Serikali ya CCM inangojea watanzania wangapi wafe ili kupata

Written by  //  05/09/2010  //  Makala/Tahariri  //  Zima maoni

Watanzania imefika wakati kutokana na mabadiliko mingi ktk ulimwengu ya kisiasa na kiuchumi na zaidi kuimarisha Muungano uwe imara nilazima tufanye mabadiliko ya katiba. Nasema hivi kutokana na katiba yetu imepitwa na wakati hususani katiba ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ina kasoro nyingi zisizo kizi pande mbili za Muungano. Hivi sasa kumekuwa na malalamiko makubwa kuhusu Mungano na kero zake.

Ili tulinde Muungano wetu? nilazima kuwe na mabadiliko ya katiba yenye kukizi pande zote husika. Sivyema kusema tu tulinde Muungano huku Muungano wenyewe ukiwa na kasoro nyingi za kikatiba. Hivi sasa kuna zana ya Wazanzibar kuhisi katiba ya Muungano ina mapungufu mengi na inatumiwa kama ni chombo cha kulikandamiza taifa la watu wa Zanzibar na kutowa fusa nyingi kwa Serekali ya Tanganyika(Tanzania). Imefika wakati watu wa Tanzania wamekuwa comfuse kwa katiba ya Muungano. Katiba ya Muungano inasema mipaga ya Tanzania ni Bara na visiwa vyote vya Zanzibar. Katiba ya Zanzibar inapinga inasema mipaka ya Tanzania ni Tanganyika na Zanzibar kwa Mujibu wa atcle of union hii ndio sahihi ya Muungano.

Comments are closed.