Makala/Tahariri

Dr.Shein:Nani Anayeupenda Muungano zaidi Zanzibar?

Rais wetu, Dr.Ali Mohammed Shein amekuwa anzunguka kila kona kuhubiri Muungano, kuwagomba wale wote wenye mawazo tofauti na yeye kuhusu Muungano; maneno ya kejeli, fedheha, stihzai na hata kuonyesha ubabe na ukali. Inanijia huruma kusikia anasema yale anayoyasema, maana ninafuatilia na kumsikiliza. Swali la mwisho linalojiuliza: Je, Dr.Shein anaujua hasa Muungano au anachupia chupia tu? Anafuata mkumbo ili yake yamuendee na abaki madarakani? Kuujua muungano, si kujua tarehe iliyoanzishwa Muungano au waliouasisi, la hasha? –“mambo yake, na vikorombwezo vyake”.

Naomba nimfahamishe Dr.Shein viongozi wa Zanzibar hasa walioupenda Muungano kwa dhati, na Muungano ukawapenda wao:

1. Aboud Jumbe Mwinyi — alikuwa Rais wa Zanzibar. Kufa kupona, dam dam — aliupenda Muungano sana, na alichukua mpaka rasilmali za Zanzibar kuzipeleka Tanganyika. Kuna kipindi Zanzibar ama tulikopesha au tuliwapa Tanganyika pesa, kulipia mishahara yao huko. Record zipo.
Jumbe alizihaulisha taasisi nyeti za Zanzibar, na kuziingiza katika taasisi za Muungao, bila ya idhni ya mtu yeyote yule. Jumbe alichukua hata vifaa nyeti vya utendaji kama vile vya xxx….ikiwemo meli zetu (MV.Mapinduzi/Maendeleo) kwa harakati za ukombozi wa Kusini mwa Afrika, Mozambique, Namibia, South Afrika n.k

Na mengine mengi mengi mengi tu, mengine haifai kuyasema hapa. Mwisho wake ni nini? ni Aibu na fedheha, na idhalali juu yake. Mwisho alipouona ukweli yalimkuta yaliyomkuta. Ameondoka na legacy ya kuandika kitabu ‘Partner-ship’.

2. Nitamuacha Ali Hassan Mwinyi, na Idrissa Abdulwakil.

3. Salmin Amour Juma — huyu naye alikuwa kufa – kupona, laizma Muungano udumishwe tu. Amefanya mengi na ameuwa, amedhalilisha watu, ili yake yamuendee, na abaki madarakani. Alikuja na sera za ‘ethnicity’ au kitaalamu ‘ethno-politics’ — kubagua watu kwa mujibu wanakotoka. Pemba-Unguja…CUF-CCM, na taka taka za kisiasa kama hizo, Uhizbu kidogo, Ukomredi kidogo, U-ASP kidogo n.k ili yake yamuendelee na asimame madarakani.
Naam, leo yuko wapi? na ameishia vipi. Siku moja moja ninakwneda kumzuru, na inasikitisha sana kuona hali alivyo sasa, kama mtu aliyekuwa ‘head of state’ wa Zanzibar. Ukweli hasa anajuta tena anajuta sana sana. Mpaka anthubutu kusema kuwa ………!!!

4. Amani Karume — naye pia amefanya mengi tena mengi mno. Huyu ndiye wa mwanzo kuichukua account ya SMZ na kuihaulisha ndani ya BoT (bank of Tanzania), that means, mishahara na mambo mengine yote ukachukue BoT kwanza. BoT sio bure, kuna charges nyingi tu, wanaojua hesabu na mifumo ya kibenki, watasema ni how much per day.per each transaction wanatulipisha BoT na tija yao ni ngapi, wanavuna mara tatu au nne kwa Zanzibar (but no thanks). Mwisho wa utawala wake Karume mdogo ni ‘love-hate’ affair na wajomba zake wa Tanganyika. yeye alikuwa akiwaita ‘ndugu zetu wa damu’. Naam, ni kipindi hichi tumeona Watanganyika wengi wameingia Zanzibar, makanisa mengi wamejengwa Zanzibar kwa kutumia mtindo wa rushwa katika sekta ya ardhi, ambayo yeye na shemeji yake Mansour waliidhiti Wizara hiyo ya Ardhi. Na leo hii eti mansour anatetete nchi, na nyie wenzangu mnafuata mdundo tu. Kama imamu-maamuma (waladhalina-amiiin)!

5. Kuna group jengine, nimeamua kuliweka mwisho: Maalim Seif Shariff Hamad na wenzake — hawa walikuwa wamaweza kuuwa, lakini Muungano UDUMU, ilikuwa kwao ni fakhari sana kuwamambia kuwa ‘wanaishi Dodoma’ au wanakwenda Dodoma kuhudhuria vikao vya CCM. Tuliona wamefanywa NINI. Kiukweli hasa, Maalim Seif alikuwa anaujua Muungano na anaupenda kuliko Shein. Na kama leo Maalim Seif atarudi CCM, basi atapewa hata Urais wa Muungano bila shaka yeyote ile, hasa ukizingatia ‘uhai wa Chama cha CCM’ kwa wakati huu.
Mnajua Maalim alifanywa nini na hatimaye ilikuwa nini.
* Katika group la Maalim Seif, mtoe Maalim Juma Duni Haji — huyu tokea hapo awali alikuwa hana ‘taste’ na Muungano, alikuwa technorat mzuri tu, but rebel mzuri pia kwa suala hili la Muungano. Nashukuru kumuona yuko hivyo mpaka sasa (juzi tu alikuwa anasema amekereka sana kuona gazeti la rai la wiki hii limeshapaisha makala ya kumtukana mwanasheria mkuu wa serikali, Othman Massoud).

Sasa, turudi tena kwa Dr.Shein — hici kweli anaupenda sana Muungano au atatufanyia dhihaka tu na kulinda maslahi yake ya uongozi. Mimi naona ni kweli, maana r.Shein, hana ‘vision’ ya Zanzibar wala ya jambo lolote kimaisha. Capacity yake ni finyu sana, na waliofanya naye pale Hospital wanamjua kwa hilo, hata alipokuwa Vice President wa TZ inasemekana alikuwa mzigo kwao kiutendaji. Inasikitisha sana kuwa kila wakati/era, Zanzibar tunapata viongozi wasiokuwa na vision wala mission, wala focus……….. !!

Tukumbuke kuwa ni utawala huu wa Shein na Kikwete – ndio tumeona kwa mara ya kwanza, holy Quran imechomwa moto (Zanzibar) na baadaye Bara, na misikiti imechomwa moto.Baadaye wanatoa excuse hizi na zile.
Wauza Unga na watumiaji wa Unga wanaachiwa, ukahaba umezidi zanzibar, wanaangaliwa tu – lakini masheikh 9sio uamsho tu) hata yeyote yule, hakuna subra, wala uvumilivu, ukisema umenaswa. Hao ndio Shein an Kikwete na Muungano wao.

Share: