Login



Fotos

Get the Flash Player to see the slideshow.

FAQ

Maswali yaulizwayo sana na watumiaji wa MZALENDO.NET

Haya ni masuali ambayo baadhi ya watumiaji wa MZALENDO.NET wakijiuliza au maswali ambayo yaulizwayo sana:

  1. “Mtu yeyote anaweza kuchapisha habari MZALENDO.NET?”:Ni kweli kila mtumiaji halali aliejisajili amepewa ruhusa ya kuchapisha habari anayoitaka kwenye mtandao huu.Hii ni kwasababu ya lengo moja la mtandao huu ni kutengeneza sehemu kwenye Internet kwa wazanzibari na waswahili kubadilishana habari wakiwa kwenye Internet.Kwa ufupi mtandao huu ambao unaitwa “BLOGI” kwa lugha ya kirahisi umetengenezwa kwa ajili yenu, kwa hiyo kila mtu ana haki ya kuchapisha atakacho, alimuradi asivunje maadili ya mila na utamaduni kwa mfano kutukana jamii n.k.
  2. Wapi nitapata maelezo ya kunifundisha jinsi ya kutumia mtandao wa MZALENDO.NET?:Kuna viungo viwili vitatu ambavyo vina maelezo yanayofahamisha kwa kutumia picha jinsi gani unaweza kuchapisha, na vitu kama kutuma video.Viungo hivyo ni :
    1. Maelezo ya jumla jinsi ya kutumia mtandao wa MZALENDO.NET bonyeza hapa
    2. Maelezo ya yanayofahamisha jinsi ya kutuma video bonyeza hapa
    3. Maoni ya watumiaji
    4. Mgawanyo wa ujumbe maalum, kama matangazo kwa watumiaji nk yanapatikana hapa
  3. “Machapisho ya zamani yako wapi?”:Upande wa kushoto wa blogi ya MZALENDO.NET utaona
    1. Migawanyo:Manaake jinsi machapisho yote yalivyotenganishwa wakati yakichapiswa ndani ya MZALENDO.NET, mfano machapisho yanayohusiana na michezo bonyeza gawanyo la michezo
    2. Kalenda:Hii ni machapisho yamegawiwa kwa tarehe, manaake kama unataka kusoma machapisho ya tarehe fulani unabonyeza tarehe hiyo, na MZALENDO.NET itakuonesha machapisho yaliyotolewa kwa tarehe hiyo tuu.
    3. Kumbukumbu:Hii ni maktaba ya MZALENDO.NET, ambayo inaweza kukuonesha machapisho kwa kuyagawa kwa miezi.
  4. Tagi ndio nini?:Tagi mitenganisho kwa kutumia “tagi”, hili ni neno jipya kwenye kiswahili lenye maana ya maada.Kwa mfano mjadala wa “mafuta”, kusoma machapisho yote yanayohusiana na mafuta, nenda mwisho kushoto na utaona vijeneno/tagi kutakuwa na tagi yenye neno “mafuta”.Hii maana yake, ukibonyeza “mafuta” manaake unataka kusoma machapisho ya MZALENDO.NET yenye maada ya mafuta pekee.
  5. Jinsi gani nitaingia ndani ya MZALENDO.NET?:Tizama juu kushoto ya mtandao wa MZALENDO.NET utaona sehemu ya kuingiza jina na neo la siri.Kama hujajiandikisha bonyeza jiandikishe na fuata maelekezo kwenye komputa yako.
  6. Mitambo ya MZALENDO.NET iko wapi?:Mitambo yetu iko kwenye bara la ulaya katika nchi ya Uholanzi.
  7. MZALENDO.NET ni mtandao wa CUF?:Hakuna uhusiano baina ya chama cha CUF au chama cha kisiasa chochote na mtandao wa MZALENDO.NET.Suala la kuzungumzia au kuchapisha maada za kisiasa ni suala la maamuzi ya mtumiaji, na tumetoa uhuru kwa mtu kuchapisha chochote anachokipenda bila kujali mrengo wa kisiasa.
  8. Nini lengo la MZALENDO.NET?:Tuna malengo mengi kwa kweli:
    1. Moja likiwemo la kutengeneza MZALENDO FUNDS/FOUNDATION kwa malengo ya kusaidia jamii kwa njia kama za michango kwenye masuala ya elimu, afya, utafutaji wa walimu kutoka Europe.
    2. Kusaidia Zanzibar kihabari, kuhamasisha jamii na kutoa muamko kwa wananchi wa Zanzibar ili wapiganie wawe na dola kamili ya watu wa Zanzibar na kuachana na upuuzi wa muungano.Kwa ufupi, MZALENDO.NET haina imani au haipendelei kuona nchi ya Tanzania inapigania kurudi kwa Zanzibar na Tanganyika kama ilivyokuwa hapo awali.
    3. MZALENDO.NET ni moja kati ya mifano ya utumiaji wa lugha ya kiswahili kwenye mambo ya kiteknolojia.Kama mujuavyo, MZALENDO.NET ni mtandao wa mwanzo kutafsiri na kutumia programu ya WordPress kwa lugha ya kiswahili.
  9. Nani wanalipa gharama za kuendesha mtandao wa MZALENDO.NET?:Kwa sasa gharama zetu ziko chini kabisa, tunaendesha mtandao huu kizalendo kwa gharama za 15$ kwa mwaka tukitoa mbali gharama za umeme.
  10. Ni nani mafundi wa MZALENDO.NET?:Kwa sasa kamati ya ufundi ina fundi mmoja ambae ni “mrfroasty”.
  11. Mbona kuna makosa mengi ya lugha katika mtandao huu wa MZALENDO.NET?:Hii ni kwasababu mtandao huu unatumia programu ya WordPress, ambayo imetafsiriwa na mafundi wa MZALENDO.NET ambao si wataalamu wa lugha ya kiswahili.Kwa hiyo tunakubali kama kunaweza kuwa na matatizo au makosa ya lugha katika mtandao huu, mafundi wa MZALENDO.NET watapenda kupokea maoni au marekebisho kutoka kwako mtumiaji.
  12. Kuna uhusiano gani wa gazeti la mzalendo na MZALENDO.NET?:Hakuna uhusiano wowote, mzalendo ni gazeti na MZALENDO.NET ni blogi au mtandao wa Internet.
  13. Zaidi nilitaka kujuwa hii blogi imeanzishwa lini?:Blogi hii ilianzishwa kimawazo tuu bila ya utekelezaji, nilipokuwa nyumbani Zanzibar mnamo mwishoni mwa 2008 hadi April 2009.Kuanzia Mei 2009 hadi June ilikuwa inatumia kiungo cha temporary au cha majaribio blog.mambo-tech.net.Hapo mambo yaliyokuwa yakifanyiwa kazi ni tafsiri ya Software/Programu iliyotumika kuendeshea mtandao huu.Mnamo kati kati ya June 2009, ndio tukaanza rasmi kuingia hewani kwa kiungo cha MZALENDO.NET.Kipindi chote hiki tulikuwa tunasambaza habari kwa kutumia computer yangu binafsi niliyonayo nyumbani kwangu, ambayo Internet Connection yake ni home-use haifai kwa kurushia website.Tulifanya hivyo kwa kuepuka gharama za endeshaji ambazo nazilipa mwenyewe.
    Mwishoni mwaka 2009 ndio tukapata mfadhili JamboIT, ambae ametupa sharti la kuweka tangazo lake na yeye atatupa account ya kurushia habari.Hapo haswa ndio mtandao huu ulipoanza kuja juu na idadi ya watu kuongezeka.
  14. Kwa utaalam wako ni watu wa aina gani wanaotembelea mtandao huu?:Hilo suala ni gumu, labda nilijibu kwa mujibu wa takwimu zetu.Wengi kutoka UK, NL, US, Tanzania (Mwanza, Arusha,Dar  na Unguja waliobaki kutoka TZ hawajulikani) na nchi zenginezo duniani zikiorodheshwa zinazidi 100.
  15. Kwa nini hawa wanachama hawataki kuchukua hizi nafasi, kukusaidia?:Aidha kwanini wanachama hawataki kusaidia, hii sio ukweli 100% manaake misaada iko ya aina nyingi.Wapo kama Mzenji na wengineo huchangia kuchapisha habari nao pia ni msaada ambao tunauthamini.
    Kwa kweli msaada pengine uliokusudia ni wa Administration (non-technical).Huu msaada siwezi kulaumu kuwa sijaupata kutoka kwa wanachama, unahitaji mtu wa kujitolea na asieogopa kujifunza vitu vipya.Inahusisha kidogo Computer literacy, ambayo kwa nyumbani ni general case kuwa ni ndogo.Kwa hiyo logic kabisa kukosa watu wa kusaidia kwenye nyanja hiyo.
    Hilo suala la Administration ninalolizungumza hapa ni technical na non-technical.Technical tunazumzia masuala ya IT na non-technical ni masuala ya CMS (Content Managment System i.e WordPress in this case).Sasa hapo ni logic kukosa au kuchukua muda mrefu kupata timu ya watu wenye sifa hizo.
  16. Hadi hivi sasa ni mipango gani muliyotayarisha hata yule mtu wa kijijini anapata habari hizi?:Hakuna jitihada yoyote iliyofanywa, kwa vile MZALENDO.NET sio gazeti, ni ngumu kuwafikishia ujumbe walio vijijini.Lakini kama kuna mfadhili atakae toa fursa ya kuweka Computer na elimu ya Internet kwenye kijiji, basi wataweza kufaidika.
  17. Kwenye kamati ya uongozi ni position gani ziko wazi? Au hiyo structure yenu iko vipi?:Hakuna kamati yoyote kwa sasa, waanzilishi ilikuwa ni mimi na mwenzangu ambae anasomesha huko SuSa.Yuko resi sijuwi hata kama ana muda wa kusoma habari za MZALENDO.NET unaweza kusema kabakia kama ni mshauri tuu.Kamati nzima ni mimi pekee kwa sasa, kwa hiyo Technical Assistance, Moderations, publishing kila kitu vimenielemea mimi.Ndio maana huwa nahimiza wanachama washiriki.Kwa vile lengo la mtandao sio kuwa blogi ya mtu fulani ni community website.
  18. Hivi mumepanga nini kwa short term na long term goals?:Short term ni kuwa just blog kama ilivyo sasa.Long term tunamalengo ya kuongeza kujitegemea kihabari na kuwa 1st stop point for Zanzibar Online news Platform.Malengo mengine ambayo yapo kichwani mwangu na nimeyaweka kwenye mtandao huu ni kuanzisha MZALENDO FOUNDATION ambayo itasaidia mambo madogo madogo kama kurahisisha walimu au wanafunzi wanaotaka kufanya Internships au kujitolea kusomesha Zanzibar na kusaidia mambo madogo madogo kwenye sekta kama za elimu, afya n.k.
  19. Ni msaada gani muhimu zaidi kwa hivi sasa unaohitajika?:Hili suala linategemea na uwezo wako na wewe unapendelea kusaidia nini.Kama ni hardcore Software Engineer specializing in Webdevelopment, unaweza kusaidia kutengeneza Plugins kadiri zitakavyohitajika na kufanya Software maintance.Kumbuka Software hii tunayotumia ni localized, ambayo tunaimaintain wenyewe ambapo kazi hiyo inafanywa na mimi kwa sasa jina natokeza kwenye Internet kama mrfroasty.Kama ni muandishi unaweza kusaidia kihabari.Kama si muandishi wala fundi wa software, lakini unataka kujifunza na kusaidia wenzako basi unaweza kusaidia kwenye Administrations za CMS.
  20. Jee kuna njia ya kuweza kuzi-download hizi video na mtu akaweza kuzi-record kwenye DVD?:Kuna aina za video 2 ambazo MZALENDO.NET inaonesha.Aina hizo ni :
    1.Video za MZALENDO.NET au ambazo mafaili ni yetu na tumeyahifadhi kwenye account yetu hapa.
    2.Video za kigeni au foreign video, hizi ni video kwa mfano zilizoko kwenye Youtube, Motionbox n.k

