Login



Fotos

Get the Flash Player to see the slideshow.

Migawanyo

Kumbukumbu

Vipi tutainasua Zanzibar na kuleta maendeleo

Plan ya kuleta mabadiliko na maendeleo visiwani Zanzibar ni kama ifuatavyo:

  1. Kuondosha chama tawala na kueka cha pinzani au mbadala ambacho ni CUF.
  2. Kurekebisha au kuvunja kabisa muungano pamoja na upuuzi wote ulioletwa na Nyerere pamoja na Karume.Badala yake kufanya Zanzibar ni nchi huria kama ilivyokuwa hapo awali kabla ya ukoloni na uhuru wa 63.
  3. Kuanza kufanya mabadiliko ya mfumo mzima wa serekali ya Mapinduzi.JKU pamoja na vikosi vya SMZ kuwa ni jeshi kamili la watu wa Zanzibar.
  4. Kufuta kabisa dhana ya Mapinduzi, na badala yake kuwacha neno hilo kwenye vitabu vya historia.Badala yake maneno kama umoja na maendeleo ndio yashike hatamu.
  5. Kupunguza idadi ya wafanya kazi wa Serekali ya Zanzibar (kumradhi hapo watumishi wa Serekali).Lakini kwa mtazamo wangu serekali ina idadi kubwa ya watumishi, kiasi ambacho wengine hawana cha kufanya wapo wapo wanakula mishahara kwa kutumia gear za kujuana.
  6. Kubadili mfumo mzima wa kukusanya kodi na mapato pamoja na transaction zote za serekali kuwa zinafanywa digitally au banking system.Hii itafuta au kupunguza rushwa kwa kiasi kikubwa.
  7. Kubadili mfumo mzima wa elimu, badala ya Centralized System iliopo sasa.Serekali itatoa posho tuu kwa wanafunzi na kuendesha viwango vya elimu badala ya kuendesha mfumo wa elimu.Kwa mfumo huu manaake, mwanafunzi anaomba posho kwa serekali, jukumu la kusoma wapi ni lake na skuli zinahitajika kufanya ushindani wa ubora kumvuta mwanafunzi.
  8. Kupunguza majukumu ya Afya kwa serekali, badala yake kuacha sekta ya Afya kuendeshwa na makampuni ya bima.
  9. Kufungua milango ya wakulima kuuza biashara zao nje ya nchi.
  10. Kuhakikisha migogoro na siasa zinapungua badala yake Zanzibar kuwa na siasa za wastani.Hizi tulizonazo naziona kama zinadumaza maendeleo.

Hayo yote nilioeleza yanahitaji kubadili au kuvunja mfumo wa muungano.Kisa na mkasa wa umasikini wa Zanzibar ni complexity ya muungano usio na maslahi na visiwa hivyo.

Ukiniuliza mie vipi tutajinasua na muungano huo, basi hatuna budi kufanya maamuzi magumu.Maamuzi hayo yanaweza kuwa hata kujitolea muhanga vizazi vya sasa lakini kuhakikisha vizazi vyetu vya baadae vinakuja kuenjoy Zanzibar yenye maendeleo na ilio huria.

Waslaaam……..
mrfroasty

Share and Enjoy:
  • Facebook
  • Twitter
  • Digg
  • MySpace
  • del.icio.us

29 maoni Vipi tutainasua Zanzibar na kuleta maendeleo

  • ashakh

    Nitachangia sehemu moja tu. Kwani nyengine ni sera zangu nitazitangaza siku ya kampeni ikifika.

    Pale kwenye “dhana ya mapinduzi” naomba ibadilike na iwe “wananchi”. Tulimsikia Nahodha, Shamuhuna, nk wataendeleza mapinduzi. Tunakumbuka vilevile kwenye Baraza la wawakilishi Mhe Aboubakar alipoleta hoja ya kuendeleza msingi ya mapinduzi wajumbe waliipinga. Walisema kuna baadhi imeshapitwa ni wakati.

    Kiongozi yeyote atakae sema ataendeleza mapinduzi tumuombe atupe hiyo misingi ya mapinduzi anayotaka kuiendeleza. Na jee inakubaliana na wakati tulionao sasa.

    Mabadiliko makubwa yanhitaji ili kuiondosha dhana hii. Tuwaachie jukumu wananchi, ikiwa wao ndio waliokuchaguwa kwa kukupigia kura. Madhila yamewapata tokea kujiandikisha, kupiga kura, nk. Hata kuwashukuru na kuonyesha hisani juu yao kuwambia hii ni serikali yenu.

    Kwa vile raia ndie aliyekuweka madarakani pia uwekwe muundo wa raia huyohuyo kukuondoa madarakani. Tusiitumie dhana ya mapinduzi kwa kumtumia raia kukuweka madarakani, lakini ikawa mbinde pale anapotaka kukuondoa.

  • watila

    mapinduzi oyeeee 3
    kudumu chama cha mapinduzi
    mapinduzi daima nafkiri hii itadumu mpaka siku ya kiyama kwa vile zanzibar ni yetu zote

    • Mumengwa

      naomba tukubaliane na ukweli kuwa mapinduzi yalitokea, na kwa maana hiyo ni historia na wala haiwezi kupingwa.
      Ukileta hoja hz huoni km bado unataka kuendeleza sumu na kasumba zile zile tu. Mi kwa maoni yangu suala la mapinduzi tuiachie historia iwe hakimu.
      Muhimu ni kuitoa nchi katika makucha ya watanganyika, na kuwaendeleza wananchi wa jamhuri ya zanzibar.
      Ikifikia nchi kuwa na neema na uhuru kamili, dhana zote potofu zitaondoka……..Mungu ibariki zanzibar, na wananchi wa zanzibar.

  • virus99

    Ninakubaliana na wewe mengi ambayo umeyaandika. lakini sikubaliani na mtindo wowote wa kutumia nguvu zaidi ya kutumia busara za kuishitaki serikali ya Muungano na kutangaza mgogoro wa katiba !!

  • mstahamilivu ismail

    ASSALLAM ALLAYKUM ?
    NAAM MIMI MAONI YANGU KWANZA TUTOKE KWENYE HUU UKOLONI MWEUSI HAPO TENA TUTAJIPANGA NA INSHAALLAH TUTAFANIKIWA TU KWANI TOKEA HUKO MWANZO ZANZIBAR ILIKUA NI NCHI TENA YA KUPIGIWA MFANO DUNIANI NA HILO NDIO WALILOLIJUA HAO WAKAFIRI KINA AMERICA NA ENGLAND KWA KUMTUMIA NYERERE WAKATUFIKISHA HAPA TULIPO.NDUGU ZANGUNI MIMI NATOA RAI SISI KINACHOTAKIWA NI KUDAI NCHI YETU TU HAKUNA JINGINE TUKISHAPATA NCHI YETU MAENDELEO YATAKUJA BILA YA HIVO TUSIDANYANYANE HAKUNA LOLOTE TUTAKALOFANYA LIKALETA MAENDELEO. TENA HAPA NAWAMBIA HAO WEVI WATANGANYIKA HATUTAKI KUA NA MUUNGANO NA NYINYI TUNATAKA VISIWA VYETU KWA NGUVU AMA HIARI TUMESHAJUA KUMBE LENGO NI KUTUTAWALA SIO HUO MUUNGANO HEWA HATUNAHAJA NAO NA ANAETAKA HUO MUUNGANO HEWA BASI AENDE TANGANYIKA AKAUNGANE NA WEVI NA WENYE UROHO WA MADARAKA SISI WAZANZIBAR TUNA SIFA YA KUKINAI NA TULICHOJAALIWA NA ALLAH.

  • Abuu Said

    @Mrfroasty,
    wacha udumla huo na kuandika utumbo , unaongea kuhusu maendeleo hujasema hizo ajira zitatengenezwa vipi, kuhusu posho la wanafunzi serikali hiyo pesa itazipata wapi na kuhusu afya wanyonge wa mungu watapata wapi pesa za kutibiwa.
    Kuhusu chama kuvunjwa kwa chama cha ccm, wewe huoni kama viongozi wenu wote wa CUF wametoka huko na bado viongozi wajuu wa chama chako ni wanafiki, wasaliti na wasiokua na msimamo.
    Kuhusu kuvunjwa kwa muungano, kivipi muungano uvunjwe wakati chama chako pia ngome yake kuu ni bara huko , huku Zanzibar hawasubutu kufunya utumbo, ungea vitu vya maana kama vile serikali tatu na haki zetu zote za Zanzibar kurejeshwa na katiba ya nchi kubadilishwa na viongozi wote wa nchi kubadilishwa na kuwekwa viongozi wapya yaani new generation…
    Ahsanteni

    • mrfroasty

      Next time ukitumia lugha hizi za dharau kwa mjumbe mwengine, hatua za nidhamu zitachukuliwa.Heshima kitu cha bure, shukurani.

      Afterall unaonekana kama umepotea njia, kutetea uhuru wa Zanzibar kwa kuitoa nje ya Muungano ni ajenda kuu za mtandao huu.Soma malengo na madhumuni ya network kabla hujajiunga, hili limeandikwa hapo juu kwenye navigation documents.

      Hapa nakutolea quote:

      # Kusaidia Zanzibar kihabari, kuhamasisha jamii na kutoa muamko kwa wananchi wa Zanzibar ili wapiganie wawe na dola kamili ya watu wa Zanzibar na kuachana na upuuzi wa muungano.Kwa ufupi, MZALENDO.NET haina imani au haipendelei kuona nchi ya Tanzania

  • zenjiboy

    Nakubaliana na mtoa mada juu ya sera mbadala ya kuletea maendeleo Zanzibar.

    Nianze na hoja namba 2. Mimi kwa upande wangu sioni sababu yoyote na wala hakuna mtu wa kunishawishi juu ya suala la kuerekebisha Muungano, hapa cha msingi ni kuuvunja tu. Ikiwa watu hawa tumeishi nao miaka 50 wakiwa katika hila za kutumaliza tu basi hakuna siku ambayo watakuwa na imani na sie, tunaweza kushirikiana nao katika jumuiya ya Afrika Mashariki lakini tukiwa nchi tofauti.

    Hoja namba 7 na 8. Binafsi sikubaliani na sera yoyote itakayomfanya raia (sio wageni) kuchangia kwa njia yoyote katika huduma ya afya na elimu. Nanukuu kutoka sera elimu ya Iceland ‘everyone should have equal opportunities to acquire an education, irrespective of sex, economic status, residential location, religion, possible handicap, and cultural or social background’. Nchi ya Iceland pamoja na nchi nyengine za Nordic zina muono huo katika haki ya kumpatia mtu elimu. Kwa wale wanoshindwa kutafsiri ni kuwa ‘kuwe na haki sawa katika kuwapatia watu huduma ya elimu’ Hii pia inahusu huduma ya afya.

    Binafsi siamini kama ubovu wa huduma zetu za afya na elimu ni kwa sababu Serikali inajihusisha na kutoa huduma hizi, ila ni kwa sababu Serikali yenyewe ni mbovu na haijali maslahi ya raia zake. Iwapo tutaimarisha ufanisi wa Serikali ni wazi kwamba Serikali itaweza kutoa huduma hizi na nyengine kwa ufanisi kabisa na hakutakuwa na upendeleo au kukosekana usawa kwa sababu za tofauti ya vipato vya watu au maeneo wanayotoka. Utoaji wa huduma za elimu ukiwa chini ya Serikali pia unahakikisha mila na desturi za kizanzibari zinalindwa tofauti na ikiwa utakuwa chini ya sekta binafsi ambazo zinaangalia ushindani hata kama ni kupotosha mila zetu. Vile vile mimi sioni maana ya mtu kuwa na wasiwasi wa afya yake kwa sababu tu ameshindwa kununua bima ya afya.

    Utaratibu wa kubinafsisha sekta za afya na elimu ni utamaduni wa kimagharibi hasa ambao wanaona utu wa mtu ni pesa na si vinginevyo. Tukumbuke wakati Obama anafanya mabadiliko ya sekta ya afya Marekani aliitwa msoshalisti kwa sababu tu ameona kama wamarekani wapatao milioni 50 ambao hawana uwezo wa kujihudumia afya zao nao wana haki ya kupata huduma. Kwa wahafidhina wa kimarekani watu hawa hawakutimia utu wao.

    Kiufupi, mimi binafsi naamini Zanzibar amabyo wananchi wote (sio wageni, wakiwemo watanganyika) watapata huduma za afya na matibabu bure na kwa usawa bila kujali mtu anaishi wapi na ana uwezo gani wa kifedha. Suala je fedha zitapatiakana wapi? Jawabu tayari umeeleza, upunguzaji wa gharama zisizo muhimu kama wafanyakazi wasiokuwa na umuhimu pamoja na matumizi mengine kama magari yasiyo na maana, na ukusanyaji wa kodi uliokamilika na usio na mianya ya rushwa.

