fikra hasi – Ingelikuwaje ingeandikwa mlinzi wa M.Seif auwa

Written by  //  09/09/2010  //  Makala/Tahariri  //  1 Comment

Ni udadisi wa kitoto naweza sema ulionijia kichwani ‘samahanini kwa utoto wangu’, ila pia tunaweza kujiuliza kupitia kwayo kwamba ni vipi wale wasiomtakiya mema na wenye kutafuta kila aina ya baya kwa MZANZIBARI huyu Mpendwa na wengi anaegombeya nafasi ya uraisi kupitia chama cha wananchi CUF, mlinzi wake ndie yangemtokeya yaliomtokeya mlinzi wa mgombeya urais wa CCM ambaye pia ni makamo wa rais kumfyatuliya risasi kijana mwenzetu wa kizanzibar na kisha kuidharau maiti yake hadi kufikia kung’ong’wa na inzi? naomba nisieleweke vibaya hapa kwani lengo ni kutafakari tu jinsi baadhi ya watu huyabeba na kuyapublish mambo kwa kumtizama muhusika zaidi ya litendwalo naomba wanaukumbi tujiulize magazeti yetu yangekuwaje tokeya kitendo hicho kutokeya.

EID MUBARAK NA RAMADAN MAQBUL..

One Comment on "fikra hasi – Ingelikuwaje ingeandikwa mlinzi wa M.Seif auwa"

  1. GSM 09/09/2010 kwa 10:41 um ·

    aslam-alaikum jamani kwanza eid mubarak kwa waislam wote
    jamani hii habari inasikitisha hata mtu kupigwa risasi kimya kimya tuuu na tusisikie na sababu ilofanywa hata huyo mtu kupigwa risasi jee mbona tunaanza mwanzo mbaya huuu kwa ramadhan hii mungu amlze mahala pema na huyo alompiga risasi inshaalah ataanza kumlipa hapahapa duniani
    kullu ammun watnum billkhayr

Comments are now closed for this article.