    Uwezekano wa kudownload:

    1.Video za MZALENDO.NET
    Inawezekana kudownload mafaili hayo kwa kubonyeza kiungo hiki , itafunguka orodha ya video zote za MZALENDO.NET.Ukibonyeza video uipendayo (single), utaona kiungo cha kudownload file la video hiyo chini kabisa ya video hiyo.

    2.Video za kigeni au foreign videos
    Hizi kwa kweli hatuna uwezo wa kuwasaidia watumiaji Download links kwa ajili ya kutizama offline.Video kama za Youtube sijuwi kwa kweli utaweza vipi kuzidownload, itakuwa inawezekana lakini hatuna mechanism ya kuwasaidia watumiaji wetu.Hapa tukumbuke sasa tunajadili video ambazo ziko nje ya uwezo wetu. Kwa mfano video za Motionbox mtumiaji au mmiliki wa video anafanya kwa makusudi katika account yake kutokuruhusu watu waidownload video hiyo.

    Hivyo tunaomba samahani video ambazo hazijamilikiwa na MZALENDO.NET, hatuwezi saidia watu wadownload.Kama kwenye chapisho kuna tangazo la mhusika, tafadhali wasiliana na mhusika huyo kupata DVD au original file.

  21. Vipi nitaijua video hii ni ya MZALENDO.NET au ni ya mmiliki mwengine?:Video za MZALENDO.NET zote zimehifadhiwa kwenye kiungo hiki au unapoitazama video mwanzoni utaona MZALENDO.NET  – Kichwa cha habari cha video (chini upande wa kushoto wa video player).
  22. Naweza kupata DVD ya video ninazotizama MZALENDO.NET?:Baadhi ya video zinakuwa na matangazo wapi zinapatikana au mmhusika wa video hiyo anapatikana.Kwa mfano RASHID VIDEO anapatikana Zanzibar na nyengine kunakuwa na matangazo na anwani za mhusika wa video.
  23. Vipi nitaweza kudownload video za Youtube?:Jaribu process kama hii http://keepvid.com chapa kiungo cha video unayopenda kudownload halafu bofya Download na uchague format unayopenda.

P:S

**Kama unahisi una suali halijajibiwa hapo juu toa maoni yako kwa kututumia barua-e admin@mzalendo.net

GR

mrfroasty

Share and Enjoy:
  • Facebook
  • Twitter
  • Digg
  • MySpace
  • del.icio.us

Maoni yamefungwa.