Habari

Mzanzibari Zinduka: Usaliti Wa Lipumba na Khammnyaharuna Sio Wakuachiwa!

Sehemu ya 2:
By Ashakh & Zamko

Asalamu aleikhum ndugu zangu Wazanzibari wa Ndani na Nje ya Visiwa vyetu adhimu, ama kwa upande wetu tunamshukuru Allah SW kwakutupa pumzi, uzima na wasaa wakuandelea kuandika makala hii muhimu sehemu ya pili.
Kama tulivosema katika makala iliopita kwamba, Mada hii itakuwa na sehemu 3 yenye kichwa cha habari hichi hichi. Sehemu ya 1 tuliitowa juzi na hii ni sehemu ya 2. Sehemu hii ya leo, tutaanza kuwachambuwa hawa akina LIPUMBA na KHAMMNYAHARUNA katika points 2 kubwa zilioko hapo chini:-

1. Tutaelezea kwa kina nini historia na mchango wa Khammnyaharuna kwa Chama cha CUF na kwa Wazanzibari?
2. Kwanini Khammnyaharuna wawe wanatoka Upande mmoja tuu wa Visiwa vya Zanzibar, yaani katika kisiwa cha Pemba na sio mchanganyiko wa Unguja na Pemba?

Kabla yakuanza kuelezea hizo pointi 1 na 2, Wazanzibari na wazalendo tunataka muelewe kwamba Visiwa Vyetu Vilikumbwa na Giza kubwa la Mapinduzi 1964. Na Kwakuwa Hatukupata kiongozi mwenye Elimu ya Dini na Dunia akatuunganisha na kuyafanya Mapinduzi ni Sehemu ya Historia yatu kama vile wenzetu wa Ujerumani na Nchi nyengine za EU walivoweka Vita vya 1 na 2 vya dunia itabakia kuwa Historia. Kwetu sisi Tulidanganywa na Kufutiwa historia yetu. Na tukagubikwa na Giza la Udictotor, Ujinga na Uongo uliopambwa kwakutiwa khofu katika nyoyo zetu.

Mimi nakubaliana na msemo wa Mashekhe wetu wa Pemba waliosema kwamba, Dhulma ikianza Juu ni jambo bay asana kwani kwa mfumo wa Siasa zetu tulizojengewa za woga, udanganyifu na woga. Hakutakuwa na mtu wakukemea dhulma hizo zilioko Juu sasa na Wananchi wa Chini matokeo yake nikuendeleza Dhulma na hujuma kwa wenzao waliokuwa wanyonge zaidi. Na haya mdio ninayo yaona yanaanza kutokea katika Visiwa vyetu vya Zanzibar.

1. Tutaelezea kwa kina nini historia na mchango wa Khammnyaharuna kwa Chama cha CUF na kwa Wazanzibari?

Khalifa Sleman Khalifa:
Ni mzaliwa wa Gando Pemba na amekuwa Mbunge wa EAF kwa muda wa miaka 5. Khalifa amekuwa Mbunge wa CUF kwa kipindi cha miaka 20. Sio chama kilichomuangusha Khalifa bali wanachama wa CUF jimbo la Gando ndio waliomtema baada ya kufurutu mipaka. Mimi binafsi Khalifa simjuwi mchango wake kwa watu wa Gando lakini kwa Zanzibar- nakumbuka alikuwa akipiga pig asana kelele kutetea au kuonyesha kukerwa na ule Muungano usiokuwa na Usawa.

Khalifa kama angekuwa ni Mbunge wa Nchi kama za Ulaya, kwa miaka hio 20 yote aliokaa basi angekuwa ameshaliimarisha Jimbo lake japo kuweka Nguzo za Umeme na kuimarisha Maendeleo katika jimbo hilo. Lakini badala yake Gando iko vile vile na hakuna kubwa alilolifanya Mbunge huyo kwa muda huo wa Miaka 20.

Chakusikitisha zaidi nikuona kwamba viongozi wengi wa Zanzibar hasa kule Pemba wanamtindo wa Kudharau sehemu walizotoka n ahata kuhamishia makazi yao katika miji ya Watu au Nchi za watu. Kwa upande wa nduguyetu Khalifa maakazi yake na mali zake zote ziko Tanganyika. Kwa siasa za wenzetu kule Ughaibuni, hili ni jambo la dharau na kusikitisha kuwakimbia wananchi wako wanaokuchaguwa kila ikifika kipindi cha miaka 5 ya Uchaguzi. Na ukimaliza uchaguzi huonekani tena hadi katika kampeni nyengine za Uchaguzi.
Tunahisi Khalifa hajaisaidia chochote CUF wala Wazanzibari katika kipindi hicho cha miaka 20 ya Ubunge wake ndani ya CUF.
Hatushangai kumuona akijiunga na usaliti kwasababu Zanzibar na Wazanzibari hawamuumi – inayomuuma ni Tanganyika kwenye mali na familia yake.

Khalifa akumbuke tuu Damu za ndugu zetu waliouliwa 2000 hazikupotea bure pamoja na mikwaju aliyopigwa yeye mwenyewe. Akumbuke fadhila alizofadhiliwa na Wazanzibari kutoka Gando. Kwa ticketi ya CUF halifa ameweza kuwanyonya Wazanzibari kwa mika 20 na sasa jaza yake ni Mateke.
Khalifa hivo hisani yote uliofanyiwa na Watu wa Gando hukuona Jaza ya kuwalipa isipokuwa Ujiunge na Lipumba- Mtanganyika ambae ni hasidi na dhalimu wa haki ya Wazanzibari? Utakwenda kusema nini Khalifa mbele ya Allah?

M- Musa H. Kombo.
Musa Haji nayeye alikuwa Mbunge wa jimbo la Chake chake, lakini ana historia ndani ya CUF. Alikuwa muasisi na msimamizi wa kupata usajili. Alikuwa miongoni mwa wakurugenzi wa mwanzo wa CUF. Miaka ya karibuni alikuwa Mkurugenzi wa Organisation na Uchaguzi

Musa Haji alikuwa muwakilishi katika awamu moja au mbili. Na mimi sijawahi kuona, au kusikia kama kuna jambo lolote la mradi wa maendeleo alioisaidia Zanzibar na Wazanzibari katika Jimbo lake la Chake.

Musa Haji ni muathirika mkuu wa siasa zetu. Mwaka 2001 alipoteza ndugu yake Bw Ali Haji Kombo kwa kupigwa risasi na kuuwawa kwenye maandamano. Ila amekuwa mmoja wa Wazanzibari mwenye jeuri na dharau kwa wanajimbo wake. Kashindwa kusubiri au kuungana na Wazanzibari wakadai Haki yao kwa njia ya umoja – badala yake ameamuwa kuwa msaliti.

Pia Naamini Mungu na Radhi za Wazanzibari hazitamuacha. Hivo tukimuuliza Musa kwanini ameingia katika mkumbo wa Lipumba wakati katiba ya CUF inaeleza wazi kwamba Lipumba sio mwanachama tena seuze kiongozi wa Taifa, atajibu nini?

Mnya= Mohamedi Mnyaa
Mohamedi Mnyaa ni mmoja wa Nusul Fadhila kama alivo Khalifa, Mnyaa amekuwa mbunge wa CUF kwa mihula 3 miaka (15). Aliwahi kufikia kuwa kiongozi wa upinzani Bungeni. Uchaguzi wa mwaka 2015 Mnyaa alishindwa na mpinzani wake CUF ikamrudisha kugombea. Hadi pale jimbo lake lilipofutwa ndio Mnyaa hakupewa tena nafasi ya kugombea.

Hakuna kitu hata kimoja Mnyaa alichoifanyia CUF au Zanzibar katika kipindi hicho cha miaka 15.

Jee kweli hawakuwa na akili yakuekeza hata kwenye miradi ya Ufudaji? Ukulima, Uvuvi?.
Jee wamewasaidia nini Wazanzibari wa majimbo yao. ? Northing. Hawana fadhila wala hawajuwi kufadhiliwa na wananchi wao. Na Wananchi wa Pemba Kwavile hawana Chama chengine wataendelea kuwapigia kura Watovu wa fadhila wengine katika uchaguzi Ujao.

Ha= Haroub:
Haroub alikuwa mbunge wa Jimbo la Chonga akiwa na kila dalili ya mambo machafu. Watu Wengi wa maeneo yale ni watu wakujipendekeza pendekeza.

Aliamuwa kuhama Chonga moja kwa moja, katika kipindi hicho alijikweza zaidi kwa Lipumba ili amrudishe kugombea. Alikuwa akirudi kikaoni humpa Lipumba milioni 2 hadi 3.

Mchango wake pia sijauona na ndio maana akawa hana uchungu na Zanzibar au Wazanzibari.

Ru= Rukia:
Huyu nayeye ni mpya katika sura za Wana CUF nayeye ni Mbunge wa Kuteuliwa Giza la njaa ya ulwa ndio lilompelekea mama huyu kuingia kundini kwa Mtarahamwe.

Na= Nassor Seif Amour:
Nassor amewaacha Wazanzibari Wazalendo wengi katika kitu cha kustaajabisha sana. Nassor ana historia kubwa ktk CUF na kijana huyu sijuwi ni kitu gani kilicho mughilibu kumfuata Lipumba.
Kama Si Jazba na Chuki zake Juu ya watu Fulani basi siwezi kupata jibu jengine. Yeye ndio katika vijana Waanzilishi wa CUF. Misukosuko kadhaa ya kisiasa imemfika ikiwa ni pamoja na kufungwa, kuwekwa ndani, kupigwa nk. Jee Nasor Sefu haoni machungu kisaliti CUF na Wazanzibari akimuunga mkono Lipumba

Lipumba CUF kaikuta tuu. Lakini waanzilishi ni akina Nassor, Maalim Sefu, Mloo, Ali Haji Pandu, Maulid Makame, Sudi Yussuf Mgeni, Hamad Rashid, Hamad Masoud Musa Kombo na wengineo.

Nassor alikamatwa yalipotokea maandamano ya Sofia Kawawa (Laana Tullah laadhim). Aliposema Sheria za Kiislamu zibadilishwe ili Wanawake Wapati haki za Urithi sawa na Wanaumme. Maandamano hayo mimi nilihudhuria na tukatawanywa na Polisi FFU, Wakati huo kulikuwa hakuna Maji yakuwasha wala Jeshi la Tanganyika bado halija vitawala Visiwa kama ilivyo sasa.
Nassor hivo ana malengo gani kuingia katika kundi hili la Lipumba na Khammnyaharuna? Hivo yale machungu ya Kuzalilishwa hadi kukosa hata kazi ya maana yeye anayafurahia?

Nassor Sefu Itakapotokea fujo kwa ajili ya unafiki wenu na kuuliwa watu wasio hatia. Mutafanya nini? Hivo wewe Nasor Sefu ni Wakutaka kumtambua Shwni kama Raisin a ukasahau HAKI ya Wazanzibari Walioporwa katika Uchaguzi halali wa 25.oct.2015?
Lipumba akimpinga Maalim na CUF ana haki kwasababu Watanganyika Walipokoma hawataki Kuiona Zanzibar inasimma wenyewe. Na hili Ndio Lengo ya yote hayo. Sasa Wewe Dodoma Umeshapewa pa Kukaa kama hapa Zanzibar patachafuka na kwenu Pemba hawakutaki?

2. Kwanini Kha-m-mnya-ha-ru-na wawe wote ni Wapemba? Yaani wamechaguliwa kutoka Upande mmoja tuu wa Visiwa vya Zanzibar na sio mchanganyiko wa Unguja na Pemba?

Wazanzibari hapa nataka mutafakari sana kwanini Sefu Ali Iddi (CCM) na Lipumba Wamewachaguwa Wakurugenzi hawa wote wenye asili ya Pemba? Sababu zitakuwa Nyeti hapa na kwa upande wa CUF kwavile wamepoteza Dira ya Kudai haki yetu na Sasa wamekuwa wanashuhulika na Lipumba tuu. Hivo CUF wameliona hili?. Lakini CC tuliokuwa hatumo katika Protocol ya Uwanachama au Uongozi tunaweza kuliona hili kama ni Njama moja kubwa ya Kuiuwa CUF kwa Kuwagonganisha Vichwa Wazanzibari Walioshikana kitu kimoja na Kudai haki yao.
Mimi kwa uoni wangu nimeona points hizi 3 ndio iliowafanya CCXM na Lipumba wawachaguwe Watu hawa. Jee Wewe una muona gani katika point hii ya pili?

1.Kuwagawa Wazanzibari walioko CUF kwa Upemba na Uunguja ili watu warudishwe kwenye Mzozo na mantiki iliopo. Kwavile baadhi ya watu wa Unguja wanakuwa week kidogo kwakutoa uamuzi mgumu. Hili ni Jungu la tope Chafu linakorogwa na Mnywaji ni Wazanzibari wanyonge. Na Watakapowagawa hivo Watu wa Unguja kwa vile wataona Chama kimeshakatika na ndani ya Huu Uongozi wa CYF ya CCM na Lipumba hamutokuwa na mtu wa Unguja basi inaweza kuchanganyikiwa na kurudi CCM hata kama itakuwa watanunuliwa kwa pesa ya CUF. Tujikumbushe Chaguzi ziliopita, kila miaka 5 CUF Unguja ikiibiwa au kuuza Kura kwa CCM. Hili litajirudia tena.

2.Jengine kwa muono wangu mimi, kuwadhoofisha wananchi wa Pemba wasiwe na Imani tena na CUF au Viongozi wa Cuf na kugoma kwenda kupiga kura na ku express Civic right zao za kiraia. CCM Wataichafua CUF kule Pemba na kuwatowa imani .

3.Kutaka Kuanzisha Fujo ili Ionekane kwamba Wapemba ndio Waliokihodhi Chama cha CUF badala yakuwa ni Chama cha Wazanzibari wote.

Makala ya 3 itakuwa na points hizi
Kiongozi gani mbadala atakae ishika CUF bila ya harufu ya chuki na ubaguzi?
CUF imepoteza Dira yake?
CUF ni nani na Nini yao ukitoa mgogoro wa Lipumba.

Nawasilisha kwenu
Wabilahi Taufiq

Share: