Ni vioja Dr.Gharib kujadili kero za muungano!
Written by administrator // 05/02/2012 // Makala/Tahariri // 7 Comments
Nadhani wazalendo wa kizanzibari watakubaliana nami kuwa mzizi wa fitna au chanzo cha kero ni muungano wenyewe.Hilo kwa sasa angalau kwenye makala hii sio kitovu cha maada yenyewe.Twende hivyo watakavyo wenyewe kuwa kuna kitu kinaitwa kero za muungano.
Ni wazi miongoni mwa kero hizo ni ule umakamau wa rais kwenda kinyume na mkataba wa muungano, ambao kiuwazi mkataba unaeleza kuwa makamu wa rais, kama rais ni wa bara basi makamu wake lazima atoke upande wa pili wa jamhuri ya watu wa Zanzibar.Hadi leo sioni kama kuna mkataba mwengine wa muungano, hivyo bado naamini kwa dhati kuwa makubaliano ni yale yale yaliotiwa saini na wasisi wa muungano.Hii kuharamisha mabadiliko yoyote yaliofanywa na bunge!
Nilipata butwaa kuona hio timu inayoongoza utatuzi wa muungano ikiongozwa na Dr.Gharib badala ya Dr.Shein.Ni wazi mtu aliengia madarakani kwa kutumia kero hatoweza kupata ufumbuzi wa kero.Hivi ni vioja vya mwaka!
Ni kuthibitisha kuwa hakuna jitihada zozote zile zinazochukuliwa.Sidhani kama wazanzibari wanatarajia kupata ufumbuzi wa aina yoyote ile juu ya khatma yao na vizazi vyao kutoka mikononi mwa Dr.Gharib, Samia Suluhu, Pinda n.k.Labda tutarajie kuitwa wahuni kutoka kwa gurupu hili (tulishawahi kutukanwa matusi ya nguoni watu hawa hawa!)…Leo twaambiwa ati wanatetea maslahi yetu!
Nimalizie kwa kusema moja, ambalo nina uhakika nalo hata nikiamshwa usiku wa manane.Hakuna suluhusho lolote la khatma ya Zanzibar litalopatikana kwa kutumia wanasiasa au viongozi.Masuala haya lazima yapatiwe ufumbuzi na wazalendo na wazanzibari kwa ujumla. Tukae mimi na wewe mzanzibari tuanze kuchakachua njia za kujikomboa!
Miongoni mwa hatua za kudai haki zetu kwa kuanzia ni maandamano ya kuelekea ikulu ya Zanzibar kushinikiza matakwa yetu.Kwa kuanzia ni kushinikiza Shamhuna ajiuzulu haraka iwezekanavyo kwa kushiriki kwake katika njama za kuhujumu uchumi na mali asili za Zanzibar.
Naziwachia jumuiya na asasi za kijamii, wazalendo, wanaharakati na wengineo wengi kujadili ni jinsi gani wataanza na maandalizi ya maandamano hayo na kupeleka barua rasmi ikulu (ikiwezakana kulala hapo ikulu hadi Shamhuna ajiuzulu!).
Wasalaam,
mrfroasty





7 Comments on "Ni vioja Dr.Gharib kujadili kero za muungano!"
na wewe utakuwepo.?
Bado kidogo niseme maoni yako ni ya kijinga, lakini bora nijibu hoja.Ukweli sitokuwepo Zanzibar.Vipi kwani kuna zaidi ?
P:S
Kama Zanzibar ni kwa ajili yangu mie binafsi na familia yangu (ambao wote hatupo Zanzibar).Basi niseme bora pirika zote zisimamishwe na tukae tukodolee macho.
Aidha kama Zanzibar ni ya wote, basi sidhani kama hoja ya msingi ni mie kuwepo au kutokuwepo.
@ kalasinga
Bali mimi naona maoni yako ni ya kipuuzi.Katika Mradi (project) wowote ule kila mmoja ana uchangiaji wake. Kuna Kiongozi mwenye hekima na fikra zalifu na ikaleta manufaa kwa umma.Kuna wapangaji(oganisers), Kuna watekelezaji wa ile fikra, na si lazima mtowa fikra ile kushiriki.
Fikra moja ilizaa pyramids, skyscrapers, Taj Mahal, The Great Wall of China, Algebra, Calculus, Alchemy,Arbic numerals, alphabets, phonetics, atomic bomb, hyrogen bomb, particle accelerators, magnetic levitation, insulin, peniciline, x-ray, TV, aerospace flights, supernova, big bang, quantum mechanics, string theory, particle physics, airconditioning,bread toaster,electro-magnetism, black holes nk.
Je wewe ulikuwepo yalpofanywa hayo yote? Na hao waliotowa fikra hizo wote walikuwepo katika utekelezaji wake. Everyone has role to play. Usiulize kikejeli nani atashiriki. Kwani wewe umelazimishwa? Kusingekuwa na viongozi na majemedari katika jeshi. Wote basi wawe askari. Una haki yako ya kikatiba kushiriki au kutokushiriki. Usilete fitna zako hapa mtandaoni.
@ Mrfroasty(Ufundi)
Proposals zako naziunga mkono kwa hamasa na shauku
@wamekuogopa ma admnistrators wenzio, maana kama mada hii ningeandika mie isingeekwa hapa.
Naonga mko hoja lkn kwa akili za wazanzibari zilizozama kwenye siasa itakua tabu kulifikia hilo.
@mfroasty
Mada yako ni Nzuri sana na yenye MAWAZO mazuri , kwamba hapa Watanganyika wameshatujua kwamba sisi Wazanzibari ni WOGA na tunapora tu. Maneno Marefu Vitendo Vifupi.
Mtu yoyote atakaeona mkutano huu wa Bilali na akina Seif ali Iddi basi atajua kwamba wamepewa Fupa yakuchukua POSHO za Walala Hoi. Kwakudai (ati) Wanakutana kujadili KERO za MUUNGANO.
Ukweli MWIZI HAWEZI KUJIHUKUMu yeye Mwenyewe, Hawa wote Wanajaza Matumbo yao kwakupitia hizo KERO ZA “MUUNGANO”. Asilani hawataweza kujifutia Kazi na wakarudi Unguja.
Maandamano ni Muhimu na siolazima kila mtu awepo kwenye Maandamano, kwani kuna wengine hawapo Nyumbani. Lakini wanaweza kusaidia kwa Njia hii au Nyengine.
Ukimya wetu wakuogopa JWT ( JESHI la WATANGANYIAKa) nikuonyesha Udhaifu tulionao kwamaba tumekubali Ktawaliwa. Tukumbuke kwavile tuna Wawakilishi wanatuunga Mkono mawazo yetu basi Maujai ya Maandamano yatakua hayana nguvu. Najuwa kwamba JWt wataingilia kati kuvuruga maanadamano lakini itakua ni WAKE UP CALL kwa Jirani Zetu kwamba tumechoka Kutawaliwa kimabavu.
HAWA NI wakulima wa shamba la mkonge na ndio maana hawajali kuhusu Zanzibari,eti viongoni wa muungano haram,LANATULLAH,HYPOCRIT, BAD MIND,ALLAH AWAANGAMIZE WAO NA FAMILIA ZAO AMIN
NIshasikia mara kadhaa au kuona maandiko humu watu wakihamasishana kuhusu kuandamanalakini sijaona hata siku moja maandaano hayo kufanyika NADHANI HATUJAWATAYARI TUNARIDHIA KUTWALIWA NA MTANGANYIKA siku zinaenda mambo yana songa mbele watanganyika wanajenga taifa lao hata tukiwa tayari wao wako mbali na kesho kutwa MIRIJA YA KUVUTA MAFUTA YETU ITACHOMEKWA SISI TULALE TU dalili ya hayo ni yale makampuni matatu tofauti yaliosaini mkataba wa UTAFUTAJI MAUTA ENEO LA TANZANIA
TUTABAKI TUANDAMANENI HAMNA LIWALO SIKU ZINAKWENDA
babu jinga kaa ufikiri mali yako inaliwa
naoma kuasilisha