KUINGIZWA KATIKA MUUNGANO MAMBO YANOIKANDAMIZA ZANZIBAR NANI

Written by  //  18/07/2010  //  Makala/Tahariri  //  10 Comments

Wabaya wetu ni wawakilishi na wabunge wetu tena kuliko hata raisi, juu ya hizi isu za kuingizwa kwenye muungano baadhi ya mambo pasipo na maslahi kwa zanzibar. lakini hili tunakuwa hatulisemi,hata kama rais aamue kitu gani hakiwezi kubadilishwa bila ya ridhaa ya wawakilishi na wabunge nasifikirii kama kunasiku waliwahi kutishiwa maisha ili kukubali kwa nguvu hoja flani au muswada flani, tukubali au tukatae hawa ndio wasaliti wetu wakuu wanoirudisha nyuma zanzibar.

Ni kweli muda flani tanganyika inaweza kuwa na ajenda zake ambazo hazina maslahi na wananchi wa Zanzibar, lakini ajenda hizo haziwezi kuwa nanguvu kama wabunge na wawakilishi wetu hawakuziunga mkono. mimi huwa nashangaa sana kwa sisi wazanzibari kuwalaumu wabunge wa tanganyika juu ya mabadiliko ya sheria zinotukandamiza wazanzibar wakati tukijua fika bila baraka za nduguzetu wabunge kutoka zanziba mabadiliko hayo yasingeweza kufanyika, au labda ni kwa kutokujua katiba inasemaje juu ya masuala yanohusu mambo muungano ndio tunawaona kama wawakilishi/wabunge wetu hawana makosa. katiba iko wazi jambo lolote linohusu muungano haliwezi kubadilishwa mpaka theluthi mbili [2/3] ya wabunge kutoka zanzibar waunge mkono, na hali haiishii hapo pia jambo hilo huhitaji kupata baraka za wajumbe wa baraza la wawakilishi ambao tunaamini wote ni wazazanzibari.

Hawa viongozi wanotusaidia kulalamikia mabadiliko kama vile mafuta kuingizwa kwenye muungano, kumfanya rais wa zanzibar asiwe tena makamu wa serekali ya muungano nk waliyashuhudia haya yakifanyika wakiwa serekalini katika nafasi za juu, tena kwa kufuatwa taratibu zote za kikatiba ambazo hazitunyimi uhuru wa kukataa yale tunayoyaona hayana maslahi nasi. hakuna hata jambo moja lililoingizwa kwenye muungano bila nduguzetu kutoka zanzibar kuhusika, baadae wanazunguka kutuhamasisha kuwalaumu watanganyika, huu ni unafiq na hatutakiwi kuupa nafasi.

Bila kuweka maslahi ya utaifa wetu mbele, tutapoteza raslimali zetu na mamlaka yetu yote. na kuwalaumu watanganyika haitotusaidia kitu huku tukijua kwamba maamuzi ya mwisho kikatiba tunayo wenyewe kupitia kwa wawakilishi wetu.

ALI KHAMIS

10 Comments on "KUINGIZWA KATIKA MUUNGANO MAMBO YANOIKANDAMIZA ZANZIBAR NANI"

  1. binamu 18/07/2010 kwa 3:59 um ·

    BWANA ALI KHAMIS, NAONA KAMA INAFAA UMMA UKUAMSHE KWANI INAONEKANA UNALALA MCHANAA, TENA UNAKOROMA. UTASEMAJE KUWA JAMBO LOLOTE LINALOHUSU ZANZIBAR HALIPITISHWI BILA KUPATIKANA KWA RIDHAA YA 2/3 YA WAZANZIBAR WENZETU NA KWAMBA TUSIWALAUMU WATANGANYIKA.
    NAKUBALIANA NAWE JAMBO MOJA TU KUWA NI KWELI TUNAO WANAFIKI MIONGONI MWETU, LAKINI PIA SIKUBALIANI KUWA TUNAWEZA KUPINGA JAMBO NA LISIPITISHWE. MFANO ULIO HAI WA MIAKA YA KARIBUNI TU NI LILE SUSLA LA ZNZ KUJIUNGA NA OIC, KOMANDOO AKAJITUTUMUA KUONYESHA UKAMANDOO WAKE LAKINI WATU WAKAMWAMBIA WEWE SIO KOMANDOO BALI NI KAMA NDOO, UNAKUWA NA KELELE UKIWA MTUPU LAKINI UKITIWA MAJI UNAKUWA KIMYA NA NDIVYO ALIVYOKUWA. MWINYI MTAALAMU WA LUGHA YA KISWAHILI NAE AKATOA MPAKA MIFANO AKISEMAA “SHARIFU AKIBWIA UNGA, ULIMWENGU UMEMZONGA” NA ZNZ KUJIUNGA NA OIC HAKUMAAANISHI KUWA SERIKALI YA ZNZ NI YA KIISLAMU, NA MFANO AKITOA KWA NCHI YA UGANDA AMBAYO 98% NI WAKRISTO LAKINI PIA NI MEMBER WA OIC, ZNZ ILIKUWA KATIKA KUTAFUTA NAMNA YA KUJIKOMBOA KIUCHUMI .
    KAAMA HILO LILITOKEA UKIWA TUMBONI, NI KARIBUNI TUMESHUHUDIA MATUKIO KADHAA YAKILALAMIKIWA NDANI YA BARAZA LA WAWAKILISHI , NA KUPATA BARAKA ZOTE LAKINI BADO YANAWEKEWA MAKWATO NA SMT, ULE ULE MTINDO UNAOTUMIKA BLW KUWANYIMA HAKI WAPINZANI HATA KWA JAMBO LA MASLAHI YA UMMA NDANI YA BARAZA KWA KUTUMIA KURA YA WENGI NDIO HIVYO HIVYO PIA KWENYE BUNGE LA MUUNGANO. NI KURA YA WENGI TU NDIO INAYOTUMIKA.
    NJIA PEKEE YA KUJIKOMBOA NI KUREVIEW KATIBA TA MUUNGANO NA VILE VIPENGELE VILIVYOWEKWA NA KUPITISHWA NA WANAFIKI WETU PENGINE KWA KUTOKUSOMA NA KUELEWA WALIFANYALO, ILI TUIOKOE ZNZ NA TUWE NA JIBU LA SUALA MBELE YA MUNGU.
    NI HISIA ZANGU HIZI.

  2. mfurukutwa 18/07/2010 kwa 5:44 um ·

    Swadakta Binamu. Kwa ujumla maelezo yako yamesibu.
    Maelezo ya Bw. Ali Khamis yana uzito kiasi lkn ktm muktadhaa kama huu kwa Znz, kiasi kikubwa cha maelezo yake ni kama kuweka ‘square peg in a round hole’!
    Ukweli ni kwamba kunakuwa na force fulani kutoka ‘Kuumeni’ dhidi ya Serikali ya Zanzibar na wawkilishi pamoja na wabunge inapokuja ktk issues za muungano.

    Lkn juu ya yote hayo, wabunge wetu kule dodoma wanakuwa hawana la kusema. Sijui ni upeo wao ni mdogo ktk kwenda sanjari na mada za vikao. Kwa ujumla, ukiangalia hansards za bunge utakuta wabunge wetu wanachangia na kuuliza masuali ya ‘kimvita-kibendera’- chapwaaaaa!! Nakumbuka yule mbunge wa Koani analalamika eti atasoma halbadiri kwa serikali ya muungano akielekeza malalamiko yake kwa Basili Mramba (wakati ule ni waziri wa fedha TZ). Hoja yake huyu mbunge eti serikali ya muungano haijaisaidia SMZ ktk kuandaa mashindano ya kombe la challenge. Halbadiri na siasa wapi na wapi!! Michango yake mingi huyu jamaa ni kama ze komedi! Inasikitisha sana hali hii kwa wabunge wetu.

    Ufupisho: zipo external forces zinazowabana wabunge wa znz kuhusu mambo ambayo SMT inataka yapite, lkn pia hali ya ‘mchoko’ kwa wabunge wetu pia ina nafasi yake ktk hili!

  3. spark 18/07/2010 kwa 6:58 um ·

    Mimi naunga mkono hoja kwa 90%.
    @BINAMU bado kumbe hata hujui ni kwanini ZNZ haikukubaliwa kuingia kwenye OIC. kwa kifupi tu katika mambo ya muungano mojawapo ni mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa, na suala la kujiunga na OIC linaiingia hapa hivyo ni serekali ya muungano yenye haki ya kujiunga tukiangalia kisheria. hata mimi ningependa kuona ZNZ ikijiunga na hiyo OIC. Kwaiyo kama kuchemsha tulichemsha tulipokubali kuweka mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa kuwa ni ya muungano.
    Suala kwamba bunge hupitisha mambo kwa kutumia kura ya wengi, hilo hufanyika tu ikiwa kitu kinachopitishwa sio cha muungano lakini mabadiliko yeyete ya muungano yahihitaji 2/3 za kila upande wa jamuhuri nasio idadi ya wabunge. tatizo letu ni kupeleka wabunge wasiojua hata katiba na hili lina miaka mingi mbele ya kututafuna.
    Nivizuri kuyaangalia mambo kisheria zaidi, na hata hiyo proces ya kujinasua bac itapitia kwenye marekebisho ya hizo sheria na sivinginevyo.

  4. Junius 19/07/2010 kwa 12:02 mu ·

    Wazalendo,
    Mleta mada kaleta hoja kwa kuuliza swali, nani anastahili kubeba lawama?
    Mimi naanzia hapo kwenye hoja ya swali lake. Ni kweli kama walivyoeleza waliotangulia kuwa mambo yanayohusu katiba au ya muungano yanapaswa kupitishwa kwa kiasi kilichoelezwa cha 2/3 ya wawakilishi wa Zanzibar na kuthibitishwa na BLW.

    Hoja itakuja hapa, kwanini tunalalamika kuwa kuna mambo yamepitishwa kinyemela au bila ya ridhaa yetu? Na hivyo nani wa kubeba lawama kwa hali hiyo?

    Siku zote husemwa kuwa historia ndiyo itakayowahukumu watu kwa matendo yao na kauli zao. Mimi nashawishika kukubaliana na mleta mada kuwa wa kubeba lawama hizi ni wawakilishi wetu au viongozi wetu.

    Lakini tatizo halipo hapo tu,ukosefu wa elimu,uwezo mdogo wa kiuongozi na kufikiri,woga na kukosekana umoja kwa viongozi na wawakilishi hao, ndiyo hali iliyotupelekea yote hayo. Si bungeni wala BLW,kote tulikuwa na watu tu na si viongozi wa kweli.

    Hebu fikiria watu kama Seif Bakar,wakati huo,amekuwa waziri wa serikali zote mbili, hajuwi kusoma wala kuandika hata jina lake, unategemea atajadili nini huyu bungeni wakati mafuta yanachukuliwa?
    Kuna mchangiaji mmoja kamtaja mbunge wa koani,nadhani ni Haroub Soud, huyu jamaa hajuwi hata kuandika jina lake,unashangaa kuzungumza habari za ramli na uchawi bungeni na kuacha hoja za maana!!

    Wasomi walikuwa hawapo?

    Wawepo wapi! na kanuni ya kimapinduzi ilikuwa “wasomi wafungwe au wauliwe”. Wakati huo tukiwa na watu kidogo walikwenda shule, serikali ya kimapinduzi iliwachimba mpaka ikawatoa roho, mifano ipo chungu nzima. Waliobaki walikuwa vibaraka tu na waoga waoga walioshindwa kunyanyua midomo yao.

    Leo nawashangaa waheshimiwa wetu wanataka kujikosha machoni pa watu baada ya kuuza nchi na mali zake, eti tuamini kuwa mambo yamefanywa bila ya ridhaa yao,umeona wapi bi harusi akabakwa na mumewe!!!! waseme ukweli wameuza nchi na mali zake,saivi wanaona haya!

    Hebu tujiulizeni mambo mangapi yalipitishwa bungeni na BLW ikakataa kuyaidhinisha na hayajatumika(mfano tume ya haki za binaadamu,sumatra n.k), iweje hayo mengine waseme yalipita kwa nguvu, nguvu ipi kama si na wao kuchangia???

    Wasitudanganye, tanahitaji nchi yetu,tunahitaji rasilimali zetu na hizo hatuwezi kuzipata kama CCM itaendelea kuwapo madarakani hata kwa kiti kimoja. Wakati umefika kwa wazanzibar sote tuwatowe vibaraka hawa wala nchi na kupisha awamu mpya kuijenga Zanzibar mpya.
    MUNGU IBARIKI ZANZIBAR
    J

  5. maumivu 19/07/2010 kwa 5:06 mu ·

    haya mambo ya wabunge wetu kutuwakilisha basi na wananchi ndio vile vile wakulaumiwa kwa kuwachaguwa hawa wabunge ambao hawana hata elimu kama mfano eti tunawakilishwa na fadau au utasikiya alikuniki anagombaniya ubunge na uwakilishi na anshinda sasa niwakati wakuwachaguwa watu wenye elimu nzuri na wenye imani na wananchi na inchi. wabunge wengine ni wanafiki tu wanalipwa maroporopo yao na magari hawana wasiwasi yao yanawaendea. na kuhusu haya mambo ya huko bungeni wabunge wa Zanzibar hata wote wakipiga kura za aina yoyote basi hawana chao hiyo ndiyo maana kutawaliwa maanake serikali ya Zanzibar ni kama kivuli mambo yote yanapangwa huko dodoma sisi ni kama watoto wachanga tu tunaendeshwa na tunalishwa tunacho pewa siyo tunachotaka kula wenyewe. basi ni muhimu wananchi kuamka na kuchagua viongozi wenye elimu wanaojuwa sheria na kutuokowa na hil jinamizi la sihivyo ndiyo tunazama tumebakiya kichwa tu sasa basi tujiokowe wenyewe maana hawo ndiyo wanatuzamisha

  6. popobawa 19/07/2010 kwa 5:08 mu ·

    Hoja za wachangiaji mada juu ya nini kilichangia kuwafanya wabunge wetu kuuza nchi yao mimi nakubaliana nazo 100%.

    Lakini kwa upande wangu nafikiri licha ya kukosa elimu na uwezo wa kufikiri juu ya athari za kisheria za maamuzi waliokuwa wakiyapitisha UZALENDO pia walikuwa hawana na wala hawajui umekaa vipi.

    Walichokifanya wabunge wetu hawa ni sawa na wanavyofanya wavuta unga. Wamechukua mali zetu moja baada ya nyengine na kuziuza kwa thamani ndogo sana tena naweza kusema ya bure ili wanenepeshe matumbo yao. Ndio maana miaka ile wabunge tulikuwa na wabunge wa maisha, hawabadiliki kwa vile walitumiwa vizuri kama rubber stamp.

    Wewe mtu una akili gani ukachukue hazina ya mafuta ukayauze kwa watu. Hata hawajiulizi basi mbona hawa wenzetu yao hawayafanyi ya pamoja. Yote haya ni kukosa uzalendo na nchi, hakuna chengine.

    Na hili la uzalendo tusipolijenga kwa waliopo na vizazi vijavyo tusitegemee maendeleo. Angalia hivi sasa tu hawa wenzetu wanaopinga maridhiano. Ok ni demokrasia na haki yao kufanya hivyo lakini jee upingaji huo unaangalia maslahi ya zanzibar? Utaona kuwa zaidi wanapinga kwa kulenga yao maslahi binafsi ama ya makundi wanayoya-support. Again, uzalendo na nchi hawana.

    Jamani uzalendo ni kitu namba moja katika kuleta maendeleo. Nchi inaweza kuwa maskini lakini kupitia uzalendo ikajikuta tajiri. Kama huipendi nchi yako basi huko tayari kujitolea kidhati kuifanya ipige hatua mbele. Niwape mfano mmoja tu jinsi uzalendo unavyofanya kazi ya kusogeza nchi mbele.

    Angalieni wenzetu wa China. Wao hata wakiongea maongezi ya kawaida tu basi hutumia neno “sisi wachina…” tena hata kama hilo jambo wanaloongelea ni baya basi wako tayari kusema sisi wachina tuna kitu fulani kibaya. Lakini they are very proud na nchi yao ndio maana wakajinasibu hivyo.

    Leo nenda sehemu yoyote huko China ukamtukane au umseme raisi wao hata kama hapana polisi,na ukubwa wa nchi hiyo basi ni dakika chache tu utashuhudia umezingirwa na kutiwa nguvuni bila ya kujua nani kapeleka habari hizo. Kila mtu ni askari wa nchi.

    Maendeleo ya China pia yanategemea sana wanaoishi nchi za nje mfano wa hawa wanzanje ambao wengine wako katika nafasi kubwa za nchi hizo. Machina haya kila wanachokipata huko basi wanakihamishia kwao ili kikaendeleze huko.

    Waliowahi kwenda China watakuwa ni mashahidi wa hili. Mfano mdogo tu haya mambo ya movies, leo DVD ya mchezo mpya ambao haujatoka hadharani huko ulaya basi utaukuta umeshazagaa China tena kitambo na unauzwa bei rahisi. Hii DVD ni mfano mdogo tu lakini machina wamekuwa wakihamisha technologia mpya kutoka nchi za ulaya kupeleka kwao.

    Marekani wenyewe taabani kwa hili. Mara ngapi wameibiwa siri na machina walioishi miaka karibu mia huko kwa kuwaamini kama ni wenzao na wengine hata huko kwao China hawajawahi kufika lakini nchi yao inawauma na wanafanya kila wanaloweza kuinufaisha.

    Si rahisi kulikuta china likawa halijui au limesahau lugha yake. Tofauti na sisi, tukitoka kwenda nje siku mbili tu basi lugha tunabadilisha na tunaona fakhari kuzungumza kimombo na mtu kama haongoi kimombo basi tunamuona mshamba, hana elimu na hajaendelea.

    Tembea miji yote duniani utakuta machina kibao wamefungua mabiashara na restaurant zenye majina ya Chinese Restaurant, nk. na maeneo mengine wana miji yao kabisa iitwayo China Town. Huko ukiingia hufikiri kuwa uko nchi ya kigeni kila kitu ni cha kichina na maongezi ni chun chun tu!

    Usiende mbali, fika hapo kwa machina wa Malindi/Rahaleo au nenda Chake Chake Pemba, kama utakosa tambi. Sasa wametufanya hata sisi tusiweze kukosa chakula cha tambi wakti wa Ramadhani.

    Sasa njoo kwetu, ni juzi tu tumeona hapa mtandaoni kuna restaurant imefunguliwa huko ungereza na kupewa jina la Kilimanjaro huku wamiliki wakijinasibu kuwa ni wazanzibari kindakindaki. Watu wengi walihoji kwa hili na wengine wakazuka kuwatetea kuwa ni sawa kuchagua jina walitakalo. Lakini kwa upande wangu mimi nalihusisha na kutokuwa na uzalendo na kwetu. Wangechagua jina lisilo na mnasaba na nchi basi ningeungana nao.

    UZALENDO MUHIMU JAMANI!

  7. ashakh 19/07/2010 kwa 10:18 mu ·

    Wazalendo tunakawaida ya kusahau.

    Munakumbuka miaka 90s viongozi wetu Zanzibar kila mmoja akikataa kwamba Zanzibar kuna uwezekano wa kupatikana mafuta!!! Dr Salmin Amour alikuwa mmoja wao. Sasa ikiwa rais kafikia hatua hiyo ya kuwadanganya wananchi unadhani wabunge/wawakilishi watafanya nini?

    Naiona hii ni chain,kila jino moja limeungana na jino jengine. Tokea viongozi wa nchi kuwa wabovu, mpaka hao wabunge/wawakilishi pia nawao ni wabovu. Haitoishia hapo pia wananchi nawao ni wabovu.

    Kulitatua tatizo hili huwezi kuanzia katikati, inabidi uanze nchani. Lakini kwenye mkufu (chain) nchani ni wapi?

  8. mrfroasty 19/07/2010 kwa 9:20 um ·

    Wananchi wanachagua mbunge/mwakilishi anaewapa rushwa.Ndio ni kweli, wananchi wa Zanzibar hawachagui kiongozi kwa uwezo wake.Wana vigezo vyake vya maajabu kabisa, kuliko duniani kote.

    Usije shangaa wananchi wakamkataa msomi, na wakampa kura zao mtu kwa ushabiki wa vyama vya siasa au kwa kuwa anawapa usafiri kwenye maziko.

    Hata kama ametoa halua au gari ya kwenda maziko ya kiislamu…BADO NI RUSHWA HIO!

  9. Junius 20/07/2010 kwa 1:00 um ·

    Mr.Froasty,
    Umenikumbusha kipindi kile cha uchaguzi wa kura za NDIYO(ndo huyo huyo) na HAPANA (isipokuwa huyo),katika jimbo moja la uchaguzi MwembeMakumbi, wagombea wa kiti cha uwakilishi walikuwa Marehemu Hamadi Ali Fadau na Dokta Ishau(sina hakika kama jina ni sawa), matokeo yake watu hawakutima kabisaa vigezo vya kiuongozi ambavyo bila shaka elimu inavichangia kiasi kikubwa. Marehemu Fadau akashinda kiti kile kwa kampeni za kichale na uchepe (nazungumza historia simzungumzi marehemu kama marehemu).

    Kwahiyo usemayo ni kweli vigezo vya watu kuchaguliwa na wananchi wetu vinachekesha kama si kusikitisha. Nasikia kuna mshona nguo za akina mama mmoja kachaguliwa kwenye jimbo moja la uchaguzi mjini magharibi akapewa mpaka uwaziri katika afisi ya waziri kiongozi. Haina maana washona nguo hawewezi kuwa viongozi tatizo sifa za uwongozi tu ndiyo maneno ya waarabu “mushkila” hapa!!!!
    J

  10. mfurukutwa 20/07/2010 kwa 1:09 um ·

    Na cha kuchekesha zaidi:
    Marehemu Fadau alichangia kwenye baraza la Wawakilishi akisema ili serikali iongeze pato ktk sekta ya utalii, ni vyema kwa wizara husika ikawapaka rangi makobe kila baada ya muda ili wataalii waweze kuvutiwa kwa mabadiliko ya rangi za makobe!! Naye rafiki yetu wa jimbo la Koani aliishauri serikali wakati akichangia bungeni kuwa isitishe kuwasomesha vijana ktk fani ya biashara, sababu? Eti watakuwa na uwezo wa kufoji cheki na hivyo serikali itakuwa inapoteza fedha!

    Kweli kila mtu ana haki ya kuwa kiongozi ktk serikali zetu lkn sifa za uongozi – maneno yako Junius – “Mushkila” tena mushkila kabiiir!!

Comments are now closed for this article.