Makala/Tahariri

Dk. Shein, kosa letu ni kumkatalia Bakari Asseid na wapambe wake

Na O.Juma,

DK. SHEIN, KOSA LETU NI KUMKATALIA BAKARI ASSEID NA WAPAMBE WAKE WA WIZARA YA KILIMO PEMBA KUGAWANA ENEO LETU NUSU KWA NUSU KAMA KIKOMBOLEO CHA KUPATA HAKI YETU.

Mnamo tarehe 9/6/2017 nilibahatika kusoma makala katika Mzalendo .net yenye kichwa cha habari isemayo:-
“SULUHISHO LA MGOGORO WA MSITU WA NGEZI NA MASHAMBA YA WANANCHI”

Baada ya kuipitia mara kadhaa makala hii, nilivutiwa na jinsi ilivyo wasilishwa nikahisi uko umuhimu wa kufatilia jambo hili kwa kina nikiwa kama mwanaharakati niliye jikita zaidi katika kufatilia migogoro ya ardhi hapa nchini kwetu.

Hatua hii ilikuja kunipa hamasa zaidi baada ya kuangalia Baraza la wawakilishi na kuona baadhi ya wajumbe wakiligusia suala hili wakiwemo mwakilishi wa jimbo la Welezo Mhe. Hassan Hamis na mwakilishi wa jimbo la Tunguu Mhe Simai Mohammed Said, Ambapo walidai kuna eneo la msitu wa hifadhi wa Ngezi umepimwa viwanja, na Mhe. Hamad Rashid waziri wa kilimo alizing’oa Beacon zilizo wekwa na watendaji wa wizara ya ardhi bila ya kushauriana na waziri mwenzake, Jambo ambalo ni ukosefu wa maadili ya uongozi na angepaswa kumuomba radhi aliye mteua pia kumuomba radhi waziri mwenzake, zaidi ya yote alipaswa kujiuzulu nafasi yake, kwani kitendo alicho kifanya ni cha kumdhalilisha waziri mwenzake tena hadharani, hivyo basi kimempelekea kukosa sifa za kuwa kiongozi katika jamii iliyo staarabika kama Zanzibar.

Baada ya kufatilia kwa kina nilikutana na wananchi ambao ni wahusika na wao hawakusita walitaka niwafikishie ujumbe wao panapo husika.
Ukweli ni kwamba wananchi hao walinionyesha document mbalimbali zinazo thibitisha kuwa eneo hilo ni mali yao zikiwemo barua za Serikali zinazo elezea kupimiwa na kupewa haki yao, Tatizo walinitajia mtu anae itwa Bakari Asseid.

Wanasema mtu huyu alishawaambia kwamba wakubali eneo hilo ligaiwe nusu kwa nusu yaani nusu liende kwa wananchi na nusu liende mikononi mwake na wapambe wake ikiwa wanataka haki yao, Vyenginevyo yeye hawezi kulizuwia eneo mda wote alio lizuwia halafu asipate faida yoyote.

Ikiwa wananchi hao watakataa atatumia ushawishi alionao Serikalini kuwaaminisha viongozi wakuu wa serikali kuwa eneo hilo ni msitu japo liko nje ya msitu, kigezo kikubwa atakacho kitumia ni kuwemo kwa miti mingi kwa vile eneo hilo wamelizuwia lisitumike kwa shughuli yoyote tena kwa muda mrefu. Aliendelea kwa kusema kigezo hicho tu, kitatosha kuliita eneo hilo kuwa ni msitu hivyo wananchi hao wachaguwe mawili. Aidha wakubali kutoa nusu eneo au wakatae eneo hilo ligeuzwe kuwa msitu wa Vumawimbi, ajabu sio msitu wa Ngezi kwa maana msitu wa Ngezi unajulikana ulipo pita ni takriban kilomita moja na yalipo mashamba hayo na umepimwa umepewa kiwanja namba 14 Makangale, Ramani yake halisi ipo na Beacon zake zipo. Huo ni msitu wa “Vumawimbi” wawakilishi wajuwe hilo, likini ikiwa wananchi wangekubali wagawane eneo hilo nusu kwa nusu na bwana huyo basi msitu huo wa Vumawimbi usinge kuwepo.

Ajabu ilioje, Jee! wanaweza kuugawa Msitu wa Jozani nusu kwa nusu endapo wananchi watakubali nusu ya msitu huo uende kwa Bakari Asseid? Jibu ni hapana. Hilo haliwezekani. Kitendo cha Bakari Asseid kuomba apewe nusu ya eneo analodai kuwa ni msitu wa serikani ni kithibitisho tosha kuwa eneo hilo sio mstitu kama anavyo dai ila kinachofanyika ni kiinimacho na hasadi kwa wamiliki wa eneo hilo. Ikumbukwe mwaka 1998 eneo hili lilikuwa miongoni mwa maeneo yaliyotangazwa kuwa ni maeneo ya utalii Zanzibar kupitia gazeti rasmi la serikali la mwaka 1998 Toleo CVII Namba 5785.

Tunamuomba Hamad Rashid amuulize Bakari Asseid anachukuwa mali ya watu na kuiingiza serikalini
Jee! Amewalipa fidia wananchi kama katiba ya Zanzibar ya 1984 toleo la 1995 kifungu 17/C kuhusiana ulipwaji wa fidia unao lingana na mali ya wananchi inayo chukuliwa na serikali? Au anafanya tu kwa matamanio ya nafsi yake?

Hamad Rashid Muogope Mungu mwisho wetu nikutiwa kwenye mwana wa ndani, usimuendekeze dhalim atakupoteza, huko mbele ya Mungu kila anae kushawishi udhulumu atakukimbia mzigo wanao kubebesha ni mzito.

DK. Shein, Bakari Asseid aliwatisha wananchi kwa kuwaambia kuwa yeye ndiye semaji wa mwisho akiamua eneo liitwe msitu basi Rais hawezi kulikataa hilo, Rais hato msikiliza waziri,katibu wa mkurugenzi yoyote baada ya kutoa maamuzi yake, hivyo endapo wananchi hao watakataa atapigana mpaka tone lake la mwisho la damu lakini atahakikisha wananchi hao hawapati haki yao hata wakapewa barua na kiongozi gani yeye atapinga kwa vitendo. Hivyo aliwaonya wasijaribu kutafuta njia yoyote ya kumfikia Raisi kwa suala hili, wakikataa wataishia kukosa haki zao kwa Rais hamsikilizi mtu yeyote zaidi yake. Bila shaka ndio ndio maana akamshawishi Hamad Rashid akang’oa beacon zilizo wekwa kisheria.

Nilicho gundua kilicho kuwepo sio mgogoro wa wananchi na serikali yao kwani kwa barua nilizi ziona za viongozi
wakuu wa serikali ni wazi serikali hana mgogoro na wananchi wake bali mgogoro uliokuwepo ni Bakari Asseid na wapambe wake kwa maslahi yao binafsi dhidi ya maamuzi ya Serikali(barua za viongozi wakuu), Mahakama na wananchi wanao miliki eneo husika.

Mwisho kabisa wananchi hawa wanasema wako tayari kutoa ushahidi wa haya waliyo yaeleza mbele ya Rais na Bakari Asseid akiwepo ili mkweli ajulikane ikiwa watatakiwa kufanya hivyo.

Sisi kama wanaharakati wa kupigania haki za wananchi, Tunakuomba DK. Shein uyachukulie kwa uzito madai haya ikiwezekana uende ziara eneo husika kwa kulitambua eneo la msitu wa Ngezi lililopimwa kisheria mwaka 1998 kwa mujibu wa ramani ili ikithibitika kuwa maeneo wanayodai wananchi hao hayamo katika msitu wa Ngezi uliopimwa kisheria mwaka 1997 basi wananchi hao wapewe haki yao ili mgogoro huu umalizike kwa amani.
Tunategemea ombi letu utalikubali.

Share:

3 comments

 1. Piga nikupige 17 Juni, 2017 at 20:42

  Poleni wananchi. Bakari Asseid sio mtu wa mchezo mchezo, huyo jamaa anajua kucheza na akili za watu anaweza nyeusi akaiita nyeupe na viongozi wote wakamkubali kua hiyo kweli si nyeusi bali ni nyeupe japokuwa rangi anayo iita nyeupe inaonekana wazi wazi kuwa ni nyeusi.
  Tatizo la viongozi wetu wanaogopana ukienda kwa kiongozi ukamshitakia mabaya unayofanyiwa na kiongozi mwenzake utamsikia akisema aaa mimi najuwa kuwa anavyofanya kiongozi fulani sio jambo zuri , lakini siwezi kumkabili kwa lolote ijapo kuwa kiongozi anaet enda makosa hayo kicheo yuko chini kuliko huyo unae mpelekea mashtaka.
  Mimi siamini kwamba ni Bakari Asseid tu ndiye anae dhulumu haki za watu, ila naamini kuna kundi la baadhi ya viongozi wenye tamaa ya kudhulumu haki za wanyonge kwa kutumia vyeo vyao. Viongozi hao ndio ambao wana mtumia Bakari Asseid afanye hayo anayo yafanya.
  Si shangai kuwa viongozi hao wako mstari wa mbele kumkingia kifua Bakari Asseid hata kwa Rais yanapo tokezea malalamiko kama haya, kwa sababu mara nyingi watu wa aina hii hufanya kazi kama timu moja yenye lengo moja hivyo inakuwa rahisi kumzunguka Rais asijuwe kinacho endelea hasa ukizingatia hapati malalamiko yoyote kutoka kwa wananchi kwa vile wananchi wamewekewa vizingiti vingi tena vigumu na masharti mazito ili waweze kumfikia Rais, hivyo basi mara nyingi Rais hupata maoni ya upande mmoja tu jambo ambalo haliwezi kuzaa haki kamwe, kwani Rais hajui watu waliomzunguka wako upande gani.

  Rais anapaswa awasikilize pande zote mbili yeye wenyewe tena ikiwezekana azikutanishe kwa pamoja ili apate kuujua ukweli, vyenginevyo ataendelea kudanganywa tu. Viongozi wanakawaida ya kulindana hata kwa maovu.

  Ninacho kijua kuhusu Bakari Asseid hilo si eneo la kwanza kulipora kwa wananchi wanyonge hiyo nikawaida yake amesha zowea na kwa vile haulizwi, ana walinzi wamemzunguka Rais kwa kumpotosha basi ataendelea kupeta tu. Hata huyo DK. Shein atawekwa kati na yeye nyeupe ataiita nyeusi.
  Mimi namjua Bakari Asseid tokea anatembea na magari ya ng’ombe kule kwao Pangani na kisauni, hizo tabia za kudhulumu hajaanza leo na huyo sijuwi kuwa atawezekana jamaa ana akili za ziada kwa kupika mambo na kufanya propaganda chafu, isitoshe anawasaidizi katika serikali, Lakini iko siku nitawataja mmoja baada ya mwengine na vitendo vyao.
  Mimi nikuulize Bakari Assed mbona hujajishtaki kwa DK. Shein pale ulipo jiuzia gari ya Serikali? Au mkuki kwa nguruwe tu?
  Ombi langu kwa DK.Shein nakuomba uwachunguze viongozi wote watakao kuja kumtetea Bakari Asseid kwa kadhia hii huenda viongozi hao wana lengo moja lakini wewe hujui.
  Pili, kwa vile msitu umepimwa kisheria mwaka 1997 kwa nini isitolewe hadharani ramani ya msitu wa Ngezi ili wananchi wakapata kufahamu maeneo ya msitu na maeneo ya wananchi?
  Tatu, Bakari Asseid aulizwe Jee! Vumawimbi ni msitu wa Ngezi au ni msitu wa Vumawimbi? Na ilikuwaje kuwaje hata Vumawimbi ukawa msitu lakini yakipita makubaliano msitu huo utaondoka?
  Nne Jee! Amewalipa fidia wananchi wanao miliki eneo hilo? Ikiwa hajawalipa Jee! Sheria inamruhusu kufanya anayo yafanya au anafanya kwa vile analindwa na walio mtuma? (Rais na Makamo wake hawahusiki)
  Ikiwa hajalipa fidia tunakuomba DK. Shein umuamuru DK.Aseeid awalipe fidia wananchi hao japo kupitiamkononi mwake kwasababu keshaiibia serikali pesa nyingi tu hashindwi ni kuwalipa wanyonge. Hata gari ya Serikali kajiuzia kinyemela.
  Hivi kweli wewe Asseid kama ni muadilifun kwa Serikali ungethubutu kujiuzia gari ya Serikali kwa ghilba?

  Nimalizie kwa kumuomba DK. Shei aitishe kikao baina ya wananchi na kundi la Bakari Assed awasikilize yeye mwenyewe, asiamini kupokea taarifa kwa mtu mwengine yeyote zaidi ya watendaji wa wizara ya Ardhi, hapo ukweli ataujuwa, Uzuri ni kwamba Wizara ya Ardhi ndiyo inayo husika na upimaji wa maeneo ,bila shaka hawa wataleta ushahidi kamili kuwa eneo linalozozaniwa limo katika msitu wa hifadhi wa Ngezi uliopimwa na Serikali au halimo, kwani wao ndio watakao toa ramani halisi ya msitu walio upima kisheria mwaka 1997. Hili ndilo suluhisho tosha kabisa. Zaidi ya hapo nikujitia kizani tu ukweli hauwezi kujulikana, ila itakuwa ni kumpa fursa Bakari Asseid aendelee na dhulma zake dhidi ya wanyonge wasiokuwa na hatia.

  Kwa kuongezeatu nikumuomba aandae ziara Rasmi itakayo shirikisha pande zote mpaka eneo husika ili akague kwa macho yake sehemu iliyopita mikaka ya msitu huo uliopimwa na Serikali ili afanye maamuzi sahihi iwapo itagundulika kuwa eneo linalo zozaniwa halimo katika msitu huo.

  Nadhani ikiwa Rais atachukuwa hatua hii yeye mwenyewe bila ya kumtuma kiongozi yeyote kwasababu wanaweza wakamletea ripoti tofauti, basi tatizo hili litaisha ndani ya masaa mawili tu wala hakutotokea mgogoro tena kati ya wananchi na Wizara ya kilimo. Vyenginevyo ataendelea kudanganywa na viongozi walio mzunguka kwa kulindana kwao na kulinda maslahi yao na sio jambo jengine
  Tunakuomba DK.Shein tatua mgogoro huu wewe mwenyewe, ili ukweli ujulikana na wenye kupotosha wachukuliwe hatua za kisheria. Tunakuomba usiishie kumwamini Bakari Asseid na timu yake hao watu wana mtandao mkubwa sana na wamekuzunguka watapanga kila aina ya uongo wakudanganye, kwa vile wamejipanga wameweka vizingiti ili wananchi wasikufikie wakakueleza ukweli.

 2. bakora 17 Juni, 2017 at 22:40

  Binafsi ninavyo mjua DK. Shein kwa hili hatokaa kimya abadani, kwani akiendelea kukaa kimya kwa jambo kubwa kama hili, atakuwa anawalea viongozi wa aina hii, na wataona sasa wamepewa ruhsa ya kufanya watakavyo katika kudhulumu haki za watu kwa vile hawakuulizwa kwa tuhuma kama hizi, wala hakuna hatua zilizo chukuliwa dhidi ya walio husika.
  Hivyo basi watajiona wako huru kujipigia mali za wanyonge wapendavyo, jambo ambalo litapelekea viongozi wengine kupora ardhi za watu hovyo hovyo kwa kutumia kigezo cha mgogoro huu huku wakiamini kwamba Rais huyu ni mkimya na mpole hivyo watafanya watakavyo kuchukua haki za watu kwa kutumia vyeo vyao na kulindana japo kwa njia ya kharamu. Viongozi kama hawa mara nyingi hudanganyana kuwa Akhera iko mbali hivyo huwa na kauli mbiu ya matumizi kwanza haijalishi matumizi hayo yawe ya halali au yawe ya kharamu, kwao wao Akhera baadae.
  Kimsingi ni DK. Shein kuandaa ziara rasmi itakayo shirikisha viongozi na watendaji wa wizara ya Ardhi hasa hasa wanaohusika na upimaji, pamoja na wananchi walio na mgogoro na wizara ya kilimo.
  Zaidi ya yote ningependa katika ziara hiyo ichukuliwe ramani ya Msitu halisi wa Ngezi uliopimwa kisheria na serikali mwaka 1997, ili Rais ajiridhishe yeye mwenyewe kwa kukagua zilimopita beacon za msitu huo . Lengo iwe ni kuutatua mgogoro huo kwa vitendo endapo itathibitika kuwa maeneo yenye mgogoro hayamo katika msitu huo basi Rais siku hiyo hiyo atowe amri ya kuwakabidhi wananchi hao haki zao. Hapo atakuwa amekata mzizi wa fitina.
  Hili ni suala la siku moja tu endapo Raisi ataamua kufanya hivyo basi kila kitu kitakaa sawa. Vyenginevyo akiendelea kutumisha ataendelea kupokea ripoti feki zisizokuwa na kichwa wala miguu. Kwani kwa suala hili tayari Rais keshatuma viongozi wengi sana mwisho anapelekewa ubabaishaji tu, watu wanalao rohoni (kupiga deal) ukweli unawekwa kiporo.

  Kutokana na suala hili kuchukua mda mrefu pamoja na kutuma viongozi mbalimbali kutembelea eneo husika kuutatua mgogoro huu lakini imeshindikana, imefika mda sasa kwa DK. Shein aamuwe kutembelea eneo husika yeye mwenyewe ili ajionee ukweli halisi ikiwa ataamua kuumaliza mgogoro huu kwa mara moja.
  Naamini akiamua hakuna kitakacho shindikana.

  DK. Shein ukiagizia tu kila siku utaendelea kudanganywa hatujui hao unao watuma wana malengo gani katika nafsi zao kuhusu eneo hilo, tunakuomba andaa ziara japo ya nusu saa tu, itatosha kubaini ukweli halisi ukitumisha utadanganywa. Viongozi wengi ukweli wanaujuwa ila wanaogopana,pia wanalindana, wakikaa pembeni wanamlaani Asseid wakiwa pamoja nae wanamsifu kwa ujasiri wa kutengeneza uongo ukaonekana kuwa ndio ukweli halisi, isipo kuwa baadhi viongozi wenye athari ya dini ndio wanao chukia maovu yake.
  Mwisho wa yote wewe ndiye msimamizi wa haki za watu katika nchi hii, tunaomba haki itendeke.

Leave a reply