Zanzibar Internationa Airport
Mi naomba kutoa mchango wangu kuhusu huu uwanja wa ndege wa Zanzibar kwani kwas asa tuna barabara moja tu ya kutulia na kurukia ndege,hii ni hatari kwani ajali ikitokea katika barabara hii ina maana ya kuwa kwa kipindi cha mda mrefu hakutakuwa na urukaji wala utuaji wa ndege. Zanzibar hatuna vifaa kwa kuinulia vitu vyenye uzito mkubwa kama ndege ,sio lazima tuwe na barabara 3 ama 4 kama viwanja vya wenzetu , uwezo huo kwa sasa hatuna ila serikali lazima ifanye mpango wa kujenga njia ya pili ambayo itwuwezesha uwanja kuwa uhakika wa kutua na kuruka ndege wakati wowote ,najua wengine watasema kuwa kuna viwanja vikubwa kama Nairobi na kina njia moja ,wao wana kreni za kuweza kuondoa ndege katika njia pindipo zitapata ajali ama kukwama,nakumbuka mwaka 2006 ilikuja ndege kutoka Hispania na ilishindwa kuruka kwa siku ile ,bahati nzuri ni kuwa ilikwama pale pa kushukia abiria na hivyo ikawa fadhali kwani ndege nyengine kutoka Italia zilikuja na kuondoka bila ya matatizo yoyote.
Pili ni kuimarisha pia huduma ya mafuta kwani kuna ndege kubwa hazitii mafuta hapa kwa kuwa hamna ya kutosha na inalazimika kwenda mombasa au dar es salaam ,hii ni aibu na inaikosesha mapato serikali na nchi kwa ujumla.tutizame kuna nchi za viswa vidogo vina huduma kamili za viwanja vya ndege.Nasikia kuna jengo jipya linajengwa kwa ajili ya kupokea abiria.Ziiimarishwe huduma za ukaguzi wa mizigo kwani kwa sasa hufanyika kwa mikono na huchukua mda mkubwa kwa mtu kutoka nje ya kiwanja wakati viwanja vya wenzetu hili ni jambo la kufanywa kwa mashine.Hili ni moja katika mambo ya kufikiriwa sana kwani hapa ndio mapokezi ya na sura ya nchi.
Serikali iyashawishi mashirika ya ndege kuifanya Zanzíbar kituo (hub)chao cha kutoa huduma (mafano Ryannair ambapo makao makuu ni Ireland na pia inatumia uwanja wa ndege wa El Prat Barcelona kama kituo(hub) chake kikuu cha safari nchini Hispania.)
Pia serikali ifikirie kuanzisha shirika lake la ndege na kama haina uwezo basi itafute watu ambao wana uwezo wa kuwekeza katika sekta hii na hili liwe suala huru ,ili mashirika yaje kama walivyokuja watu kuwekeza kwenye utalii,hii itasaidia sana kutoa ajira kwa Wazanzibari.






One Comment on "Zanzibar Internationa Airport"
Mtoa mada hongera kwa uzalendo wako wakupenda kuona mabadiliko nchini mwako.Hivyo ndivyo inavyotakiwa kwa kila mmoja wetu kuona kuwa nchi yetu inapiga hatua ya maendeleo.Hata hivyo maamuzi makubwa kama hayo hayafanywi kwa vigezo kama ulivyotoa wewe.Kuna tathmini za kiuchumi huwa zinafanyika katika kutoa maamuzi ya kipi kijengwe au kisijengwe.Jee ni nini faida zake za muda mrefu,gharama zake na mambo mengine.Sasa ukiona viwanja vikubwa vya wenzetu kuliko hivyo vya kwetu havina hizo njia mbili,basi hilo wamelifanyia tathmini siyo kwasababu wana kreni la kunyanyua ndege pindipo pakitokea ajali isipokuwa kuna sababu kubwa za kiuchumi kuliko hiyo ulioitumia wewe.Jee kwanini usishauri basi na sisi tununue hiyo crane badala ya kujenga njia nyengine ambayo kwa miaka itakaa bila ya kutumika wakati kuna mambo mengine ya kufanya kwa kutumia pesa hizo.Nafikiri hayo mengine uliyoshauri yamo kufanyiwa kazi nategemea ujenzi wa jengo jipya unaoendelea utatatua baadhi ya mambo uliyoshauri, na hilo la shirika la ndege kama hujasikia basi ningependa kukufahamisha ya kuwa hiyo ni moja ya ahadi alizotoa Maalim Seif mgombea wa urais wa CUF, kuanzisha Zanzibar Airways pindipo chama chake kitaingia madarakani.