Makala/Tahariri

MUDA UMEFIKA WA KUUTAZAMA TENA MUNGANO WETU NA KUREKEBISHA KWA PALE USIPORIDHISHA

MUDA UMEFIKA WA KUUTAZAMA TENA MUNGANO WETU NA KUREKEBISHA KWA PALE USIPORIDHISHA.

Leo ni tarehe 26 April. Miaka 53 iliopita Viongozi wa wili kutoka Tanganyika na Zanzibar walikubaliana kuunganisha mamlaka mbili huru na kuifanya kuwa nchi moja inayoitwa Tanzania.

Tuzungumzie CHIMBUKO LA WAZO HILI KWA LEO HII NA KIPI CHA KUFANYA ILI KUIDUMISHA.

Suala la kuunganisha nguvu mbili ili kupata jambo moja kubwa na bora zaidi si jambo baya. Ni jambo jema ambalo huwezi kuliepuka kulinganisha na kanuni ya maumbile na maendeleo ya dunia yetu ya sasa.

Tukubali kwamba hakuna nchi inayoishi katika dunia ya pekee. Na hakuna nchi kwenye falsafa hii hii inayoweza kuishi kama kisiwa. Kwa maana ya kwamba, vipo visiwa vinavoishi ndani ya dunia hii lakini bado havijajitengenezea dunia ya kisiwa chake. Hii inamaanisha kwamba sote tunategemeana. Mwanadamu mmoja anamtegemea mwengine, hivyo hivyo nchi moja pia inaitegemea nchi nyengine katika kuendelea kuwepo kwake na maendeleo na/ usatawi wa watu wake.

CHANZO CHA MUUNGANO.
Vipo vyanzo mbali mbali vinavyonyesha kutokea kwa au kuwa ndio sababu halisi ya kutokea kwa Muungano wetu huu.

Ukiwachia mbali suala la udugu na mahusiano ya karibu baina ya watu wa Zanzibar na wale wa bara, hususan watu wa mwambao wa Afrika ya mashariki. Historia inatufunza kwamba kulikuwa na maingiliano ya kiimani, familia na uchumi yaliojengeka baina ya watu wa visiwa hivi na wale wa pwani ya Azania. Hata kabla ya kuzaliwa kwa Kristo( Nabii Issa A.S). Hii inaonyesha kuwa tulishaungana mioyoni na mwilini kabla ya tukio hili adhiim.

Pili, mwanzoni kabisa mwa miaka ya ukombozi Afrika kulikuwa na wazo la kuifanya Afrika moja yenye kiongozi mmoja. Kwa maana ya kwamba nchi yoyote itakayokuwa huru basi itakuwa huru kujumuishwa kama ni sehemu ya nchi moja kubwa iliochini ya mtawala mmoja. Ndoto hii ililenga kuanzishwa kwa United States of Africa- U.S.A.

akati wa kipindi hicho kulikuwa na viongozi wawili mashuhuri ambao walikuwa ni icon ya ukombozi wa Afrika. Naweza kusema kuwa viongozi hawa walidhamiria kujenga Afrika moja yenye nguvu. Katika kuliendea jambo hili mambo mawili yalijitokeza ambayo yalikuwa ndio matatizo /kikwazo na kupelekea kutokufanikiwa kwa dhamira yenyewe.
1) Magwiji wawili walikutana kwa wakati mmoja. Hakuna mabwana wawili na/ mafahari wawili wanaoweza kukaa kiti kimoja. Dr. Kwame Mkuruma (rais wa kwanza wa Ghana na Mwalimu. J. K. Nyerere. (Rais wa kwanza wa Tanganyika.

Watu wawili hawa walikuwa na tofauti ya mawazo na walitatizana.
A) Dr. Kwame Mkurumah aliamini kwenye ya haraka iwezekanavyo. Kwa maana ya kwamba nchi zote zilizokwishakupata uhuru zianze kuyakabidhi mamlaka yake kwa rais wa Afrika na zile ambazo bado zinapigania kujikomboa basi zisaidiwe ili zikomboke na ziunganishwe kuwa majimbo ya nchi moja kubwa.
B) Mwalimu J. K. Nyerere, aliamini katika mchakato. Kwa maana tuanze kidogo kidogo kwa kuanzishwa kwa jumuiya huru za kikanda na hatima yake ni kuziunganisha na kufanya nchi moja.

Katika idea hii basi watu wakajikuta katika mkanganyiko mkubwakwab i wawili hawa wote walionekana kuwa na maslahi yao binafsi walioyaficha chini ya mioyo yao na kushindwa kuuyaweka wazi. Hasa suala la NANI ATAKUWA RAIS WA AFRIKA? MAKAO MAKUU YASERIKALI NA na mfano wa hayo.

Baada ya sitofahamu hii Nyerere aliendelea naj uhudi zake za kuidumisha idea yake na kuanza kuwashawishi viongozi wa afrika ya mashariki akiwemo Mzee Karume.

Kwa maelekezo na msaada wa Marekani na ingereza (rudia kitabu cha PRAGMATISM OR PAN-AFRICANISM cha Shivj) Nyerere alifanikiwa kuyafanya mapinduzi na hatimaye kuinganisha Zanzibar na tanganyika na kupekea Zanzibar kuendelea kusahaulika na Tanganyika kujuilikana kama ndio Tanzania yenyewe.

Kwa hofu ya kupoteza mamlaka zao nchi kama Kenya walionekanaku sita sita kujiunga na EAC na hatabaada ya kuabguka kwa hile ya awali bbaada ya vita vya amin na nyerere, viongozi wa Kenya walionekanakushere hekea jambo hili kwa mizinga ya shampeign.

MAONI YANGU.

1) Jambo la umoja na msikamano ni jambo jema sana. Ni kwetu kuutunza Mungano huu kwa kutazama mapungufu na kuyafanyia kazi.

2) Mda wa kuutazama upya mungano huu umefika. Waliouasisi hawakufanya jambo baya. Ilikuwa ni hatua ya awali iliofaa kwa wakati huo. Ni kwetu kuamua kwa kinachotufaa kulingana na mahitaji na wakati. Muungano wa kisiasa umepitwa na wakati.

3) Raia wapewe nafasi ya kusema aina ya muungano na vitu vya kutunganisha ili kila mmoja awe ameshiriki katika kujenga nyumba yetu inayonekana kuchakaa.

Nihitimishe kwa kusema mambo mawili.

Hali ya sasa ya mungano huu ni kama mama mjamzito alifikia kujifungua. Kama mama atajibana na kumzuia mtoto huyu asitoke basi mama atajidhuru na mtoto atadhurika.

Pili. Si kweli kama kuna mtu au kikundi cha wat u wasioutaka muungano huu bali wengi wetu haturidhishwi na aina hii ya muungano. Kama hatua za haraka hazitochukuliwa basi tusitarajie kama kelele hizi zitaisha.
Tukae nakukumbuka “ngoma huanza na hailele hailele”

TUNAHITAJI MUNGANO WA KIUCHUMI ZAIDI YA MUUNGANO WA KISIASA.

UHURU BILA YA NGUVU YA KIUCHUMI NI HEWA.

MUNGANO USIOLETA MAENDELEO YA KIUCHUMI NI KUTAFUTIANA UGONVI USIO NA HAJA.

Mwenye busara husikiliza anayoambiwa.

AL-HABSHY.

FB

Share: