Madai kuhusu Jumbe, zidi ya Maalim Seif, hayana mashiko.
Written by ole // 25/08/2010 // Makala/Tahariri // 54 Comments
Na.B.OLE,
Waswahili wamenena kwamba mchele haukosi chua hapana budi kwa mpishi kuchambua ili isimuharibie biriani yake.Ni kawaida katika jamii, ikiwa utakuwa mkweli basi kuna watu watakuchukia kwa tabia yako hiyo. Kwa upande mwengine ukiwa mnafiki basi kuna baadhi ya watu watakuona ni mtu wa maana japokuwa wewe ni muharibifu katika jamii hiyo.
Kuna baadhi ya watu wachache ambao kutokana na Maslahi yao binafsi siku zote hupenda kuitumia fursa hii kuwachanganya Wazanzibar kuhusu madai yasio kuwa na msingi wowote zidi ya Maalim Seif.
Watu hawa wanashindwa kuandaa hoja zenye mashiko za kumpaka matope Maalim Seif, matokeo yake huleta hoja ya kuhusishwa kwake na kujiuzulu kwa Mh. Jumbe, na wengine husema hatumpendi kwa sababu tu alifukuza watu kazi alipokuwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Kama hayo hayatoshi, wengine huishiwa na chakusema badala yake humsingizia Maalim kwamba wakati alipokuwa Waziri Kiongozi , alifanya ubaguzi kwa kuwasomesha Wapemba wengi.
Lakini kuna wale ambao wamefyatuka kiakili basi husingizia kwamba Maalim anataka kuleta Waarabu, lakini watu hawa husahau kwamba baadhi ya wazee wao ama baba au mama ameoa au ameolewa na Mwarabu, sasa wanapokuja na hoja kama hii, basi ni kusema wanajitukana wenyewe.
Nasema kwamba madai haya hayana ukweli wala mashiko yeyote, lengo la hawa wanaotoa madai haya ni kumchafua kiongozi huyu baada ya kushindwa kuona udhaifu wake. Kuna watu ambao mawazo yao na akili zao ni chache kufikiri, wao huchukua pumba za maneno kutoka kwa watu wengine bila kuzichambua na kupata ukweli ulivyo, hawa ni wale wanaoambiwa mutakula udongo wakajibu ndio, kumbe yule anaewambia hivyo yeye anakula Basmati.
Kwanza nianze na haya madai kuhusu Jumbe, wanaopakaza kasumba hizi ni watu ambao hata wao wenyewe hawajifahamu sikwambii kujua hicho wanachokizungumzia. Mh. Jumbe bado yuko hai mbona hamuendi kumuuliza kadhia hii ili kupata ukweli wa mambo ulivyo, badala yake munakaa pembeni kutoa maneno ya kashfa kwamba Maalim Seif ndie aliesababisha kujiuzulu kwa Mh, Jumbe. Mbona Jumbe yeye mwenyewe hajawahi kutamka hilo, kwa nini mumsingizie Mzee wa watu ambae kwa sasa hataki kusikia hata hilo neno siasa likitajwa ?
Pia wengine huenda mbali kwa kusema kwamba oh! Jumbe alikuwa anataka Serikali tatu. Haya madai sio ya ukweli kabisa Jumbe hakuwa na nia hiyo bali alikuwa na ajenda yake ya siri binafsi, ndio mpaka leo hii Mh Jumbe amekuwa kimya na hataki kuzungumzia kuhusu kazia yake hiyo.
Mh. Jumbe ingelikuwa kweli anataka Serikali tatu basi mtu wa mwanzo ambae angelimkubali ”idea” yake hiyo asingekuwa mwengine bali Maalim Seif, kwani Seif sio mpumbavu kiasi hicho katika kupigania maslahi ya nchi.Yeye anajua ana uwezo wa kutambua dhahabu na shaba, mchele wa Mapembe na Basmati.
Kihisoria tunaona kwamba uongozi wake Jumbe hakuleta mabadiliko makubwa kiasi hicho zaid ya katiba , pia Mh. Jumbe alikuwa akiongoza kimapinduzi mapinduzi na wala hakuwa kiongozi mzuri kwa Wazanzibar.Mh. Jumbe alikuwa akiishi na kuongoza katika dunia yake yeye mwenyewe binafsi, utashi wake na hisia zake ndizo zilizokuwa kama washauri wake.
Mh. Jumbe alifanya mambo mabaya sana katika uongozi wake ndio maana leo hii ukamuona ameikimbia siasa na ukimkumbusha analia machozi ,akikumbuka aliyoyafanya. Kama kuna watu hawaoni na wala hawataki kusikia basi nitawapa mfano moja tu wakati wa uongozi wa Jumbe ni kitu gani kilitokea.
Ni Rais wa mwanzo Zanzibar kujenga kiwanda cha POMBE pale maruhubi Zanzibar na wakati huo Zanzibar ilikuwa kituo kikubwa cha Elimu ya dini,kwa wale wanaomsakama Maalim hili hawalioni au ndio wanalifumbia macho kwa sababu halikufanywa na Maalim Seif? Athari ya kiwanda kile zilikuwa ni kubwa sana kwa Zanzibar na mpaka leo hii bado zinaendelea kwani Zanzibar imekuwa ni kituo kikuu cha kujengwa mabaa ya ulevi na idadi ya wanywaji imekuwa ikiongezeka kila uchao,vijana wa kike na kiume ndio wahudumu wa mabaa hayo, jamani kuna mtu atapinga , mbona hamsemi haya ?
Katika yote aliyofanya Mh. Jumbe basi hili analijutia maishani mwake na alifika kuiomba Serikali imuuzie kiwanda hichi baada ya kuelewa kwamba alifanya makosa makubwa kukijenga enzi za utawala wake. Sasa sijui kama hili alikubaliwa na Serikali au la. Lakini kama halikukubaliwa basi tutamuomba Rais anaekuja ikiwa atakuwa Maalim Seif amsaidie Mh. Jumbe kilio chake hicho, kwani hakuna kubwa kwa Muumba.
Sasa wale wanaokurupuka wakasema kwamba Maalim ndie aliemfukuzisha Jumbe walete hoja nyengine, kwani sisi tunajua ni siri gani ambayo alikuwa ameipanga Mh. Jumbe, Wahenga wanasema kwenye kuku hapamwagi mtama.
Kwa vile mzee wetu huyu alijua makosa yake na kutaka Mafra kwa Mola wake kwa yale alioyafanya Zanzibar basi Inshallah Mola amsamehe kama katubia kweli. Kwani sote ni Binaadam na tunakosea lakini ukitanabah unatakiwa urejee haraka kwa mola wako.
Dai jengine ni lile la kufukuzwa watu makazini. Mimi naona nivichekesho sana kwa wanaoshikilia madai haya. Kwa fikra zangu mimi huyu ndie kiongozi anaefaa kwani anaonesha utendaji wake kama kiongozi. Itakuwaje mtu ameajiriwa na Serikali kwa mikataba na akubali kufuata masharti ya kazi matokeo yake akashindwa kufanya kazi yake. Sasa wewe kama kiongozi utachukua hatua gani ? Waliofukuzwa wote, ilikuwa ni haki yao na walistahili, kwani walishindwa kuwajibika. Taifa linahitaji wachapa kazi sio wazembe wanaopenda kuvaa makoti ya Wazee wao.
Maendeleo na ufanisi katika kazi hayawezi kufikiwa ikiwa Wafanyakazi hawaelewi kanuni za kazi. Ndio ukaona kwamba Zanzibar na Tanzania kwa ujumla Maendeleo yanadorora kwa sababu ya utendaji wake ni mbovu. Nchi haiwezi kuendeshwa kiyakhe yakhe, lazima misingi na kanuni zifuatwe, hili halina mjadala kinyume na hivyo tutakuwa tunajidanganya na hatuwezi kufikia popote pale.
Hapa ningependa nitowe mifano michache kuhusiana hili ili tuweze kupata picha halisi ya utendaji wetu Visiwani ulivyo. Mwalimu ameajiriwa kuwafundisha Wanafunzi S.M.Z, sote tunaelewa kwamba Mwalim anatakiwa kuripoti kazini saa kumi mbili kamili za asubuhi, sasa inafika saa tatu kamili Wanafunzi wameshafika darasani ,Mwalim hajafika shuleni bila sababu zozote za msingi, mpaka inafika hadi Waziri wa Elimu anafika Shuleni Mwalimu hayupo hivi ndivyo sheria zaki zinavyosema ?Hawa wanafunzi wategemee nini na wakifeli tukaanza kulaumiana tumeonewa. Atapasi vipi Mwanafunzi wakati Mwalimu mwenyewe anashindwa kuwajibika.
Mimi binafsi nimeyashuhudia haya wakati nikiwa katika Mafunzo Zanzibar. Ikiwa wewe ni kiongozi niambie utachukua hatua gani ya wazembe kama hawa ? Halafu mukae museme OH! Tumeonewa Seif katufukuza kazi,acheni upuuzi wenu huo, mbona huko Ulaya munakobeba mabox munafika kazini kwa wakati na munafuata sheria zote na ukicherewa hulipwi na matokeo yake unafukuzwa kazi kama hukujirekibisha au kwa sababu hao ni Wazungu ? Tunacho kizungumzia hapa ni utendaji na hizi ndizo kasumba ambazo baadhi ya watu wanazo ni wavivu na hawataki kuwajibika matokeo yake wanakuja kuleta sababu zisizo msingi.
Wazalendo wenye madai ya aina hii hawana budi kujirekibisha kwani maendeleo siku zote yanataka utendaji na uwajibikaji hatuna budi kujifunza kutoka kwa wengine ambao uzumbe na uvivu haupewi nafasi badala yake sheria za kazi ndizo zinazopewa kipau mbele.
Mwisho kabisa ningependa kuligusia hili dai la Maalim kuwasomesha Wapemba. Hizi ni pumba ambapo mimi binafsi naona haya hata kulizuingumzia suala hili. Kwanza wanaoleta hoja hizi nataka niwaulize hivi Seif alikuwa Waziri kwa muda gani au tokea sitini na nne baada ya Mapinduzi ? Maanake Wasomi walikuwepo wengi tokea enzi hizo Kisiwani Pemba, lakini kubwa zaidi Seif tokea afukuzwe kwenye Serikali ni karibuni robo karne sasa hivi, jee hivi sasa hakuna tena Watu wanaosoma kisiwani Pemba au wote wanaosoma hivi sasa wanasomeshwa na Seif ?.
Wacheni kumchafua Maalim bila sababu maalum Seif ni kiongozi wa watu wote wenye kuitakia mema Zanzibar.Kamwe hamuwezi kumchafua kwa visingizio hivyo, badala yake ningelipenda muwe wawazi kwa kuleta hoja za msingi na zenye mashiko.
Mbona watu hawamzungumzii vibaya Dr. Salimin na Dr Gharib bilali ambao hawakuficha chuki zao wakati wa utawala wao kwa kuwanyima watu wenye asili ya pemba fursa zote za Kisiasa na kiuchumi, au mkuki kwa Nguruwe tu lakini Binaadamu ndio unakuwa mchungu. Serikali yao walifika kutunga sera maalum zidi ya Wapemba, Sera hizi niliziona kwa macho yangu pale ikulu mbona hayo hatuyasikii au kwa sababu hakufanya Seif.
Wanaompinga Maalim lazima walete hoja zenye mashiko, lakini wasikurupuke watu kutoka maskani wakaanza kuleta pumba ambazo hazina ushahidi wowote. Dunia ya leo inahitaji wasomi wenye hoja za kweli sio mawazo ya kufikiria tu.
Wazanzibar wote ni ndugu hatuna budi kuachana na tofauti zetu ambazo zinarudisha nyuma maendeleo yetu. Lazima tukumbuke kwamba maendeleo ya Zanzibar yataletwa na Wazanzibar wenyewe ikiwa tukashikamana kwa pamoja. Tusiwape nafasi hawa wachochezi ambao muda mrefu sasa wamekuwa wakibomoa ngome yetu imara ya Zanzibar. Ufa huu uliopa hauna budi kuzibwa tea kwa ”CONCRETE” kabla ya ukuta kuvunjika.Maridhiano ndio dawa ya maadui wa Zanzibar.







54 Comments on "Madai kuhusu Jumbe, zidi ya Maalim Seif, hayana mashiko."
mimi nafikiri hata hatukutakiwa kuupoteza mda kuwajibu watu wasiokuwa na hoja za msingi kama wale tuliowaona hapa [muhimu&ismailia]hawakustahiki hata kuletewa uchambuzi zaidi kwani mawazo yangu naamini walichokiweka hapa wao binafsi sio wanachokiamini ila hutaka kuwalisha watu chuki zao juu ya mtu na wanatambuwa kwamba walio wengi wanafahamu ukweli uko wapi lakini wao walisukumwa zaidi na chuki zao binafsi za kutompenda mhusika hakuna zaidi ya hilo, na mtu wa aina hiyo sifikiri kama itapatikana dawa juu yake, ila si vibaya kwa uchambuzi huu kwa vile maradhi yao wanaweza kuwambukiza watu wengine wasio wenye kutafakar, ila ukweli yote uliyoyaleta hapa ndio ukweli simuoni mwengine kwa sasa kiongozi wa kuingoza zanzibar yetu ila ni MAALIM SEIF na inshaallah ndie atakuwa kiongozi wetu [sio mtawala] wa zanzibar mpya yenye dhamira mpya na matarajio mapya.
Mimi naona haina maana kuendelea kusoma maada za mtandao huu kwa sababu hoja zote kuhusu siasa za cuf na ccm na zaidi mtu akichangia maada akaisema vibaya cuf basi anaonekana msaliti si lazima kila mtu aipende cuf kila mtu na mpenzi yake Mimi naona huu ni mtandao wa cuf
@B.Ole,
Kwa mara ya kwanza nimediriki kuona your level of reasoning and judgement on history. Binafsi licha ya kuwa naunga mkono siasa za mageuzi bado hainipi legitimacy ya kuwa fanatic and bias katika mambo muhimu ya ujenzi wa nchi hasa historia.
Nilijitokeza wazi kupinga upotoshwaji wa historia ya Zanzibar katika kitabu cha Ramadhani Mapuri, titled “Zanzibar Revolution 1964 and its Achievements”. Leo nashuhudia tena kitu kama hicho kutoka kwako Mh. B.Ole,mtu ambaye mda mrefu nimekuwa nikisoma maandiko yako positive katika mtandao huu.
Bw. B.Ole ulichokiandika hapo juu kuhusu kadhia ya Jumbe na Seif ni upotoshaji mkubwa, uliokosa maelezo ya kutosha ya utafiti na rejea za uhakika uliojaa upendeleo (bias) na ushabiki(fanaticism).
Naomba tutofautine kuhusu suala hilo tu hayo mengine mimi sina haja nayo kwakuwa ni mambo ya kibarazani na vijiwe vya kahawa.
Nimebahatika kusoma maelezo ya pande zote mbili kuhusu kadhia hii moja, yaani ya Maalim Seif(mtandao wa hakinaumma) na yale ya Mzee Jumbe kupitia kitabu chake maarufu cha(Partnership). Nimeweza kuweka mizania ya kupima maneno ya Mzee Jumbe na Maalim Seif na kujuwa kuwa hawa wote wawili alisababishiana kuanguka kwao na kuiangusha Zanzibar.
Kwa kuwa ndg.
Bole hukuwa na rejea ya hoja yako, ni wewe uliyekosa mashiko ya hoja yenyewe kwa kuwa umehukumu kiushabiki na kiitikadi jambo ambalo ni baya kuihukumu historia, na ndiyo maana nikakataa maelezo ya Omar Mapuri ya kuihusisha CUF na mfumo wa siasa za sasa za mfumo wa vyama vingi na zile za kipindi cha ukombozi kwa maana ya ZNP/ZPPP affiliation.
Jumbe ameeleza wazi katika maelezo yake kuwa harakati zake za kudai serikali tatu zilikuwa zinahujumiwa na watu ndani ya serikali yake, waliokuwa wakiendesha siasa za makundi, ambao Nyerere aliwatumia kwa wao kujijuwa ama kutojijuwa.
Jumbe anasema, aliamini hivyo kwa kuwa alishawaondoa vibaraka wa Nyerere mapema ambao aliamini wangelikwamisha mpango wake wa kuimezua zanzibar, akatoa mfano wa kumfukuza aliyekuwa mwanasheria mkuu zanzibar,Damian Lubuva, aliyeletwa na Nyerere na pahala pake akamuajiri mwanasheria Bashiri Swanzy kutoka Ghana.
Jumbe, alimuamuru Swanzy kuandika petition ya kupeleka mahakama ya katiba ili muungano wa Tanganyika na Zanzibar ujadiliwe upya kama ilivyokubaliwa awali. Jumbe anaeleza kuwa katika hali asiyoitegemea alishangaa dokumenti hiyo muhimu ilimfikia Nyerere kabla ya kufika mahakama ya katiba. Nani aliyeipeleka huko? Jumbe hakusema ila subiri maelezo ya Maalim Seif.
Mpaka hapa utaona kuwa mpango wa Jumbe ulishakwama maana Nyerere alichukua hatua za haraka kuitisha mkutano wa chama Dododma na kumfurusha Jumbe madarakani.
Maalim Seif, nimesoma maelezo yake mara mbili mbili kama ya Jumbe, ila kitu nilichokuwa sijaridhika kuwa hajakataa(kama unavyokataa wewe Bole) kama hakukuwa na atagonistic working enviroment between him (seif)and Jumbe.
Anaeleza Maalim Seif kuwa, mashaka yake na mpango wa Jumbe kuwa alihofia kama angefanikiwa kuunda serikali tatu,ingetumika kuwahujumi wao. Nilichoshindwa kumuelewa Maalim Seif ni kuwa alikusudia nini alipokuwa akisema “…mpango ule ungetumika zidi yetu” hii “yetu” alimaanisha nini? akina nani ambao walikuwa bora mpango ule ufeli kuliko Zanzibar kujimezuwa kutoka muungano wa kidhalim?
Zaidi ya kumuhujumu Jumbe, hapa maalim Seif kaonesha kuwa zilikuwa siasa za ubinafsi zilizokosa ukomavu na mtazamo chanya wa baadaye.(he is humanbeing by the way).
Maalim kadhalika, hakukataa kuwa alichangia mpango ule wa Jumbe kufeli,kwa hofu ya kuwa ulitumika kuwahujumu wao, na kwa hiyo hatutegemei kuwa hakuishabikia hatima ya Jumbe.
Kwenye makala ile ambayo nimeitafuta tena kule kwenye mtandao wa CUf na Da salma sijaiona tena labda imeondolewa,Maalim Seif kwa kauli yake amesema alimtegema Nyerere “kumdhibiti” Jumbe na dhamira yake, ambayo yeye maalim Seif anasema haikuwa njema kwao.
Hapa ni wazi aidha maalim na wenzake walimtumia ama walitumika na Nyerere, kufanikisha dhamira zao walizozijuwa wao wenyewe kum’ngoa Jumbe, huku Nyerere akiwatumia wao kwa dhamira zake alizozijuwa yeye mwenyewe. Hapa siwezi kusema kuwa wazo la Maalim Seif na wenzake na lile la Nyerere kuhusu vita zidi ya Jumbe lilifanana.
Ila ukweli ni kuwa mpango ulikuwa mmoja kati ya Maalim Seif na wenzake na Nyerere zidi ya Jumbe kwa melengo tofauti ikiwezakana, kama nimemuelewa maalim Seif,kwa matokea sambamba (ya kum’ngoa Jumbe).
Ni wazi kuwa kwa dhamira yoyote aliyokuwa nayo Maalim na kundi lake zidi ya Jumbe ndiyo iliyopelekea Jumbe afeli na kufukuzwa. Nilisema mwanzo kuwa wote hawa walichimbiana kaburi la kuzikana kwani baada ya “ushindi” wa Maalim Seif zidi ya Jumbe, serikali mpya iliyoundwa ilijumuisha karibu kundi lote la Maalim seif lililopambana na Jumbe.
Na baadaye fitna hazikukoma na maalim akaondoka na kundi lilelile lilopambana na Jumbe, Mshindi akabaki mmoja tu, Julius Nyerere on Zanzibar downfall.
Nimeshangaa sana ndg. Bole, umekuja na mambo ya barza za kahawa. Kweli kama binaadamu Jumbe ana makosa yake, au unataka kunambia na Maalim Seif kipindi chote yupo serikalini alikuwa kama malaika? Kuwa Jumbe hakufanya kitu, na kubeza hata hayo machache aliyoanzisha ni akili ya kitoto katika kusoma historia.
Leo hii kama Jumbe asingeanzisha baraza la wawakilishi,ile hoja ya Mh. Abubakar Khamis Bakar ya kuanzishwa GNU ingeanzia wapi?
Leo hii Jumbe kama asingeanzisha katiba ya Zanzibar (ambayo ww unaibeza) tungepata wapi leo fursa ya kusema “zanzibar ni moja kati ya nchi zinazounda jamhuri ya muungano…”na kufuta ile dhana ya bezo na dharau ya watanganyika kuwa tumemezwa? Je, hii si hatua ya kuanzia kujikomboa na asili yake ni hiyo katiba?
Bole, si vizuri mtu kama Jumbe ambaye kama alifanya hayo mabaya, ukawa unayasema kwa kumfedhehesha hapa jamvini, yeye ni binaadam, unajuwaje siri yake na muumba wake?
Jumbe amefanya dhambi gani kubwa ya kuwashinda hao masahaba watukufu katika maisha yao ya ujahili ambao leo tukiwataja tunasema ‘radhi allahu anhum’?
Kweli, ndugu Bole, inayumkunika kusema Jumbe asubiri Maalim Seif aingie ikulu, ndiyo labda ombi lake la kupewa kiwanda cha pombe litakubaliwa etc? huu siufinyu wa busara ya kiungwana kwa mtu kama wewe unaetumia kalamu ya uandishi vibaya?
Mbona humtaji kwa mazuri, hana au huyajuwi? Nimeyasema ila wewe umeyaona si kitu na hayo hayo ndiyo chanzo cha maalim leo kuingia huko ikulu, maana kama pasingekuwapo na katiba aliyoinzisha jumbe na baraza la wawakilishi kujadili, hiyo hoja ya GNU,ingejadiliwa Dodoma, na maalim Seif asingeiona ikulu mpaka kufa kwake!
Tumekaa miaka mingapi Zanzibar hatuna chuo kikuu na vijana wetu wakifaulu kidato cha sita wanafelishwa bara na hao wanaopita wakifika huko wanasomesha kozi za social science tu.
Leo hii kwa msaada wa Mzee Jumbe tumeweza kujengewa chuo kikuu cha mwanzo zanzibar tunguu, na vijana wetu wengi wamepita hapo, hivi sasa wanafanya Phds katika vyuo vikubwa ulimwenguni, au hujuwi hata Zitto Kabwe alipita hapo?
Umeona kiwanda cha pombe tu? Ni miaka mingapi Maalim Seif amekuwa waziri wa elimu, wazo hilo la kuwa na University zetu hakuwa nalo? Huoni alichofanya Jumbe kuwaomba Dar el imaan, Jedda, wajenge chuo kikuu ni kama sadakati el jaria ambayo imefuta lile baya alilofanya mwanzo, ambalo wewe Bole unashikilia kama hoja ya kumtia ubaya mzee Jumbe?
Ndivyo tulivyofundishwa na kiongozi wetu wa umma Mtume Muhamaada s.a.w? si yeye amesema kuwa tutangulize wema baada ya jambo baya? na si ndivyo Jumbe alivyofanya?
Je, si ni wakati wa Jumbe zanzibar ilipata kituo cha televisheni ya rangi ya kwanza Afrika nzima hata Tanganyika haikuwapo? yote hayo si mafanikio kwako Bole?
Tufikeni pahala ndugu Bole tukubalini kuwa Zanzibar kama taifa limepitia mikondo mingi ya majaribu. Kila zama zimekuja na mambo yake ya faida na yasiyokuwa na faida, mabaya na mazuri, ya kufurahisha na kuchukiza.
Isionekane hata wale wanye maarifa na elimu wanashindwa kutumia neema aliyowapa Mungu kuwaelewesha wenzao mambo haya kwa namna bora ya kuepusha mahusiano mabaya baina ya watu.
Wajerumani hawajawahi kukataa kuwa Hitler ni kiongozi wao, na alifanya mabaya yake, lakini kamwe hawajakataa mazuri yaliyoipa fahari Ujerumani na kuwa taifa pekee lililofanikiwa kukomboa rasilimali na utajiri wake kwa njia ya kibabe kutoka kwa wakoloni (rejea Versataille treaty 1919)mpaka leo wajerumani wanajivunia hilo na aliyelifanya ni Hitler.
Ndiyo pale ninapoona kuwa hata sisi tuna mengi ya kujifunza kwa kila history maker wa visiwa vyetu, si vyema kuwafundisha watoto wetu mabaya ya utawala wa kisultani wakati yapo na mema mengi tu kuzidi hayo mabaya yamefanywa na utawala wa kisultani yanapaswa yaenziwe na kukumbukwa.
Yapo mengi tu wamefanya ambayo kama yangelienziwa vizuri Zanzibar ingekuwa zaidi ya Singapore. Ni wakati wao ambao dola ya Zanzibar ilikuwa kituo kikuu cha biashara Afrika mashariki yote na mwambao wa bahari ya hindi, hili ni zuri na lingepaswa watoto wetu wajuulishwe.Zanzibar ilipiga hatua kubwa kielimu na maarifa ya dini na dunia mpaka wasomi wake wa wakati huo wakipata sifa kutoka dola kubwa za Ottoman na Uingereza.
Watu kama Bole na wengine mnaopata kuandika katika mitandao au pengine mawazo yenu kuchapwa na kusomwa na watu mbali mbali, mngetumia fursa hiyo kuelimisha historia kwa nia ya kujenga umoja zaidi kuliko kufufua malumbano ya zama hizoo.
Karibuni tu nimesoma habari ya maalim Seif akisema wazi kuwa hayo maridhiano yaliyozaa GNU, asipewe sifa yeye na karume bali kuna watu walifanya kazi hiyo akamtaja mmoja wapo mzee Moyo, inaonyesha wazi kuwa Maalim amepevuka kifikra na kama angekuwa na fikra kama hizi kipindi kile cha msuguano wake na Jumbe, basi leo hii tungekuwa na hadithi nyingine, laikini yote hayo ni mapito tunasonga mbele sasa.
Laikini kila binaadamu ni mkosa na mbora wao ni yule anayetanabahi na kutubu. Jumbe alikuwa, kama binaadamu, na makosa yake, na ameonekana kutanguliza wema kuyafuta, Mungu anajuwa zaidi, na Maalim Seif kadhalika, kama binaadam amekua na mapungufu yake, ametanabahi na ametubu(rejea katika hotuba yake ya ufungaji wa kongamano la kuungamkono kura ya maoni)
Hivyo, sote tuanzieni hapa na kuendelea, hayo mambo unayoyaleta Bole ukitaka kuyachimba huyapati kwa hivyo unavyotaka kwa kuwa walioshiriki bado wahai na ukweli huujuwi peke yako sote tunaujuwa. Mimi nilitegemea mda huu siasa hizo za akina Mapuri zimeshapitwa na wakati, tunazungumza lugha ya umoja sasa.
Hujasikia wewe hata hao Kisonge baada ya kusikia mabadiliko ya katiba yana define hadhi ya Zanzibar katika Muungano(japo haitoshi kwa maoni yangu), walisikika wakisema, “…bora!bora! na tuuvunjilie mbali…!”, kama wangefanikiwa kupinga kwao wangepata kusema hivyo?
MUNGU IBARIKI ZANZIBAR
J
@mtu kwao
Huu mimi naamini si mtandao wa CUF ila ni wa wazalendo kama jina linavyonesha na hapa kumbe ndugu yangu umejiweka wazi kumbe ukiwa hupendi cuf ndio hata kila kiongozi wa cuf umchukie ? sababu hapo alielezwa kufaa kuiongoza nchi ni MAALIM sio cuf kwa hiyo hata kuna wengine hatupendi ccm ila kuna tunawaona wakitajwa kufaa uongozi husema ndio anaweza bila kumtizama anatoka wapi na inshaallah kuwa na subira uiyone serikali itakayoongozwa na MAALIM SEIF naamini haitajali mtu anapenda cuf au ccm kitachotizamwa ni uwezo wako binafsi ALLAH ATUPE UHAI…ZANZIBAR MPYA,DHAMIRA MPYA NA MATARAJIO MAPYA..
Ndugu Junius, Napenda ufafanuzi wako juu ya hii kadhia ya Jumbe. Wewe huoni kitendo cha Alhajj Aboud Mwinyi Jumbe kukiuwa chama cha ASP au kukiunganisha na TANU na kuwa na CCM na hapo hapo kukipa chama mamlaka yote ya kiserikali hilo lilikuwa kosa?
Baadhi ya wachambuzi wa mambo ya siasa za Zanzibar, wanahisi Alhajj Aboud Jumbe alikuja kuimaliza Zanzibar kwa kitendo chake kile.
Nadhani kuna sehemu nyingi Maalim Seif amekuwa akimsifia Alhajj Aboud Jumbe kwa baadhi ya mambo aliyo yafanya yakiwemo hayo uliyo yataja, zaidi kitendo chake cha kuwaruhusu vijana kwenda kusoma akiwemo Maalim Seif Shariff mwenyewe. Wakati mmoja Almaruhum Prof Othman, aligusia hilo na kusema aliwahi kuambiwa na Jumbe kuwa Maalim Seif ni “his creation” na hilo Maalim Seif halikatai, kwani siasa haikuwa ni chaguzi yake. Nadhani unapo muuangalia Jumbe unamuangalia kwa sura mbili; moja msomi lakini nyengine ni Mwanamapinduzi. Kama ulibahatika kusoma makala za Ali Nabwa, unaweza kupata picha vipi Jumbe alikuwa.
Ndugi yangu Junius sijuwi kama unafahamu, ile timu ya wana Mapinduzi hawakupendezwa hata kidogo kwaa Jumbe kuwaingiza wapemba kwenye uongozi wa juu wa serikali na hasa wasomi. Ni wao ndio walio kuwa wakipanda na kushuka kuhakikisha hawa vijana wanaondoshwa. Sasa Maalim Seif akisema “sisi” si yeye na wachache waiwili watatu tu! Kuna wengi wamepotea na mpaka leo hawajulikani wapi walipo. Kwenye ukumbi wa Jamii foroum kuna mtu anauliza” wakati Karume alipo uuliwa, kulikuwa na mahaini; wako wapi baadhi yao na wanajulikana kwa majina?” Jamani mambo yamebadilika, hali haikuwa hivi, tusione leo tupo hapa Mzalendo tuna fursa kama hizi tukaona mambo yalikuwa ni hivi hivi. Sisi wengine wazee wetu wamesalimika kwa rehma za Allah tu. Lakini fitna na majungu yalipikwa na leo pengine hata kuzaliwa tusingezaliwa.
Kwa hiyo na tufunguwe ukurasa mpya na tugange yajayo. Jumbe anaweza kuandika na kujilabu atakavyo na Maalim Seif pia na Ali Sultan pia, atakuja Natepe naye pia, …
Duh! Mambo hayo! Unajua sisi wengine ni vijana wadogo sana ki umri lkn hatukubali kunyweshwa pumba ndio maana tunataka mtu aongee kwa dalili zenye mashiko. Kwa hiyo nawaomba wachangiaji kutoa links ambazo mtu anaweza kupata reference kama anwani ya kitabu na wapi kinapatikana au link ya internet etc.
Binafsi nimefurahishwa sana na waoni ya junius kwani hakubez upande mmoja. Amesoma hoja za pande zote mbili ile ya jumbe na ile ya seif hivi ndio mimi ninavopenda.
Mimi pia ningependa nisome hivo vitabu vyote viwili cha jumbe na seif ili nipate ufahamu wangu lkn sijabahatika kuvipata.
Kwa mujibu wa maoni ya junius mimi nakubaliana nae kua mada hii ya B.OLE imekua bias kwa kukosa kutaja mazuri ya jumbe badala yke kusema kua utawala wa jumbe haukua na mabadiliko makubwa.
Kuanzisha katiba na baraza la wawakilishi ni mambo makubwa ambayo ingefaa apewe tunzo maalum jumbe na mimi nitamtambua miongoni mwa wazalendo wa kweli kwa mambo haya. Angalieni dr salmin yeye katuondolea pasport na kutuletea tra.
Pamoja na mapungufu hayo yaliotokea tujue kua hakuna mkamilifu ispokua allah kwa hiyo hata huyu B.OLE haya ni mpungufu yake ingawa mada zake kwa ujumla zinakua nzuri.
Inawezekana seif na jumbe wote walikosea lkn wamejutia sasa mkombozi pekee aliebakia ni maalim seif tumuungeni mkono.
@ mtu kwao hujalazimishwa kuendelea kusoma lkn ujue tu huu ndio mtandao wa wazalendo. Kuisema cuf vibaya sio tatizo lkn ujenge hoja zenye mashiko.
Mimi natamani niikosoe cuf kwa baadhi ya mambo lkn mda wa kuandika mada sina na pia jinsi ya kuchapisha sielewi nahitaji mda zaid wa kituo nijifunze mwenyewe.
Unapomkosoa mtu maana yake unampa nafasi ya kujirekebisha au sivo?
@Kassim
Nimekuelewa vizuri. Nafikiri upo sambamba na mimi, nilisema hapo juu kuwa Jumbe naye alifanya makosa yake vile vile. Ila sijuwi kama umeifahamu vizuri hoja ya Bole, ambayo mimi sikubaliani nayo hata kidogo. Iwe kana kwamba Jumbe hakutii amri ya kusujudi kawa bilisi na Maalim Seif alikuwa malaika maana alikubali kusujudu?????
Hoja ya Bole ni kuhusika kwa maalim Seif kwa kujiuzulu Jumbe. Bole anakataa kwa kudai kuwa wanaosema hivyo “wanawachanganya Wazanzibari” na “wanampaka matope Maalim Seif…”. Katumia neno “kuhusika”, kana kwamba wakati kadhia ile inatokea Maalim Seif hakuwapo kabisa, wakati alikuwa serikalini na kwa maneno yake hakukataa kuhusika kwake ila Bole anamkatalia!
Nakubaliana nawewe kuwa ni kweli Jumbe aliingia kwenye mtego wa Nyerere wa kuiuwa ASP, ambayo ilikuwa the only mouthpiece ya Zanzibar ndani ya Muungano, jambo ambalo Nyerere hakulipenda, akalazimisha ivunjwe. Wakati Jumbe anagutuka mda ushapita na mambo yeshajichanganya, akafanya haraka kutafuta katiba na baraza la wawakilishi.
Mwisho Bole anafika mbali zaidi amkashifu Mzee Jumbe kwa sifa mbaya, anadiriki kusema “alifanya mabaya katika uongozi wake…”,(kana kwamba alitakiwa awe mkamilifu tu), “hakuleta mabadiliko makubwa kiasi hicho…”. Wakati wewe ndugu Kassim, umesema mwenyewe kuwa ni yeye Jumbe aligeuka siasa za kimapinduzi na kuwaweka wapemba serikalini huku akiwakera wanamapinduzi wenzake, Bole kwake yeye si mabadiliko makubwa!
Anasahau kuwa Jumbe alikuwa tofauti kimtazamo na wanamapinduzi wenzake, yeye alikuwa +msomi,licha ya mapungufu yake, aliamini nchi inajengwa na wasomi, maendeleo yanakuja kwa ilimu,ndiyo maana hakujali kuwaingiza wapemba wasomi serikalini, na ndoto hiyo anaishi nayo hata leo, ndiyo maana alichuna uso wake kuwapatia wazanzibar chuo kikuu, Alhamdullillah, wengi wanafunuka sasa, fursa hizo hazikuwapo wakati huo.
Nimemaliza kama ulivyomaliza kuwa kwa sasa tusongeni mbele tukitaka kujuwa nani mwema na nani mbaya tutafika kuona hata hapa mtandaoni sote wabaya. Kumbe migogoro hiyo ilitakiwa tujifunze suluhu zake tuwafundishe vizuri watoto wetu wasirejee makosa, leo kuna watu wanaitumia fursa hii vibaya kupotosha!!!!
MUNGU IBARIKI NCHI YA ZANZIBAR
J
A.Alaikum.
Mie sina mengi sana ya kusema ila nataka kusema mawili matatu tu kwa kuwa binaadamu kila mmoja kapewa na uwezo wake na kila binaadamu ana mapungufu yake, mie naona kama huyu Bole kapitikiwa kama alivyopitiwa Mheshimiwa Jumbe na Maalim Seif katika kuandika kwake.
Ila sie binaadamu tuna ila moja mtu afanye milioni moja mazuri akifanya mawili matatu tu mabaya basi yale mazuri yaliyokuwa mengi yote yanafichwa na yale mabaya yaliyokuwa machache.
Mie nakubaliana na J alivyosema kwani mangapi mazuri yaliyofanywa na Mheshimiwa aboud Jumbe hata amlaumu sana wakati yeye kaandika baya moja tu katika kusoma haya makala ya Bole kuwa alijenga kiwanda cha ulevi na nataka kusema kitu kidogo,kile kiwanda kama sikosei ni kiwanda cha sukari na manukato hiyo ulevi imo lakini katika matatu moja ndio lilikuwa baya ambalo linawezwa kuwa lisizalishwe kama kweli linaonekana baya,kwani hakuna viwanda vinavyozalisha kitu kimoja tu au viwili.
Mie natakakusema kukosea imo katika maisha ya binaadamu na ndio maana M.Mungu akaweka malaika wawili kwa binaadamu mmoja kuwa anaandika mema na mwengine kuandika mabaya, kwa kuwa binaadamu katika maisha yake atafanya lolote kati ya hayo.
Bole naona umeandika lawama Nyingi kuliko makosa uliyoandika kwa Mheshimiwa Jumbe, nakuomba tu kama ukitaka kuandika unatakiwa uache jazba za uCUF na UCCM uangalie huku na kule ili uwe muandishi mzuri.
MUNGU IBARIKI ZANZIBAR.
ndugu ole kwa hili maalim hasafishiki .lilosalia maalim mwenyewe akubali yaishe na tusahau yalopita kwani ushahidi upo na mashahidi pia wapo .
A/s
ndugi junius nakuunga mkono maoni yako mazuri naya nasisismua zaidi , umejibu vizuri sana b ole naona km kaingia maji hakutegemea hivo
mimi nataka kumpa kidogo kuhusu kiwanda cha pombe kilisha fungwa zamani tuu tokea awamu ya dr salimini kam huna habari b ole , nahayo madai kuwa km jumbe ndie alie aliye leta taswira zapombe sio kweli kulewa mtu ni nafsi yake tuu nahiyo pombe haikuanza enzi zajumbe usimzulie babu wa watu saivi kilamtu na balaa lake
A,alaykum ndugu wanamzalendo,
Kwanza, nianze na kisa cha Nabii Issa A.S. Siku moja akiwa amefuatana na wanafunzi wake waliuona mzoga wa mbwa. Wanafunzi wake wakaanza kutoa habari mbaya kuhusu mbwa yule. Sijui ananuka, sijui anaanza kutoka mafunza n.k. Ndipo Nabii Issa aliponyanyua sauti nakusema ” Uzuri ulioje wa weupe wa meno ya mbwa huyu!”. Wanafunzi wake walishangazwa sana na kauli yake hiyo, ndipo alipowajibu kuwa “Nyinyi muliyaona mabaya yake mukayaanza kuyasema nami nimeyasema yale yaliyo mazuri yake”. Tunachojifunza katika kisa hichi ni kuwa katika kumuangalia mtu au kitu lazima kutakuwa na mema na mabaya yake, mara nyingi watu hukimbilia kuyazungumza mabaya wakayaacha mema wakati hutakiwa kuyaanza yale yaliyo mema.
Nikija kwa Al-habib B.Ole, labda nikukumbushe tu kuwa ukweli ni kitu mbali na mapenzi ni kitu mbali. Mara nyingi tunapozungumza mambo yetu lazima tuuzungumze ukweli japo unakwenda kinyume na mapenzi yetu. Mada yako ya awali ya kuwataka wazanzibar wamchague Maalim Seif ilikuwa nzuri na nadhani ilikuwa inatosha kwa mtu mwenye fikra zake kujua ameambiwa nini. Mada yako ya leo haina mashiko hasa bali unaonesha utashi wako zaidi juu Maalim Seif.
Nafasi ya Maalim Seif kisiasa katika visiwa vyetu hakuna asiyeijua lakini pia tuelewe kuwa yeye ni binadamu kama binadamu mwengine, hivyo haifai kumtakasa kana kwamba hawezi kufanya kosa au hajawahi kufanya makosa. Ninavyoamini mimi kuwa katika siasa zetu ambazo tumekuwa nazo hakuna katika viongozi wetu waliopita ambaye hakuweza kuvikosea visiwa vyetu iwe kwa namna moja au nyengine. Hivyo si sawa kuwazamisha wengine na huku tukiwatakasa wengine.
Cha msingi na ambacho ni muhimu sana kwetu sisi wazanzibar ni kujengeana dhana nzuri na kuweza kuzizika tofauti zetu ambazo kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikituumiza takriban nusu karne sasa. Ningekuomba Alhabib B. Ole kwa moyo safi kabisa uisome vizuri na kuifanyia kazi makala ya Al-akh Ally Saleh inayosema “Tukiikoroga sumu tutashindwa kuinywa, au tuinywe tufe”. Kwani naamini wewe ni mtafiti mzuri sana ila wakati mwengine mapenzi yako yanakuwa juu kuliko ukweli.
Tumuombe Allah azikubali funga zetu na pia kutusamehe makosa yetu, ya wazazi wetu, viongozi wetu na waislamu wenzetu katika kumi hili la msahama.
Mungu Ibariki Zanzibar, Amiin.
Asalam alaikum wazalendo.
Mie nahisi hapa kwenye suala la Maalim Seif na wenziwe kuhusika na kadhia ya Jumbe, wafuasi wake wakubali tu. B. Ole anasema hoja za wenziwe hazina mashiko ila yeye anakuja na utetezi kwamba kwenye kuku wengi usimwage mtama, hayo ndio mashiko yake.
Nilikuwa nimejipa likizo kidogo kuchangia maoni hapa mtandaoni ijapokuwa huwa napitia makala kila siku ya Mungu, nahisi malumbano tu yamekuwa Mengi. Wengi wetu mawazo yetu ni ya kufungamana kiitikadi basi hata mwengine akijaribu kutoa hoja basi upande wa pili hauipi nafasi. Imekuwa kama mijadala ya muumin na atheist, akiambiwa kwamba Mungu hakuna asiloweza, akahoji, kwa hiyo anaweza kuumba jiwe kubwa hadi mwenyewe asiweze kuliondosha.
B. Ole, kubali tu kwamba binaadam sote tuna mapungufu, na Maalim Seif nae aliteleza hiyo 1984, alitanguliza nafsi yake over mustakbali wa Zanzibar. Tunaweza kumu excuse kwamba alikuwa mdogo kiumri, hakuwa na upeo wa kutosha wa kuona mbali kwa wakati huo, wakazidiwa kete na Nyerere. Istoshe, kama ni adhabu ya kosa hilo basi tayari keshaipata ya kutosha, maanake malengo yake kisiasa hayakutimia kipindi hicho.
Nawasilisha.
Karibu Shk.Mzenji, ni kweli muda umepotea MZALENDO.
Anyways, Zamani kidogo niliwahi kuandika makala yenye kichwa “Ni kweli M.Seif alitetea Muungano”.Hii maada haina tofauti sana na hii ya B.Ole kimantiki.
Nahisi Junius amejaribu vizuri kueleza kwa hoja zenye mashiko.Hili suala naomba tusilitizame sana kisiasa.Huko tutakuwa tunazungumza pumba tupu, personally naona M.Seif alichemka kisiasa kwenye sakata hili.Hata umtetee vipi kama alikimbilia kuepuka mauti, bado hoja yangu itabakia kuwa alichemka!
Sasa narudia tena hoja yangu kuwa tuache kushabikia siasa, na badala yake tutizame masuala kimaslahi ya taifa…kwa maana hio maslahi mbele, halafu siasa ifuate.
Reality tuna chaguo mbili Shein Vs Seif.Hapo la kutizama Zanzibar ina matatizo gani makuu na yupi yupo katika nafasi nzuri kuweza kufanikisha.Nitaanza na matatizo ya Zanzibar kwa wakati huu (sio huko kwenye historia).
1.Tunahitaji heavy renovation kama si kuvunja muungano kabisa!
2.Uchumi wa Zanzibar umebanwa kila sekta (tukiacha kodi za wauza ubuyu na samaki!).
3.Ushirikiano wa Zanzibar na jumuiya za kimataifa umebanwa kama si kufungiwa kabisa
4.n.k (you name it…the list is long!)
Jee, nani kati Shein na Seif yuko kwenye nafasi nzuri ya kurekebisha matatizo haya ???
Jibu langu licha ya kuwa nafahamu makosa ya Seif wakati wa Jumbe, bado namuunga mkono!Nadhani pia nina sababu za msingi za kumsamehe kihistoria na kudili na real issues on the table.
Mrfroasty nakubaliana na wewe mia kwa mia, kwenye hili. Mie narudia tena sijafungamana na chama chochote kisiasa, ila nina matumaini kwamba tutakuwa better off kama Maalim Seif atakuwa rais kuliko huyo dk. Shein.
Nasema hivo kwa sababu moja tu, hata dk. Shein awe na uwezo kiasi gani kiutendaji basi itakuwa ni sawa sawa na nyoka mwenye sumu kali alietolewa meno! CCM sio Zanzibar tu hata bara tushazoea lazima wawang’oe meno marais wao.
Besides, viongozi wetu wengi katika serikali tulionao hivi sasa wamejisahau kupita kiasi katika kutekeleza majukumu yao, its about time wananchi wawaoneshe kwa vitendo kwamba wamechoka.
Nawasilisha.
watu wakisema nami niseme
B Ole,
Kwanza naomba samahani kama nitakukosea,
Katika mkutano wa mwisho wa Maalim Seif, alisema hatopenda na chama hakitopenda, kuona kampeni za kukashifiana, (mwenzetu unaanza kwenda siko,)
Tafadhali usichezee kusi na tanga bovu
Usiingie kwenye ngoma usioijuwa,(Salmin Amour)
Kwasasa ni vizuri tukaleta makala za maendeleo na nini cha kufanya baada ya mawimbi na dhoruba tulizoziwacha nyuma kwani ukimchunguza bata utashindwa kumla
Kwahayo machache tu, tusitafutane undani
Ahsante
Assalam alaykum!
Bado B. Ole hajapewa hoja kama asemavyo yenye mashiko ya kumtia ila au kasoro Maalim Seif juu ya kadhia ya Jumbe kujiuzulu. Ni sawa na mtu kukuambia sikupendi, lakini kwanini hunipendi, ukasema sikupendi tu!
Nikichukuwa kauli ya Bwana Enzi Taalib, anasema “Huwezi kuyajuwa mambo ya CCM mpaka uwe ndani” Kila siku tunasoma mambo ya SMZ yalivyo kuwa yakiendeshwa. Tunaelezwa kuwa kabla Sheikh Abid Aman Karume kufikiwa na mauti, alikuwa haelewani na Nyerere. Ikawa Jumbe na mwenziwe mwengine wa Bara jina limenipita, ndio walio kuwa viongo baina ya Nyerere na Karume. Kwa hiyo misuko suko na dharba Jumbe alikuwa akiyafahamu a baina ya Nyerere na Karume. Jana nikaeleza kuwa aliyekuja kuimaliza Zazibar ni Jumbe na haya kutokana na wachambuzi wa siasa za Zanzibar. Karume hakusoma na baadaye akaja kutanabahi. Alhaj Aboud Jumbe amesoma, tena kule Makerere alikuwa hagusiki, lakini naye akaja akaichukuwa Afro shirazy Party na kuiunganisha na TANU na baya zaidi ati chama kikapewa mamlaka yote. Sasa mimi najiuliza nani aliyempa Nyerere nguvu hizo za kumuangusha Aboud Jumbe? Jibu mutatowa nyiye!
Ninavyo fahamu mimi wazo la serikali tatu si la watu wa Mapinduzi wala Nyerere. Kwa hiyo lile lilikuwa ni wazo la Aboud Jumbe Mwinyi pekee. Tayari Karume alikusha fanya makosa ya kujiamulia mambo kipekee bila kuwashirikisha wenzake. Na ajaabu ya Karume, kwenye harakati za Mapinduzi, yeye hakuhusika kabisa na wala hakuwa akijuwa, lakini yeye akaja kuwa na kibri. Mimi najiuliza, kama kweli Jumbe alikuwa na nia njema juu ya serikali tatu, kwa nini asiwashauri wenzake wa karibu alau wale wana Mapinduzi wenzake? Tusiwe wenye kuchapia matau tu, nila ya kuangalia mizizi!
Ukikosa bahati… Tunavyo elezwa, kuwa hizi nyaraka zilipatikana kupitia Khatib Hassan. Yeye kama usalama wa taifa aliyesomea huko Germany, ndiye aliye ziiba. Zikakabidhiwa kwa Dr Salimin , Amur, Maalim Seif na dr Salim Ahmed Salim. Hawa wakashauriana, jee tufanyeje. Hawa ni watu wanne. Wawili wanatokea Pemba na wawili kutoka Unguja, wote wakawafikiana hili jambo liripotiwe kwa Nyerere. Kwa hiyo kazi ikaanza kwa rashid Kawawa na baada yakamfika Sokoine na huyu ndiye aliye fikisha kwa Nyerere. Mimi hujiuliza, kwanini haisemwi, Dr Salim, Dr Salmin, Hassan Khatib na Maalim Seif ndio waliyo chafua lengo la Jumbe au ndio sababu ya Jumbe kujiuzulu. Lakini ahaa, Ni Seif tu ndiye mwenye damu ya kunguni, hawa wote chambilecho Junius ni Malaika! Maneno ya vijana, wee wacha si bure!
Tujaaliye Maalim Seif ndio mkorofi. Kesi ishafika kwa Nyerere na sasa anasomewa madhambi yake. Hawa wana Mapinduzi, akina bavuwai, Natepe, Kimara, Moyo, orodha ni ndefu. Kwanini hawakuweza kumtetea Jumbe? Unaweza kuona hili ni kosa lake Jumbe mwenyewe. La u kama angekuwa amewaarifu wenzake, basi yasingemfika haya. Makosa kama haya aliyafanya Karume na mwisho tena anatanabahi wapi, na kifo hicho. Kifo ambacho kinahusishwa na Nyerere. Zanzibar ni nchi, huwezi tu mtu mmoja kujiamuliwa mambo mazito kama haya. Karume alishindwa hata kumjulisha mwanasheria mkuu wake Judge Dourado. Na huyu naye akaja kumkwepa tena akaenda Ghana, yote nini kuficha siri. nakumbuka mara moja Maalim Seif aliwahi kuzungumzia kuwa alimtafuta huyu mtu na waliwahi kukutana Uganda. Ni Hadithi ndefu…
Lakini hebu tumuangaliyeni huyu Maalim Seif. Jamani huyu ni mtu wa maajabu! Kwenye CUF, tunaambiwa CUF ni Seif na Seif ni CUF. Hawa Dr Juma Duni, Prof Lipumba, akina Prof Msafiri, Dr Dedesi, akina Jussa wote ni bendera. Anachosema Maalim Seif wao hewala. Jee na wakati huo wa Jumbe huyu mtu alikuwa hivyo hivyo? Kuwa akisemacho ndio huwa ambri?
Kiasi B. Ole aseme hoja hazina mashiko. Mtu aasema akijali nafsi yake. Jee yupo mwenye kuujuwa msimamo wa Jumbe ulikuwa vipi? Jee munafahamu wakati ule Jumbe naye alianza kubadilika kiasi kwamba akaanza kuweka watu ndani bure bure? Sijuwi munafahamu licha ya yeye kuanza kuleta mabadiliko kwa kuweka chombo cha kutunga sheria, baraza la wawakilishi, ni JUmbe huyu huyu akaweka ndani vijana wa Muslim Brotherhood. Mmoja kaka yangu na mukitaka zaidi nendeni kwa Said gujwi mutapata haya. Jamani hapa musilete kauli za CCM. 2001 wameuwa watu karibu 100, wao wanasema hapana, ni 21 tu! Lakini hawa bado ni watu. Sasa na hapa wanasema Maalim Seif akilinda nafsi yake, jee wewe upo tayari kutowa nafsi yako? Jee munajuwa baada kumaliza hiyo moja ya Maalim seif, kuna uhakika gani kama asinge endelea na wengine?
Sheikh Ali Muhsin serikali yao baada ya kupinduliwa, wakawekwa jela miaka kumi. Baadaye akawa yupo Dubai. Kule licha ya kuwa alijihusisha na dini sana na kutafsiri quran na kuandika vitabu vingi vya dini, lakini bado akijali uwatani wake. Zanzibar ikimuuma, kwa hiyo alikuwa akitowa usgauri wake naakiisema SMZ. Jumbe kama kweli ana uchungu na Zanzibar, mbona kakaa kimnya? Jamani siasa ni lele mama. Hamujui nini kinaendelea. Kama kweli Maalim seif alikuwa adui wa Jumbe, leo hii wasinge kuwa marafiki!
Wakati naanza kuchangia kwenye ukumbi huu. Mwanzoni nikichukizwa sana. Kitu si kitu, pumba! kitu si kitu Maaalim Sef mnafiki! Kitu si kitu Mohamed Seif Khatib mnafiki!! Nikawa nasema jamaani hebu toweni ushahidi. Nilikuwa sieleweki, baadaye kidogo kidogo, hizi kauli zikapunguwa. Ukaja wakati wa maridhiano, yakasemwa mengi hapa. Sijuwi CCM hivi, sijuwi Maalim Seif kibaraka. Hakuna maridhiano. Unafiki tu, unafiki tu blah blah. Na si hapa tu, hata huko Zanzinet. Ikaja hoja ya Abuubakar, watu wakasema weee, wakaponda weee, sijuwi haipiti weee. Mwisho Maalim Seif hafai asigombaniye. Mara wengine mimi sina chama, lakini kwenye kuponda ni Maalim Seif tu, hapondi CCM. Sasa mambo yakaiva, hoja ikapita, maridhiano yakashamiri, watu sasa hawapigwi tena. Ramadhani ya uchaguzi wa 2005, watu walikula kisago kizuri, mara hii Alhamdullah. Mpaka sasa hivi hakuna aliyewekwa ndani, alhamdullah!!! Mpembahashiki, Mwenyezi Mungu mkubwa, katupa wawili badaka ya mmoja! Alhamdullah. Akipata Shein ni Mpemba, akipata Seif ni mpemba… Wale wapondaji na walio shika bango kumpaka matope Maalim Seif. Jee munawaona hapa ukumbini? Wengine wamehamia sijuwi jamii forum, matusi mtindo mmoja juu ya Maalim Seif…shabashy kuna mmoja anasema Maalim seif ana ajenda ya siri ya kuvunja Muungano, duh! mfa maji hata hajuwi akisemho.
Tunataka hao walio soma kitabu cha Jumbe cha “Zanzibar and Tanganyika pantership” watupe maalumati. Mimi sijakisoma, lakini walio kisoma, wanavyosema mule ameonesha kasoro nyingi tu za muungano huu wa Tanzania. Kwa hiyo siwezi kuzungumza chochote juu ya kitabu chake.
Tunatka busara kwa maslahi ya Zanzibar, kama alizo zionesa Mzee wetu Hassan Nassor Moyo. Yeye anakubali kuna makosa yalitendeka kwasababu hawakuwa wakielewa mambo zaidi kama vijana wa sasa hivi waliobahatika kusoma zaidi na zaidi. Kwa hii hoja ya Jumbe, itazungumzwa hapa hapa kwenye online, huko Zanzibar hatuisikii na wala hatuto isikia kwenye majukwaa ya siasa kwa nakubaliana na B. Ole hii hoja haina mashiko na kama ina mashiko, kwani haizungumzi huko Zanzibar kwenye majukwaa?
Salaam za Ramadhani!
Sina budi ila kumshukuru B.Ole kwakuileta mada hii, nakuwashukuru wale wote walikua wamechangia mada hii.
@B.Ole: kama ulivoeleza ujumbe huu umetufanya tuelewe nini kilichotokea baina ya Jumbe na Maalim Seif. kwanikama hukuandka ujumbe huu uliolenga (lawama chache kwa Alhaj-Aboud jumbe).Ndugu Junuis asingetufafanulia nini kilichotokea. nanukuu maneno yake.
“Tufikeni pahala ndugu Bole tukubalini kuwa Zanzibar kama taifa limepitia mikondo mingi ya majaribu. Kila zama zimekuja na mambo yake ya faida na yasiyokuwa na faida, mabaya na mazuri, ya kufurahisha na kuchukiza.”
Lakini nataka wenzangu wanielewe wazi kwamba B.Ole ni binadamu kama wengine. Kwahivo binadamu kukosea ndio maumbile yake. Na sidhani kama B.Ole atakua ameingia “MAJi” kama ndugu wengine wanavodai. Ila atakua amesoma makosa yake na kujirekebisha katika uandishi wa makala za mbele.Tukumbkeni kwenye mada ile ya Ally Saleh inasema kuna watu wakipenda kitu wanakua hawajifichi.
Binaadamu maisha yote tumo katika kutafuta Elmu. Na hapa mtandaoni pa Mzalendo ni vile vile. Tunapata elimu kupitia kwa wenzetu wanaojia historia ya Zanzibar very well kama Dr. Juinus.
@frasty: mambo ulioyaeleza ni muhimu lilobakia tuanze kupigacampeni ya kuchagua kiongozi ambae atalivua guo hili jeusi la ukandamizaji wa Visiwa na Maendele yake. Nalo ni Muungano,kama tunavjua waswahili husema ..”Ukupigao ndi ukufunzao”.
Hii inamaana kamba Maalim Seif anajua alifanya makosa fulani wakati wa Jumbe.Na hakua mpevu wa Siasa kama alivo leo.
Yeye ndie anaejua ni vipi zanzibar ilianza kutaka kujinasua na Muungano huu haramu. Na yeye ndie aneyejua jinsi yakuinasua zanzibar isimalizwe kumezwa na chatu Tanganyika/Tanzania. Ndio maana amejaribu tena kugombea uraisi wa zanzibar kwamatumaini ya kuiyokoa Zanzibar na Wazanzibar kwaujumla. Huyu ndie alepigwa na ameshajifunza.
Sasa wazanzibari tuache hitilafu zetu ila tuudumishe:
Umoja, Amani Na Utulivu tulioletewa na Vioongozi hawa. Idumu Zanzibar Wadumu Wazanzibari.
Bw Kassim una jazba, punguza munkar,
mimi sitosema lakini ya Jumbe na Seif ndio hayo kwa yayo maji ya futi kwa nyayo,
Kosa alilofanya Jumbe ndilo alofanya Seif,hapo ni kifupi tusitupe kuku kwenye mtama mwingi kwani atavimbiwa
Si Seif wala Jumbe isipokuwa wote wanajuwana mpaka Salmini na Kikwete, Sie tu tulio huku tunahemkwa,
Kwahiyo B ole na Kassim tugange lijalo,
Nateketea, Nadhani umekusudia tusimwage mtama kwenye kuku wengi. Umemaliza kwa maneno mazito ” Tugange yajayo” na tuyagange yajayo yaliyo pita si ndwele. Na ndio maana tukawa tunaungana na B. Ole kuwa hoja haina mashiko. Na wala hakuna Jazba, tunajaribu kuelemisha watu. Usitake kutafsiri aya za Quran kijuu juu tu, hutazifahamu. Tizama ya pili inasemaje na ya mbele imesema nini. Laa si hivyo utajizonga.
CUF ishazinduwa ilani yake. Kama unapigia kura CUF, fahamu hakuna ajenda ya kuvunja Muungano. Kwa hiyo ni vyema kusoma ilani hiyo vizuri, usije kusema CUF wamekuhadaa. Jimbo kwa jimbo tena nchi kavu…
Mara moja lilikuja ombi kule Zanzinet kutoka kwa Prof Ghuna wa Kent. Kila mtu ajieleze anajinasibu vipi uzanzibari wake.Alikuwa anataka kuandika kitabu kuhusiana na Zanzibar. lakini hatoweza kuandika mpaka apate hisia za watu. Lakini ilipita miezi bila kupata chochote.
Ndipo Hamza Rijal, akasema sisi Wa-Zanzibari kwa mdomo tu, ahaa umefika. Mtu atasema weee mpaka mapovu ya mate yatamtoka. Mpe karatasi aandike…! Mara moja vijana wa Chake Chake baada ya uchaguiz wa 1995, kila mmoja ukali, twataka kumuona Maalim Seif, ugomvi. Chuma kikatuwa Pemba, haya nishafika… ikabaki wajuwa maalim hawa CCM ni wash-nzi keli hivi hivi na vile… akaa zogo lote ni hayo tu!
Akija Ulaya ndio hayo hayo. Wengi wanao piga kelele na kulaani hapa, wakimuona uso kwa uso, hawa raised hizo issue zao zinazo wakereketa. Kubwa, kubwaa, kubwaa watasema Maalim Seif unajuwa CCM si wakweli! Nyinyi muko Ulaya, nchi huru kumuambia kiongozi lolote, basi safari yako yote kutoka ulipo toka kuacha ya kwako ya muhimu, basi hata humuulizi hili la Jumbe? Ndio ya waandishi, wataandika porojo kwenye magazeti kuhusu Seif na Jumbe, wakifanya mahojiano, hili hawaulizi! kuna nini hapa?
Bw Kassim au ndugu haya uwe
Mimi sitotafsiri Qur-ani kwa siasa hata siku moja, nimekwambia kuwa Seif na Jumbe wanajuwana siri yao wanaijuwa ila sie twapiga kelele tu hatuna tulijuwalo,tumo tu tunahemkwa
Mimi ndio kabisa sijuwi nisemalo wala niandikalo seuze ya Seif na Jumbe, halafu niandike Qur-ani kwa yao mmmhhh po simo. kwa hilo wala sitojizongapo kama kipole
Mimi nionalo ni sie kugeuzwa ngoma ya janjawidi kwa faida ya wengineo,
Nasema tena tusitafutane undani, tena naongeza tusitafute mchawi tutakosa mtotongwa na maji ya moto,
kwahiyo shauriyo
Nateketea,
Naona unaandika kimipasho pasho tu! Sijakuambia utafsiri quran ustadhi wangu. Nilicho kusudia, kuwa kuna watu hupenda kuchukuwa aya ya quran kutafsiri atakavyo. Na hivi ndivyo wakiristo wanavyo fanya. Kwa hiyo kuichukuwa aya kati kati au mwisho haitoleta maana. Kwa hiyo kuchukuwa ya Jumbe na Maalim Seif pale panapo kufurahisha wewe tu, ina kuwa ni makosa. Lazima uzame na uibuke na lulu kwa kutafusa chanzo ya yote hayo. Kwanini ghafla ghafla?
Ahsante sana mrfroasy/mzenji kwa nasaha zenu, kwakweli huu siwakati wa kulumbana. MALUMBANO haya; hayaleti faida yeyote isipokuwa ni kupoteza wakati wetu kwa kujibizana mambo yalopita ambayo huweza yakaturudisha nyuma na kututonesha majaraha ambayo yameshaanza kupowa.Lilopita limeshapita; sasa tugange lijalo.Jambo lakulumbana kiholela mimi nahisi sasa mbora tulipigie full stop [.]
Hakuna binaadamu mkamilifu wala alokuwa hawezi kufanya makosa ata iweje.
Yoyote alofanya makosa na akakiri; halafu akarejea kwa mola wake, basi
M/Mungu ni mwingi wa REHMA huweza akamsamehe na kumfutia madhambi yake.
Mimi shakhsiyya, nawaomba nyote WAZALENDO mutumie BUSARA NA HIKMA ilituweze kuweka upande tafauti na itikadi zetu. Sote hapa ni WAZANIBARI KHALISI KWA DAMU. Wahenga wamesema:- DAMU NI NZITO KULIKO MAJI. Kwahivyo yeyote yule atakayeteleza ulimi au kufanya MAKOSA, basi niwajibu wetu kumsamehe au kusameheyana.
Kwanini M/Mungu katuletea huu MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI?? Kwasababu alijuwa kuwa viumbe vyake vitaweza kufanya MABAYA AU MAKOSA na wengine hukiri wakarejea kwake [M/MUNGU] kwa hivyo mwezi huu umeletwa special kwa kuomba maghfra, kuomba toba kwa wale wanaohisi kuwa wamefanya makosa.
Na wengine watakatifu alowajaaliya M/Mungu huwa mashghuli sana katika hii dini yetu ili kujipaliliya hassanati na thawabu kwa wingi matumaini yao ni PEPO.Inshallah M/mungu atatujaalia waislamu wote waingie PEPONI.
AMEEN.
Ndugu zangu nyote WAZANZIBAR, hebu tukaye makini sana na tufikiri wapi tulipo fikia na iwapi NCHI YETU YA ZANZIBAR?? Mimi napenda kuwakumbusha kuwa NCHI YETU YA ZANZIBAR imeshazama kutoka kwenye miguu mpaka kifuani
sasa imebaki sehemu yakichwa tuu, tusipo amka kwa haraka tukaiokowa basi hata hii sehemu ya kichwa itazama NA WAZANZIBARI watabakia patupu. Wahenga wamesema:- mwenye macho hambiwi tazama. Tumepewa akili tuitumie kwa manufaa mema na faida itakayo tuongoza katika maisha ya kisasa, amani, utulivu, maendeleo na mustakbal wetu na vivyazi vyetu vinavyo kuja. Tuna myezi miwili tuu ilobaki kuelekea UCHAGUZI, kwahivyo chemsha bongo lako na uiokoe nchi yako ZANZIBAR.
NAWAKILISHA
RAMADHANI KAREEM
MUNGU IBARIKI ZANZIBAR.
a.alykm naomba niwashukuru wana ukumbu kwa kutoa hisia zeno kwa ujuzi mkubwa inaonesha kuwa mumekomaa ndugu wazalendo.nasubutu kusema alhamdulilah zanzibar tuna vipaji vya kutosha vinavoweza kudadavua mambo.naomba niwe mchangiaji wa mwsho kwa kutoa nasaha tu KWA KUWATAKA WAZALENDO NA WAZANZIBAR WOTE Tusiitumie historia kama nyenzo ya kurejesha ubaguzi na nivyema kuitumia historia kama ni chachu ya kuikomboa zanzibar kwa tukijiuliza nani wakulaumia? tutapata jibu kuwa ni sisi wazanzibar wenyewe ingawaje roho za vizazi vipya hazitokua radhi kwa kuwakosoa na kuwalaumu wazee wetu lakini tujua kua hata wao haligutuka na ikawa too late.lilobaki tumchagueni kiongozi ambye tunahisi ateuweka muungano ktk hali tunayoiridhia kwani huu waleo anayeumia ni kina vuai,machano,hamadi na yusuf lakini kina kamugisha,mangi,mbonile na mdigo wanaufurahkia.nawatakieni kila la kheri mungu ibara unguja,pemba,visiwa vilivyo vizunguka,bahari ya hindi yake na watu wake.allah give us light.ameen ramadhani njema
Njinji watuwazima wa zamani msitutushe kwa kuandika historia za zamani na watu tusio wajua, Jumbe, nyerere, nk,
Tunachokitaka ni maoni ya Zanzibar mpya, Zanzibar mpya, Zanzibar, Ukombozi wa zanzibar amboa wakombozi wake ni mimi na wewe na maalim Seif kwani ni kiongozi pekee alioe weka wazi, msimamo wake kuhusu Zanziba na kujenga muungano bora kwa pande zote mbili..
Zanzibar haijulikani kama nchi, Tunazalilishwa hata kufika viongozi wa siasa kusema kama muungano ukivunjika ni Wazanzibar ndio watapata shida(haya ni matusi).Nimeishi nchi za nje, marekani,latini,asia,ulaya, sehemu zote hizo wanajua kuwa Zanzibar sio nchi bali ni mkoa katika mikowa ya Tanzania,,
Zanzibar mpya ni sisi turudishe hadhi ya Zanzibar na tuko tayari kuwaonyesha watu kama tunaweza kujitegemea,Tutakuwa bega kwa bega na kiongozi wowote atakayekuwa na msimamo wa kuikomboa zanzibar kama Vile Seif Sharifu kwani ameweka wazi katika maelozo yake,(Zanzibar,Tanganyika,Tanzania)
Jumbe yuko hai kama Seif, kwa nini Jumbe asitueleze msimamo wake kuhusu Zanzibar huu ni wakati mzuri sisi vijana tukapata kumfahamu? (THESE ARE BIG FISH, TRYING WANT EAT DOWN THE SMALL FISH)
Mimi niko tayari kuijenga Zanzibar mpya na kama utaniuliza kwa mfumo huu wa muungano uliokuwapo sasa ni mzuri?
Jibu langu laaa, na siutaki huu muungano,,
Je wewe? shauri yako…
Jamani ee
Naona kama tunapiga hatua za nyuma sasa, jee ndio lengo?
Tunaanza kutafutana huyu hivi yule vile, sivyo hivyo na wala haitokuwa ndivyo
Tunasema tupige mstari wa yaliyopita haya tupigeni, lakini isiwe tena aaa mbona huyu mzuri na yule mbaya, hapo hatutokwenda
Kama tunataka Zanzibar njema hebu tuwacheni hizi choko choko, na haya maneno eti walisema madai ya Jumbe kuhusu Seif sio kweli au hata iwe kweli, jee tuanze kuhukumiana sasa?
Nasema hatutoweza na wala hatuwezi kupiga hatuwa ikiwa tutakuwa nayo mawazo kama hayo,
Nilisema hapo juu tugange lijalo, na tusitupe kuku kwenye mtama mwingi, kusudi tukizidi kutupiana maneno wenzetu wa mrima ndipo watakapoona ala kumbe hawa ni moto wa kifuu?
hebu tupunguze jazba, naona kila mtu kakusudia, jamani tutizame nini mustakbali wetu tusirudishe ya Jumbe na Seif hayatutofalia kwa sasa zaidi ya kutugawa
Kwenu Wanaukumbi.
Kwanza kabisa napenda kuchukua nafasi hii kuwa shukuru wale wote waliochangia mada hii. Hii ni kuonesha kwamba kweli Wazanzibar wanauchungu na Zanzibar yao.
@ Pili niungechukua nafasi kumpongeza Sheikh KASSIM kwani yeye anaelewa kwa kiasi fulani ni kitu gani kilikuwa kimejificha katika kadhia hii. Baadhi ya wachangiaji hawaelewi ni siri gani ambayo Jumbe alikuwa ameificha nyuma ya pazia.
Sishangai kwani uhuru wa kusema na kuandika ndio kwanza unapatikana sasa, Na mpaka hii leo kuna watu bado wanaogopa kuzungumzia ukweli kwani wanakumbukia enzi zile ukisema hakuna chumvi dukani ukalishwa gunia mbili kule kwa bwamkubwa.
@Junius nashukuru kwa maelezo mazuri ambayo umeyatoa pia nachukua nafasi hii kukupongeza sana lakini bado mimi nasimamia kauli yangu ile ile kwamba Madai ya kujiuzulu Jumbe, zidi ya Maalim Seif hayana msingi wowote.Bado hujatoa ushahidi wenye mashiko.
Bado hakuna hata mmoja alie toa hoja za msingi kuhusu hili, tunachotaka ni hoja sio malumbano. Kama kweli Jumbe alikuwa na nia kuleta SERIKALI TATU kwa nini hakuwashirikisha Wazanzibar wenzake na wakati huo Siasa baridi ilikuwa imeshamiri visiwani. Kama hilo ni kweli nitajieni mtu mmoja ambae alikuwa anaujua mpango huu wa Jumbe halafu tujenge hoja.
Sheikh Junius inaonekana wewe huzielewe vizuri siasa za Zanzibar na kule zilikotokea. Ningekushauri ukatafute REF. kwenye gezeti la Dira au kama upo hapa Zanzibar basi jaribu kumfuata mtu anaejulikana kama ALI NABWA atakupa picha yote juu ya kadhia hii kwani yeye alikuwa akimfahamu vizuri Mh.Jumbe wakati wa uongozi wake.
Iko siku mada hii nitaizungumzia kwa kirefu lakini Narudia tena kwamba Mh. Jumbe hakuwa na nia nzuri bali alikuwa na malengo tofauti na Wazanzibar wenzake na hii ndio iliomfanya asiwashirikishe Wazanzibar wenzake. Jumbe aliendesha SERIKALI kimapinduzi mapinduzi licha ya usomi wake lakini alijua fika kwamba alikuwa anaandamwa vikali na Wasomi wa Zanzibar katika Serikali yake kwa vile hawakuridhika na jinsi ya muelekeo wa Zanzibar kupelekwa Bara.
Wazalendo nia ya kuikomboa Zanzibar haikuanza baada ya vyama vingi . Siasa baridi ilianzia tokea baada ya Mapinduzi ya sitini na nne. Wazanzibar wenye uchungu waliliona hilo tokea enzi zile na harakati zilianza kuitafuta Zanzibar. Maalimu na kundi lake walifanya harakati tokea wako kwenye Serikali ya chama kimoja.
Sasa leo hii kwa vile watu hawajui ni kitu gani kilinachoendelea mara nyingi huchukua kesi za maskani na kusema kwamba Maalim ndie alisababisha yote haya , lakini ukweli hawataki kuutafuta chanzo kilikuwa nini.
Wazalendo kundi la kuipigania Zanzibar liliongozwa na Pande mbili za watu wa Wazanzibar yaani Wpemba na Waunguja. Katika kundi hili na DR. salmin bin Amuor alikuwemo na hata baadhi ya mikutano ilikuwa ikifanyika kwake kwa siri, Pia Dr. Salim Ahmed Salim, Seif Sharif, Mzee Machano,Hassan Khatib alikuwa mtu wa Usalama,Alhaj Pandu na wengine.
Ukiangalia hapo utakuta kuna mchanganyiko wa Waunguja na Wapemba kwamba wote walihusika. Kilichotokea ni kwamba baadhi yao waliwageuka wenzao kwa kufuata maslahi yao binafsi na kupatikana makundi mawili makubwa.
Kundi moja la Maalim Seif na wenzake lililoendelea na mapambano huku kundi la Dr. Salmin na wenzake wakafuata madaraka na ulwa licha ya kujua kwamba nchi inapotea na hapo ugomvi kati Unguja na Upemba ukaanza kupaliliwa.
Nani aliekuwa hajui kwamba Maalim Seif na DR.Salmin walikuwa marafiki wakubwa ? Wazalendo toeni hoja zenye mashiko sio hadithi za vijiweni. Hawa watu wengine wapo hai Zanzibar ni ndogo fuatilieni ili mupate kujua ukweli hasa ni kitu gani.
Narudia tena kama kweli JUMBE alikuwa na nia njema kwa nini hawakuwashirikisha Wazanzibar wenzake na wakati huo Baraza la Wawakilishi lilikuwepo kwa nini hoja haikuletwa Barazani kujadiliwa ?
Unataka kuniambia kwamba maamuzi makubwa kama hayo yana fanya na mtu mmjoa akishirikiana na Mwanasheria wa kukodiwa, mbona hili haliingii akilini Wazalendo. Hivi enzi hizo tuseme Zanzibar kulikuwa hakuna watu waliosoma sheria mpaka akodiwe mtu kutoka nje. Nasema tena leteni hoja zenye mashiko ?
Kwa mtowa mada mimi naona niayake ni kumsafishia mtu ili aonekane mwema miongoni wa wananchi kwa hilo hana kosa kwasababu hayo nimapenzi yake juu ya huyo mtu,lakini ikiwa tutarudi nyuma hayo madai yanayodaiwa kuwa huyo mhusika kayafanya basi yote yanaukweli kuwa kayafanya hata na hili la kumpinga marehemu iddrisa abdulwakil alipokuwa rais wa zanzibar kufikia kuitwa jina ambalo mimi siwezi kumuita yote hayo ilikuwa nimsukumo wa kiongozi huyo.
Chamuhimu sasa hivi yote hayo tuchukulie yame pita na hakuna binaadamu mkamilifu sote tunamapungufu yetu japo ukweli utabaki kama niukweli na uwongo utabaki kuwa ni uwongo.Nakutakieni ramadhan njema.
@B.ole,
Kwa heshima na taadhima naomba tusiende kwenye malumbano hasa kwa kadhia hii ya Seif na Jumbe. Sikatai kuwa sizifahamu siasa za Zanzibar,licha ya kuwa nimezaliwa, kukulia, kusoma Zanzibar, wala sikatai kuwa kuna watu wanajuwa kadhia hii zaidi ya mimi ninavyoifahamu,ila tunapopata nafasi kueleza kiasi ya tunavyoifahamu basi tujitahidi tusiingize itikadi na ushabiki wa kisiasa, kama tunakusudia kuwaelimisha watu.
Zaidi,umenishangaza kidogo wakati unasema mimi sizifahamu siasa za kwetu,wewe unaonyesha mwenyewe kuwa hata hayo yanayoendelea zanzibar huyafahamu vizuri, hivi unajuwa kuwa ALI NABWA ni marehemu? na gazeti la DIRA halipo tena? au sijakuelewa vizuri unaposema nimtafute ALI NABWA na kufanya rejea gazeti la Dira!
Angalia sasa, wakati unashikilia na kukataa kuwa Maalim Seif hakuhusika na kujiuzulu Jumbe, wakati huo huo maelezo yako yanakubali. Kumbuka ulitumia neno “kuhusika”. Mifano umetoa(rejea malezo yako vizuri)ya “uhusika” wake, umeeleza uhusiano wa harakati hizo zidi ya Jumbe na Maalim alivyo play role, sijuwi uhusika upi umeukusudia wewe tufafanulie tafadhali.
Bole, umeongea kitu muhimu katika kufanya utafiti kuhusiana na rejea(references).Hii ni muhimu ila unapofanya rejea angalia kuna za namna nyingi. Kubwa zao ni rejea zinazopatikana vyanzo vya awali (primary sources) na zile zinazopatikana kwa mkondo wa pili (secondary sources).
Hizi za mwanzo watafiti wanazichukulia kuwa ni za kutegemea zaidi (reliable) na hizi za pili ni muhimu kwa kuwa awali zimeshafanyiwa tafiti nyingine. Hata mambo ya historia yanataka tafiti za kina na rejea za uhakika na kutegemea, siyo tujisemee tu.Nilieleza hapo juu kuwa nilisoma maelezo ya Jumbe mwenyewe (first hand information) na yale ya Maalim Seif kadhalika kama rejea.
Ukinambia nimtafute ALI NABWA (ambaye hivi sasa ni marehemu) au nifanye rejea gazeti la Dira (ambalo halipo)nakuwa sikuelewi. Kwa mfano ingekuwa, Mzee Nabwa na Dira, bado vipo. Kumbuka hivi vyote viwili vinajenga kada ya kihabari. Na katika utafiti wa kihistoria si vitu vya kutegemea moja kwa moja kabla ya kufanya utafiti kwa vyanzo vya awali wa awali, hawa wanakuwa wameripoti tu.
Ningetemea kwanza unambie kuwa nimfuate Maalim Seif, Jumbe na wale wote waliokuwa bado hai ambao walishiriki kadhia hiyo, au maandiko yao, na siyo wale walioripoti tu kama NABWA NA DIRA.Nakubali kuwa vyombo vya habari na wanahabari wana nafasi yao katika kufanya rejea lakini si wakutegemea sana kwakuwa si mara nyingi wao kuwa primary sources.
Jengine muhimu, umekuja na hoja mpya sasa, kuwa kwanini Jumbe hakuwashirikisha wenzake katika mpango wake na kwanini hakuipeleka hoja hiyo barazani na hata akakodi mwanasheria wa nje?
Anaeweza kujibu vizuri masuala haya ni Jumbe mwenyewe. Ila usisahau hali ya siasa ya wakati huo na aina ya jambo lenyewe.Jumbe alishasema kuwa ndani ya serikali yake kulikuwa na makundi yakivutana, maalim anaunga mkono dai hili la Jumbe na kukiri kuwa misuguano ilikuwapo kwa kundi lake kuitilia shaka hatua ile ya Jumbe. Hivyo,Jumbe alikuwa na sababu ya kuwa mwangalifu katika hali ile, nakubali kuwa huenda alikosea kwa kutojiridhisha na hofu yake, japo ilim-cost.
Aina ya jambo lile ndugu Bole, halikuwa lakupelekwa baraza la wawakilishi, ni suala la kikatiba, na mahakama ya katiba ilikuwapo, Jumbe kama rais kama mwananchi alikuwa na haki kuandaa petition hiyo. Mazingira ya kiadui, mivutano, kutoaminiana na usaliti, haya yote yalimfanya Jumbe awe kuliko mwangalifu na achaguwe watu maalum kufanikisha mpango wake,mmoja wapo ni Ramadhan Haji Faki, aliyekuwa msaidizi wake nambari moja.
Labda tukubaliane kitu kimoja Bole,hili jambo linataka tafiti zaidi kuliko gazeti la Dira na waandishi wa habari pekee. Vyanzo vipo vya uhakika zaidi. Ninachokusisitiza unapotazama mambo hayo usiingize itikadi na ushabiki wa siasa. Hapa unaweza kuja na matokeo mazuri ya utafiti.
Sote tunampenda Maalim Seif na tunatamani awe kiongozi wetu kama kesho, lakini Maalim Seif ni binaadam, tusikatae mapungufu yake kama tunavyokubali mema yake ambayo ni mengi tu.
MUNGU IBARIKI NCHI YA ZANZIBAR
J
huu mjadala ni mzuri lakini tu hatari yake ni kwamba utaexpose mengi ambayo kwa wakati huu wa mariadhiano sio mazuri kuibuka.ningewaomba wachangiaji hasa kwa heshima na utukufu wa mwezi wa ramadhani tusitishe mjadala huu kwani ni mzito mno na kama yakianikwa hadharani mambo basi yatakua kuliko shubiri hayamezeki.
tukubalini yaishe,tugange yajayo.
Ndugi yangu Junius, nataka nikuvuliye kofia kwa maelzo yako. Maelezo kama haya ungeyatowa tokea awali, basi B. Ole hata sisi wengine tungefahamu vizuri. Lakini mwanzoni naweza kusema kama ulitaka kumsafisha Jumbe na kumkandamiza Maalim Seif kama vile wengine walifahamu hivyo kuwa B. Ole anataka kumsafisha Maalim Seif na kadhia hii.
Na tuzidi kufanya tafiti. Tuwaulize wahusika. Kwenye kufanya tafiti si lazima uende kwa muhusika. Kama ni hivyo basi mengi yangeshindikana. Dira limefungiwa lakini kopi zake zipo hata hapa Mzalendo zipo. Na hiyo habari anayo zungumzia B Ole nayo ipo na hivi karibuni niliwahi kuisoma hapa hapa ukumbini. Marehemu Ali Nabwa alikuwa muandishi mashuhuri kwa Zanzibar na naweza kusema hakuna anaye mpata na yatapita miaka kumpata mtu kama yeye. Ana kipaji cha kuandika na bongo lake lilikuwa likifanya kazi vizuri.
Mimi nafahamu misimamo ya Maalim Seif. Si mtu mwenye kuweka kinyongo. Naamini kama Jumbe amemfanyia makosa Maalim seif, basi Maalim Seif amesha msamehe halikadhalika Jumbe. Kwasababu najuwa ni watu wanao sikilizana vizuri tu. Laini kuna hawa wachapiaji na wazushi. Mmoja naona kashanza kuleta habari za Idris Abdul wakil na Maalim Seif. Masikini hajuwi yaliyo pita baina ya Maalim Seif na Almarhum Alhajj Idris. Nadhani lengo lake ni kupotezea watu muda na malengo. Hapati mtu hapa.
Kuna wengine wapo Jamii forum baada ya kuona hapa hawajafanikiwa na mada yao ni hii ya Jumbe & Seif… Masikini roho zao. Tuko kwenye maridhiano. Na ulimwengu unafahamu hilo. Salamu za kheri na baraka kila kona ya ulimwengu huu zinakuja Zanzibar. Inshallah baada ya oct 31, 2010 nguruma zitasikika mpaka maziwa makuu kama wasemavyo. Watu wamesha amua kuacana na tafauti zao na kuamua kujenga nchi yao.
SHUKRAN NA AHSANTENI SANA WATOAJI MAONI JUU YA MADA HII. KWA KWELI YOTE
MAONI YALOTOLEWA HAPO JUU NI MAZURI SANA NA YA KUSISIMUWA.TUMEYAFAHAMU
KINAGA UBAGA. KIFIKRA NA YALIVYO ELEZWA; BASI TUYAMALIZIE KUWA WOTE WALIFANYA MAKOSA.NI JAMBO LIMESHATOKEA NA LIMESHAPITA.NIMFANO WA MAZIWA YALIYOMWAGIKA HUWEZI KUYAZOWA NA UKIJARIBU KUYAZOWA, BASI UTAZOWA TOPE.
NDUGU ZANGU NAWAOMBA TUYAMALIZE HAPA YALIVYO FIKA, YATOSHA SANA. NA KWAKWELI HAWA TUNAOWAHUJUMU KWA MAKOSA YAO, NI WAZEE WETU, WENYE UMRI MKUBWA NA SIHAYO TUU, BALI WENGINE WANAUMWA MARADHI YA MOYO, PRESHA NA
MARADHI YA KISUKARI, HATARI YAKE NI MMOJA WAO AU PENGE WOTE KWA UJUMLA
KUJAKUTEMBEA KATIKA COMPUTA ZAO NA KUONA VIPI WANAVYO HUJUMIWA, HUWEZA WAKAPATA KIHORO CHA MFAJJA’A NA HAPO YAKATOKEA MENGINE YASIORIDHISHA
KWA JAMII YETU, NA HUENDA LAWA ZIKAWEZA KUANGUKIA KWA WATOWAJI MAONI.
SIHIVYO TUU, BALI TUNAWEZA KUUPOTEZEA SIFA HUU MATANDAO WETU.
MIMI NA MUOMBA MR.B.OLE, UKINAFASIKA UFANYE UTAFITI WA VIPI TUTALINDA HAKI ZETU WAKATI WA UCHAGUZI, HATUWA GANI ZICHUKULIWE ILI TUIOKOE NCHI YETU. AHSANTE SANA.
NAOMBA M/MUNGU ATUTAKABALIE DUA ZETU, SALA ZETU, SAUMU ZETU NA ATUFUTIE MADHAMBI YETU NA ATUPE HUSNI KHITAM WAKATI AKITUHITAJIA NA PEPO IWE NI MAKAZI YETU YA DAIMA.
AMEEN.
NAWASILISHA
RAMADHAN KAREEM
MUNGU AIBARIKI ZANZIBAR.
Ameen Ameen Ameen!
s/a
@junius asante kwakunisomeshea b ole inaonekana alikimbia darasa kidogo huyu , manake kazoe kuandika utumbo hapa
Aslm Alykum Waungwana.
Kwanza natumia nafasi hii kumpongeza mwandishi wa makala hii,kwani pengine bila ya yeye kuleta makala hii,sisi wengine tungeendelea kuonekana ni wasaliti kwa yale tuliyokwisha yaeleza huko nyuma juu ya matatizo waliyonayo viongozi wetu wa kisiasa Maalim Seif akiwa mmoja wapo.
Pili napenda pia kuwapongeza wachangiaji kwa kuonesha mwanzo wa kupevuka katika utowaji wa maoni.Nasema ni mwanzo wa kupevuka kwasababu katika kuchangia jambo hili wengi wa wachangiaji ambao wamekuwa na tabia ya kupinga jambo kwasababu ya mapenzi tu waliyonayo kwa mtu,na siyo kwa hoja,kwa mara ya kwanza wameonesha kuunga mkono ukweli.
Pamoja na kwamba wengine wameendelea kuwa ving’ang’anizi na walemavu wa mawazo,ninachoridhishwa nacho kuwa ukweli wa mambo uko wazi,na wenye masikio wamesikia.
@Junius:Pengezi za dhati kwako kwa maelezo yanye ufasaha na uliobebwa na miongozo ya kitaalam katika kuelezea namna ya utafiti unaopelekea katika kupata usahihi wa mambo.Kama B.ole ni mja wa kutaka kujifunza asiyoyajua basi amepokea mafunzo na kama ni wa ubishi na ang’ang’anie.
NAKUBALIANA NA KILA MWENYE WAZO LA KUACHA YALOPITA NA KUGANGA YAJAYO KWA FAIDA YA NCHI YETU YA ZANZIBAR.
Lakini sikubaliani na yeyote anayejaribu kutushawishi kuwa eti tusilijadili hili kwa kuhofia kuvuruga mshikamano.Kujadili jambo hili kutasaidia kutupatia faida zifuatazo:-
1.]Kuwa na tahadhari juu ya kuwaamini moja kwa moja viongozi wetu wa kisiasa.Jambo ambalo litachochea kuamua kuweka sheria za udhibiti wa viongozi hao pale wanapofikia kudhani kuwa mawazo yao pekee ndio yenye maamuzi ya mwisho juu ya hatima ya watu wanaowaongoza.
2.]Kuepukana na tabia ya kuwaona viongozi kama malaika jambo linalowapelekea kuwa na kiburi,hali ambayo matokeo yake ni kuzaa udikteta na kudharauliana.
Napenda pia nitumie nafasi hii kuwataka baadhi ya wachangiaji watueleze kile hasa wakitakacho au wanachokusudia pale wasemapo juu ya neno “HOJA ZENYE MASHIKO”kwani nikionacho mimi ni kuwa wanaodai jambo hili ndio wao wanaofanya kinyme chake.
Hoja zilizotolewa na @Junius zinahitaji yule ambaye ni muumini wa mila na itikadi ya ukaidi na ubishi uliokithiri ili aweze kuzipinga.
Ima kwa wale wanaojaribu kutukataza kutoangalia yalopita wana sehemu fulani ya kukubalika kwa mawazo yao kwa maana tu ya kuganga yajayo,bali maelekezo ya muumba mbingu na ardhi yanatutaka tujifunze kwa yaliyokwisha pita.Hii itatusaidia kukasimu nguvu ya madaraka ya tunayemkabidhi madaraka,awe Seif Sharif,Shein na yeyote yule.
Kuna aliyedai kuwa wapo wenye maneno mengi na vitendo zero,nakubaliana naye,lakini pia ni vyema mukaelewa kuwa pia kuna udhaifu mkubwa wa kumuepusha Sheif Sharif na wauliza maswali wanaoonekana kuwa ni wakorofi.Nalisema hili kwa ushahidi kwani mimi binafsi yalishanifika hapo LONDON pale CUF ilipoingia muafaka mwingine na CCM baada ya uchaguzi wa 2000 na baadae kuja kuwaeleza wazanzibari wa UK ni kwanini alikubali kuingia katika muafaka huo.Wahusika walianza kwa kuuliza,yule ni nani na harakati zikaanza kuhakikisha kuwa sitauliza swali lolote maana mmoja kati ya marafiki zangu wa karibu si kwa nia mbaya bali kwa ari na jazba ya kutaka kusikia nini Seif Sharif atakachojibu,akaponyokwa na moja kati ya maswali niliyoyaandaa kwa mmoja kati ya waandaaji wa mkutano ule.
Ndipo mkakati ukawekwa kuwa wahakikishe kuwa sitomuuliza Maalim hata swali moja.
Huu ni ukiritimba unaoendeshwa na baadhi ya watu ambao kwa ujinga wao wanadhani wanamsaidia Maalim bali wanamuharibia yeye na sote kwa ujumla.
Kwasababu mimi nafahamu majibu ya Maalim Seif kuhusu tatizo lake na Jumbe ndio maana nikakubaliana na maelezo ya @Junius,lakini endapo bado watu wanahofu na maelezo hayo Bado Maalim Seif ana nafasi ya kutupatia jibu la swali hili.Mtandao huu bila shaka yeye anaujua na anajuwa kila kinachojadiliwa humu.
Kwa kuongezea ni kwamba miongoni mwa maelezo aliyoyatowa kuhusu kushiriki kwake katika kuuvuruga mpango wa Jumbe Sheif Sharif alisema kwamba Aboud Jumbe alitaka kuyafanya hayo katika wakati usikuwa muafaka,lakini kwa bahati hakutupatia maelezo juu ya wakati gani ni muafaka kwa hisia zake yeye.
Huu ulikuwa ni moja kati ya udhaifu wake.
Wazalendo tunachotafuta hapa si malaika au nabii bali kiongozi,ni vyema tukachagua kiongozi anayekubali udhaifu wa njia tulizikwisha zipita kabla zikatuangamza,nakiri kuwa utafutapo mtu huyo kati ya tulionao basi pa kumpata ni ndani ya chama cha CUF,awe Duni,Seif,Hamad Rashid nk.Seif Sharif anatufaa lakini ni vyema tukakiri udhaifu wake kama Jumbe na binaadamu mwengine yeyote yule.
Wachangiaji katika mada hii kwa hakika wamechangia kwa mitizamo tofauti na hisia totauti. Inabidi uwe na maarifa uweze kuchambua.
Kwa ufupi mkutano ule ambao Mhe. Aboud Jumbe, ilitangazwa kuwa amejiuzulu nyadhifa zake zote alizokuwa nazo, Serikali na Chama. Ulikuwa ni mkutano wa Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM. Zipo minutes, wasemaji wote waliyochangia sakata la Mhe. Jumbe, walinukuliwa na taarifa za kila mjumbe zipo mpaka leo.
Mimi kwa jicho langu, nilisoma maelezo ya mkutano mzima na taarifa zote za wasemaji yaani wachangiaji wa pande zote, wale walioshadidia ubaya dhidi ya Jumbe na wale waliyokuwa pamoja na Jumbe, kumtetea.
Kuna kundi la akina Maalim Seif, Ali Haji Pandu, Juma Othman, Hamad Rashid, Khatib Hassan na wengi tu. Hili lilikuwa dhidi ya Jumbe.
Kundi lililomtetea Mhe. Aboud Jumbe, walikuwamo Ramadhan Faki, waziri kiongozi wa mwanzo wa Zanzibar, mara baada ya kuundwa kwa Baraza la wawakilishi. Yeye Ramadhan Faki, ndie aliyemwambia Nyerere 1+1=3 kitu ambacho kilimkera sana Nyerere.
Baadhi yao waliyokuwamo katika hili kundi la Ramadhan Faki, kumtetea Mhe. Jumbe ni pamoja na Seif bakar na wengine wengi na baadhi yao waliwahi kuweka kwa muda katika vifungo vya nyumbani ili kupisha kuchafuka kwa hali ya hewa.
Mimi kumbukumbu za mkutano wa tokeo lile nilizisoma kupitia mmoja wa wajumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa CCM. Mheshimiwa huyo, ambaye alinipa kitabu hicho cha kumbu kumbu, ilikuwa katikati 1984, alikuwa ni Katibu wa Chama (CCM) Kusini Pemba.
Ninachotaka kusema ni kuwa huu mjadala kwa sasa hauna maana, bora tuuwache. Sababu maelezo ya watu wote waliyosema katika mkutano ule bado yapo, yanaweza kuamsha aina nyengine ya watu kufanyiana chuki. Sababu maelezo ya pande zote mbili yanatoa hisia si zakawaida. Jamani a jamani iliyopita si ndwele.. tugange lijalo.
@mrfroasty,
TUNAKUOMBA Utufungie maoni tafadhali sote tumeelewa vya kutosha nani anatufaa kuwa kiongozi wa zanzibar mpya, yenye dhamira mpya na matarajio mapya YALIOPITA SI NDWELE, ‘INSHAALLAH TUTAFIKA..
ramadan kareem…
@mtu kwao hasahau
kwanini maoni yafungwe au ukweli unauma?take it like man. boy!!wacha watu wadibate watakavyo.
@junius na hokani
ahsanteni sana kwa hoja zenu ambazo zilikuwa breathtaking wow!!.jamaa mmempa darasa la kutosha kama hajafahamu kazi kwake huyu jamaa anaejiita ole kwakweli kajidhihirisha yeye mwenyewe kwamba mabanda hamna na kama kasoma basi nafikiri either kichwa maji au kifuu tundu.cha ajabu sijui anaishi dunia gani hata ashindwe kuelewa ali nabwa amefariki dunia na gazeti la dira halipo tena.ama kweli ukipenda basi chongo utasema makengeza.upenzi wako wa maalim umefuturu ada.maalim seif yeye mwenyewe kakiri lakini wewe unamkatalia.
@b.ole
nakuomba ungefanya research kwanza kabla hujaandika huo utumbo hapo juu niliwahi kukwambia before kwamba uko over bias .nashukuru hata hao cuf wenzio wameliona pia
Jamani ee hamujasikiapo wale jamaa zangu waloangusha mnazi kwa kuhesabu makuti?
nawengine wasema baraatu mpemba si ntumbatu basi hata umkekete hakubali, ndo nayaona leo
Mtu kila aambiwalo yeye ashikilia tuu
hebu tumpishe bilisi na ramadhani hii, haya makala mengine maudhui yake ni nini hasa ? si kutafutana huku,
Nasema ya Seif na Jumbe tuwaachie Seif na Jumbe ila kama tunataka kuyajuwa tusije tukatafutana mchawi nani,
Kosa la Jumbe ndilo lile lile alofanya Seif
Kuchamba kwingi…….
UKIMCHUNGUWA BATA HUWEZI KUMLA
Mimi hushangazwa na baadhi ya watu. Wao mada wanazo penda zile za magovu govi mikaruzano. Ukisoma hayo maoni yao utaona wanatoka nje ya mada.
B Ole ameandika kitu na akatowa hoja zako. Junius akasoma akaona kuna makosa yamefanyika na yeye akatolea maelezo na sis wengine tukanadika tujuwavyo. Kuna tulio jaribu kutafuta chanzo ya yote hata yakajiri, kuna wale walichapia chapia bila kutowa hoja yeyote ya msingi. Hawa wengine inaonekana mada za B Ole zilikuwa zikiwachoma siku nyingi, kwa walipo pata mahali pakutolea joto lao wamepapata wakaingia mkumboni.
B. Ole kasikiliza maoni yote mwishowe akamjibu Sheikh Junius kwakistarabu na kwahoja. Kwa upande wa Junius, kwa vile alitaka kuandika kwa hoja akakubali kukubaliana kwa baadhi ya mambo na kusema sote tuna hitaji kufanya makosa kwani haya mambo ni mazito na bado hatuyajuwi. Sasa hiyo darsa anayo pewa B Ole ipo wapi.
Mwenye kusoma hakai akajigamba, huinuwa kalamu na karatasi na kuandika. Kukaa ukasema mwenzako hajasoma hiyo haitoshi. Andika makala kamili kujibu hoja. Kama B Ole inaomekana kuegema upande wa Maalim Seif hebu wewe andika ya upande wa Jumbe. Nyinyi si watoto wa ASP/CCM? Lazima mutakuwa munajuwa kwasababu watu wenu walikuwa jikoni.
Zanzibar watu wamepeya kisiasa, wacha mjadala uendelee. Uhuru wa kusema ni moja ya tawi la demokrasia makini. Hii haito haribu maridhiano wala haito muharibia Maalim Seif kwenye kampeni zake. Amejipanga vizuri na fomu tayari kasharejesha.
Sheikh Junius na kaka yangu B. Ole mjadala na uendelee. Kuna watu wanapalilia mambo. Wanataka kuonesha kwamba wawili nyinyi munashambuliana, kumbe kinyume chak munaeleweshana na mumefikia tamati kuwa natufanye tafiti zaidi. Na imedhhirka hivyo kwenye maoni yenu, kila mmoja kwenye kujibu amejaribu kurudi kwenye hoja. Shabashy hivi ndivyo ninavyo penda mijadala iende. Sio neno si neno pumba, neno si neno mnafiki… neno si nenoatabeba msalaba!
Kassim
Tafadhali usijibirue kama pweza aliyekikaangoni,
Hivi kusema nyinyi ni watoto wa ASP wazee wenu wankuwa jikoni manaake nini hasa?
B ole kafanya tafiti kwenye Dira basi, kapewa tafiti za huyo Sief kwenye maneno yake mwenyewe na tafiti za Jumbe kwenye kitabu chake alichokiandika mwenyewe, sasa wewe bado wasema ooh hakuna mashiko, nikuulize wataka ushahidi wa mnyamwezi?
Haya nauliza tena hivi wewe unayesema ulitafuta chanzo cha yote hata yakajiri, hebu nipe hicho chanzo chako,
Nami nakuuliza moja la muhimu kuliko yote hayo niloulizapo hapo mwanzo Hivi Jumbe alipoezuliwa wewe abaa ulikuwa wapi na ulikuwa na umri gani?
ukinijibu hilo kilillahi na saumu hii, ndipo tutaweza kuyajadili mengi mengineyo
aloo n’shakomaa! sitii langu neno… maana hili jina lako limekusibu… wateketea kweli kweli. Huwezi kunipa ambri ya kutaka kujuwa umbri wangu na wapi nilikuwepo. Vile vita vya badri na vyengine wewe ulikuwepo? Mbona unavijuwa na uavielezea kwa ghibu…! Nina hakika na ujumbe huu utatafuta pakutia ila na mipasho! Maasalama
Weye@MUUNGUJA umemwambia @b.ole nanukuu.hata hao ma cuf wenzako wanakukosoa.samaha sipingi itikadi ya mtu bali ninashangaa kumbe wewe ccm!lahaula wala kuwwata ila bilah.KUMBE NI MIONGO YA WALOPINGA KURA YA MAONI KWA KUSEMA HAPANA?jamani huyu jamaa tumuepukeni kwanh hana mema na zanzizibar mpya.inaonesha yuko tayari wazanzibar sote tufe but union should stand still.i am runing away,bs i am afraid tha guy.mungu awabariki wana ccm na wana cuf wote pamoja na kuwajalia hao wachache ccm waingie cuf kuliko na sera za uwazi haki na usawa.ramadhani njema
Abaa wantia ngeu, waniangusha hivi,
haya, naona mjadala ushaufunga na hata jua halijatoka.
nakupa mji uende machomane uwe juu ya pigili usije ukadaswa na kipole kwani yuwaja
shauriyo
Kuhusu suala la Jumbe mimi sitaki kumtetea hata mmoja. Najua jambo moja tu Mwenyezi Mungu kasema Dua ya mtu aliyefunga na aliyedhulumiwa hairudi. Vile vile naelewa ya kwamba mtu anapomdhulumu mwenzake, anapotataka kutubu kwa mwenyezimungu basi inabidi kwanza amuombe radhi yule aliyemdhulumu na ikibidi amrudishie haki yake ndiyo baadaye atubu kwa Mwenyezimungu. Mimi kwa maoni wote waliotumia madaraka yao vibaya wakafuja pesa zetu za uma waje hadharani watuombe radhi sisi wananchi waliotudhulumu na sio wakae majumbani wakilia, halafu tukatokea watu wazima tukamsemea Muungu uongo kuwa keshawasamehe watu hao ameshawasamehe wakati yeye hajasema popote.
Mimi kuhusiana na Kufukuzwa kwa Jumbe ilikuwa kafara yake mwenyewe aliyoifanya 1981. Watu watauliza ni kafara gani?
Watakaokumbuka vizuri mwaka ule kulinunuliwa meli mbili na sherehe za ufumbuzi zilifanyika Pemba. Jambo baya alilolifanya matayarisho ya sherehe zile yalifanyika mwezi wa Ramadhani, yaani shule zote za Pemba tulichezeshwa ngoma mwezi mzima kwa ajili ya matayarisho. Jambo la pili baya Sherehe zilifanyika Siku ya Sikukuu (siku ya Idi). Wanafunzi tulitolewa majumbani mwetu asubuhi saa 12 asubuhi hatukuwahi hata chai kunywa sikwambii kusali Idi. Tulichukuliwa tukenda tukafungiwa Geti Wete bandarini kuanzia asubuhi tukichezeshwa ngoma mpaka saa kumi alipokuja Mheshimiwa baada kusali Laasir. Walisahau kuwa na sis ni Binaadam hata Maji hawakutupa sikwambii kula ya mchana. Tulirejeshwa Majumbani kwetu wengine saa 8.00 za usiku hata chakula kilichobakia kilikuwa kineshaliwa daku kwa ajili ya kufunga Sita. Yaani walitufungisha Siku ya Idi siku mbili mfululizo. Mimi ni mmoja niliyesema siku kama kweli mwenyezi mungu yupo basi atatulipia hapahapa duniani. Na kweli hakumaliza hata miezi 6 alitolewa. Mimi ni mmoja tu lakini kuna maelfu kama mimi walioteseka siku ile walio na wakaomba dua kama hizo. Kama dua ya mtu mmoja aliyefunga hairudi jee ya watu Elfu moja? Nafikiria kuna watu kwenye mtandao huu ambao wanaikumbuka siku hiyo wataungana na mimi.
Tunaelewa vile vile mikataba ya Kujenga Karakana pesa zililiwa vipi, Tunaelewa huo ununuzi wa meli ya kwamba yalikuwa mameli makongwe yaliyotiwa rangi tu, Tunaelewa mkataba wa ujenzi wa njia ya Bububu, Tunelewa ni huyo huyo Jumbe aliyenunuwa Jeti akawa anafuturu Saudia na Daku Zanzibar. Hizi ni pesa zetu mimi na wewe na hatujamsikia hata siku moja akituomba radhi. Jee wewe utakapofika siku ya hisabu ukaja ukaambiwa limebakia jema moja tu ingiye peponi jee utakubali ajaziwe yeye na wewe utumbukizwe motoni? Misamaha yote watu lazima wasameheyane hapa duniani huko kutakuwa na hisabu nyengine na atakuwa tayari kuwatosa jamaa zake na familia yake yote alimradi aokoke yeye, Seuze Jumbe aliyekuwa akipeta kwa pesa zetu?
Pole sana ndugu yangu wamtambwe ila unaelekea kuigeuza mada. Jumbe hakuna asielewa kwamba utawala wake ulikuwa na mabalaa chungu nzima, ila nahisi kwenye mada hii sisehemu yake. Anaejadiliwa ni maalim Seif kwa vile ni mgombea urais, Jumbe is irrelevant.
Jumbe kama Jumbe tumuache kwenye historia, huo mkasa uliopelekea Jumbe kulazimishwa kujiuzulu umeelezwa kwa vile alikuwa katika harakati ya kuitetea Zanzibar, tukisema kwamba maalim alimsaliti Jumbe, issue sio kwamba alimsababishia Jumbe kupokonywa urais, ila ubaya ni kule kukwamisha hatua ya Zanzibar kujinasua na muungano mbovu.
Suala linalohitaji kujibiwa hapa ni kwamba, kama kweli maalim na wenzake ambao wamo katika harakati za kuomba nafasi za uwongozi walishiriki kukwamisha hatua hiyo, walifanya hivo kwa sababu gan na kama ni kosa je wanakubali walifanya makosa, na wanamikakati gani wakipewa nafasi kuhakikisha warekebisha hayo makosa? Usijarib kujustify uovu wa Jumbe kwamba ndio ilikuwa halali kwa maalim na wenziwe kutounga mkono hiyo petition.
Nawasilisha.
Assalam alaykum!
Hii mada ni nzuri. Ni nzuri kwasababu inaonekana kuwavutia wengi. Imekiwa mithili ya mpiga zumari; pale alipulizapo, huweza kuwatowa nyoka pangoni. Ni ujuzi mkubwa kuweza kumtowa nyoka pangoni kirahisi kama hivyo, sijuwi kuna siri gani. Na hapa likipulizwa zumari hili lijulikanalo Maalim Seif kumsaliti, huwatowa wengi pangoni, kuanza kucheza kwa mbwembwe kama fanyavyo nyoka.
Kuna baadhi ya wenzetu walio bahatika kupata kuingizwa kwenye daftari la kuduma la kupiga kura, ikifika oct 31, 2010, watapata fursa kwenda kuwachaguwa viongozi wao kuanzia udiwani, uwakilishi, ubunge na hata Rais kwa Zanzibar na Muungano. Ni vyema kufanya chaguzi lililo sahihi kwa kumjuwa yule unaye mpigia kura, na sio kupigia chama tu. Kwasababu hujuwi athari zake.
Wengi wa wagombea wetu ni watu ambao tunawajuwa kwa kitambo>Na ni wau ambao wapo kwenye uongozikwa siku nyingi. Kuanzia serikalini na sasa wakiwa nje ya serikali. Ni vyema kujifunza na makosa yao. Si busara kumchaguwa kiongozi msaliti na hsa kama takuwa amefikia kuisaliti nchi. Kesi kama ya Maalim Seif ni shutma kubwa na kama ina ukweli inapaswa kuzingatiwa. Makosa yasijirejee, ameweza kulifanya hilo, akiwa waziri tu, jee akipewa Urais anaweza kuwa mtu aina gani?
Nisinge penda kumuhukumu moja kwa moja, kwa hiyo langu kubwa kujisomea tu mani ya watu. Hivi huyu mtu na usomi wake na uzanzibari wake kindaki kindaki, Mpemba fyoko, aliwaza nini kuisaliti Zanzibar kiasi hichi? Wallah kila inapo zungumzwa hii mada, bado sijapata maelezo ya kina, kwa vipi huyu mtu pwuuu kuja tu na uwamuzi huu! Manaake yataka mtu uwe umekwaruzana na naye kwa kitambo au kuna tishiyo kubwa la kweli kweli na sio tu udhani likifanyika hili, huyu jamaa ataniweka ndani na nitasahaliwa huko huko! Mhh bado mimi naonakuna jambo hapa, japo iwe kuibiana na wanaawake unajuwa tena viongozi walivyo!!!
Msaliti huyu na kibaraka cha Nyerere, naona alikuja kuwa mashauri mzuri wa Al hajj Ali Mwinyi. Akaja kumuunga vizuri kwenye azimio la Zanzibar. Ikawa Zanzibar ni njema atakaye na aje. Akaja kuwa msimamizi mzuri wa sera yao ya mtakula. Mabondeni alikuwa hatoki. Karafuu bei ikapanda. Ikawa twaambiwa ukichupa pishi tano mia mfukoni… Zanzibar ikawa Dubai ya Afrika. Uhuru wa kusema ukawa umeimarika. Almarhum Abdul-wakil, akafanya naye kazi vizuri, licha ya kuwa aakipkea shindikizo la kumuondoa madarakani, kama asemavyo mwenyewe Maalim Seif… Akaenda jela, huko huko tunaambiwa aliweza kuandikakurasa zisizo pungua arubaini juu ya vyama vingi. Tuambiwavyo tume ile, iliyapa uzito wa pekee maoni ya msaiti huyu na ikapita jamba jamba kwa vipi aliweza kuandika maoni yote haya yakaweza kutoka nje! Jamani huyu mtu mimi ananitatiza kweli.
Vyama vingi tayari vishakuja. 1995 uchaguzi ukafanyika kwa mujibu waCUF na mkurugenzi wa tume ya uchaguzi Aboud talib ni kuwa Maalim Seif ameshinda kwa asilimia isiyo pungua 60% Na Kwa mujibu wa Salim Juma Othman, kuwa Maalim Seif alishinda lakini matokeo yalibadilishwa kwa kumshauri Nyerere. Waliopigiakura wengi ni watu wanao mfahamu Maalim Seif akiwa ndani ya serikali, kwa hiyo unafiki wake wakiulewa vizuri sana, lakini ajabu ameweza kupata asilimia hiyo ambayo kwasasa kwa lugha ya CCM ni ya kishindo! Na tujaaliye hiyo 49.2 ya SMZ, lakini bado ni kubwa kwa msaliti huyu kuweza kuipata.
Miminadhani wasaliti ni wengi. Kama wewe mpiga kura, unajuwa unaye mpa kura ni msaliti na bado ukazidi kumpa madaraka. Basi na wewe uwa ni msaliti. Wasaliti miminadhani wapo wengi. Tulikuwa tuna kiti chetu umoja wa Mataifa na nasikia mpaka leo kipo, sema hakikaliki kwa mavumbi! Nani aliyesababisha yote haya? Mimi nadhani ni wana Mapinduzi akiwemo Jumbe. Sasa kaa tunaambiwa ya Jumbe tusayazungumze kisahapiganii urais, bas wazo langu mimi si vyema kumuachia msaliti huyu Maalim Seif kukamata urais. Mnafikini mnafiki tu. Mtume (S.A.W) wakati anaondoka, kuna asahaba kumi aliwacha usia wasipewe uongozi na sababu kubwa ni kutokana na UNAFIKI wao, ikaja kusaidfu Saydina Omar (R.A) akamchaguwa mmoja wao, lakini bila ya kujijuwa, alipatataabu sana kusikia hivyo, mwishowe Mwenyezi Mungu akamjaalia akaweza kumuondoa mnafiki huyo na akwa amefauli kw ahilo.
Kwa hiyo oct 31, 2010 ni siku adhimu ya kufanya maamuzi. Huu ni wakati wa uwazi na ukweli. Tumeyasikia ya Maalim Seif na vituko vyake. Kusomesha wapemba, kuisaliti Zanzibar nk nk. Ikifika siku ya mamuzi kura yako weka panapo stahiki. Na mimi hasa nataka waweke kwa Dr Shein. Huyu hana majungu, mpole, mtu safi, hana magurupu, zaidi ya yote msomi aliye bobea kwa hayo machahce tu, kweli Maalim sif anampata huyu mtu? Tusiangaliye chama, tuangaliye mtu mwenyewe na uwezo wake. Sio kazi haki, sawa huku ndani ya nafsi yake mchafu….
Kidumu chama cha mapinduzi, ushindi juu kwa Dr Shein, zidumu fikra za Mwenykiti na baba wa taifa…
@ kassim naona swaum imekulevya kiasi ambacho hujui hata unachoandika.
Wazalendo huyu jamaa tumuache kwani anataka kuturejesha ktk mjadala ambao tumesha ujadili na umesha malizika.
Wanaume hufanya jambo likamalizika banaa ukiona mtu anarejea mzozo ushaosuluhishwa basi jua ni mwanamke au anatabia za kike.
Maelezo ya @ kassim hayafahamiki na yamekalia kinafiki hivi ukilinganisha na maelezo ya siku za nyuma.
@Mzenji
Ahsante, you sound so philosophical
@Bosco
Ni sawa unavyosema kwa kiasi, bali waungwana hawakashifiani,tunaweza kueleweka vizuri tukijieleza bila ya kushambuliana. Then, hapa mimi binafsi sijaona hicho unachokiita “mzozo” katika mada hii ndiyo maana tumejitahidi sote kujadili kwa ustaarabu kadiri tulivyoweza,ingawa tone zilipana wakati fulani. Hivyo sioni tatizo kama mjadala utaendelea kama kuna mambo ya faida zaidi kuelezana.
J
@kassim:Pamoja na kwamba ulichoandika ni kiswahili,bali kwa mtazamo wangu nahisi kuwa bado kunahitaji tafsiri.
Wengine nadhani wameharakia kwa kusema kwamba Ramadhani imekulevya,mimi sina hakika na hilo.
Kupinga au kukubali ulichoeleza kutategemea tafsiri uliyokusudia.
Lete tafsiri Maalim @kassim.
-Hokani, hicho ni kiswahili… kama unanafasi soma tena na soma maoni yangu ya nyuma nadhani unaweza kuelewa nini nakusudia.
-Bosco maoni yako ni mazuri na yanafaa kuzingatiwa. lakini kumbuka mwanamke wa karne hii ana haki ya kuskiliza kwenye mambo a siasa. Kwenye U-islamu, Basi Mtume wetu (S.A.W) alikuja kumkomboa mwanamke na kuwa huru tokea kuja wake.
-Mimi nishaeleza msimamo wangu na nishakupa wapa ushauri wenzako nini wafanye na wewe una uhuru huo huo wa kusema utakalo. Na wasomaji kama Hokani wenye kutaka kujuwa mambo watauliza kwa pale ambapo hawajafahamu.
-Hokani, naam usemavyo ndivyo hasa, kukubali na kutokukubali ni maamuzi ya mtu binafsi.
- Kwa upandewangu nimefikia maamuzi ya kumpigia Dr Shein, baada ya kusoma maoni mengi hapa juu ya Maalim Seif kuwa ni msaliti, ni mtu mweney kujali nafsi yake. Kwa kuchukuwa tahadhari, ndio nikaona kuepusha mengine makubwa, kwani huyu mtu asikaye nje ya serikali. Nadhani nilikuwa na maana hiyo kma nayo itaeleweka.
@kasim
mwanzo nilikufahamu kwamba wewe si mmoja waliopata bahati ya kuandikishwa katika daftari baada ya kuona hiki ‘nanukuu’
Kuna baadhi ya wenzetu walio bahatika kupata kuingizwa kwenye daftari la kuduma la kupiga kura, ikifika oct 31, 2010, watapata fursa kwenda kuwachaguwa viongozi wao kuanzia udiwani, uwakilishi, ubunge na hata Rais kwa Zanzibar na Muungano. Ni vyema kufanya chaguzi lililo sahihi kwa kumjuwa yule unaye mpigia kura, na sio kupigia chama tu.
na mwisho ukasema nawe pia utapiga kura siku hiyo! labda tuweke sawa hapa inawezekana sikukuelewa mimi tu; hapa ulipoandika ‘
- Kwa upandewangu nimefikia maamuzi ya kumpigia Dr Shein, baada ya kusoma maoni mengi hapa juu ya Maalim Seif kuwa ni msaliti, ni mtu mweney kujali nafsi yake. nategemea ufafanuzi kutoka kwako @kasim
-Mimi kamwe sipo Zanzibar na kwa mujibu wa taratibu za zec basi mimi sina sifa ya kupiga kura. Hizo ni mbwebwe tu za uandishi. Lakini kama ningepata nafasi basi namjuwa nani wa kumpa kura yangu. Hata hivyo napenda kukushukuru kwa lugha yako ya kistaarabu. Kwa hiyo yule juha mmoja nataka afahamu kuwa kumbe bado kuna watu wanasoma maoni yangu. ha ha ha
-Kwasababu yashaelezwa mengi na kwa kipindi hichi licha kuwa kunfanyika kampeni, lakni wao tayari washajuwa na wakumpa kura, labda wale watu ambao husema mimi sifungamani na chama chochote, hawa wanaweza kuwa mpaka sasa hivi hawajajuwa na wa kumpa kura. Jambo ambalo siamini kuwa kuna mzanzibari ambae hana chama. Kama si mwanachama, basi unamapenzi na chama fulani. Ukisikia mtu anakuambia sina chama juwa huyo ni CCM, anajaribu kujifcha tu.
-Kwa kumalizia, mtu kwao hasau, mimi na ujuha wangu basi kura yangu simpi Dr Shein, wala CCM yeyote. Ile ni kuwafurahisha Makada tu. Wewe sifa zote nilizo oredhesha juu ya Maalim Seif bin Shariff bin Hamad al-shirazy na ushupavu wake, nikashike maneno ya mitaani keli kan’saliti Jumbe, sijuwa wajuwa huyu mtu mbinafsi. Sijuwi kasomesha Wa-Pemba, sijuwi anataka kuvunja muungano. Kura yangu kwake ni michango yangu kwa chama, kimawazo na kifedha.
Kwa hayo machache, nadhani ndugi yangu nitakuwa nimekusaidia, kama bado hujaridhika na maelezo yangu, usichoke kuniuliza na inshallah nitakujibu kwa kila nukta yenye mashaka.
-Kidumu chama cha Mapinduzi na fikra za mwenyekiti!
nanacho amini mimi kamani kweli au vipi pamoja na timu yooote iliyoshiriki hebu kamuulizeni tunae mwita Dr Salimini Amur walio taka kumpiduwa Jume alikuwa yeye na nani halafu walipo feli ninani na nani walio tiwa ndani kwa kesi ile baadae yeye Salimini akiwa ndiye kiongozi wa wenziwe mikutano mingapi yasiri dhidi ya Sirikali ya Jumbe nayeye ndiye mtendaji mkuu wa hayo baada ya kushindwa hayo ndiyo akampata nani atamfunga paka kengele kama nikweli ndiyo Maalim akamfunga namzigo huu mpaka leo umeuangukia allahu yaalam asante sana