Makala/Tahariri

Mafuta na gesi: Zanzibar imefunikwa tena vumbi la macho ?

Zitto Kabwe :

Kwa mujibu wa habari kutoka blongi mbali mbali za bongo, Zitto amechapa :

Kesho jumamosi wabunge tumealikwa kwenye semina kuhusu sera ya Gesi Asilia. Tumegawiwa tayari nakala zetu, tena zipo kwenye lugha ya kimombo.Ikumbukwe kwamba kuanzia tarehe 22 – 23 Mei 2013 kutakuwa na mjadala wa bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini. Semina hii ni maandalizi ya Bajeti hii.

Jambo la kushangaza ni kwamba wakati sera ya Gesi Asilia ipo kwenye rasimu na ndio kwanza wabunge tumeletewa kutoa maoni, Serikali tayari imetangaza tena kugawa vitalu vya Mafuta na Gesi kwenye Bahari kuu na Ziwa Tanganyika Kaskazini.

Zabuni hii mpya ya vitalu vya utafutaji imetolewa wakati kuna maamuzi ya Bunge kuzuia ugawaji huu mpya mpaka sera ya Gesi Asilia na Sheria ya Gesi vikamilike.
Haraka hii ya serikali kugawa vitalu bila sera wala Sheria inatoka wapi? Nitashangaa sana wabunge kukimbilia posho za semina hii na kuhalalisha maamuzi yasiyo zingatia maslahi ya Taifa Kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Uamuzi wa kugawa vitalu vipya bila kwanza kuwepo Kwa sera na Sheria mpya unapaswa kupingwa Kwa Nguvu zote.
Tafuta mbunge wako, mwambie asikubali maamuzi haya ya serikali.Tumalize kwanza sera na Sheria ndio tugawe vitalu vipya. Gesi sio viazi, haiozi.

Kwa mujibu wa utafiti wangu mfupi, mwishoni mwa mwaka 2012 Balozi Seif alitoa habari kuwa serekali ya Zanzibar imefikia makubaliano kuondosha suala hili kwenye orodha ya mambo ya muungano.Ahadi ilitolewa kama sijakosea, basi ni kuwa suala hili litasimamiwa chini ya serekali ya watu wa Zanzibar.Hii ni habari sote tuliokuwa tukiomba dua na kufurahi kuisikia.

Nimejaribu kadiri nilivyoweza kuipata rasimu hii mpya ambayo itajadiliwa na wabunge bila ya mafanikio.Nimefanikiwa kupata Draft I, ambayo nadhani namba 3 itakuwa ni muendelezo na uboreshwaji.Kinachonishangaza na kunipa mshtuko, haya makubaliano ya Dr.Shein na raisi Kikwete hayako kwenye maandishi wala katiba.Haishii hapo, hii rasimu ambayo inajadiliwa na wabunge wetu haina sehemu (jisomee mwenyewe pia) haina sehemu inayotoa maelezo ya kisheria kuhusiana na makubaliano ya maraisi hawa.

Kila ninapozama deep katika nyaraka hizi, napata hisia hasi.Zanzibar imefunikwa tena vumbi la macho ?

Share: