Kama Karume angekuepo angesema nini juu ya siasa za Zanzibar
Written by popobawa // 11/07/2010 // Makala/Tahariri // 8 Comments
- Zama hupita na mambo hubadilika!
Lakini watu ni tofauti kidogo kwani licha ya zama hizi kubadilika kwa kasi bado kuna watu ambao wanapendelea mifumo ya zamani ieendelee kuwepo. Watu hawa katika zama za sasa hujulikana kama “wahafidhina”
Wahafidhina ni watu ambao husukumwa zaidi na falsa za nyakati zilizopita ambazo zilizowajaa vichwani mwao wakiamini kuwa ndio njia pekee sahihi ya kufata. Si watu wanaokubali alama za mabadiliko ya nyakati kirahisi.
Mmoja ya wahafidhina waliobaki ni Bakari Shamte, mshiriki mgandivu wa mapinduzi na mmoja wa muasisi wa ASP. Kama ilivyo kawaida ya wahafidhina, ni watu wenye misimamo mikali huku wakiamini ya nyuma ndio sahihi na yanapaswa kuendelezwa katika zama zote zijazo, tena kwa gharama zozote.
Hapa tunaweza kujikumbusha dhana nzima ya “Mapinduzi Daima” kuwa nayo ni ya kihafidhina. Wahafidhina hawa wamesahau kuwa hakuna cha kudumu milele. Hata dunia nayo itaondoka, seuze mapinduzi ya kibinadamu.
Tumeshuhudia wazi wazi mhafidhina Shamte akisema kuwa CCM ya sasa ni legevu kwa vile tu haitoi msukumo wa adhabu ya mkong’oto kwa raia kama vile ilivyokuwa ikigawa dozi ya adhabu ASP ama CCM ya miaka ya 1990 – 2000.
Zama hizo watu walikuwa wakitoweka bila ya taarifa. Na kutoweka huko kulimaanisha kutokurudi tena. Wengi inasemekana waliuwawa kinyama kupitia mipango hii na hadi leo taarifa zao hazijulikani. Kwa vitendo hivi akina Shamte waliiona ASP kuwa ni imara sana na ndio maana leo wakaanzisha vikundi kama Kisonge kuendeleza mkong’oto huo.
Cha kujiuliza ni kuwa kwanini wahafidhina hawa wanafurahia adhabu na mauaji kama kwamba wao si binadamu wenye roho, hisia za uchungu ama maumivu?
Wengi wa wahafidhina hawa wameshaondoka duniani ingawa bado kuna baadhi yao wanaendelea kuishi.
Shamte ni mmoja tu wa wahafidhina hawa ambae bado hajaonyesha mabadiliko yoyote na anaendelea kupingana na upepo unaovuma. Pengine tuseme wahafidhina wote hawawezi kuwa sawa kwani binadamu ni wenye kubadilika kulingana na jinsi wanavyoelimika juu ya uhalisi wa misimamo yao.
Naamini Shamte hawezi tena kuumudu upepo huu wa mabadiliko. Lilobaki akubali ukweli na aachane na sera zake za chuki na kifisadi. Lakini suala kubwa linabaki kuwa jee wahafidhina wengine kama wangekuwepo wangefuata nyayo za Shamte?
Zaidi watu wangependa kujua msimo wa Abeid Karume binafsi, ambae ni muasisi wa mapinduzi hayo. Kwa vile Karume naye keshaaga dunia si rahisi kujua uhalisia wake juu ya suala hili. Lakini watu wanaweza kum-judge kulingana na historia yake.
Hivi Karume angekuwepo angeweza kuzuia vyama vingi? Nini angesema juu ya suala la muafaka na serikali ya umoja wa kitaifa? Jee Karume angekubaliana na Dk. Shein kuwa mgombea wa CCM kinyume na nadharia zake za watu wa aina fulani wasitawale? Wazalendo kazi kwenu kumsoma father Karume!







8 Comments on "Kama Karume angekuepo angesema nini juu ya siasa za Zanzibar"
…..BARAKA SHAMTE, WANAKISONGE NA WENGINEO WENYE MWAZO MGANDO WAMEPITWA NA WAKATI…..HAWASOMI NYAKATI….JAMII YA LEO HAIWAFAI.
Kwanza ninachukua fursa hii kumpongeza mchangiaji wa mada ya hapo juu. Ni kweli bado kuna baadhi ya wahafidhina ambao wanatamani kuziona zile enzi ya kuchapana watu. Lakini ni dhahiri kuwa kwa kweli wahafidhina wa aina hii haiwafai Zanzibar ya leo yenye upendo na maridhiano. Lakini kwangu sioni ajabu mtu kama Baraka Shamte kuwa na mawazo mgando hajui analolifanya anajifikiria kuwa yeye ni Afro-shirazi pekee yake, hajui kuwa wako Afro-shirazi wa kweli lakini wanahisi mabadiliko ni hatua katika maendeleo. Sasa huyu Bwana mdogo Baraka Shante na Wana kisonge tunataka tuwaone. Kimsingi CCM haiwahitaji lakini wao ndio wanaoihitaji CCM wagange njaa zao.
Inastajabisha leo mwaka 2010, lakini kina Baraka na wenzake wa Kisonge wan ataka turejee nyuma mwaka katika miaka ya 1995. Olewenu mumechelewa hatana nafasi ya kurudi miaka iliyopita. Kaeni pale Kisonge wakipita wasamaria wema muowaombe ganga njaa. Huu sio ule wakati wa wa watu kukaa maskani kuomba wapita njia hiyo haikuwa tabia wala sifa ya Wazanzibar. Kwa Wazanzibar hiyo ni ila na niabu kubwa na fedheha………………Ebuu badilikeni tuondoweni chuki za ukewenza ambazo hazina sababu hasa kwa vile dini yetu inaruhusu kuowa mke zaidi ya mmoja…………Vinginevyo, kama mumenuna na unawanaokuunga mkono anzisheni chama chenu CCM hakiwafai kwa vile ni chama chenyekuleta mabadiliko.
wala sifa
ASEME NINI KARUME MKUBWA?
yeye si ndie kinara wa kutia adabu watu, watu wakipotea hovyo hovyo wakati wake, kamuulizeni ali sultan issa kafanywa nini na mpaka leo hii yuko hai, mnajua karume mkubwa kamfanya nini HANGA, nafikiri z’bar ingekua haipo tena, au wangebakia karume family watupu na mahafidhina wengine, maana ukikaidi amri ya bwana unapotezwa, muulizeni Amani Thani Ferouz atawaeleza mmoja mmoja alietiwa adabu na bwana mkubwa, mie kwa mawazo yangu huyo karume mkubwa ndio nunda zaidi, maana sijui hata kama dr bilal angethubutu kuchukua form ya urais na komando salmin asingeonja kiti cha urais wa zanzibar.
alamsiki
Aa,wanaukumbi,ama mimi nimeishi karibu na akinawatu kama shamte, na huyu shamte wenyewe nikokaribu nae mkunazini, shamte nimtu mmoja mwenye akili zakijinga sanaa,na nimtu mmoja anae mwaga sumu mbaya sanaa,na nimmoja aliyekuwa akitowa mawazo kwenye maskani,wakati wa salmini ,ya watu kuadhibiwa amecheza part kubwa sana ktk kuadhibiwa watu enzi zile,na nimtu aliyekua hana banda ,ndio ukaona anazungumza kama tupo ktk miaka ya 70s,kumbe dunia imeshapiga hatu sasahivi,watu wamesha starabika kabakiya yeye na baadhi ya wahafidhina wenzake,yeye shamte hajiulizi wakuuu wamapinduzi waliokua wakitisha na walikuwa na sauti ,akina natepe ,moyo,leo wanasema waziwazi yakuwa siasa za zamani hazitufai,na wahafidhina hawafai kupewa nchi sasahivi,ujuwe wameona mbali na waoowanaumwa na mapinduzi kuliko wewe shamte, shamte wewe nikibaraka na mtu wakujipendekeza kwa wakubwa tu,huna lolote ambalo unaweza kufanya,zaidi ya mdomo ,nimesikiliza mahojiano ya shamte na idhaa ya kiswahili ya garmany,nimekuona nimtu ambae una mawazo tope,bado unafikiri watu wamo ndani ya box,unasema yakuwa ccm imekufa umefikiria marangapi kusema maneno hayo,yani kwakua hampati kupiga watu hampati kupita madukani kunyanganya,ndio unasema ccm imekufa ,pole sana ,jiandae kukaa kijiweni tena kwa miaka kumi kama umriupo,na hiyo nyumba unayokaa,wenyewe wameshakuja kuidai kazi kwako,wewe hushangai hata komandoo waudongo,hakumunga mkono bilali mara hii,hujuwi kama mambo yanabadilika wakati unabadilika ,wewe mawazoyako nifitna tuuu,na kuwaza mabaya,kumbuka wewe nibinaadam,tengeneza aghra yako sasa,jua lisha zama,usishindane na wakati, komando kasalim amri,mimi sitakikusema sana shamte maana hapo ulipo huna nguo,funika kombe……….? ALLAH TUNAKUOMBA USIWAPE NGUVU WATU WENYE MAWAZO KAMA SHAMTE KWANI WEWE UNAWAJUWA ZAIDI KULIKO SISI, ALLAH TUNAKUOMBA UTUVUSHE SALAMA AMINN
JAMANI HUYU MTU BARAKA (NAQAMA) SHAMTE NI MTU AMBAE NASIKIA ATI KAMFANYIA MAMBO MAOVU MAKUBWA BABA YAKE MZAZI SHEIKH MOHAMMED SHAMTE.
IKIWA NI KWELI BASI MUTANIKUMBUKA KWA JINA KWAOMTU KUWA HUYU BARAKA AU BALAA ANA MWISHO ULIO MBAYA SANA IKIWA ATAJIFANYA HANA MUDA WA KULETA TOBA KWA HAYO ALIYOMFANYIA BABA YAKE MZAZI NA BAADHI YA WAZANZIBAR WAKATI WA MAPINDUZI NA WAKATI WA SALIMINI.
ALLAH SUBHAANA WATAALAA AMEKATAZA HATA KUMFINGIA USO MZEE WAKO SEUZE KUMSABABISHA AADHIBIWE NA KUDHALILISHWA. KATIKA HISTORIA YA MITUME TUNAONA NI JINSI GANI SAYYIDNAA IBRAHIM A.S ALIVYOKUWA AKIMUOMBEA DUWA MZEE WAKE JAPO NI KAFIRI. PIA SAYYIDNAA MUHAMMAD SALA NA AMANI ZIWE JUU YAKE ALIVYOKUWA AKIMTHAMINI ABUU LAHAB BILA YA KUJALI MAOVU ALIYOKUWA AKIMFANYIA.
JAMANI TUTAHADHARI SANA NA WAZEE WETU HATA KAMA NI WAOVU TUWAHESHIM NA KUWAPENDA NA TUWALINDE NA KILA BALAA, LA KAMA TUNAPUUZA YATATUFIKA MAMBO MAKUBWA SANA KAMA DALILI ZISHAVYOANZA KWA BARAKA (BALAA) SHAMTE.
AHSANTENI
TUNAOMBA MUTUWEKEE HIYO PICHA YA BARAKA SHAMTEE BORA AITWE BALAA SHAMTE HUYU JINA HUYU LIMEMDHURU.
HUYU MUHIMU YUKO WAPI AU KAPATA MSHTUKO WA MOYO?
kwaomtu maneno umeyamaliza, hata mimi nilishawahi kuyasikia hayo. Naamini sana na mimi kama jina halimfai, na maustadhi watatuweka sawa hapa lakini naona bora aitwe BALAA SHAMTE
salamu wazanzibar, kwa kweli muuliza hoja unashekesha kweli kweli inaonyesha mzee karume humjuwi, unasikia tu sifa zake , kiufupi tu marehemu karume alibadilika kabla ya kifo chake na walio karibu nae watakwambia , wanasiasa wa hizbu wote walihukumiwa vifo na baradha la mapinduzi na sio karume , wale watu arubaini lakini wenye maamuzi ni watu kumi na nne hao ndio wauaji nyerere akiwaita watu ovyo ovyo,wanapo uwa matokeo yake anaambiwa karume watu wote wakawa wanamlaumu , mwisho karume kaamua kuwaashia wote jela,na kule jela kukabadilishwa jina kukawa kunaitwa chuo cha mafunzo, na mwisho akataka kuvunja muungano kabisa , na serikali yake iliwakusanya wote kufanya nao kazi , uma part , zpp, na makomredy , lakini baadae wakamgeuka tena hapo ua ua ikaanza na mtoto wa nyoka kamata chinja, kwa hivyo si tegemei kama angali endelea na sisa za chuki na ijapokuwa yeye na watu wake 14 walifanya hivy, na kuhusu huyu baraka shamte nadhani hana radhi ya marehemu baba yake ambaye alikuwa waziri mkuu wa mwanzo zanzibar , na alipo pinduliwa aliteswa sana na hawa watu 14 na alihukumiwa kifo auliwe lakini karume kamsamehe , kwa hivyo huyu shamte ni mwenda wazimu hatuwezi kumjaji kwa vile ni chizi. kiufupi tu shein ni bora kuliko bilali kwa hali yoyote ile kwa wazanzibar wameshachoka na sisa za chuki.
Assallam Allaykum ?
KARUME YEYE NDIO MSHENZI NA NDIE ALIE TUFIKISHA HAPA KWA TAMAA ZAKE ZA UROHO WA MADARAKA HAKUTOSHEKA KUWAUA WAZANZIBAR WASIO NA HATIA MATOKEO AKAENDELEA KUWAUA HATA HAO WAUWAJI WENZIWE, NA YEYE NDIO HASA WA KULAUMIWA KWENDA KUVIHONGA VISIWA VYETU KWA KAFIRI NYERERE MATOKEO NA YEYE MWENYEWE AKAWA KAMA SANAMU TU. BILA NA BARADHULI HILI KARUME ZANZIBAR ISINGALIFIKA HAPA.