Makala/Tahariri

Mzanzibari Zinduka: Usaliti wa Lipumba na Khammnyaharuna Sio wakuachiwa.

By Zamko & Ashakh

Asalamu aleikhum ndugu zangu Wazanzibari wa Ndani na Nje ya Visiwa vyetu adhimu, ama kwa upande wetu tunamshukuru Allah SW kwakutupa pumzi, uzima na wasaa wakuandika makala hii muhimu. Makala hii itakuwa na Phase 1, 2 na 3. Hii ya leo tutaanza naphase 1 tu.
Kabla yakuanza hio phase 1, nataka Wazanzibari nyote muelewe kwamba migogoro katika Vyama ni jambo la kawaida. Na migogoro hii huja na kupita, lakini mgogoro ulioko CUF kwavile ni wakuandaliwa na CCM na malengo yake ni kuwazuia Wazanzibari kupata HAKI yao ya Ushindi wa Uchaguzi halali wa 25.oct.2015. Ndio pesa nyingi ilioibiwa chamani inatumika kuendeleza mgogoro huu ambao. Lipumba alishauriwa na Sefu Ali Iddi kuwatumia baadhi ya Viongozi wa Pemba ili awaingize katika TIMU yake ya Hujuma ili wawatoe Wananchi na CUF katika msimamo wake.
Pia nataka ieleweke wazi kama sisi hatuikingii kifua CUF, laa hasha. Tunajuwa katika CUF kuna matatizo kama ilivyo vyama vyengine vyote. Lakini matatizo ya CUF hayata ondoka kwa akina KHAMNYHARUNA kujiunga na Lipumba. Matatizo ya CUF yataondoka wakati Wazanzibari watakapo pata Haki yao ya Ushindi na Wananchi na Viongozi kuifumua CUF na kuijenga upya.
Makala ya 1:
Kwanza nini maana ya neno KHAMNYHARUNA? Khamnyharuna maana yake ni: –
Kha= Khalifa. 2. Mny= Mnyaa. 3. Ha= Haroub. 4. Ru= Rukia. 5. Na= Nasor.
Kisheria hasa LIPUMBA ni nani? Lipumba ni:-

Rai tu wa kawaida kama mimi na wewe na sio Mwanachama wa CUF labda tuseme ni Kibaraka wa CCM kwasababu alijiuzulu mwenyewe na Kikao cha CUF chenye wajumbe waliotimia walikubali kujiuzulu kwake. Na kwisha kumfukuza Uwanachama. Hivo Lipumba kwa sisi Wazanzibari sio Mwanachama, wala Katibu wa Chama na kundi lake ni dogo sana. Hivo Lipumba asijaribu kuja kutuchafulia Visiwa vyetu akahisi kwasababu ana Ungwa mkono na Akina Khamnyharuna. Atabakia Salama. Ku Sucrify Msaliti mmoja katika hao kwa ajili ya Kuinusuru Nchi yetu na chama chetu ili kirudi kwenye malengo yetu ni Halali kwa kila Mzanzibari. Tukumbuke Tulikotoka na tunakotaka kupelekwa na kundi hili.

Kwakuanzia na makala yetu nataka kwanza Wazanzibari muelewe ni nini hasa Malengo ya CUF kwenu nyinyi Wazanzibari? Malengo ya CUF ni: –
1. Kutambuwa Uwepo wa Zanzibar kama Nchi (Visiwa) Huru.
2. Kuwatambua Wazanzibari na Kuilinda Identity Yao Popote pale Walipo.
3. Kuitetea ” HAKI” za Zanzibar na Wazanzibari wa Ndani na Nje ya Visiwa vyetu.
4. Kuleta Usawa kwa Wazanzibari wote wa Ndani na Nje ya Visiwa vyetu.
5. Kuwaunganisha Wazanzibari wote wa Ndani na Nje kuwa kitu kimoja kama Wazanzibari.
6. Kuheshimu na Kuzilinda Haki zao, Utu wao, Mali zao, Mipaka yao, na Rasilimali zao
7. Kuleta Maendeleo ya kijamii kwa Wazanzibari bila kubaguwa rangi, kabila, jinsia au sehemu anayotoka mtu.
8. Kuleta Mamlaka kamili na maendeleo ya kiuchumi kwa kutumia rasilimali zao za nchi.
9. Kuwaunganisha Wazanzibari na Majirani zao wa Africa na Nje ya Africa.
10. Kuisimamia Zanzibar na Kujenga Uhusiano mwema Kitaifa na Kimataifa utakao leta mafanikio kwa jamii na Dunia kwa ujumla.

