Kuhusu

Utangulizi:

Nakala hii lengo lake ni kufahamisha jinsi ya kutumia websaiti ya mzalendo.net.Toka tumefungua rasmi websaiti hii, tunashukuru wale wote waliochangia kwa njia moja au nyengine.Kuna mambo ambayo ni muhimu kama watembeleaji kutoa maoni yao.Mafundi wa blogi hii, kuna mambo hawana uwezo wa kuyaona au kuyagundua, na wanategemea maoni kutoka kwa watembeleaji wake.Mnaombwa tafadhali kutoa maoni yenu haswa pale mnapoona hitilafu zimejitokeza, mfano unapogundua neno ambalo limekosewa kuandikwa na mengineyo.Unaweza kutuma moja kwa moja mzalendoinfo@gmail au kuacha maoni kwenye “Mapendekezo” katika gawanyo la “ujumbe maalum”.

Wanachama wote waliojiandikisha kwenye mzalendo.net, moja kwa moja wanapewa haki ya kuwa ni waandishi.Hii ina maana mtu yeyote anaejiandikisha kwenye blogi hii anaweza kuchapisha na kuandika habari.Lengo la mzalendo.net ni kuwakilisha maoni na habari zinazotekea Zanzibar zikiripotiwa na wazalendo wenyewe kutoka visiwani.Japo habari zengine hazijazuwiwa lakini tunarajia habari zinazopendelewa hapa mzalendo.net ni za kizanzibari kuanzia siasa, michezo,tafiti na mengineyo.

Baada ya utangulizi huo mfupi, sasa tuanze kusoma unahitaji nini na jinsi gani ya kuchapisha.Kwa ufupi mzalendo.net imetengenezwa kwa kutumia programu ya WordPress, na kutafsiriwa na mafundi wa hapa mzalendo.net.Tunajivunia kuwa mzalendo.net ndio blogi ya mwanzo kuchapisha habari kwa kutumia programu hii kwa lugha ya kiswahili.Kuachana na lugha ya kiswahili inayotumika hapa mzalendo.net, blogi hii haina tofauti yeyote kiufundi na blogi nyengine yeyote ya WordPress.Tunatarajia baada ya kumaliza kusoma nakala hii utaweza kujiandikisha na kuanza kuchapisha habari.

  • I.Unahitaji nini ili uweze kuchapisha?

Jambo la mwanzo ambalo mtumiaji aweze kuwa mwandishi wa blogi hii ni lazima ajiandikishe, kutembelea na kutoa maoni si lazima kujiandikisha.Maelekezo yanayofuata chini kwenye II yataeleza jinsi ya kujiandikisha na mzalendo.net.

  • II.Jinsi ya kujiandikisha

Fungua Internet Brauza yako kama Firefox, Opera au Internet Explorer, na andika anwani hii:http://www.mzalendo.net/

halafu angalia upande wako wa kushoto na tafuta sehemu ifuatayo(kushoto chini karibu na mwisho) kama inavyoonekana kwenye picha hapa chini:

Jinsi ya kuingia

Jinsi ya kuingia-mchoro 1

Bonyeza “Jiandikishe” kuweza kufungua akaunti ya uchapishaji, na fomu ifuatayo itapatikana:

drawing2

mchoro 2

Chagua jina unalopenda kutumia, na anwani yako ya email(barua-e), andika herufi zilizopo kwenye rangi nyeusi halafu kubali mkataba na bonyeza “Jiandikishe”.

Angalia barua zako kupata uhakika wa usajili huo, neno la siri pamoja na jina utatumiwa kwenye barua zako.Ukishapokea jina na neno la siri kwa barua endelea na sehemu ya III (kuingia kwa mara ya mwanzo).

  • III Uingiaji ndani ya akaunti ya akaunti kwa mara ya mwanzo

Mara baada ya kupata jina na neno hilo, rudia kwenye “mchoro 1″ hapo juu.Lakini mara hii jaza jina na neno la siri kama ulivyotumiwa kwenye barua na ubonyeze “Ingia”.

Nukuu:
Kwa english tunasema neno la siri pamoja na jina ni “case-sensitive”, maana yake “a” sio sawa na “A”.
Kwa hiyo ingiza neno la siri kama lilivyotumwa na sio vyenginevyo.

drawing4

Ukiingia ndani ya mzalendo.net kwa mara ya mwanzo-mchoro 4

Ukimaliza uingiaji ndani ya mzalendo.net kwa mara ya mwanzo utapata picha iliopo hapo juu.Soma ujumbe wa rangi nyekundu, unashauriwa kubadilisha neno la siri rahisi ambalo utaweza kulikumbuka.

