Makala/Tahariri

Pana Mwenye Sifa?!

Tuwajadili wagombea waliojitokeza kwa upande wa watawala na kutazama kama wanaweza kuwa mwanga mzuri wa uongozi ujao katika Tanzania.

Mheshimiwa Samuel Sita.

Miaka 10 ya utawala unaomalizika umetusomesha kwamba hatuhitaji uongozi unaosema hivi ukafanya vyengine. Na kwa Mheshimiwa Sita kama mwenyewe alivyojiita Mzee Chura, na hasa uongozi wake katika bunge la katiba tunamuona ni kiongozi asiekuwa na vigezo vinavyohitajika katika uongozi wa juu wa nchi. Si mjasiri wa kusimamia ukweli, ni jeuri wa demokrasia na msanii wa kusema hili huku akificha yalio moyoni mwake. Anaviasili vya udikteta, asie na hekima na anaweza kuzidi kuligawa taifa kwa uongozi wa hadaa na ujanja ujanja. Akiwa waziri katika Afrika Mashariki, ameshindwa kuwa mwanadiplomasia mzuri wa kuvunja migongano ya wazi baina ya Tanzania na nchi wanachama wa EAC na hata ushauri kwa Bosi wake haukuwa wa kuzaa matunda ya umoja wa kiafrika. Legacy yake ilikuwa katika nafasi ya spika wa bunge la jamhuri lililopita lakini alikosa uadilifu, umakini, heshima na ustaarabu katika bunge la katiba lililopita kwa kuweka maslahi ya ugombeaji wake wa Urais kwanza kuliko utu. Hatuhitaji Rais wa namna yake hasa baada ya taifa kuingia katika mpasuko mkubwa ambao na yeye ni mshirki namba moja wa misuguano iliopo.

Mheshimiwa Wasira.

Taifa linahitaji rais alie na haiba, mwenye upendo, hekima, busara na uongozi imara wa demokrasia kwanza. Mheshimiwa Wasira amekosa yote na kinachoogopesha katika utawala wake ni kuwa tayari kwa matumizi ya ubabe, nguvu na kutothamini heshima ya maoni tafauti na ya kwake. Ataliongoza taifa kwa nguvu ya chuma, na kuitumia ofisi yake kama ni sehemu ya kuzima upinzani kwa nguvu zote. Tukumbuke kauli yake kwamba wapinzani hawataalikwa tena ikulumkwenda kumuona Rais, hapa ni waziri tu seuze rais itakuwaje? Tumemsikia juzi akisema wasiokubali rasimu ya vijisenti wahame chama akionyesha kukosa ustaarabu wa kuhimili maoni tafauti ya wengine na hata malumbano anayoyaongoza kwa safu ya Mzee Warioba na Butiku inaonyesha namna ya uongozi wake utaojaa malumbano na ujuwaji usiohitajika kwa sasa. Tunahitaji rais ajae akiwa ni rais wa wote, atakaeweza kuliunganisha taifa na kuwa msikivu wa demokrasia na muumin wa mabadiliko. Mzee Wasira si turufu ya ujenzi wa taifa lenye diranya mabadiliko, maendeleo na serikali ya umoja bali ni dikteta aliejificha ambae “potential” ya nguvu kubwa za nafasi ya urais katika viganja vyake ni mtafaruk mkubwa mbele yetu.

Mheshimiwa Sumaye

Akiwa Waziri Mkuu kwa miaka 10 ya utawala wa Che Mkapa, hastahili nafasi ya urais kwanza kwa kuhusika na uongozi wa juu ulioridhia mauaji ya Mwembe Chai na yale ya 2000 ya visiwani. Mbali ya yote, wakati wake na huu wa sasa hauna tafauti, hakuna legacy ya kweli yenye kutoa vielelezo vya matarajio mapya akiwa rais wa nchi hii. Kama ni rushwa, yeye pia ni mshiriki mkubwa wamrushwa katika chaguzi za ndani na kuu kwa kipindi chake, wala asitufanye tuamini kwamba rushwa ndani ya CCM ni zao jipya ambalo halikuwapo katika utawala wake. Walishindwa kukisafisha chama kwa mikono ya rushwa miaka 10 akiwa waziri mkuu ataweza kuzuiamsasa wakati jini lishapea? Hana usafi, hana legacy, hana utetezi kwa matumizi makubwa ya nguvu kwa wananchi na hana jipya la kumuamini tena kushika uongozi wa nchi.

