Uteuzi wa Shein wawafurahisha na kuwaudhi wana CCM

Written by  //  10/07/2010  //  Makala/Tahariri  //  19 Comments

Na Salma Said,

WANACHAMA wa chama cha mapinduzi (CCM) ambao walikuwa na matumaini makubwa ya wagombea wao kuchaguliwa kuwakilisha Zanzibar katika kinyanganyiro cha urais wa visiwani kupitia chama hicho waonekana dhahiri kuvunjika moyo mara baada ya kutangazwa Dk Ali Mohammed Shein juzi usiku.

Hali hiyo imejitokeza mjini Zanzibar katika sehemu mbali mbali Unguja na Pemba ikiwemo maeneo ya starehe ikiwemo vilabu vya pombe ambapo baadhi ya watu waliamua kuvunja chupa ukutani kuonesha hasira zao juu ya kutochaguliwa kwa Dk Mohammed Gharib Bilal katika nafasi hiyo.

Juzi Nec ilimtangaza rasmi Dk Shein kuwa amechaguliwa kwa kupata kura 117 na kuwashinda wapinzake wake Shamsi Vuai Nahodha kwa kura 33 na Dk Bilal ambaye alipewa nafasi kubwa ya kupitishwa na Nec huku wafuasi wake wakiwa wamejiandaa kwa sherehe kubwa ikiwemo maandalizi ya ngoma na fulana maalumu.

Hata hivyo baadhi ya wananchi wakiwemo wana CCM wanaounga mkono maridhiano wamepokea kwa furaha uteuzi wa Dk Shein na kusema kwamba ni kiongozi pekee atakayeweza kuwaunganisha wazanzibari huku wakiwapongeza wajumbe wa Nec kwa kufanya maamuzi yaliozingatia maslahi ya taifa.

“Tumefurahi sana na tumepokea uamuzi wa Nec kwa furaha ingawa wengine wamekasirika ndio kama mnavyoona kule chupa zile zinavunjwa na wengine wamemwaga pombe lakini sisi tumefurahi na tunaomba wana CCM wenzetu tuungane ili tujenge chama chetu tusiwape mwanya wapinzani wetu” alisema Omar Ali Haji.

Uchunguzi wa Mwananchi Jumapili katika mji wa Zanzibar ulibaini usiku mzima na jana asubuhi katika vijiwe na kahawa na maskani za chama cha CCM zilibaini ukimya mkubwa ambapo sio jambo la kawaida ikiwemo maskani kaka ya Kisonge ambayo inajulikana kwa mbwembwe anapochaguliwa kiongozi wa CCM.

Maeneo ambayo watu walikuwa wakinywa vinywaji baridi huku wakifuatilia mkutano wa Dodoma ni pamoja na mitaa ya Maisara, Gofu, Kwa Raju, Ghymkana na hoteli ya Bwawani ambayo mwishoni mwa wiki hupata wageni wengi wa vinywaji.

“Hatujafurahi hata kidogo lakini hatuna la kufanya nah ii kuvunja chupa ni kuonesha hasira zetu kwa sababu chaguo la wazanzibari tokea uchukuaji wa fomu za urais wa CCM ni Dk Bilal” alisema Kijana mmoja.

Mazingira ya ukimya katika maskani za CCM jana mjini hapa zilifuatiwa na kuwasili kimya kimya kutoka Dodoma kwa kikundi cha wana CCM ambacho kilikuwa kimemsindikiza Dk Bilal kwa ajili ya sherehe ambazo zingeanzia huko huko Dodoma na kumalizikia Zanzibar iwapo Dk Bilal angetangazwa kuwa mshindi.

Baadhi ya wasemaji wa kikundi hicho kilichojumuisha maskani maarufu ya Kisonge cha mtaa wa rahaleo, walidai kwamba kutoridhishwa na mchakato mzima wa uchaguzi wa Nec kutokana na kushindwa mgombea wao Dk Bilal wakidai mgombea wao ndio anayekubalika zaidi na angeweza kukibadilisha chama na kukijenga upya kutokana na uongozi mbovu uliopo hivi sasa.

Baraka Mohammed Shamte ni miongoni wa wana CCM ambao walieleza wazi hisia zao za kutoridhishwa na ushindi wa Dk Shein na kusema kwamba katiba ya CCM ni mizengwe na inahitaji mabadiliko ya haraka ili wazanzibari wasichaguliwe kiongozi wao na watu wa Tanzania bara.

“Tumepokea uteuzi wa Shein shingo upande na baadhi yetu hatushiriki katika harakati zozote za kampeni ya uchaguzi kwa sababu sio chaguo letu na lazima katiba ya chama ibadilishwe wazanzibari tusichaguliwe kiongozi tuweze kuchagua wenyewe maana ingelikuwa ni kiongozi wa tanzania sawa lakini ni kiongozi wa Zanzibar vipi aje kuchaguliwa huku” alisema kwa hasira Shamte.

Shamte pia katika kujenga hoja yake hiyo ya kutoridhika na Dk Shein alihoji na kutaka Shein ataje mambo matatu mazito ambayo amewafanyia wazanzibari katika kipindi cha miaka kumi ya utawala.

“Hatujatendewa haki kwa kuachwa Dk Bilali kilichofanyika ni mizengwe mitupu na kuanzia sasa hatutakubali kuchaguliwa kiongozi tunasema wazi wazi kuwa hatujaridhika na kama tukiendelea na tabi hii ndio tunakimaliza chama chetu tokea hapo chama Zanzibar kinakufa kutokana na uongozi mbovu uliopo viongozi wote wanakiuwa chama na kiongozi pekee mwenye kuweza kukihuisha chama ni Dk Bilal” alisisitiza kada huyo.

Aidha alisema hata kama Dk Bilal atapewa nafasi nyengine ya juu (mfano makamu wa rais) bado kiu yao haijamalizika kwa lengo ni kuitumikia Zanzibar na sio jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Akizungumzia suala hilo Said Hassan alisema kwamba utaratibu wa kuchagua rais ndani ya chama Zanzibar ni lazima limalizikie Zanzibar kutokana na kwamba ni jambo hilo linawahusu zaidi wazanizbari wenyewe hivyo kuna kila sababu ya wenyewe kuchagua kiongozi wao bila ya kuwashirikisha viongozi wa Tanzania bara.

“Tuna masikitiko makubwa kwamba hatutaweza kuzungumza nanyi (waandishi) kwani tumepokea maagizo kuwa tusizungumze chochote kuhusiana na matokeo ya uchaguzi Dodoma ingawa hatukuridhika na tulikuwa na malalamiko yetu na dukuduku kubwa tulipanga kulitoa mbele yenu waandishi lakini …tunafuata maagizo na hivi sasa tunakwenda zetu nyumbani tukiwa na huzunikubwa” alisema mfuasi mmoja ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini.

Taarifa za awali zilizosambazwa kwa vyombo vya habari Zanzibar ni kufanyika kwa kutano wa waandishi wa habari na wafuasi wa Dk Bilal ambao waliondoka usiku wa juzi mara tu baada ya kutangazwa matokeo huko Dodoma na kuwasili bandarini Zanzibar majira ya saa 9:30 jana.

Hata hivyo taarifa za baadae zimeelezwa kwamba mkutano huo hautaweza kufanyika baada ya wahusika waliopanga kukutana na waandishi wa habari kuingia mitini kwa madai kwamba wamepata maagizo kutoka ngazi za juu kutozungumza chochote na waandishi wa habari na kutakiwa kurudi nyumbani kimya kimya.

Lakini baadhi ya wafuasi hao walikataa kutii agizo hilo wakilalamika kuwa hawakutendewa haki kwa kiongozi wao na kutishia kukihama chama na kuwataka waandishi wa habari kuhudhuria siku ya urejeshaji wa kadi za CCM kwa chama ambacho watakitaja baadae.

Mashabiki hao walionekana wakiwa na hasira kubwa walidai kuzivua sare za CCM ambazo walikuwa wameondoka nazo kwenda nazo Dodoma kwa ajili ya kusherehekea ushindi wa Dk Bilal lakini muda mfupi baada ya kutangazwa Dk Shein wamezivua na wameahidi kutozivaa tena.

“Tunaomba waandishi mtupe muda zaidi mtapata baadae na tunaomba hata hizo kamera zenu kwanza wekeni chini kwa sababu hatutaki kupigwa picha. Chama kimetuangusha na kimetuvunja moyo sana wana CCM Zanzibar, na tunajitayarisha kurudisha kadi za CCM lakini kwanza hatusemi tutajiunga chama gani” walisema mashabiki hao huku wengine wakiwa wamejifunika nyuso zao.

19 Comments on "Uteuzi wa Shein wawafurahisha na kuwaudhi wana CCM"

  1. zenjiboy 10/07/2010 kwa 7:24 um ·

    walevi tu hao, pombe ikitoka kichwani watarudia huko huko

  2. muarab 10/07/2010 kwa 7:43 um ·

    A a,wanaukumbi,jamani nduguzangu wakisonge naona siasa badohamjazijua,leo mnatueleza yakuwa mnataka raisi wa znz achaguliwe znz, nimaraisi wangapi wamepita na wote wamechaguliwa dodomaaa? mbona waliporudi kuwa waoo ndiowagombea wa ccm hamukuwakataa? sasa niwaulize siku zote mlikuwa wapiii? au mambohaya yameanza leo? kumbukeni wanapo shindana wawili mmoja hushindwa,na huyo SHEIN kumbukeni ni ccm mwenzenu au chama chenu hakiwataki watu wasehemu fulani? nakama ndio hivyo kwanini mlikwenda kutafuta wadhaminii?na kumbesiwenzenu? au baniyani mmbaya kiatu cheke………….? hamuachi nyinyi nakasumba mbovu,kumbukeni mnavyopanga nyinyi na ALLAH hupanga vyake,nia zenu hazipo safi ndio ALLAH kawafedhehi, namusipo piga kura nyinyi siotatizo kwani hamzidishi wala hampunguzi kwani mambo yote yameshapangwa kura saba zinatosha,nafikiri nyinyi nimashahidi yakua znz hapahitaji kura panahitaji kutangazwa tu, na tume ipo,nashukuru yakuwa na nyinyi mmeuonja utamu wa matokeo, wenzenu wamesha yazoeya, amakweli kichungu huonjwa,mimininawaombeni jamaa wa kisonge maskani dada,yakua muekitu kimoja muondowe tofauti zenu tumechoka namatatizo ,musitake kuanzisha malumbano ,kumbukeni muume wa MAMA niye………..?hayanimambo madogo na niyakupita tu,znz sasahivi tunahitaji umoja, utulivu,maelewano.na mshikamano,siasa za kibabe zimepitwa na wakati,mwishonasema ,makundi ndio mwisho,mahafidhina mwisho na maskani ndio mwisho, HONGERA MH SHEIN ,TUNAKUOMBA ALLAH UTUZIDISHIE AMANI NA UTULIVU AMIIN

    • pozitivu 11/07/2010 kwa 8:16 mu ·

      @ MUARAB
      aka? wewe mwarab mzima unamfagilia shein ambae hata dini hana, badala ya kumshauri asilimu kwanza, haya tuone sasa shein atapata kura ngapi z’bar ktk uchaguzi hapo oktoba, kwa taarifa yako tu, ccm z’bar ndio imefikia kikomo, maana jamaa zangu wote wa kisonge washaamua kuwa kwa sasa ni mtu kujitafutia riziki yake na familia yake basi, kikwete aibu kwako baba, mana safari hii labda ulete jeshi lako lije lipige kura hapa zanzibar, kisonge ndio hivyo tena, kura zilizobaki z’bar za ccm hata hamsini hazifiki, labda shadya karume awe amewaandikisha wale wanyamwezi wake wa tunguu wanaomlindia.
      mungu ibariki zanzibar yetu

  3. Annur 10/07/2010 kwa 7:44 um ·

    Hapa zenjiboy umenifurahisha kweli kweli. Tizameni wnavyo fanywa kama watoto wadogo. Eti hawana ruhusa kuongea na waandishi wa habari na wengine kujifunika uso kwa khofu, Iko wapi demokrasia wnayojidai kila siku.

  4. Mwinyi Mkuu 10/07/2010 kwa 9:28 um ·

    We all hit a time in our life when we become the victims of our own stupidity. Chalk it up to desperation, lapse in judgment or just sheer boredom. At some point or another, we all find ourselves battling against that little voice telling us, “C’mon… this is a great idea!” Then, you’ve got the people who never even bothered putting up a fight

  5. sarhan salim 10/07/2010 kwa 9:50 um ·

    salamu wazanzibar, cuf walisema 2005 safari hii hatukubali ngangari matokeo yake wakazungukwa mwembetanga wakapigwa mabomu ya moshi kwa muda wa siku tatu tena ramadhani, sasa nyie watu wa kisonge mmekwenda dodoma kwa vishindo na kelele mmerudi kimnya kimya kama maji ya mtungini , kumbe lile jina la makamando halikufaeni , mmegeuzwa mbwa koko , hayaa kina kina bakari shamte rejesha card ya ccm uje cuf tukushezeshe msewe

  6. kibakora jaz 10/07/2010 kwa 9:56 um ·

    A/Alaikum,nampongeza mh Shein kwa kuteuliwa kuwa mgombea kwa tkt ya ccm,kwa kweli ccm wametumia hekima kubwa kwa kuinusuru Zanzibar kwa kumchagua mh SHEIN .Visiwa vya znz vilikuwa ktk mtihani mkubwa lakini kwa uwezo wa M/Mungu wale wote waliokusudia kurudisha maafa ktk visiwa vyetu M/Mungu kawapeperusha,

    DR BILAL ni mmoja kati ya watu wakuogopwa kama ukoma ktk visiwa vyetu,bado tunakumbuka madhila makubwa ambayo hayatasahaulika na yatabaki kuwa historia ktk visiwa vya znz.

    Ndugu zangu hakuna kitu kibaya ktk dunia kama ubaguzi,nchi haiwezi kupiga hatua yeyote ya maendeleo ikiwa kiongozi wa nchi hiyo anawabagua wananchi wake mwenyewe ktk matabaka,hiyo ndiyo sifa ya komandoo BILAL .

    Mwisho namshauri comandoo BILAL,NA WANA MASKANI,WAHAFIDHINA,JANJAWID,COMANDOO SALIMINI WAKATAFUTE GONGO WANYWE NCHI YETU TUNAHIHATAJI VIONGOZI WENYE UPEO WA UONGOZI,UONGOZI WA KIDICTETOR HAUNA NAFASI TENA KTK DUNIA HII.

  7. mohamed ngwali 10/07/2010 kwa 10:37 um ·

    hao wanaosikitika ni waongo wanalilia ajira tu, siyo kama kiongozi wao ataleta maendeleo.dr bilal ni scapegoat. mwenyenzi mungu akujalieni mchaguliwe kiongozi huko bara.mkichaguana wenyewe kwa wenyewe si mtatumaliza pamoja mna vizazi vyetu. wengi wenu bado mna mentality za karne ya 19 kwenda chini, tumepindua, simwenzetu hamjuwi kwamba multiparty ni ushindani wa political ideology siyo uhaini.mimi si mwanachama wa chama chochote kile lakini ccm wametumia hakima ya hali ya juu

  8. obama2 10/07/2010 kwa 10:52 um ·

    ASALAM/ALAYKOUM, NDUGU ZANGUNI NAPENDA NIKUKUMBUSHENI JAMBO LOLOTE LENYE KHERI LZM WATATOKEA AKINA ABUJEHEL.

  9. obama2 10/07/2010 kwa 10:54 um ·

    ASALAM.NAMINI WALOUDHIKA WOTE SIO WANAOPENDA MASLAH YA WAZANZIBAR

  10. jumanji 10/07/2010 kwa 11:43 um ·

    HAYYAAA HAYYAA MAMBO YAMIVA MARA HII ZANZIBAR KWA MARA YA KWANZA TUTASHUHUDIA MBWA MARA HII ANAINGIA MSIKITINI KAMA WALIVYOSEMA WALE WAHAFIDHINA YA KWAMBA MPEMBA KINGIA IKULU NI SAWA NA MBWA KINGIA MSIKITI HAKUNA KWA KUKIMBILIA MARA HII KOTE MPEMBAAAAAAAAA

  11. mnyonge 11/07/2010 kwa 12:50 mu ·

    Nyinyi kisonge mlijinasibu kwamba mtafanya mapinduzi leo mmekuwa mnaogopa hata kupigwa picha HAHAHAHHAHAHA Mnaogopa camera mtaweza kufanya mapinduzi Shamte huna mpya wewe huna lolote rejesha card yako ya CCM Hiyo kama kweli wewe Kidume unaongea sana huna laa maana rudisha card tukuone kama kweli hukuwafiki matokeo ya dodoma wewe ulikuwa ushajipangia apate Bilal na wewe Upewe japo ukubwa wa MAJANJAWIRI UPINGE WATU BAKORA

  12. Heart 11/07/2010 kwa 1:08 mu ·

    Njaa na madaraka walio ahidiwa vinawasumbua tu, vinyamkera hivyo.
    Mh AMANI alipopitishwa kule DODOMA wanacc tulikereka na kupayuka ovyo ovyo mpaka maskani kaka KISONGE kama inavyijiita ikasambaratika ikazaliwa KACHORORA MASKAN kwakuwa wao walikua wanauunaga na wanaendelea kumuunga MH AMANI. Mikakati mingi ilipangwa ya kurejesha nyuma chaguo lile lkn siku ya mapokezi walijitokeza wale wale walimpinga na kumlaki kwa kua tu walitafakari wakaona watakosa FUPA la kuramba.

    Lakini sasa ni wale wale wamejitokeza tena kumpinga Dr SHEIN chaguo la ccm. Haaaahaaaa! haaaaaaa! msijifiche jitokezeni hadharani kwa majina, sura na kauli kama Shamte. Kadi zenu ngapi haaakaaaaakaaaa! chaachee na mtandao wenu mdogo na hauna nguvu yoyote dhaifuuuu.

    SISIM JUU JU JU ZAIDI!

  13. mhoma 11/07/2010 kwa 2:33 mu ·

    Imekua leo vituko kwenuu kuchaguliwa mbona mambo ya kawaida mumesahau historia, hasira hasara mnavunja chupa buree, mmenuna , leo mnaogopa hata kupiga picha,mmenywea kwani nyinyi mlitarajia nini baada ya kufanya uhuni wote hapo mjini pamoja na vipeperushi mna siasa za kale za kimasikani tu mtaelimika lini na mtastaarabika hilo ndio funzo hongera nec, walio wastaarab ccm wenzenu hawana kinyongo na alieteuliwa lakini walijua wazi kuwa nyinyi wahuni ndio mlomponza bilali dodoma na kwa waasisi wa mapinduzi msimtafute mchawi yeye mwenyewe Bilali hili analitambua, leo hii ati Baraka Shamte anasema chama kina mizengwe,ikiwa ww umeenda na mgombea wako dodoma kivyako chama hakikujui inayotakiwa na ccm ni NIDHAMU NA UTII NDANI YA CHAMA NA KWA KILA MGOMBEA NA WAPAMBE WAKE sasa nyie kisonge jiulizeni nani kamponza Mgombea mloenda nae,ongeeni basi na waandishi wa habari km nyinyi vidume,CCJ inatafuta watu znz umesikia Baraka Shamte,haki imetendeka dodomaa anayepinga angelikataa hapohapo holini,mbona ulikimbia unasemea unguja mia na kumi na saba nyingi sanaaa kwa hamsini na nne. Miaka kumi ijayo utasema na njaa yako.Ila poleni wana kisonge lamuhimu rejesheni kadi kama mnaziweza njaa zenu chomeni moto mashati yenu ya kijani hadharani tuwaone, msikae maskani mtafute shughuli nyengine za kufanya.huo ni usia wangu mduchu kwenu Umesikia Baraka Shamte na wahuni wenzako,Kigumu chama cha mapinduzi.

    • pozitivu 11/07/2010 kwa 8:01 mu ·

      mhoma hebu sikiliza kwanza ndugu yangu, ikiwa wewe unapenda haki basi ccm haitatokea siku wakatenda haki, hebu tiza walivyomnyamazisham samuel malecela, yuko wapi sasa, nawaambia wana kisonge wote wasikate tamaa kwani wao ndio wana uwezo mkubwa sana wa kuleta mabadiliko ktk ccm z’bar, kwanza tukampokee bilal kwa shangwe, halafu tujiandae kumpigia kura maalim seif kipenzi cha wengi hapa visiwani, ila seif nae eti nae kawapongeza nec ya ccm kwa kumchagua shein, yeye seif shariff anajua ni nini hasa kimetokea huko dodoma? bora anyamaze na yeye asubiri tumpigie kura< alichofanywa bilal safari hii aina mpya tu ya mapinduzi daima, ila safari hii mtindo wa kisayansi zaidi, bilal tulia baba njoo kwetu tukupe msikiti usalishe kwani wewe dini unaijua, mwachie SHEIN na urusi wake, shein hata dini hana kama yule dingi mwenye kadi namba 2 ya ccm ( kingunge), mzee wetu baraka shamte leo hii ndio unasema ccm ina mizengwe, mbona sku nyingi sana imeanza hivyo, hapa kwetu ni unafiki tu, ambao hautatufikisha popote.
      mungu atusaidie na zanzibar yetu

  14. depsis 11/07/2010 kwa 3:41 mu ·

    @ Bakari Shamte: Mizengwe umeiona leo tu alipopigwa chini Bilal? Mbona alipochaguliwa Salmin hukukataa matokeo na kusema amepita kwa mizengwe? Unataka upate wewe tu ukikosa basi haki haikutendeka.

    Kuimarika chama kumbe mnamaana ya kuimarisha vilabu vya pombe. Jamaa zako wamevunja machupa ya ulevi kwa hasira. Kamwe Mungu hatokuwa pamoja na nyie. Hii si silka yetu wazanzibari.

    Leo tumeona wazi kuwa Bilal kumbe ndio hauziki na handsome Shein ndio ana mvuto! Angalia kura alizopata zaidi ya mara mbili ya Bilali. Ni fujo na kelele za maskani tu zile. Debe tupu haliachi kukoroma. Bora hata Nadhodha basi ana wafuasi wengi zaidi. Almanusra amtie ng’ware Bilali.

    Hawa Kisonge nao ni sawa na mbwa koko tu. Kujitia kubweka lakini wakitishiwa na nyau basi wanakimbia. Kama nyinyi wanaume mbona mnaogopa kamera na pia mnaogopa amri za mabwana zenu wa Dodoma? Hamna jipya katafuteni mavi ya kuku mubanje!

  15. maalim 11/07/2010 kwa 11:11 mu ·

    Salaam.
    depsis ” nyau ” ndio mnyama gani? anatisha..? au Jogoo huyooo…?

    kisonge mpaka kisongeke.Wakipewa PIPI tu watanyamaza hao.

    Shukran.

  16. balozi mchafu 11/07/2010 kwa 11:38 mu ·

    ccm ni chama thabiti na chenye historia ndefu hakina mfano hapa tanzania…kuchaguliwa kwa maalim dr shein ni kwa ajili ya kuimarisha chama na kuondoa kasumba ya wazanzibar kutaka rais kutoka pemba kama seif…wanachama wa ccm wanaohuzunika kuhusu ushindi wa shein ni kawaida hawez mtu kushangiria kitu baadae akakosa halafu ukamuona anafurahia kushindwa kwake
    kidumu chama aha mapinduz
    chama halisi kwa watanzania(wazanzibari mumo humo)

  17. ashakh 11/07/2010 kwa 12:07 um ·

    @jumanji, taratibu baba. tunayo miezi 3 kufikia uchaguzi. Kipindi kirefu hichi kwa maisha ya mwanadam. Lolote likitokezea (M/Mungu tunusuru) kura inapigwa tena.

    Furahi kiasi tu ya mboga kuwa angalau mara tuna matumaini ya kuepuka hile shari ya chaguzi zilizopita. Huku wengi wakiwa na matumaini ya Zanzibar kupata usalama na umoja.

Comments are now closed for this article.