Wewe Susa Mmasai anakula

Written by  //  06/02/2012  //  Habari  //  19 Comments

Wazalendo
Naendelea kuwaleta ladha ya pwani. Harfu ya asumini iliyochanganyika na harfu ya maziwa ya ng’ombe. Sasa hivi kila kipembe cha nchi yetu kumekuwa na uoungufu mkubwa wa watu kuona wanavaa kofia na kanzu za msikitini. Badala yake ndio kama hivyo munavyojionea wenye, ni mavazi ya rubega huku kukishikwa marungu mikononi na majisu viunoni.

Tuendelee kujitayarisha na kuikomboa nchi yetu

Utafikiri tuko Arusha. Hapa tunapata mapumziko bbada ya kupigwa na juwa kali wakati tunalisha majani ng'ombe wetu

Hivi ndio mandhari ya Darajani town inavyoonekana. Imepambwa kwa haiba ya kimasai badala ya ile ya kanzu na kofia

Unalo la kusema! Jamaa hapo anaonekana akipiga ndogondogo labda atafanikiwa kuondoka naye

19 Comments on "Wewe Susa Mmasai anakula"

  1. zamko 06/02/2012 kwa 11:01 mu ·

    NA WATAENDELEA ZAIDI KWASABABU SASA WANBAMAPINDUZI (SHAMUHUNA ) NA WENZAKE WAMESHAVIUZA VISIWA.

    TUSUBIRI MPAKA HAYO MAOMBI YA TANGANYIKA YA NYONGEZA YA BAHARI YA HINDI YAKUBALIWE. HUKO UNITED NATION.

    HAPO UTAWAONA WANACHUNGA NGOMBE WAO HATA KULE VITONGOJI, WAMBAA, MAKAANI NA KWENGINEKO.

    MIMINASHANGAA HUYU ALIEMWAMBIA SHAMUHUNA AUZE KISIWA CHA UNGUJA NI NANI?

  2. mahuluku tabu 06/02/2012 kwa 12:08 um ·

    Smz ina uamuzi gani kuhusu hawa wasasi ?na ukipakachua pengi tayazi washauziwa uraia wa Zanzibar ,kusaidiwa na hao masheha wanaowanyima wa Zanzibari vitambulisho vya uraia,wakawapatia wamasai

  3. makame silima 06/02/2012 kwa 12:34 um ·

    Hili la hawa sungusungu wa Kimasai tulioletewa ni ni dogo tu katika Agenda na Mikakati ya viongozi wa Tanganyika wakishirikiana na Wanafiki wetu wenye kujalimatumbo yao na kuviuza visiwa na asili ya utu wetu.

    Viongozi wetu wa Smz WAKE UP, hivi karibuni kulikuwa na gazeti moja la Marekani linaitwa New York time lilinukuu kuwa Uchumi wa Tanzania unanaweza kukuwa mara moja pale watakapoanza kuchimba mafuta yao.

    Sasa kwa mtizamo wangu na kupima nyakati na mambo yanavyo kwenda nimekushanya mambo mengi yenye kunitia wasi wasi na kuona huenda walafi wachache wakaviuza visiwa kama vile mali ya wazee wao.

    Kinacho nifanya nikubali kuwa huenda Marekani na mataifa ya Ulaya wamesha pata harufu kuwa Tanzania hususani Zanzibar Mchemba upo na kinacho angaliwa hivi sasa na mataifa hayo ni umahiri wa nchi hizi mbili Tanganyika iliovaa koti la Tanzania au Zanzibar inayosema mafuta hayamo katika Muungano kama vile menaral za Tanganyika.

    Ujuwe kuwa Norway wanajitahidi kusimamia pande zote mbili Tanganyika au Zanzibar yupi atakayekuwa mmiliki wa mafuta na marekani hiyo hiyo na wao wanatega , Ndio ukaona viongozi wa Marekani na Ulaya hivi sasa hawatoki Tanzania.

    Mujuwe safari ya Geoge W Bush sio bure Tanzania kusema bada ya kutoka kaja kupunga upepo? na Balozi wa Marekani kutowa misada mbali mbali Tanzania hususani Zanzibar kusaidia tasisi mbali mbali sio bure.

    Agenda ya Marekani siku zote wanaseha hawapigani bila faida , kwa hio na kuitongoza Tanzania hivi sasa sio bure na mutakuja kunambia , na Norway kafadhli hata pesa za kupelekwa hao watu wa kwenda kuwasilisha hilo ombi UN , munazani ni Bure.

    Kwa hio ikiwa Wazanzibar hatukujifunga kibwewe na kuwafunga Wawakilishi wetu vibwewe kuwa tenga wenye kutuuza Basi tutakuja kushtukia tumeshatumbukizwa katika mtego na mwicho wa kushtuka na tutakuwa tunakamatana mashati wenyewe.

    Waswahili wanasema ukimuonelea haya mkkeo basi hupati mtoto katu, au ukimuangalia usoni Nyani basi huwezi kumuuwa bali atakuuwa wewe.

    Kwa hio na sisi tuwalee na tuwadekeze akina Shamuhuna na wenzake , Bada ya kumchombeza Mtoto kulia Basi tutalia sisi.

    YAKIWAUMA SEMEN.

    • believe 06/02/2012 kwa 12:59 um ·

      Ama kweli viongozi wetu wa Smz ni Mabar—? hikweli hawaoni kuwa hawa wenzetu wa Tanganyika wao ni kujivutia upande wao tu? Kama kweli hawa wana mapenzi na sisi basi kuna mambo mengi wanayakwepa kuyafanya kutokana na roho mbaya zao.

      Kwanza kukuza uchumi wa Zanzibar nijambo muhimu sana kwa Wazanzibar, tugeona hawa wenzetu wa Tanganyika wangesema hivi pesa za mamilioni yaliotumika kujenga viwanja vya Mpira wangesema angalau tuinyayuwe Zanzibar kwa kujenga Uwanja wa ndege na wao Uchumi wao ukuwe no, au Kujenga Bandari kubwa lakini haya yote huyapiga chenga na huwa tongoza viongozi kwa kuwapa vijipesa ili waoze visiwa.

      Lakini wasisahau viongozi wetu wa Smz kuwa kidogo wapewacho hasara yake ni kubwa.
      Wao vyao wanavikumbatia vyetu ndio tuwape vipi? Kama ikiwa Tanzanet,Gasi ya Songo songo, Almasi za Mwaduwi na Makaa ya Mawe hizo sio za Muungano vipi Mafuta ya Zanzibar yawe ya Muungano?.

  4. Bosco 06/02/2012 kwa 1:22 um ·

    Hapo ndio pana afadhali, ukitaka kuwaona kwa wingi nenda kwenye idara za serikali wamejaa wao tu. Ukenda maeneo ya mashamba kama makunduchi utafikiri kuna mkutano wao.

    Karibuni wazanzibari nao watakua na utamaduni wa kukeketa wanawake. Hahaha.

    Juzi nilikwenda halmashauri kuchukua fomu ya kununua kiwanja nikakutana na mchaga nae anachukua fomu amenunua kiwanja, nikasema dah nimeshapata jirani mchaga, wazenji mukiuza viwanja musiwauzie hawaaa ah.

  5. Ghalib 06/02/2012 kwa 4:15 um ·

    Hapo kama sikosei darajani,hao wamasai kila mmoja ana kipande cha ukaazi wa zanzibar,kama hamuamini mpeni kazi ashakh atawambia ukweli.

    Huo ndio muungano,baada ya miaka 20 wazanzibari watakuwa kama wapalestina.

  6. Lutfia 06/02/2012 kwa 4:42 um ·

    ni kweli Ghalib wapalestina walikua kama vivi waizrail Mungu amewalani hawana nchi ndio maana wana ngangania palestina na wazungu wanajua ndio maana wanawalinda kwa hali na mali na sisi sio kama tunabagua lakini kijisiwa chenyewe kidogo sasa watu wa mashamba hawana hata pa kulima kwa wanyamwezi wamefoji kila mahali na viwanja watavimaliza kweli si uongo na masheha ni watu wasoelimu huko vijijini ina hitaji waelimishwe kama ni ukereketwa sasa hakuna tena ulobaki ni ukombozi tufahamishane kwa kila mmoja wetu wengine naamini hawajaelewa kinachoendelea ndani ya nchi yetumpaka sasa sababu TV ya zanzibar haionyesi maendeleo au yanayopaswa watu kufahamu kusudi wabaki na ujinga mambo haya mpaka lini jamaniiiii

  7. kafiri orijino 06/02/2012 kwa 8:00 um ·

    Ubaguzi..

    • Ghalib 06/02/2012 kwa 8:27 um ·

      @Urijino

      Ubaguzi wetu wa kula maslahi ya vizazi vyetu,ni haki yetu,kukubali na kukataa muungano ni haki yetu,sisi ubaguzi wetu hatuuwi kama munavyotufanyia nyinyi wazanzibari ,mulituuwa kwa bunduki ,muliwabaka dada zetu,mulitufanyia kila mabaya,unafikiri tumesahau 2001 ?

      Ubaguzi umeletwa na watanganyika zidi ya wazanzibari,na sisi nasi tumekuwa maadui zenu,na ubaguzi huu tutaudumisha hadi kuuvunja muungano,hapo sisi tutakuwa hatuna tatizo na nyinyi.

      Ubaguzi wenu umezidi,office za muungano,uwakilishi wa kimataifa katika muungano,ajira ndogo ndo katika muungano, mzanzibari hana haki katika muungano.

      Unategemea nini ?

      Mi nasoma blog za kitanganyika,nasikia wakisema kuwa wazanzibari ni wabaguzi wanataka kujitenga,kwa nini ? Mbona hatuwasikii hawa waengereza wakisema wascottish ni wabaguzi wanataka kuvunja muungano ? Iweje iwe kwa wazanzibari tu ? Kuna udugu gani baina ya wazanzibari na watanganyika kwa miaka 48 ya muungano ? Angalia muungano wa UK zaidi ya miaka 200 mbona hakuna mambo ya kibaguzi juu ya muungano ?

      Watanganyika siku zote wanajifanya wao ndio top eti wasomi wanajua siasa,basi sisi tunajua zaidi,na tutaendelea vita juu ya kuigomboa zanzibar yetu hatua kwa hatua,hatuwimbiii.

      • kalasinga 07/02/2012 kwa 3:18 mu ·

        sasa kama ndio sawa na hii kazi ianze muwahamishe ndugu zenu walojazana huko bara kama wakimbizi wa kisomali ili wasipate sababu ya kuwa wapemba wamejaa karakoo, na ilala na sehemu nyingi kwa hao wanaotubagua. hebu rudini mwakwenu muone kama na wao hawatotafuta safari..isiwe kama hadithi za wabunge wetu wako wanasema hawataki muungano lakini bungeni ndio wa kwanza kufika

        na kesho likianza zoezi hili hakuna mtu wa unguja ataeathirika kwani sisi tupo na unguja yetu daima milele ila wapemba itakuwacost kwa utangi tangi wao wasiojua kukaa kwao halafu wao kwao pemba asende mtu. si watu makini kabisa lack with positive attitudes which lead them in to the darkkness of law minded, finaly poor decision and failure.

        ubaguzi wa mzalendo kiboko kuliko wa sultan.

      • Ghalib 07/02/2012 kwa 1:54 um ·

        @Kalasinga

        Wazanzibari sio kama hawawapendi watanganyika kama unavyofikiri wewe,tatizo ni kwamba hivi visiwa ni vidogo na vina eneo dogo,serikali imeshindwa kuzibiti waingiaji kutoka sehemu nyengine ambao sio wakaazi wa zanzibar.

        Wazanzibari wanahofia kupoteza identity yao,kutokana na uchache wao,hivyo basi kuwepo na udhibiti wa wageni,hata waje morogoro nzima ,lakini kuwepo na utaratibu wa uingiaji,waingie kwa passport,hao unao waona wewe,smz huwa wanawapatia vibali vya uzanzibari haliyakuwa sio wazanzibari.

        Kwa maana hio wananchi wameona mbali suala la identity yao kwa vizazi vyao,viongozi wao hawaoni hili kwani wao wanaangalia maslahi yao binafsi,inatuuma sana kuona wageni wanaingia zanzibar bila ya misingi yoyote,hatujui kama wafanya biashara,au wafanyakazi,wapo wapo tu,wengine wanalala njee hao unao waona wewe.

        usiseme ubaguzi.

        Mwaka jana Rais wa ufaransa alikuwa akilalamika katika EU kutokana na wageni ambao wanao toka romania walivamia ufaransa ,wakawa wanalala njee,kazi zao omba omba,wizi katika maduka.

        Mbona haikutoka katika media kama ni ubaguzi,hali yakuwa sheria ya EU inawaruhusu kuingia nchi yoyote kama ni kutoka EU ? Lazima kuwe na mipaka ambayo kila nchi inalinda maslahi yake.

        Wazanzibar sisi tuende sote tanganyika hakuna athari yoyote itakayo waathiri kwa sababu sisi ni wachache hata milioni 1 laki tano hatufiki,angalia watangnyika wako zaidi milioni 40 waje mkowa mmoja tu wa morogoro basi tumeumia wazanzibari hatuna hata pa kupumua.

        Lazima tulinde nchi yetu zidhi ya wageni kuwe na limit maalum ya uingiaji wageni,sio kuingia kama choo,hivi ni visiwa sio mainland,kwa nini UK wao hawajaikubali shengein visa ? Nafikiri UK ingelikuwa ishajaa kwa watu wanavyo ipenda hii nchi.

        Wacha waseme ni wabaguzi lakini ukweli ndio huu,habaguliwi mtu kwa rangi hapa wala mavazi,mgeni yoyote ambaye sio mzanzibari lazima awe na limit ya kuishi visiwa hivi.

  8. stafeli 06/02/2012 kwa 10:35 um ·

    lakini kama mscottish hakufukuzwa england wala kuonewa taabu kuishi hapo, sasa kwa nini sisi wazanzibari tuone taabu kuwa wamasai sasa wameamua kuja kuishi zanzibar? Kwani wao si watanzania? na je hakuna wazanzibari wengi tu wanaoishi mikoa mbali mbali ya nchi hii ya Tanzania? kesho england na scotland zikigawanyika, maana yake kila mwenye kwao arudi? kama ni hivyo basi tusubiri inshaallah tuipate zanzibar baadae tuwarudishe wamasai makwao na sisi wanzibari tunaoishi mikoani bara turudi makwetu! Ngoma draw! au vipi?

  9. sinalawy 07/02/2012 kwa 6:35 mu ·

    Marehemu Mzee Karume alieunganisha nchi aliweka mipaka. Kwa mfano kila Mzanzibari aliyetimia miaka 18 lazima ame na kadi yake ya uraia (narudia tena KADI YA URAIA sio ya ukaazi) na usafiri baina ya visiwani na bara ulikuwa wa PASSPOTI japo ya karatasi. Na mingi mengineo ya kuulinda U-Zanzibari.

    Kaondoka yeye na haya yote yemeondoka.

    Tumlaimu nani?

    • mnazimmoja 07/02/2012 kwa 7:22 mu ·

      Mimi na wewe au ?

      • sinalawy 07/02/2012 kwa 7:36 mu ·

        Wala si uongo, na tulikuwa tunafurahia kuondoka ile tabu kwenda branch ukachukue barua halafu uende ofisi ya migration ukajaze fomu ya kuomba passpoti ya miezi mitatu.

        Wakati ule tuliyaona mazuri. Ila mie sikufurahi kundoshwa kadi ya uraia, nilikuwa nasubiri kwa hamu kutimia miaka 18 ili na mimi niwe na kadi yangu.

        Suali ni kuwa kuna ubaya gani tukiyarudisha?

  10. Embesakua 07/02/2012 kwa 2:55 um ·

    Mola wetu mlezi amekataza ubaguzi ktk qurani yake, cha kushangaza watu bado tukunywa sumu ya ubaguzi.

    Mtume wetu alizaliwa makka, kafia madina, kazikwa madina, nitafurahi km nitaona wamasai wote wamegeuka kuwa waislam tukaishi nao vizuri raha mustarehe.Watu wa tashkili hapa ndo muda wa mmasai kuingia Msikitini akatoa adhana na mwisho akakabidhiwa kibla insh.

    • Ghalib 07/02/2012 kwa 3:30 um ·

      @Embesakua

      Hapa hatuzungumzii ubaguzi tunazungumzia suala la uvamizi katika nchi yetu,na uvamizi huu hauendani na maadili yetu,lakini pia kitu cha msingi kabisa ni identity yetu ya uzanzibari tunahofia kupoteza katika miaka 20 ijayo,hivi ni visiwa sio mainland,tuna eneo dogo,tuna watu kidogo,ardhi ndogo,ni vyema tukalinda nchi yetu.

      Hii ni zanzibar njema atakae aje,lakini sio kuja kama machungwa kuwe na mpanga maalum ya uingiaji katika visiwa hivi,la si hivyo tutaendelea kuwa koloni la watumwa na tutendelea kuwa na ubaguzi dhidi ya wazanzibari,wewe ubaguzi tuseme huoni,katika serikali ya smz,ukiwa mpemba hupati kazi,aidha uwe mmakunduchi,mdonge,mtanganyika.

      Haya baada ya miaka 20 kuna vizavi vipya vya kitanganyika vimezaliwa zanzibar ndio watakao pewa ajira na ndio watakao shika usukani wa nchi,hapo mzanzibari ndipo utakapo jutia.

  11. Embesakua 07/02/2012 kwa 3:52 um ·

    @Ghalibu

    Nimekufahamu vizuri ila ujue wao pia ni binaadam na wana haki ya kuishi sehemu yeyote ya huu ulimwegu.
    Nadhani ktk watu wanaoharibu tamaduni za watu hapa duniani sio wamasai ni wazungu ndio nambari one kwa kuchafua tamaduni lakini baadhi yenu nyinyi wazalendo ndo hujiskia fahari kwa kua nchi imejaa wazungu wakenda uchi, na kuleta ulevi na madanguro. sasa nani anaharibu identity kati ya mmasai na hao wanaitwa watalii.

    kwani wewe hujui kwamba hawa wamasai wamekuja hapa kwa sbb kubwa ya mahoteli ya kitalii. na lengo lao kubwa ni kulinda, na hii imekujwa kwa sbb watoto wa kizanzibar kazi ya ulinzi hawaiwezi wanaona haya ati mayoo wanaitwa?

    Mimi nadhani kwa sbb mnawaona ni maskini ya Mungu tu ndo mnawachukia lakini wangekua matajiri basi mungewaita hapa waje kufanya utalii.
    Kuna hata wahindi ambao ni ashaddu minal katil lakini ndio wanaongoza kwa rushwa na ufisadi ktk nchi hii na wameshiriki ktk ufisadi mkubwa km EPA, RICHMOND na mengine mengi lakini husikii lawama.

    Usimdharau Mmasai huenda akawa bora kuliko wewe, km ttzo ni identity basi na tuanze kuwafukuza machina yalojaa tele huko mjini, na wazungu wenda uchi na ambao biashara ya ulevi imeshamiri kwa sbb yao.

    • Ghalib 07/02/2012 kwa 5:32 um ·

      @Embesakua

      Naanza na suala la EPA na RICHMOND

      Suala hili halituhusu wazanzibari,kwa maana hiyo huo ufisadi unao ongea wewe ni tanzania bara hapa tunaongea kuhusu zanzibar sio tanzania bara/tanganyika.

      Suala la mzungu na mmasai,kwanza ufahamu mzungu sizani atatoka kwao huko bila ya kuingia zanzibar kuonana na immigration,hata kama atashukia dar basi lazima atapitia immigration,kwa maana hio hawa tunawatambua ni nani na wamekuja kwa madhumuni gani na wako zanzibar kwa muda gani.

      Wamasai wanakuja zanzibar na makabila mengine kutoka bara sio kwa kufanya kazi tu,bali kuongeza nguvu na kuuwa utamaduni wa zanzibar,kila siku zikienda makanisa yanazidi,pia chama cha ccm kwa vile sera ni moja ,hawa wageni wa kitanganyika wanapokuja zanzibar wanawapa haki zote kuliko mzanzibari,moja ya haki hiyo wazanzibari hadi muda huu hawajapata vipande vya ukaazi,zan ID.

      Pia wamasai imejulikana kuwa wanapatiwa vipande vya ukaazi,cad za chama cha ccm,ili kuongeza nguvu za chama chao cha kikaotliki.

      Mzungu anatembea uchi zanzibar ni kweli lakini sio uchi wanao tembea wamasai maziwa njeeee,au huwaoni,wazungu watavaa vipensi,watajianika katika mahotel na vichupi vyao kwenye bahari ambako kwenye mahotel,na suala hili ni suala ambalo la kulaumiwa serikali sio wananchi.

      LAKINI wananchi wana haki kulinda nchi yao kwa njia yoyote,alimuradi iwe sahihi,sizani kama ni kosa kuchukia wageni,hata hizi nchi tunazoishi sisi tunachukiwa na wazungu hali yakuwa tumepewa haki za kuishi na tunaishi kihalali tukiamua wakati wowote tunarudi kwetu,au wakiamua wanatuvyang’anya haki zao na kuturudisha.

Comments are now closed for this article.