Makala/Tahariri

Suluhisho la mgogoro wa msitu wa ngezi na mashamba ya wananchi

SULUHISHO LA MGOGORO WA MSITU WA NGEZI NA MASHAMBA YA WANANCHI NI KUONYESHWA RAMANI HALISI YA MSITU ULIOPIMWA NA SERIKALI JUL 1997 NA KUPEWA KIWANJA NO.14 MAKANGALE.

Imekuwa ni kawaida kwa baadhi ya watendaji wa Serikali kutumia mamlaka yao vibaya kupora haki za wanachi kinyemela kwa kisingizio cha uamuzi wa Serikali.

Jana nilimsikiliza mwakilishi wa Welezo Nd. Hassan Khamis (Mkwezi na Mkulima) akizungumza kwa ukali sana, alipokuwa akichangia hotuba ya bajeti Wizara ya ardhi kuhusu msitu wa hifadhi wa Ngezi kuwa umekatwa viwanja. Ikumbukwe kwamba vita hii ilianzia kwenye mijadala ya redio baadae magazati na sasa Baraza la wawakilishi.

Ni wazi kwamba mwakilishi huyu na wenzake walifatwa na kundi hilo kwa lengo la kuzuwia haki za watu zisipatikane kama walivyo kusudia. Kama kwamba haitoshi wawakilishi hao walipewa vielelezo na watu hao mpaka vya wakati wa mzee Hassan Nassor Moyo alipokuwa waziri wa kilimo vinavyo thibitisha kuwa eneo la Ngezi ni eneo la msitu wa hifadhi

Mnamo mwezi wa July mwaka 1997 wizara ya kilimo iliomba kupimiwa eneo la msitu baada ugomvi na wanachi wenye mashamba yaliyo pakana na msitu upimaji huo ulifanyika na msitu huo ukapewa kiwanja No: 14 Makangale, hilo sio siri linajulikana kila mahala na beacon zake zipo. Sasa huko kwenye mashamba ya watu wamekwenda kufanya nini? Mbona walipo pima mwaka 1997 hawakufika kwenye mashamba ya watu wanakodai kwamba hivi sasa ni eneo lao? Au mzee moyo alikuwa waziri mwaka 1998?

Ukweli ni kwamba Baada ya kiongozi mmoja (jina kapuni) kuteuliwa akapewa nafasi ya misitu wizara ya kilimo, baada ya kuona mashamba ya wananchi yaliyopo karibu kilomita moja na beacon za msitu halisi uliopimwa na Serikali, alivutiwa na mashamba hayo kwa matamanio ya nafsi yake, na akafanya dhulma ya kutaka kuyaingiza mashamba hayo katika msitu wa hifadhi kinyume na sheria. Aliamua kujitengenezea ramani mpya ya msitu ambayo ndio aliyo wakabidhi wawakilishi kwa lengo la kupotosha umma. Lakini pamoja na kutengeneza ramani hiyo bado mipaka halisi ya msitu huo inaonekana. Nimeweka ramani aliyo jitengenezea lakini pamoja nahayo alishindwa kuondosha mpaka baina ya msitu na mashamba ya wananchi, picha halisi inajieleza.

Hii inaonyesha wazi kwamba ukweli anaujuwa ila analo alilolikusudia kwa wananchi hao lakini ukweli hausemi. Tunaiomba Serikali itende haki kwa hili.

Tunataka wizara ya kilimo ieleze walipimiwa na nani kwenye yale mashamba ya watu baada ya ule upimaji halali ulio fanyika July 1997? Pia waeleze wameyapatapataje mashamba hayo? Jee! wamelipa fidia kwa wananchi hao? Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 toleo la mwaka 1995 kifungu 17/C imeweka wazi kuhusiana na sheria za uchukuwaji wa mali ya mtu. Kifungu 17 Hakuna mali ya mtu yeyote itakayo chukuliwa kwa nguvu na hakuna maslahi au haki yoyote inayo tokana na mali hiyo iliyo chukuliwa kwa nguvu isipokuwa pale ambapo masharti yafuatayo yametimizwa. Miongono mwa Masharti hayo ni kifungu 17/C Sheria imewekwa kuhusiana na umilikaji au uchukuaji huo kwa kutoa fidia inayo lingana. Jee! Wizara ya kilimo ilikamilisha taratibu hizo au imepora tu? Naomba kuwasilisha by Ally Rashid.

Tagsslider
Share:

3 comments

 1. Piga nikupige 9 Juni, 2017 at 15:04

  Huyo kiongozi bila shaka atakuwa ni Bakari Asseid akisaidiwa na mtu mmoja anaeitwa Said Juma, hawa watu inaonyesha hawajali hata kama kuna Mungu na watakwenda kuulizwa siku ya kiama juu ya dhulma waliyo ifanya kwa binadamu wenzao.
  Niwakumbushe tu watu hawa kuwa Mungu hamsamehe mwenye kudhulumu mpaka akamuombe radhi aliye mdhulumu.
  Bakari Asseid na wenzako mnapata moyo mgumu kiasi gani kudhulumu haki za watu hali ya kuwa mipaka ya msitu wa ngezi ipo na na inajulikana kisheria? Hivi humumuonei haya hata Mwenyezi Mungu kwa munayo wafanyia wanyonge wa Mungu? Au kwa vile mashamba hayo hayakuhusu. Si ya baba yako wala ya mama yako? Hivi ingekuwa ni mashamba yenu ungeyapora kama unavyo yapora mashamba ya wazee wa wenzako kwa ghilba na uadui? Jee! ungeikubalia serikali iwachukulie ardhi yenu ya halali bila ya nyinyi kulipwa fidia? Kwa taarifa yako kwenye mashamba wale palikuwa na kijiji wenye mashamba yale walikuwa wakiishi palepale, walihama pale kwa matatizo ya vyepu na tete. Pamoja na hayo hadi leo hii athari za ukaazi wa watu ndani ya eneo lile bado zipo. Ndani ya mashamba yale mna kibla cha msikiti ambacho hadi leo hii hakija bomoka waambie maafisa wenzako wakakibomowe uondowe ushahidi mwengine? Ukweli utabakia kuwa ukweli tu. Mashamba yale siyo msitu, msitu unajulikana isipokuwa kinacho fanyika pale ni matamanio ya Bakari Asseid kutaka kupora haki za wanyonge kwa kisingizio cha msitu, nia ya kufanya hivyo anaijuwa mwenyewe.
  Ushauri wangu kwa Bakari Asseid achukuwe mashamba ya wazee wake ayapige karantini yasitumike kwazaidi ya miaka 30 mpaka yageuke msitu kama alivyo yazuwia mashamba yale yakawa pori baadae mashamba hayo ayapore kwa wazee wake ayageuze msitu wa Serikali. Tuone wazee wake watakubali?
  Ramani hiyo hapo juu inaonyesha kuwa hayo ni maeneo mawili tofauti.
  DK. Shein tunakuomba komesha dhulma za aina hii. Sio jambo zuri hata kidogo watu kutumia vyeo vyao kudhulumu wanyonge, kumbuka wewe ni mchunga na utaulizwa umezichungaje haki za watu.

  Kama ulikuwa hujui leo umejua Tunakuomba ufanye uchunguzi mwenyewe huko huko Serikalini utagundua ukweli.
  DK.Asseid ni muongo muongo muongo wa kupigiwa mfano kwa unyama huu anao ufanya kwa wanyonge bila kujali kuwa kuna akhera, halafu anajitia kanzu kubwa na kofia eti ni muislamu kumbe dhulma tupu.

Leave a reply