RECRUITMENT

AS,

MZALENDO RECRUITMENT

Tunapenda kuwatangazieni kuwa tumeona ipo haja ya kufanya recruitment au kusaidiana katika nyanja ya kuwaendeleza vijana wenzetu wa kizanzibari katika sekta ya elimu hususan elimu ya juu.Kwa lengo la kutengeneza damu mpya ambayo inaweza kutusaidia katika maeneo mbali mbali ya habari.

Kama tunavyojua kama tulikuwa tokea mwanzoni tuna lengo la kusaidia jamii ya kizanzibari.Kwa hiyo kuna mwenzetu amekuja na wazo la kusomesha kijana mmoja wa kizanzibari mwenye shahada ya mwanzo yaani Degree katika masomo ya art.

Mawazo yaliyopo ni 2 kumsomesha au kumsaidia ajiendeleze na elimu hiyo:

  • Kwa harambee (yaani michango ya wazalendo wengine) hapo UDSM.
  • Au kwa njia ya kumtafutia scholarship nje ya nchi.

Hivyo kama yupo kijana hapa MZALENDO aliesomea masomo ya art kama sheria au mengineo na anataka kujiendeleza shahada ya 2 Msc katika Media tunaomba atuandikie barua-e admin@mzalendo.net au ahmedhemed@hotmail.com

Masharti:
Kijana awe mzanzibari mwenye degree ya mwanzo kwenye masomo ya art na ana interests za kusomea media kwenye shahada ya pili.
Tunapendekeza asizidi umri wa miaka 35 (sharti dogo tunaweza kubadili mawazo kwenye umri)
Awe ni mzalendo na mwenye nia ya kujitolea kwa jamii pale anapohitajika na anapokuwa na uwezo.

GR
UONGOZI WA MZALENDO.NET

One Comment on "RECRUITMENT"

  1. ari mpya 23/01/2010 kwa 5:12 um ·

    Mambo mazuri hayo!!! kazi kwenu vijana wa kinyumbani kuchangamka.

    Wasi wasi wangu nikuwa mzalendo.net inabidi iwe makini na hili ili tusije tkaharamikia mtu kama Seif Khatibu ambaye baadaye akajakuwa ndio anayetaka kuwatia vitanzi wazanzibari.

    Uangalifu na mipango mikubwa ni lazima ipangwe ili kuhakikisha kwamba atakaye saidiwa atakuwa ni mzalendo wa kizanzibari na anastahili kusaidiwa na sio mtoto wa tajiri ambaye mzee wake anauwezo wa kumpeleka hata marekani kusoma anchotaka halafu akaja kuiangukia nafasi hii.

    Nimategemeo angu kwamba hadi tangazo hili limetolewa basi nilazima mipango na mchakato wa kumpata huyo kijana itakuwa imeshaandaliwa vile vile.

    Ikibidi kuwashirikisha watu wenye ujuzi juu ya hili basi ni bora hilo lifanywe!!

    Ahsanteni

Leave a Comment

You must be logged in to post a comment.