Ndugu zangu Wazanzibari, hayo hapo juu ndio Malengo makubwa ya CUF, hivo tunatakiwa tuzinduke na tujiulize masuali. Ni nani Mtetezi wa hayo?

Wazanzibari tusidanganywe na tusikubali kugombanishwa na watu wa BARA, kwani wao Wana Nchi yao ya Tanganyika iliokuwa na Mapori ambayo hata kuguswa hayaja guswa. Sisi tuna Vijisiwa vyetu vidogo sana ambavyo kama itatokea Umwagaji wa Damu au jenginelo – basi hakuna Mtetezi. Huyo Lipumba na hao Nduguzetu wa damu (Tanganyika) likitokea “Tatizo” hapa Zanzibar wengi wao Hulifurahia tatizo hilo.
Ni nani alietetea Maslahi ya Zanzibar na Wazanzibari hadi ukaja Uandikwaji wa Katiba mpya kama sio Allah kuwapa Imani Wazanzibari Wazlendo na CUF?

Ni nani aliepigania Suali la Mafuta na Rasilimali za Zanzibar ikiwemo uzuiwaji wakuiba rasilimali ya Mafuta ilioko katika kisiwa cha Fungu Mbaraka kama Sio Allah kuwapa Imani Wazanzibari wazalendo na CUF?
Ni nani aliepinga suali ya Kura ya Maoni ya Rasimu ya CHENGE na CCM kama Sio Allah kuwapa Imani Wazalendo Wazanzibari na CUF?
Ni nani aliepinga Uchaguzi haramu ulioletwa na Wahafidhuna wa CCM wakisaidia na maadui zetu (CCM -Tanganyika) kama sio Allah kuwapa imani Wazanzibari wazalendo na CUF?

Jee mumeona jinsi gani wazanzibari walivoitikia wito na kuiacha CCM Zanzibar kuadhirika katika Uchaguzi Ule wa 20. march 2016?
Hapa nataka munielewe wazi kwamba tusichukulie kuwaona CCM wanaongoza Nchi. Viongozi wote wa Nchi2 hizi Tanaganyika na Zanzibar hawana Amani ndani ya nafsi zao kwa dhulma waliowafanyia Wazanzibari. Wanaongoza Nchi kwa khofu na izara yakushindwa na wako kama Gamba la Koa tuu. Hawana lolote lile na hawaiwezi Nguvu ya Umma unao dai haki kama utasimama pamoja. Isipokuwa kutumia Vyombo vya Dola. Ikiwa sio Jeshi na Polisi CCM isingekuwapo tena. Hasa kwa Upande wa Zanzibar. Hilo CCM wanalijuwa na ndio maana Wamefanya mikakati yote ya Kumtumilia LIPUMBA na baadhi ya Vibaraka hao niliowataja hapo juu.

Ni nani aliepiga Kelele kuhusu kisiwa cha Fungu Mbaraka, kama sio Allah kuwapa uwezo Imani Wazanzibari wazalendo na CUF?
Nataka tuelewe ukweli kwamba hakuna wakuleta mabadiliko hayo kama Sio CUF. Tayari tumeweza kuona Jinsi Zanzibar Ilikotoka- kuanzia kwenye UDICTOTOR. Baadae ukaja Ukoloni Mambo leo Wa Chama kimoja (CCM) na kuambiwa kwamba Chama ndio kilichokuwa kimeshika hatamu. Katika vipindi hivo kuna watu hawavikumbuki kwasababu hatukuwa tumezaliwa, lakini tulisikia hadithi zake. Bila ya kuelezea hapa. Lakini tunaweza kutofautisha baina ya Tawala za SMZ zilizokuwa zikiongozwa na Chama kimoja – na ule utawala ulioongozwa na Mfumo wa GNU.
Makala itaendelea Phase 2 Ambayo tutawachambuwa hawa Khamnyharuna na nini Wamewafanyia Wazanzibari katika kipindi chote cha Ubunge na nyazifa zao za uongozi ndani ya CUF.

Tunawaomba Samahani ikiwa tumewakosea.

Share: