Karibu katika mtandao wa MZALENDO.NET!
MZALENDO.NET ni blogi ya kisasa ambayo inakuletea habari mbali mbali za dunia.Blogi hii ina malengo mengi ikiwemo ile ya kutoa nafasi kwa wazanzibari, ambao wanaonekana kuachwa nyuma kidogo na masuala mazima ya mtandao.Zanzibar ni sehemu yenye matukio mengi, lakini la kushangaza kuwa habari na matukio yanayotokea katika visiwa hivyo ni chache sana kwenye mtandao.
Mtandao wa MZALENDO.NET unaendeshwa kizalendo na watumiaji wake, hata wewe unaweza kuchangia kama mdau wa Zanzibar kwa njia yoyote unayoweza, kama utoaji wa habari kwa picha,vidio hata mp3 za matukio mengi ambayo unahisi wengine watafaidika.Watu wote wamepewa haki ya uandishi bila ya ubaguzi, tafadhali unaombwa ujiandikishe kuweza kupata haki hizo za kuchapisha katika mtandao huu.
MZALENDO.NET ina malengo mengi katika jamii ya kizanzibari, kati ya malengo hayo ni:
- Moja likiwemo la kutengeneza MZALENDO FUNDS/FOUNDATION kwa malengo ya kusaidia jamii kwa njia kama za michango kwenye masuala ya elimu, afya, utafutaji wa walimu kutoka Europe n.k
- Kusaidia Zanzibar kihabari, kuhamasisha jamii na kutoa muamko kwa wananchi wa Zanzibar ili wapiganie wawe na dola kamili ya watu wa Zanzibar na kuachana na upuuzi wa muungano.Kwa ufupi, MZALENDO.NET haina imani au haipendelei kuona nchi ya Tanzania inapigania kurudi kwa Zanzibar na Tanganyika kama ilivyokuwa hapo awali.
- MZALENDO.NET ni moja kati ya mifano ya utumiaji wa lugha ya kiswahili kwenye mambo ya kiteknolojia.Kama mujuavyo, MZALENDO.NET ni mtandao wa mwanzo kutafsiri na kutumia programu ya WordPress kwa lugha ya kiswahili.
Tunatarajia utafurahia blogi yetu.
Kwa maswali zaidi wasiliana au tuma ujumbe/maoni katika mtandao huu au kwa barua-e admin@mzalendo.net
Timu yako,
MZALENDO.NET

Habari maarufu