Makala/Tahariri

Raha na tamu ya Zanzibar

Ukusanyaji wa nyaraka za kale na kumbukumbu za matukio tofauti katika nchi ni njia mojawapo ya kuweka historia ya nchi na uhai wake kwa faida ya kizazi kilichopo na kitachokuja.

Kichwa cha habari hii kimeinuliwa kama kilivyo kutoka katika mtandao wa youtube, na sifa zote ziende kwa mwenye umiliki wa chaneli hio, kwa jina maarufu Bin Seif .

Kama ni mtembeleaji wa chaneli ya youtube, utapotaka kupata kumbukumbu za matukio ya Zanzibar hasa utamaduni wa taarab, basi huwezi kulikosa jina la Bin Seif na maandishi yake katika video anazoziweka yanayosomeka maarufu kama ipende Zanzibar(Love Zanzibar)

Bin Seif amefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kuweka kumbukumbu za matukio tofauti ya Zanzibar, hasa ukusanyaji wa utamaduni wa nyimbo za taarab kutoka za kale hadi za sasa jambo ambalo hata serikali imeshindwa kulifanya.

Kwa wale wanaotamani kulifuta jina la Zanzibar ni wazi kwamba wanapokutana na kumbukumbu za kila aina kama hizi za utamaduni wa sehemu wanayotamani kuifuta, basi hujua kwamba kazi pevu ipo mbele yao kwani ukweli wa mambo ni kuwa ili watu waweze kusahau ama kuwasahaulisha uwepo wa sehemu fulani, basi ufutaji wa utamaduni na kumbukumbu ni jambo muhimu.

Hongera Bin Seif kwa kazi ya khiari ambayo umuhimu wake ni mkubwa katika jamii, kama maandishi ya video zako yanavyojitokeza kama love Zanzibar, naamini kwamba ni kweli unaipenda Zanzibar na ni mshabiki namba moja wa kauli hio.

Share: