ZANZIBAR MPYA HII HAPA
- UHAKIKA WA MAENDELEO YA HARAKA UPO
- TUFUTE MAZOEA MABAYA
By Zdaima
Mwanadamu kwa kawaida hupenda kudadisi kutokana na mazingira yaliyomzunguka. Mwelekeo wa upepo na kasi yake,mazingira yalivyo kama ni ardhi yenye mavumbi,takataka au kama upepo unapita bila kizuizi ndivyo watu waliokaribu wanaweza kukisia athari za upepo huo kule utakakomalizia.
Naam na zanzibar Mpya yenye maendeleo iko hivyohivyo yawezekana .
Yawezekana kutokana na mazingira yalivyo na vile yatavyodumishwa kuwa hivyo {hili ni sharti} zanzibar ikapata maendeleo ya haraka. Mwelekeo ulivyo uko katika hili la Kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa na ikawa ya kitaifa kweli.Kwa mtazamo wangu Zanzibar yenye maendeleo lazima Serikali ya kitaifa ijayo izingatie haya na kuyatekeleza
Kwanza Serikali hio iwe imepatikana katika ile sura halisi ya maridhiano ili kuhalalisha utawala wa dhati usio na manunguniko kwa upande wa pili wa washirika ,hii ni hatua muhimu ya kwanza.Katika kuwapata viongozi wachaguliwe wenye uwezo halisi kwa vigezo vyote vya kiongozi bora {hii ni kazi ya wananchi wakikosea tu basi ovyo} hasa kwa hali ya sasa ya Zanzibar ambayo inahitaji waokozi na wakombozi katika masuala yote muhimu kama nchi.Yakifanikwa haya tutafika huko.
Serikali hio itakuwa na uwezo wa kusimamia mambo yake na ni lazima isimamie mambo hayo bila woga .Kwa wazanzibari wazalendo wanatarajia serikali itafanya haya
kuondoa vizingiti vyote vinavyorudisha nyuma maendeleo ya wanzanzibari katika muungano uliopo baina ya Tanganyika na Zanzibar kwa kufuata misingi ya kidemokrasia,mikataba ya kimataifa,na kikatiba lakini bila kupotezwa kwa muda kwa visingizio vyovyote vile.Kwa mfano kuondoshwa kwa suala la mapato katika muungano,Mahusiano ya kimataifa.Mambo haya mawili tu kwanza Zanzibar inaweza kupiga hatua .Itakuwa na uwezo wa kuingia mikataba mikubwa ya mashirikiano ya maendeleleo, tazama Rasilimali za bahari na fukwe zake .mikataba hii ikelekezwa katika kupata bandari kubwa na za kisasa na wakaachiwa Wazanzibari{serikali} kusimamia wenyewe mapato sijui itakuwaje hapo. ikiwekwa Bandari huru Zanzibar ktk mazingira hayo ni muda mfupi tu maendeleleo tayari.Kukiwekezwa katika utalii wa kisasa na uwekezaji wa kisasa kwa mfano kwa mazingira ya zanzibar pakiwekezwa katika huduma za mahoteli,na mikumbi mikubwa ya mikutano ya kimataifa utalii utakuwa,shughuli za biashara zitakuwa{bussiness Activities zitaongezeka} tazama kule Arusha tu Tanganyika wanafaidika vipi na hili pamoja na ufisadi ulioko ,watu wake wanalingana na idadi ya wakaazi wa Zanzibar sikwambii hizo fursa nyengine zilizopo.
Serikali hio kuajiri watu wenye taaluma zao na ijali utaalamu wao .katika hili uzembe utaondoka hasa ktk utumishi wa umma na ufanisi utaongezeka .Zanzibar ina wataalamu wengi sana nje ya nchi na ndani ya nchi na hawajatumika au wanatumikia nchi za watu,ina wafanyabiashara wengi ambao hawatki hata kujulikana kwao kotokana na mazingira yalivyokuwa hawa watapata fursa ya kuja kuendeleza kwao
Wazalendo wana matumaini ya serikali hio kusimamia usawa katika hali zote katika ajira,uwakilishi,maendeleo,huduma n.k hii ni nguzo ya mshikamano na umoja miongoni mwao
Matumaini mengine ni kuondolewa kwa mfumo mbaya wa utawala wa ndani ambao umeota mizizi ya kubebana kwa kujuana au wa kiitikadi ambao huondoa fursa za watu wengine kutumia vipaji vyao kwa aili ya Zanzibar hili likishughulikiwa kwa makini maendeleo yatakuja tu.
Hii mada ni ndefu sana lkn kwa ufupi tu Serikali hio ikiweza kudhibiti vyanzo vyake vya mapato bila kuingiliwa,ikiboresha mfumo wa utumishi serikalini ,ikiingai katika uwekezaji wa kisasa .ikijali wataalamu wake,ikazingatia usawa wa kijamii katika mambo mbalimbali,ikaweka utawala wa kisheria na uwajibikaji Zanzibar Itaendelea kwa muda mfupi tu .Zanzibar watu wake ni kidogo na ina fursa nyingi sana za kiuchumi ambazo hazijatumika .Sekta ya biashara na utalii tu pamoja na utumishi serikalini kama itaimarishwa Wazanzibari watahitaji wageni kuja kufanya kazi hapa.Zikikuwa shughuli za biashara kila mmoja anamuajiri mwengine,Wenye magari wataacha tenda za mizigo,matajiri watawajiri wabebaji na wasafirishaji,maghala yataongezeka, wauza chakula watauza kwa wakati,mzunguko wa fedha utaongezeka kwa watu wote hatimae kipato kitapanda .Kwa nini maendeleo yasije? Sikwambii kilimo na uvuvi na nyanja nyengine
Mwisho yote haya yanahitaji viongozi makini,majasiri,wazalendo wa kweli,wenye uwezo na nia ya dhati kwa Zanzibar .Tufanye jitihada kuwapata hao na wakati ni huu.
Mungu ibariki Zanzibar na watu wake .Ameen