Mheshimiwa Khamis Kingwala

Kijana, msomi na mwenye kujitambua. Kwa sasa hatuhitaji rais kwa sababu tu ya ujana wake na elimu yake, bali hekima, ukweli na msimamiaji wa haki bila ya kupinda. Urais wa muungano kwa sasa hatuhitaji kiongozi wa majaribio hasa baada ya mpasuko ulioko baina ya pande mbili unaotokana na rasimu ya vijisenti. Tunahitaji experience ya mtu mwenye uwezo wa kuunda serikali ya umoja na kusimamia upya ujenzi wa misingi ya demokrasia madhubuti huku akiitumia hii phase kama ni platform ya mabadiliko yatayomwezesha mwananchi wa kawaida kufaidika na matunda ya nchi yake. Ili kijana akubalike kwa nafasi ya urais lazima awe ni uwezo wa kuongoza wa kuzaliwa na sifa za utendaji na usimamizi wa haki usio na shaka. Kuwa tu rais wa wanafunzi wa vyuo vikuu si kigezo tosha cha urais katika nchi iliopea rushwa na ufisadi, dhulma, ukosefu wa haki na uadilifu. Hatujawahi kumsikia akijiweka kando na uongozi usiojali haki, kama vile wa Deo wa PAC au Bibi Bulaya alietayari kukosoa policies zisizo na haki. Hana legacy nzito ya kujivunia zaidi ya utetezi wa mama ntilie huku akiwa miongoni mwa wale waliofuta uwepo wa maadili ya uongozi katika rasimu. Mchanga mno kwa nafasi ya urais hasa kutokana na mazingira ya sasa yalivyo na umuhimu wa Rais mwenye kukidhi hitaji la conflict resolution, mwenye kuheshimiwa na kuaminiwa.

Mheshimiwa Makamba Jnr.

Mmoja niliefikiri anaweza kuwa kiongozi tunaemhitaji kutokana na alivyojikubalisha na mazingira ya mabadiliko. Kauli ya kutamani udikteta imemtoa kabisa katika kinyang’anyiro cha urais sawa na unapokuwa chuo kikuu ukachezea Disco. Ukweli unabaki nae kwamba ni mchanga kwa nafasi ya urais na hata kile tulichofikiri kuwa nacho kama kipaji cha uongozi wa kuzaliwa kimetuangusha kwa matarajio yasio na vigezo. Hawezi kujiepusha na rushwa kutokana na background yake, hata legacy yake haimpi nguvu za kuwania nafasi kubwa nchini. Ninaposema kipaji cha uongozi wa kuzaliwa namtazama kama Sokoine na kwa vijana hawa wa chama tawala waliojitokeza simuoni yeyote mwenye kipaji na uthabit wa uumin katika demokrasia na utawala wa haki.

Mheshimiwa Lowasa

Kujiuzulu kwake nafasi ya Waziri Mkuu ni kielelezo tosha cha kukosa kigezo cha kushika nafasi kuu nchini. Tuhuma alizonazo kama hajazitolea ufafanuzi mapema, mbali ya kumkosesha vigezo inawezekana kabisa kuishia mahakamani huko mbele kwa matumizi mabaya ya mamlaka yake na fedha za wananchi. Bado siamini kwamba yanayosemwa ni ya kweli lakini bila ya uthibitisho tosha wa yeye mwenyewe kujieleza na kujisafisha atabaki kuwa miongoni kwa mafisadi wakuu wa nchi hii wasiojitambua. Kama alishindwa kuitetea serikali akiwa waziri mkuu hadi akajiuzulu atawezaje kushika usukani wa urais akiwa ni mtuhumiwa namba moja wa ufisadi? Jee kuna rais wa nchi yenye kujivunia demokrasia na uadilifu ambae alishawahi kujiuzulu nafasi yake kabla ya kuwa rais kwa tuhuma za ufisadi halafu akaweza kuomba nafasi kubwa bila ya kusafishwa kwanza?

Mheshimiwa Membe

Ni sehemu ya utawala huu huu wa kisanii na mmoja wa wanaopigiwa kelele visiwani kwa kuwa ni chanzo cha migogoro baina ya pande mbili. Kushika madaraka kwake tusitarajie mabadiliko yoyote zaidi ya kulindana baina ya wahisani na kulipana fadhila. Ni mmoja wa safu hii hii ya utawala uliosheheni rushwa, hivyo sioni mabadiliko yoyote chini ya uongozi wake zaidi ya kurithi yale ya sasa na ya kuendeleza. Tulipofikia hapa tunahitaji kiongozi wenye nia na ari thabit ya kuzuia rushwa, ubaguzi, ukosefu wa haki na uadilifu na kuwa tayari kuunda serikali ya technocrats badala ya makada na wahisani waliochangia kampeni.
Safu hasa itayoweza kuwavuta wananchi ni kukisaidia tena chama tawala kurejesha heshima yake na kufungua kurasa mpya ya mabadiliko ni ya mfano wa Dr Salim Ahmed Salim ambae kwa sasa sijamuona aliebobea vigezo zaidi yake, ukitazama umri wake, hali yake, background yake, uadilifu wake na muumin wa kweli wa muungano wenye haki, usawa na heshima kwa kila mmoja.

Tagsslide
Share: