Makala/Tahariri

Utata Kuhusu Muungano wa 1964

Juzi nimekutana na mmoja wa wanaharakati, anayeitwa Rashid Salim Adi — alinihadithia kuwa azma/nia ya kupeleka kesi nyengine mahkama kuu ya Zanzibar kuhusu hati ya Muungano. Nilimuuliza maswali mengi sana juu ya suala hili la muungano, ukwlei wake, usiri wake na uwazi wake pamoja na yale ninayoyajua.

Kama alivyoandika Othman Massoud huko nyuma: Maswali mengi Kuliko Majibu! — title of his paper.

Kwa upande wangu, ninaona conspiracy kubwa kuhusu Muungano huu, na kweli ‘hakuna anayejua hasa ukweli’. Kwa nini?

1. Tumeona picha ya Karume-1 na Nyerere wakitia saini mkataba wa Muungano wa 1964, mkataba huu ‘hakuna anayejua upo wapi, na uhalali wake na timeframe (muda wake) kama ulihitaji kuwa mwisho mwaka xxxx, na kama kuna kipengele (annex/anendum) inayosema inahitaji kufanyiwa review (mapitio, labda baada ya muda fulani).

2. Karibuni hivi, Rais wa Zanzibar, Bob Shein — alisema kuwa ‘mkataba wa muungano anao, na upo pale Ikulu Zanzibar, ndani ya drawer la pale Ikulu, anayetaka akauone’. Ukweli wa kauli hii hakuna anayejua, maana wadadisi wameona kama vile ‘danganya toto, au tisha toto’; maana pale haupo, na kuna watu wamejitokeza kutaka kuuona, pia — hawakuruhusiwa.(???).

3. Hivi karibuni, Wabunge walitaka kujua ya kuiona hati ya Muungano, Anna Makinda, spika, kama kawaida yake, aliwajibu ufedhuli na jeuri na kuonyesha kile kile kibri chake cha CCM na kujisahau kama yeye ni ‘Spika wa Wote’. Sasa, jamani, kama wabunge wa nchi – wanadai kuona hati kama hii muhimu ya uhai wa NCHI, wamenyimwa, nani mwengine anastahiki kuiona au kujua?? Uko wapi utawala wa sheria na ule unaoitwa ‘separation of power’? Inavyotakiwa kama, tuseme, hati hii ni classified, basi wabunge walikuwa waonyeshwe pia katika mazingira kama hayo, so long, wamekula kiapo kuhusu kutunza siri za dola (state). What’s the big deal here….! “kunani balahau Shein na Kikwete”?

4. Katika kile kitabu cha Dr.Harith Ghassany, kinachoitwa — KWA HERI UHURU….kuna chapter or para inayosema kuwa ‘hati ya muungano haikutiwa saini upande mmoja’ yaani Karume-1 hakutia saini, kitu ambacho mimi nina shaka nacho sana sana. Document hii, kwa mujibu w akitabu hichi (Dr.Harith) ameipata Makao Makuu wa UN, then secretary general alikuwa U-Thant. Swali: je inawezekana vipi UN kukubali document iliyotiwa saini upande mmoja tu. Ni UN ya aina gani hiyo?? Maswali ninayojiuliza — UN ilikuwa na imekuwa corrupt kiasi gani. Mimi ninafahamu kuwa katika era tuliyonayo, UN ni pahala bogus kabisa, si pahala pa maana sana, na kijiwe tu cha akina Asha Rose Migiro na wenzake kama hao. Vipi UN, wanakubali au wamekubali document kama hii (iliyotiwa saini upande mmoja). Inatisha kidogo kusikia UN inafanya mambo kama hayo?

5. Je, wajumbe wa baraza la wawakilishi wao hawana haki ya kuuliza, kuhoji na kutaka kuuona mkataba/warka huu wa Muungano au wao wanasubiri ‘Nkataba’ mpya. Mimi ninaamini sana taasisi kama hizi:bunge au BLW — lakini zimekuwa hazionyeshi sana umakini na kujiweka kama inavyotakiwa kuwa. Mimi siamini kupiga kelele ukumbi wa Bwawani au Beit -el yamin au wapi sijui. Kwa mtindo huu tulioukubali, sidhani kama tutapa haki ya Zanzibar ndani ya muungano, hata siku moja.

6. Je, kwa nini wajumbe wa BLW wasitie pressure kwa rais wa Zanzibar (kama sehemu ya executive) na wawakilishi kama legislature — branch of the state, na wakamdai Bob Shein huo ‘nkataba’ wa Muungano wa 1964. Kama kweli ni wawakilishi, na wamejiamin hivyo, naona ‘Action — katika kikao cha BLW kijacho’ — please. Hapo ndio nitamjua Jussa, au Mansour au Hamza na Mshimba n.k — wapiga zumari wetu na firimbi!! Maana wao kazi yao kubwa ni kusema kama vile watoto wa sanamu waliotiwa ufunguo au zile saa za zamani za ukutani, ukizijaza ufunguo — basi zitalia mpaka …….

Share: