MUUNGANO NA UENEZAJI WA UKIRISTO ZANZIBAR!

Written by  //  27/04/2010  //  Makala/Tahariri  //  6 Comments

Ningependa kutowa mawazo yangu machache kuhusiana na huu ukoloni uitwao muungano.

Nimekuwa nikijiuliza kwa nini wenzetu wa tanganyika wamekuwa wapo kidete kuupigania huu muungano licha ya wananchi takriban wote wa taifa la ZANZIBAR kutoutaka !

Nilichogundua ni kwamba mbali na faida nyingi za kiuchumi,kisiasa,kijamii na kiutamaduni wazipatazo watanganyika hapa ZANZIBAR ,kubwa kabisa linalowafanya watanganyika wawe tayari KUUWA ili muungano huu uendelee kuwepo si jengine zaidi ya nafasi kubwa wanayoipata katika kuueneza ukiristo(ukafiri) katika visiwa vyetu vya unguja na pemba.

Izingatiwe kuwa ingawa takwimu zinaonyesha waislam ni wengi zaidi kuliko makafiri hapo tanganyika.lakini nyanja zote muhimu zimemilikiwa na wakiristo huku waislamu wakiacha wakiwa duni,masikini na wasiokuwa na dira yeyote ile .
Hivyo imekuwa ni wajibu kwa kila mkiristo(wenye madaraka) kuhakikisha wanapigamnia kuwepo na muungano maana kufanya hivyo ni kuhakikisha ukiristo unaenezwa na kusambazwa katika kila pembe ya ZANZIBAR. ili kuondosha sura iliyopo kuwa ZANZIBAR ni taifa la waislamu kwa asilimia mia.
Na hapo ndio watakuwa wamekamilisha jukumu la kiroho.

Namalizia maneno yangu machache kusisitiza kuwa muungano nia yake kubwa ni kuutokomeza UISLAMU katika visiwa vyetu hivi.

Waislamu tuamkeni.

6 Comments on "MUUNGANO NA UENEZAJI WA UKIRISTO ZANZIBAR!"

  1. kibakora jaz 27/04/2010 kwa 5:13 um ·

    a/alaikum, ndugu yangu mtoa mada maneno yako ni ukweli mtupu na hilo hasaa ndilo lililokusudiwa na hawa waasisi wa huo muungano wao,kuthibitisha haya mtizame karume mara tu baada ya haya mauaji ya 1964 kilichofuatia hapo ilikuwa ni kuutokomeza uislam kwa kuwafukua au kuwauwa mashekhe,pia kufunga taasisi zote za kiislam na chinja chinja ndio ikawa dini yake LAANATULLAH M/MUNGU AMUWEKE4 PAMOJA NA FIRAAUNA INSHAALLAH

  2. sedouf 01/05/2010 kwa 5:53 mu ·

    KIBAKORA JAZ maneno yako na maneno ya mtoa mada yanaendana sawa sawa kabisa.

  3. kwaomtu 01/05/2010 kwa 9:33 mu ·

    MIMI NAHISI MWANDISHI AMEENDA MBALI SANA KABLA YA KUANGALIYA ATHARI YA MAINGILIANO BAINA YA JAMII. WAKATI JAMII ZINAISHI KWA PAMOJA ATHARI NI LAZIMA ITAKUWAPO. ILA TUJIULIZE TU JEE TUNASHERIA GANI ZA KUDHIBITI UHAMIAJI?

    IKIWA LEO ZNZ TUTAKUWA NA SHERIA ZA UINGIAJI NA UTOKAJI KWA KUTUMIA PASI BASI HII NI ISSUE NDOGO SANA. MTU ANAEINGIYA ATAJUILIKANA MUDA GANI ATAKAA ZNZ NA LINI ATAONDOKA.

    KAMA NDUGU YANGU MWANDISHI UNAANGALIYA UPANDE MMOJA TU WA SHILINGI HILO NAPINGANA NA WEWE, KWA SABABU NA HAO MAKAFIRI KUTOKA TANGANYIKA WANAOINGIA ZNZ BASI ASILIMIA KUBWA HUPATA KUSILIM.

    TATIZO LINALOTUKABIL NI KUWA VIONGOZI WALIOKUWAPO WANATOA MWANYA MKUBWA KWA MAKAFIRI HAWA KUWA NA NAFASI KUBWA NA NYETI NDANI YA SERIKALI, NA WENGINE WANAFIKIA KUWA NA UWEZO WA KUMILIKI ARDHI NDANI YA ZNZ.

    KWA MUJIBU WA SHERIA YA ZNZ MTU KUTOKA TANGANYIKA HANA RUHUSA KUMILIKI ARDHI NDANI YA ZNZ, LAKINI LEO UTASHANGAA UKIENDA SEHEMU ZA NYARUGUSU, KITOPE, KIBELE,CHAANI,MWARIHAKOGI,KIEMBE SAMAKI,DOLE NA SEHEMU NYINGI NYENGINEZO ZIMEJAA MAKAFIRI NA WAO NDIO WANAOONEKANA WANA THAMANI KUBWA ZAIDI YA WAZANZIBAR.

    WAZANZIBAR WENYE ASILI YA PEMBA LEO WAKIMILIKI VIWANJA WANABOMOLEWA NA KUMBIWA ATI WAMEVAMIYA MASHAMBA YA WATU NA HATUA ITAKAYOCHUKULIWA DHIDI YAO NI KUBOMOLEWA NYUMBA, NA CHA KUSTAAJABISHA MTU HUYU MASIKINI KABLA YA KUJENGA KAFUATA TARATIBU ZOTE ZA KISHERIA NA ZOTE ZINAMRUHUSU KUJENGA.

    NAHISI TUKIWA NA SHERIA MADHUBUTI ZA KUILINDA ZNZ BASI TUTAFANIKIWA TU, WAJIBU WA VIONGOZI NI KUACHA KUFIKIRIA KUWA WATAISHI MILELE NDANI YA MADARAKA, MADARAKA MUDA WAKE NI MCHACHE TU, WAO WAJUWE FAIDA YAO NI HASARA KWA TAIFA ZIMA NA WATU WAKE, WASIFIKIRI KUWAPA MAKAFIRI HATI ZA KUISHI ZNZ NDIO KUTAWAPELEKEA WAO KUPIGIWA KURA TU, BALI WAJUWE NDIO NCHI WANAIANGAMIZA KWA KUWAPA WASIO NA HAKI DHIDI YA WALIO NA HAKI.

  4. sedouf 01/05/2010 kwa 10:11 mu ·

    KWAOMTU fikra zangu ni kuwa jamaa hajakosea.
    anafahamu hayo uliyosamema ya muingiliano katika jamii ila hapa kuna ajenda ya siri (sasa sio siri tena) kuwa wenzetu wanatumia mwanya huo wa muungano kueneza ukiristo visiwani mwetu.

    Nani atafikiri akilini mwake kuwa PONGWE kunaweza kuanzishwa kanisa.
    Nani anaweza kuamini kuwa kiwengwa kunaweza kuanzishwa kanisa?

    Wanyamwezi wanaletwa kwa makundi zanzibar kwa misingi miwili mikuu.
    a) kuja kutetea utawala wa ccm ambao hauna nguvu visiwani hapa.
    b) kuja kueneza ukafiri hapa kwetu.

    Karibuni nimeona picha ya kafiri pinda akiwa kakumbatiwa na mapadri utafikiri yupo vatikani.wenyewe huita ni dayosisi yao!
    wazanzibari tumekwisha !!!!

  5. depsis 11/05/2010 kwa 3:44 mu ·

    Mbali na viongozi kutokuwa waadilifu, baadhi ya waislamu pia wanachangia kumwagwa kwa makanisa hapa Zanzibar. Na wamekuwa wakiuza dini yao kwa masurufu machache.

    Makafiri wanatumia njaa za watu hawa kutimiza malengo yao. Kwa mfano, kanisa lililopo barabarani pale Mbuyu Mnene limesimama kwa mchango wa muislamu njaa. Makafiri walimrubuni kwa vipesa ili anunue kiwanja wakijua kuwa wakijitokeza wao basi hawatopewa. Alifanya hivyo na matokeo yake ni kanisa tunalolishuhudia leo.

    Kwa kweli makafiri wamepania sana na wanatumia huu upenyo wa kisiasa, njaa za watu pamoja na maelewano mabaya ya wazanzibari kupenyeza makanisa mengi inavyowezekana. Kwa vile kipindi hichi wenyewe hatuelewani si rahisi mtu kuacha ya siasa na akashughulikia ya dini. Tutakapotanabahi tutakuwa tumeshazingirwa!

    Kwa sasa makanisa yaliyojengwa hapa Unguja tu pekee kipindi hichi cha miaka 5 yanapindukia 1000 kama unataka hesabu kamili basi tembea uone.

    Lengo la makanisa haya ni siasa, udhibiti wa Zanzibar na dini. Pamoja na kanisa lenyewe pia hujenga nyumba za kuishi wakristo wao ile wasipate bugudha za mitaani na wanapotaka kuwatumia kwa shughuli zao basi inakuwa rahisi.

  6. sedouf 11/05/2010 kwa 7:37 um ·

    KAMAKAFANYA MAKUSIDI KUWANUNULIA MAKAFIRI KIWANJA CHA KANISA BASI NI LAZIMA LAANA YA MUNGU ITAMUANGUKIA.

Comments are now closed for this article.