Login



Fotos

Get the Flash Player to see the slideshow.

Tafsiri

Utangulizi
Internationalization na localization ndio maneno ambayo yanatumika kueleza jitihada za kutengeneza WordPress ipatikane kwenye lugha zengine mbali na kiengereza.

Operesheni ya kutafsiri ina hatua mbili.Hatua ya mwanzo ni watengeneza programu kuweka njia na mbinu za tafsiri hiyo kufanyika ili tafsiri iyo ya watu mbali mbali duniani iweze kutumika.Watengenezaji wa WordPress wameshafanya hatua hii,ki ilivyo WordPress inaweza kutumika kwa lugha yoyote ile.

Hatua ya pili ni tafsiri yenyewe, hii ni ile tafsiri ya maandishi kuandikwa kwenye lugha nyengine pamoja na utamaduni mwengine kwa kutumia nyenzo zilizopo.WordPress imeshatafsiriwa kwenda kwenye lugha nyingi (angalia WordPress kwenye lugha yako kwa maelekezo zaidi).Kwa ufupi nakala hii inaelezea jinsi gani ya kutafsiri WordPress

Kutafsiri WordPress

Kabla hujaanza kutafsiri WordPress kwenda kwenye lugha yako, angalia WordPress ya lugha yako kama ipo.Inawezekana ikawa tafsiri iyo ipo au kuna kikundi cha watu tayari wako kwenye harakati za kutengeneza tafsiri hiyo.Kujua jiunge jitambulishe na uliza hapo kama kuna mtu yeyote ambae anafanya kazi hiyo.Kuna listi ya [http://codex.wordpress.org/L10n:Localization_Teams timu za kutafsiri na timu zinazojitengeneza , ambazo unaweza kuangalia kama kuna tafsiri inayotengenezwa.

Sifa
Jaalia kuwa tafsiri ya WordPress kwenye lugha yako haipo bado au kuna mtu anaifanyia kazi, na unataka kujitolea kusaidia kutafsiri kwenye lugha yako.Unahitajika kuwa na sifa zifuatazo ili ufanikiwe kufanya tafsiri iyo:

* Unahitajika kuwa unazungumza lugha zote mbili kifasaha kabisa Kiengereza na lugha yako ambayo unataka kutafsiri.
* Unahitajika kuwa na upeo wa PHP, kwasabab kuna baadhi ya sehemu utahitajika kusoma kodi za watu za PHP ili uweze kujua jinsi ya kutafsiri.
* Utahitajika pia kuwa mjuzi wa vitu kama vitendo, viunganishi n.k ili uweze kueleza vyema.

Kuhusu Locale:
Locale ni mchanganyika wa lugha na diyalekti.Mara nyingi Lokale ni ufupisho wa wa nchi kwa mfano Tanzania (Swahili).Locale ya msingi ya WordPress ni Kiengereza.

Teknolojia ya kutafsiri:

Watengenezaji WordPress wamechagua [http://www.gnu.org/software/gettext/gettext.html GNU gettext] kama ndio nyenzo ya tafsiri iyo.Teknlojia hii ya gettext inatumika sana kwenye tafsiri ya programu, kiilivyo ndio teknojia baba ya tafsiri ya programu huria.

Gettext inatumia tafsiri ya kila neno baada ya neno ambalo linaonekana na mtumiaji, kama ni paragrafu au neno moja.Kwenye WordPress kama hayo yanatengenezwa, na kutafsiriwa na kutumiwa na mafaili ya PHP ya WordPress kwa kutumia function ya __() au _e().

__($neno)

Tafuta moduli ya neno kwa tafsiri, na peleka tafsiri hiyo kwa PHP, kama $neno halionekani basi rudisha $neno

_e($neno)

Tafuta neno katika moduli kwa tafsiri, na peleka kwenye PHP echo.Kama tafsiri haionekani basi rudisha $neno.

Nukuu
Kama unatfsiri Dhimu au Plugini, ni bora kutumia ext Domain.Angalia Uandishi wa Plugin kwa maelekezo zaidi jinsi ya kufanya hivyo, dhimu zinafata mkondo mmoja.

