Makala/Tahariri

Kwanini Z’bar isiwe nchi huru?

Malisa GJ

Hebu tujadili kdg kuhusu Z’bar kwa fikra huru. Kwanini Z’bar isiwe nchi huru? Tunahofia nini? Kwanini nguvu nyingi zinatumika kuifanya Z’bar iendelee kuwa tegemezi kwa Tanganyika kuliko juhudi za kuitafuta Z’bar huru? Kwani Z’bar ikiwa nchi huru yenye mamlaka kamili kuna athari gani kwa Tanganyika?

Inadaiwa moja ya sababu za muungano ni mambo ya kiusalama. Kwamba jiografia ya Zbar ilivyo ni rahisi kutumika kuishambulia Tanganyika. Lakini je kama tutakua na mahusiano mazuri na Z’bar kwanini watumike kutushambulia? Mbona Cuba kijiografia imekaa katika eneo ambalo ni rahisi sana kuishambulia Marekani lakini Marekani hajawahi kulazimisha muungano ili kuondoa hatari hiyo?

Na tunashambuliwa na nani? Kwanini? Anyway hata kama kuna watu wamepanga kuishambulia Tanganyika je ni lazima waitumie Zbar? Na je hatari ya kushambuliwa inaondolewa kwa kulazimisha muungano? Mi nadhani hatari ya kushambuliwa ingeweza kuondoka kirahisi kwa kuruhusu Zbar kuwa nchi huru then kuwa nao marafiki. Wazanzibari wengi ni ndugu zetu waliotoka bara. Tuna unasaba nao. Hawawezi kuruhusu ardhi yao itumike kushambulia ndugu zao wa Tanganyika. Kwahiyo hatuna sababu ya kuwa na hofu.

Kwa maoni yangu Muungano umedumaza zaidi maendeleo ya Z’bar kuliko kuchochea maendeleo. Z’bar ingekua huru yenye mamlaka kamili isingekua hivi ilivyo leo. Z’bar ndiyo taifa la kwanza barani Afrika kuwa na kituo cha televisheni (ZBC) na Televisheni za rangi kwa mara ya kwanza Afrika zilionekana Zbar na Morocco. Wastani wa pato la taifa kwa mtu mmoja mmoja (Per capital income) kwa Wazanzibar kabla ya muungano lilikua dola 25,000 kwa mwaka, karibu shilingi milioni 50 za sasa. Lakini per capital income ya wazanzibari leo ni wastani wa dola 2000 kwa mwaka, karibu milioni 4. Wamerudi nyuma mara dufu.

Ulinzi wanategemea Tanganyika, elimu Tanganyika, fedha Tanganyika etc. Yani karibu kila kitu ni kwa hisani ya Tanganyika. Hata Rais wao akisafiri nje ya nchi hatambuliki kama Rais kwa sababu hakuna taifa liitwalo Z’bar. Kiti cha Z’bar umoja wa mataifa kiliondolewa rasmi mwaka 1964 baada ya muungano.

Yapo madai pia kwamba mji mkuu wa kibiashara wa umoja wa falme za Kiarabu (UAE) uitwao Dubai ulipaswa kujengwa Zbar. Yani leo Zbar ndo ingekua Dubai. Watu wangetoka huko duniani kuja kufanya shoping zao Zbar. Lakini ilishindikana kwa sababu ya kukosa mamlaka kamili ya kuamua kama nchi huru.

Sasa nauliza kuna athari gani kwa Zanzibar kuwa taifa huru? IELEWEKE kuwa sipingi muungano. Najaribu kutafakari. Watu wengi hutoa majibu mepesi kwa kutaja kile kiitwacho faida za muungano.

Eti kuna free movement ya watu. Lakini je hatuwezi kuwa free movement bila kuungana? Mbona raia wa Swaziland na South Africa wanafanya free movement (bila passport) na hawajaungana kuwa nchi moja? Hata Africa mashariki tuko na mpango wa kuwa na free movement ya kwenda nchi yoyote within East Africa bila passport lakini hiyo haimaanishi tutaungana kuwa nchi moja.

Kwa nia njema hebu tujadili kwanini MUUNGANO wa Zbar na Tanganyika ni lazima?. Na je baada ya miaka 50 ya kuungana kwanini nchi hizi mbili zisiruhusu wananchi wake waamue kama wako tayari kuendelea nao ama lah through refferendum?

Maana inavyoonekana ni kama vile Wazanzibar wamechoshwa na muungano lakini tunawakalia kimabavu. Hata wakiomba kura ya maoni waamue hatma yao hawapewi. Sasa ikiwa ndivyo, tuna tofauti gani na Morocco ambao wameikalia Sahara Magharibi kimabavu? Mwal.Nyetere alipata wapi ujasiri wa kuikemea Morocco na kuomba iondolewe kwenye umoja wa OAU wakati alikua anafanya yaleyale ya Morocco kwa Zbar?

Je tulimfukuza Sultani ili tuikalie Zbar kwa niaba ya Sultani? Je wazanzibar walifanya mapinduzi ili “wakaliwe” na ndugu zao Watanganyika?

Uhuru una maana gani kama sio uhuru kamili? Kama umemfukuza mtu aliyekua anakunyima chakula, akaja mwingine anakupa chakula lakini anakunyima nguo, je utajiita mtu huru? Je Zbar ni huru? Katibuni tujadili. Be rational, avoid emotions. Tunajadili kwa maslahi mapana ya nchi.!

Fb

Share: