Kuna maana gani kusherehekea 9Dec uhuru wa Tanganyika wakati

Written by  //  05/09/2010  //  Makala/Tahariri  //  2 Comments

Mimi sio mwana sheria lakini nashindwa kufahamu hii katiba ya Tanzania na huu mfumo mzima wa Muungano wenu. ikiwa Tanganyika imepoteza utaifa wake na imekufa? Jee hizi Sherehe(Matanga) za 9December uhuru wa Tanganyika zina faida gani?.

Mimi nahisi kwa mtazamo wangu hizi sherehe hazina maana na zinashukuwa ma bilioni ya pesa za Wazanzibar kwa jina la Muungano bila idhini ya upande upande mmoja uliomo ktk Muungano ambao ni Serekali ya watu wa Zanzibar kufanyiwa ufujaji (Israf) kwa kitu kisicho (exist any more). Mimi nahisi kikatiba hili ni kosa Kufuja pesa za Muungano na kuna haja ya wazanzibar kufungua kesi ya madai. Kimtazamo pesa za sherehe zinatokana na mfuko wa Muungano wa Tanzania na ikiwa Zanzibar ni Sehemu moja ya Muungano huo, na wala wao hawafaidiki chochote na sherehe hizo.

Hivi karibuni wazanzibar walikuwa katika Joto ya jiwe muda wa miezi 3 hakuna pesa ya Muungano ilio tumika kuwaonelea huruma Wazanzibar walivyokuwa wakimenyeka kwa joto kali na kiza. nikwanini leo wazanzibar mukubali besa zenu zifanyiwe Birthday ya marehemu Bwana Tanganyika?.

Hivi sasa wazanzibar wamesha fika mbali kutatua matatizo ya Muungano wao na matunda yake yanaonekana na tayari Zanzibar ni Nchi na mipaka yake. Nasaha yangu ni kuwashauri Wa-Tanganyika wafufue Tanganyika yao ilioko nyuma ya pazia la Tanzania sio hivyo wazanzibar wamesha washtukizia ujanja wenu kuwa Muungano ni Dirty Trick na muelekezea ncha mwenzake china humpata yeye. sihivyo mutakuja kubaki NO NAME. Mungu libariki Taifa la Zanzibar na wazanzibar wote.

2 Comments on "Kuna maana gani kusherehekea 9Dec uhuru wa Tanganyika wakati"

  1. Salmin Kiluwa 05/09/2010 kwa 8:43 um ·

    Hizi sherehe za uhuru Tanganyika zinasherehekewa kwa jina la Tanzania. Kwa uono wangu mfupi ni kwamba Zanzibar pia ilipata uhuru wake 10th Dec 1963. Lakini hapa pana kitendawili wanaukumbi. Kwanini sherehe za Tanganyika zimebaki kila mwaka lakini ile sherehe ya uhuru wa Zanzibar imefunikwa. Jee Zanzibar si nchi na Taifa kama Tanganyika? Hichi ni kitendawili naomba mukiaguwe wanaukumbi
    Salmin

  2. MTANGANYAKA 05/09/2010 kwa 10:58 um ·

    MAAJABU MAKUBWA. HICHI SIO KITENDAWILI NI KIZUNGUUKUTI.

    LIDUMU TAIFA LA ZANZIBAR NA PANAPO MAPENZI YA BWANA MOLA, HAKIKA DUAA NA SUBRA, MATESO NA DHULMA, KEJELI NA KIBRI, TWANGA NA BURUZA, FUNDA NA FYETUWA (RISASI), MIAKA AROBAINI NA SITA NA UPUUZI, HAKIKA YOTE HAYO AMEYAPOKEA NA HAPA ANAUTHIBITISHIA UMMA WA KIISILAMU DUNIANI KOTE KUWA HAKUNA NENO LAKE HATA MOJA LILILO LA MZAHA, SUBRA INATHIBITISHWA HAPA “HAKIKA MWENYE KUSUBIRI”, BASI NAA’M PENZI LA BWANA LIMETUFIKIA INSHAALLAH. NA HAPANA SHAKA BASHASHA ZAKE TAYARI MWILINI ZINATUTUMBUIZA, UTULIVU UPO, UPENDO WARUDI, MSHIKAMANO NAA’M, ALHAMDULILAH REHMA ZAKE ATUONGEZEE, AMIN.

    KILICHOBAKI WAUNGWANA NI KIZUNGUUKUTI SIO KITENDAWILI, TENA HICHI NI CHETU WENYEWE UNGUJA NA PEMBA SIO TANGANYIKA NA ZANZIBAR, HAO HAWATUWEZI NA WAJUWA KUA HAWATUWEZI. NASEMA NI SISI WENYEWE KWA WENYEWE. HAPO ZAMZNI NAKUMBUKA KULIKUWA NA MTIRIRIKO MZURI WA WATU TOKA UPANDE MMOJA WA VISIWA KWENDA WAPILI WA VISIWA. WATEMBEZI HUWA WAKIBEBA MAKAPU NA MASUSU, MKIWA NA MAKUKU NDANI YAKE, MANDIZI, MABORIBO MAKUBWA MITHALI YA KICHWA CHA BINADAMU. WENYEJI WALIKUWA WAKIWAITA WATEMBEZI “VIBUWA” ETI KWA WINGI WAJAO, LAKINI WALLAHI WAKISHOBOLE MABORIBO PAMOJA, WAKICHEKA PAMOJA, WAKIPENDANA AND THE MOST IMPORTENT OF ALL WAKIELEWA THE JOKE ON THE GROUND. WALLAHI HAWAKUHADAIWA NA MAJI YALOWATENGA HATA SIKU MOJA.

    KIZUNGUUKUTI CHETU IS PURE ARTIFICIAL, INGEKUWA VYENGINEVYO NDIO INGELIKUWA MTIHANI KWANI HAKUNA AWEZAE KUBADILISHA IKAWA KIFO HAKIPO. THAT’S NATURAL. LAKINI KWETU SISI KUMETOKEA KWA BAHATIMBAYA, SOME TIMES KWA MAKUSUDI, KUKAWA NA SOME SOSIAL IMBALLANCE ALONG THE YEARS BAINA YA VISIWA VYETU, JAMBO AMBALO LIMEPELEKEA UPANDE MMOJA KUJENGA HISIA HAZIKUTAKIWA ZIWEPO, TO BEGIN WITH, LAKINI ZINAZOELEWEKA KIHAKI LILAHI. YAMETOKEA MATENDO YAKIBINADAMU, KISICHOWEZA KUBADILISHWA AU KUREKEBISHWA NI KILE TU BWANA MOLA ALICHOSHATUPANGIA. MATENDO YA BINADAMU YOTE YANAREKEBISHIKA. WHAT WE NEED MOST IS TO BALANCE THE EQUESTION, (JAMANI KINGEREZA NDICHO HICHOO)THE SOSIAL ONE. TOKIFAULU HAPO NA HAKUNA LAKUTUFELISHA, BASI CHECHE TULIZONAZO ZA KUTOAMINIANA ( TUSIKATAE ZIPO)ZITATOWEKA, UPENDO TULIONAO UTAFICHUKA KWA KILE KIASI KILOJIFICHA.

    NA HICHO NDIO KITENDAWILI/KIZUNGUUKUTI KINACHOMKABILI MAZANZIBARI WA LEO NA KESHO.

    MTANGANYIKA HAJATUWEZA HAPO, HATUWEZI LEO WALA HATOTUWEZA KESHO NA HILO NI TAMMAM KISHWANI MWAKE. TUSIPOTEZE WAKATI DEALING WITH WHAT WE ARE NOT TO DEAL WITH.

    MOLA IBARIKI NA UITUKUZE ZANZIBAR NA JAMII YAKE, AMIN.

    NAWAKILISHA.

Comments are now closed for this article.