Unaweza kusema kuwa gettext inafanya mambo yote ya WordPress, japokuwa kuna baadhi ya sehemu za programu ya WordPress ambazo gettext haiweza kutumika angalia Mafaili ya Kutafsiriwa Moja kwa Moja kwa maelekezo zaidi.

Mafaili ya POT(Portable Object Template)
Hatua ya mwanzo ya kutafsiri au kulokalaizi programu ni kutafuta kodi za WordPress na kutafuta function za __() na _e().Function hizi zitalist ujumbe wote na kuweka kwenye templeti faili la POT ambalo linatengeneza msingi wa tafsiri.Kwa ufupi, unaweza kudownlod POT la WordPress, huhitajiki kutengeneza mwenyewe.Mafaili mbali mbali ya POT yanaweza kutengenezwa kwa ajili ya plugini, dhimu kama watengeneza vijiprogramu hivo watakuwa wametumia __() au _e() kila kwenye maandishi ndani ya programu hizo

Mafaili ya PO(Portable Object)

Hatua ya pili katika operesheni hii ni mtu anaetafsiri kutafsiri tungo au sentensi zote kutoka kwenye faili la POT kwenye lugha inayolengwa, na kuhifadhi yote Kiengereza na lugha inayolengwa kwenye faili la PO.

Mafaili ya MO(Machine Object)

Hatua ya mwisho ni kutengeza faili la MO kutoka kwenye faili la PO.Hii inaweza kuwa tofauti kutemea unatumia programu gani.

Programu za Kutafsiri:
Kama kawaida ya ulimwengu wa komputa kuna programu nyingi ambazo zinaweza kufanya kazi hii, hizi ni baadhi ya programu ambazo zinaweza kutumika:

Launchpad

Project ya Ubuntu Linux ina websaiti ambayo inaruhusu kutafsiri ujumbe bila ya kuangalia faili la PO au POT, na ulisafirisha moja kwa kuwa MO.

Nukuu:
Watafsiri wengi wanaona Rossetta kuwa ni kianzio kizuri, lakini mara wanajiona kuzongwa na mlomlongo wa sentensi za tafsiri, wengi wanaamua kubadili na kuanza kuhriri mafaili ya PO kwa kutumia programu kama poEdit au Kbable(Lokalize).Hii inatokana na kuwa Rosseta inakosa utafutaji wa maneno na mambo mengine muhimu kwenye ufanisi wa tafsiri.

Pootle
Ni programu huria inayotumia mtandao kufanya tafsiri.Sava ilioko Locamotion.org sasa imewasha tafsiri za WordPress.

PoEdit

Programu huria inayopatikana kwenye Window, Mac na Unix/Linux ambayo ni rahisi kuhariri mafaili ya PO na kutengeneza mafaili ya MO.

Kbabel
Hii ni programu nyengine huria kwa kuhariri mafaili ya PO ambayo inapatikana kwenye Linux kwenye KDE.

Nukuu:
Kuanzia toleo jipya la kde-4 programu hii imeboreshwa na kuitwa Lokalize, ambayo imekuwa nzuri zaidi kushinda hiyo Kbabel.

GNU Gettext

Gettext yenyewe pia inatoa zana nyingi za kutumia komando kutengeneza POT, kurekebisha PO, na kutengeneza MO.Hii ni kwa wale wanaopenda kutumia komand.

Kutafsiri kwa kutumia Launchpad

Kuna nakala hii hapa kwa maelekezo zaidi

Tafsiri kwa kutumia Pootle (Locamotion.org)

  • Jisajili na ufungue akaunti kwenye sava hiyo, na mtumie barua-e kiongozi mmoja kuongeza lugha yako.
  • Kabla hujaanza kufanya tafsiri kitu chochote, kwanza ingia.Maandisho yanaweza kuangaliwa na mapendekezo yanaweza kuingizwa na watembeleaji bila ya kuingia, kutafsiri ni lazima uingie.
  • Tembelea nakala ya lugha yako, kwa mfano Kiswahili
  • Share and Enjoy:
    • Facebook
    • Twitter
    • Digg
    • MySpace
    • del.icio.us

    Maoni yamefungwa.