Siasa za zanzibar hazina muelekeo wa maendeleo.
Written by ole // 12/07/2010 // Makala/Tahariri // 3 Comments
Na.B.OLE,
Zanzibar ya leo inahitaji kuwa na misingi madhubuti ya uchumi na maeandeleo kwa wananchi wake ambao wameteseka kwa muda mrefu sasa .
Kutokana na siasa za Zanzibar hivi sasa haionekani kwamba kuna muelekeo wowote wa kimaendeleo.
Hii ni kutokana na mpaka karne hii tuliofikia kuona kwamba viongozi na wananchi wa Zanzibar wanashughulikia zaidi siasa za ubaguzi na chuki jambo ambalo haliendani na maadili pamoja na misingi ya maendeleo kwa Taifa au jamii yeyote ile.
Ili maendeleo yapatikane lazima pawepo na misingi thabiti pamoja na sheria mahususi ambazo zitaambatana na ushirikishwaji wa Wananchi.
Yote hayo ni mambo ambayo kwa sasa Zanzibar hayapatikani na wala haionekani kama kuna muelekeo au dalili za aina hiyo.
Mpaka leo watu wanashindwa kutofautisha baina ya siasa na maendeleo na hata hao viongozi wa juu wameichukulia siasa kama ni njia ya ugomvi na mifarakano ili waweze kutawala wananchi kwa misingi ya dhulma na uonevu.
Kiongozi mzuri ni yule ambae anajali maslahi ya nchi yake pamoja na maendeleo kwa raia wote bila kubagua kama huyo anatoka wapi au ni kabila gani.
Madaraka isiwe ndio sababu ya hata kuondoa ubinaadm wetu na kuwafanya watu wengine waonekane kama hawahusiki kwenye jamii.
Muelekeo wa viongozi wetu ni tofauti na wako mbali na mawazo ya aina hiyo ya kuwaunganisha wananchi, matokeo yake wanazungumzia kuhusu visasi , uhasama, ugomvi na madaraka tu.
Mara nyingi wao hujikita kwenye maslahi yao binafsi, jambo ambalo husababisha mitafaruku miongoni mwa jamii.
Zanzibar haina budi kufuta siasa hizi chafu ambazo haziuziki kwa bei yeyote ile.
Wazanzibar hatuna budi kujenga na kudumisha ustaarabu wetu ambao misingi yake sio ya kuiga kama wengine, mababu na mabibi zetu ndio walio turithisha na tulichukulie hili kama ni asili yetu.
Kutokana na hali hii hatuna budi kuwakataa viongozi wabovu ili tuondokane na mawazo machafu ambayo husababisha kujengeka kwa hasama zisizo kwisha.
Hali hii hupelekea hata demokrasi kutoheshimiwa na wala kuonekana umuhimu wake katika jamii.
Hatuna budi Wazanzibar kuondokana na siasa za aina hizo na badala yake tuwe tayari kubadilika kwa kujijengea misingi thabit ambayo italenga kwenye maendeleo ya Taifa na kuwaunganisha Wazanzibar wote.
Pia tuache ushabiki na badala yake tushirikiane katika kuleta maendeleo kwa pamoja kwa kuchagua watu wenye muelekeo wa kuongoza na ambao wanaweza kuipeleka Zanzibar kwenye mabadiliko.
Hatuna budi kuona dhulma haifai katika jamii na kama kuna viongozi na watu ambao wanafikiria kwamba dhulma ndio itakayo jenga maendeleo yetu basi itakuwa wanajidanganya.
Mfano wa wazi tunao hapa Zanzibar, Wazanzibar tujiulizeni tatizo ni nini hasa ?
Jibu kama utapenda ni dhulma, hili ndio tatizo kubwa na mpaka hao viongozi tunaowachagua basi huiba na kubadilisha matokeo na ndio maana ukaona hatufiki popote pale.
Chaguzi zote zinaenda na rushwa, wizi matusi ,ugomvi ,wizi na dhulma, sasa katika hali kama hiyo tunategemea maendeleo ya aina gani na kwa nani ?
Lazima tubadishe kwanza haya yalio kwenye nafsi zetu ndio baadae tuelekee kwenye ujenzi wa nchi yetu.
Ukabila kati ya upemba na unguja hautawasaidia Wazanzibar na matokeo yake tutakuwa tunajimaliza wenyewe kwa wenyewe kama hivi tulivyo sasa.
Maendeleo yatapatikana na kujengwa na Wazanzibar wote kuwa kitu kimoja, kupendana na kushirikiana kwa pamoja.
Sio kweli kama jirani atatusaidia yote, kutuchaguli viongozi na kutupa maendeleo, wazanzibar hawana budi kuzinduka, kwani habari ndio hii.







3 Comments on "Siasa za zanzibar hazina muelekeo wa maendeleo."
Umenena Biole,
Moja:Lakini haya yatakujaje ikiwa katiba ya nchi haindani na mabadiliko, nikisema hivyo ni kua vipi tuko katika vyama vingi wakati katiba yetu ni ya chama kimoja?
Pili: Hatuna upinzani Zanzibar bali tumezungukwa na Wanafiki tu, Viongozi takraban wote wa Cuf ndio wale waliokua makada miaka ya nyuma , walipofukuzwa na chama tawala ndio wakaleta chama hichi cha Cuf .
Tatu: Hatuwezi kwenda popote pale ikiwa mimi leo nina miaka 28 , tangu nazaliwa mpaka leo nasikia jina la Karume , seif, salmin sasa tujiulize hii jamii ni yakwenda na wakati au tuko tu katika hali ya static.
Ahsanteni
@Abuu Said,
Unasema CUF wote ni makada waliofukuzwa kutoka CCM, ulishawahi kupoteza muda na kutafiti ni kwanini walifukuzwa?
Mie plan yangu ya kuleta mabadiliko visiwani Zanzibar ni kama ifuatavyo:
1.Kuondosha chama tawala na kueka cha pinzani au mbadala ambacho ni CUF.
2.Kurekebisha au kuvunja kabisa muungano pamoja na upuuzi wote ulioletwa na Nyerere pamoja na Karume.Badala yake kufanya Zanzibar ni nchi huria kama ilivyokuwa hapo awali kabla ya ukoloni na uhuru wa 63.
3.Kuanza kufanya mabadiliko ya mfumo mzima wa serekali ya Mapinduzi.JKU pamoja na vikosi vya SMZ kuwa ni jeshi kamili la watu wa Zanzibar.
4.Kufuta na kabisa dhana ya Mapinduzi, na badala yake kuwacha neno hilo kwenye vitabu vya historia.Badala yake maneno kama umoja na maendeleo ndio yashike hatamu.
5.Kupunguza idadi ya wafanya kazi wa Serekali ya Zanzibar (kumradhi hapo watumishi wa Serekali).Lakini kwa mtazamo wangu serekali ina idadi kubwa ya watumishi, kiasi ambacho wengine hawana cha kufanya wapo wapo wanakula mishahara kwa kutumia gear za kujuana.
6.Kubadili mfumo mzima wa kukusanya kodi na mapato pamoja na transaction zote za serekali kuwa zinafanywa digitally au banking system.Hii itafuta au kupunguza rushwa kwa kiasi kikubwa.
7.Kubadili mfumo mzima wa elimu, badala ya Centralized System iliopo sasa.Serekali itatoa posho tuu kwa wanafunzi na kuendesha viwango vya elimu badala ya kuendesha mfumo wa elimu.Kwa mfumo huu manaake, mwanafunzi anaomba posho kwa serekali, jukumu la kusoma wapi ni lake na skuli zinahitajika kufanya ushindani wa ubora kumvuta mwanafunzi.
8.Kupunguza majukumu ya Afya kwa serekali, badala yake kuacha sekta ya Afya kuendeshwa na makampuni ya bima.
9.Kufungua milango ya wakulima kuuza biashara zao nje ya nchi.
10.Kuhakikisha migogoro na siasa zinapungua kiasi na badala yake Zanzibar kuwa na siasa za wastani.Hizi tulizonazo naziona kama zinadumaza maendeleo.
Hayo yote nilioeleza yanahitaji kubadili au kuvunja mfumo wa muungano.Kisa na mkasa wa umasikini wa Zanzibar ni complexity ya muungano usio na maslahi na visiwa hivyo.
Ukiniuliza mie vipi tutajinasua na muungano huo, basi hatuna budi kufanya maamuzi magumu.Maamuzi hayo yanaweza kuwa hata kujitolea muhanga vizazi vya sasa lakini kuhakikisha vizazi vyetu vya baadae vinakuja kuenjoy Zanzibar yenye maendeleo na ilio huria.
Naenda kulala…waslaaam,
mrfroasty
ASALAM. WAUNGWANA:
Kwanaza nachukua nafasi hii kwa kumpongeza B.OLE kwa makala yake nzuri na inayoendana na siasa za muda huu na tunazozihitaji hasa kwa zanzibar ya baadae.
@ Abu said,umwuliza kuhusu katiba ya sasa kua ni ya chama kimoja hilo ni la kweli,lakini ndio pakupingania sasa tukadai katiba ya vyama vingi ili itufae sote na iendane na wakati tulio nao,na hilo ni jukumu langu na lako wewe tukishirikiana na wazanzibari wengine.
Kuhusu kua viongozi waupinzani ni wanafik,hilo sikubaliani na wewe kwani wao niwatu walopingana na siasa za kinyerere ndio maana wakajitenga na kuamua kuunda vyama visivyo na muelekeo wa kinyerere.
Hoja yako ya kua wao wote walikua ccm zamani hio ni hoja dhaifu sana,kwasababu kwa mtu yoyote wamakamu kuanzia miaka 50 basi utakuta alikua ccm ni kutokana na wakati hule kua lazima kujiunga na ASP (CCM) baada ya mapinduzi.
Hata kama isengekua lazima basi huwezi kumuhukumu mtu kwa hilo,kwani kina SAIDNA UMAR(R.A) walikua makafiri na walipo uchukia ukafiri wakawa waislam, Mtume Muhamad (SAW) hakuwaona kua ni wanafik bali aliwaona ni mashujaa.
Kuhusu suali lako la tatu, kuona manina ya karume Salmin,seif n,k. hio sio sababu ya kufanya tusiende mbele kwani hao niwatu kama sisi,kitu muhimu kwanza kukubali mabadiliko na kushirikiana kwa kua wamoja na kuheshimiana kati yetu,huku tukikubali kusameheana na kusahau tofauti zetu za kiitikadi au uzawa.
lakuliangalia kwasasa ni utaifa namslahi ya Zanzibar,baadae hao kina Seif,Salmin na Amani, tutawaweka pembeni tutakuchagua wewe kijana mdogo na mpya usie guswa na siasa za kale,kama wewe utakua na uwezo huo na utakua tayari kuwatumikia wazanzibari na Zanzibar mpya,au mtu yoyote atakae kua na sifa zitakazo waridhisha wazanzibari kua atawafaa kua kiongozi wao.
Lakini yote hayo hayatakuja kama hatukukubali,kuzizika chuki tulizo nazo miongoni mwetu.
Mfano wa zanziba ni humu mzalendo.net tunaona watu walivyo zipa nafasi chuki kwa kumchukia mtu fulani,kwakua yeye tu hampendi au hakubaliani nae kifkra,basi hapo hushindwa kuzuia chuki zake na kuanza kumtukana mtu au kumuapiza kisa kaona jina tu lamtu huyo,kwamfano wako tuliona kuapiza, kutukana na kukejeli kama vile Dr bilal,Dr Salmin;Maalim Seif n,k. nawahakikishia Wazanzibari wenzangu kua kwa staili hii hatutafika,na kama kweli tuna nia safi basi sisi tulio humu Mzalendo tuanzeni kwakuwa wastaarab ili iwe mwanzo nzuri na tuwe mfano kwa ndukgu zetu hasa wale walioko zanzibar.
Maneno hayaniishi nikizungumzia haya.ila nibora niwaache hapo na nimatarajio yangu kua sasa tutaanza siasa nzuri humu ndani ya mzalendo kwanza kwani hii ni picha halisi ya siasa za nyumbani.
ahsanteni.