  • IV.Kubadilisha neno la siri:

Bonyeza “Ndio, Nipeleke kwenye profaili yangu” na fomu kama ya hapo chini itapatikana na hapo utaandika neno jipya la siri.

drawing5

Ubadilishaji neno la siri-mchoro 5

Maelezo yafuatayo, yatafahamisha jinsi ya kuchapisha maandiko ndani blogi hii ya mzalendo.net.


  • V.Jinsi ya Kuchapisha Habari

Tizama upande wa kushoto, na tafuta sehemu iliandikiwa “Machapisho” (mchoro 6), bonyeza na utaona menu ya kuandika chapisho jipya”Ongeza Mpya”.

drawing6

mchoro 6

Bonyeza “Ongeza Mpya”, utapata sehemu ya kufanya uandishi.

video2

Sehemu ya uandikaji habari-Mchoro 7

Mwanzo ni kichwa cha chapisho hilo, na sehemu ya pili ni umbilo la chapisho.Ukiangalia kwa kulia kwako utaona “Kwa uangalizi” na “HTML”.Kwa uangalizi ni modi ya uandishi kwa jinsi chapisho litakavyojitokeza baada ya kuchapishwa, na kwa “HTML” ni kwa utumiaji wa kodi za “html”.Kama hujuwi “html”, tumia “kwa-uangalizi”.

  • VI.Kuingiza Picha,Video/Muziki:

Jinsi ya kuingiza picha, video, muziki, vyote vina tumia Pakia/Ingiza.

  • VII.Migawanyo/Tagi za machapisho:

Kama utakumbuka kuna habari, na ndani ya habari kuna habari za kitaifa n.k, unaweza kuchagua gawanyo la chapisho kama inavyoonekana upande wa kulia.

drawing8

mchoro 8

Picha nzima wakati naandika chapisho hili unalosoma:

tutorial

mchoro 9

  • VIII.Kupata msaada:

Kupata msaada zaidi wakati unafanya uandishi nenda kulia juu kabisa wakati uko ndani ya akaunti yako, halafu bonyeza “msaada”

drawing9

Kidirisha cha maelekezo kitafunguka na bonyeza “Posti” au sehemu unayohitaji kusoma kwa maelekezo zaidi.
Tunaomba samahani maelekezo hayo ni utumiaji wa WordPress si nyaraka za mzalendo.net kwa hiyo lugha haitokuwa kiswahili bali ni kiingereza.

drawing10

mchoro 11

Nukuu:

Usishangae baada ya kubonyeza chapisha, toleo lako halitokeo mbele ya mzalendo.net.Hii inatokana na kitu kinaitwa “Cache”, lengo lake ni kuongeza speed ya websaiti yetu, ambayo inahifadhi nakala zote za mzalendo na kuzirusha kwa speed zaidi.Itajitokeza mbele ya mzalendo.net kwa muda uliopangwa na utaratibu huo wa “cache”, kama unaweza kuliona chapisho lako kwenye orodha ya machapisho (linakiwa liwe chini ya “ujumbe muhimu”), hapo kama lipo ndio tayari limeshachapishwa.Hakuna mtu wa kupitia chapisho lako kabla halijakubaliwa!

Maombi

Kama mkataba wetu unavyosema, tafadhali usitukane na kutumia lugha za matusi.Ngono na ufuska haviruhusiwi kabisa katika blogi hii, watumiaji watakogundulika kuenda kinyume na makubaliano ya mzalendo.net watafungiwa mara moja.Unaombwa kuripoti mtumiaji anaevunja maadili ya jamii yetu.

Mnaombwa kujiskia huru hapa, sisi sio gazeti wala kampuni, tunajivunia kuwa ni sehemu ambayo watu wote wanaweza kutoa maoni na mawazo yao na dunia nzima kuona nini kinaendelea na wazanzibari wanasemaje kuhusiana na masuala ya mustakbali wa nchi yao.

Asanteni.

MISAADA ZAIDI:

IRC CHANNEL:freenode channel #mzalendo

Vyanzo:
http://codex.wordpress.org/Writing_Posts

Leave a Comment

You must be logged in to post a comment.