.kama kiongozi atafukuzwa kazi basi ujue his political view iko against na yule mtawala
ashakh mungu akitujaaliya safari hii kuna kila dalili maalim seif atachukua urais. sasa mimi nasubiri kwa hamu hayo maendeleo within 100 days kama alivyotuahidi.
@ muunguja umemkandia zamko. Lkn na mimi najibu pia hata kama huja niuliza mimi kwani kama una lazima ujibiwe na huyo uliemuuliza basi mtumie sms na usiandike humu mtandaoni kwani ukiandika humu halafu sisi tukakuona unakosea hatuwezi kukunyamazia kwakua eti tu hujaatuuliza sisi. Huu mtandao si wa mtu mmoja au 2 tu ni wa wazanzibari wote.
Tuje kwenye mada @ muunguja unasema unasubiri maendeleo within 100 days. Na sisi pia tunayasubiri inshallah lkn hiyo ilikua ni ilani ya CUF ya mwaka wa uchaguzi 2000-2005 na 2005-2010. Ama ilani ya CUF ya mwaka 2010-2015 mimi sijaona ahadi ya siku 100
kama ipo niambie na kama haipo basi nakwambia kua serikali inaendeshwa kutokana na ilani ya uchaguzi wa mwaka husika.
Nakupa mfano; ilani ya CCM ya mwaka 2005-2010 ilikua pia inataja kulishughulikia suala la mahakama ya kadhi lkn japokua hawajalishughulikia lkn ktk ilani ya 2010-2015 jambo la mahkama ya kadhi halipo tena ktk ilani ya CCM.
Mimi nahisi Tuongee kwa uhalisia wa mambo na sio kiushabiki jamani huku tukijua kua hii ni ramadhan tusije tukasema uongo.
RAMADHAN KARIM.
@muunguja: Muunguja mimi sina nickname mbili. ni (zamko) tu ndio ninayoitumia. Nimekujibu vile kwasababu huu ni mtandao kila mtu ana uhuru wakusoma maoni, kutjibu,na kutoa hoja.
Jengine kitakacho leta mabadiliko Zanzibarr ni uongozi bora wenye Vision za kmaendeleo.uchapaji wa kazi unaopinga uvivu, ulalahoi na utegeaji. Tunaposirikiana na nyinyi wana wa Mapinduzi ambao munaamini kwamba Mpemba kuingia ikulu ni kama Mbwakuingia msikitini. Basi tutaleta Changes.
Tunapokuwa hatuna chuki za upemba uunguja kama lizonazo wewe muunguja, samuhuna, na wenzio tunawajua nyote basi tutawezakudumisha Aani na utulivu wakweli. na tukawasaidia ndugu/ jirani zetu wa tanganyika.
Jibu jengine mimi sukukimbia kwetu na wala sijajificha uhaibuni kama wewe muunguja uliokwenda/pelekwa kusoma USA kwa ticket ya Ukada na uwana Mapinduzi (CCM SMZ). halafu ukangangania in USA. Mimi ninasheria yakingia Unguja na Pembana kurudi nahuko ndiko nilikozaliwa, jenga, na ndiko nitakako zikwa ishallah.
Hapa nilipo ukifa tu kama wish yakonikurudishwa nyumbani basi laaah mush-kel unarudishwa. na sio kama wewe huko uliko