    Naomba pia utueleze jinsi gani utaweza kupunguza tofauti baina ya maskini na matajiri iwapo unaona hili ni muhimu katika kujenga uwiano minongoni mwa wananchi.

  • Mohammed Maalim

    Mrfroasty,

    Hicho ulichopendekeza kinaweza kuwa njia moja wapo ya kuleta mabadiliko ya kweli zanzibar, hata hivyo njia hiyo sio salama na ya manufaa sana kwa nchi yetu ya zanzibar. nadhani wakati umefika sasa zanzibar kuwepo na think-tankers wa kuangalia mambo kwa muelekeo bora zaidi. cha muhimu zaidi ni lazima yapatikane mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi na kwa kweli kwa njia zinazotumika sasa kwa maoni yangu hilo litachelewa sana. Aidha option ya kuvunja muungano “rakadha” itatuletea matatizo makubwa hata katika jumuiya ya kimataifa. Muhimu zaidi kama alivyosema mchangiaji mmoja kuwa tudai haki zetu kwa kupitia serikali kakamavu ya zanzibar kwa mfano tudai mfumo wa serikali tatu wenye kuipa mamlaka kamili zanzibar ya kujipangia na kusimamia mambo yake yote ya kiuchumi na kimaendeleo nk.

    vile vile nachukua nafasi kuwaomba wachangiaji na wajumbe wote tujaribu kutumia lugha nzuri na maneno mazuri yasiyoudhi sana, hayo ndio mafundisho ya dini. naamini ukumbi huu unaweza kusaidia sana kupanga mambo kadha wa kadha ambayo nayo yatasaidia kuleta mabadiliko na maendeleo huko visiwani.

    mungu ibariki zanzibar

  • zamko

    Natoa shukrani kwa ndugu mtoa mada na waliochangia.

    Mimi naungana na mawaz yote yaliotajwa kwenyemada hii, kuwa Zanzibar kama itapata viongozi wazuri wenye busara, elimu, uadilifu wa kiungwana ya dini na maendeleo. Basi tunaweza kujinasua na kuendelea. Lakini lamuimu ni UMOJA wa Viongozi na Wananchi kwa ujumla.

    Kuhusu Muungano ni lazima ufanyiwe markebisho makubwa sana, hii itawezekana ikiwa wazanzibari wote tuko kitu kimja na hatuna makundi kama hay yaliojitokeza hivi karibuni.(mfano: kundi la Bilali Karbu, kundi la Sheni, kundila malim Seif.N.k). Ndugu wazanzibari wa CCM na CUF yoyote atakae pata Uraisi ikiwa kura zimepigwa kihalali basi tumpe Support yetu na tuanze chepter pya ya mapambano ya kuifufua Zanzbar na watuwake.

    Kuhusu kufutwa kwa ukusanyaji wa kodi na kukusanya kodi kwakupitia DIGITAL BANK. hili ni wazo zuri sana na tutafuta rushwa kwa iasi kikubwa sana. nakupa hongera mtoa mada.Hata nchi zilizoendelea EU countries zinafanya hivyo, kila bussines transucions na Other Charges zinapitia kwenye Digital Bank automatical.

    Kwamawazo yangu:
    Elimu kama alivotoa mawazo ndugumtoa mada, naongezea kidogo tu. kuwe na mfumo mpya wa Elimu ya msingi na sekondari: Specialisation ya subjects, wanafunzi wapewe fursa ya ku-specialise na subjects wanazo zifamu vizuri. kuliko kuwa force watoto wasome subjects zote.Small subjects its the better, understanding.Mtu aliekua ni mzur wa science aelekee kwnye fani hiyo, aliekua ni mzuri wa Electric aelekee kwenye electric n.k

    Jeshi:wazanzibari tunatakiwa tuwe na sera kama za Waisraeil, kila family itoe mtoto ambae atajiunga na eshi la polisi,FFU,JKU naUsalama. Hii iwe nilaw ya kila Mzanzibari halisi, lazima atoe mtoto mmoja.

  • Big Boss

    Asalam alykum
    Kwanza kabisa kwa ndugu zangu mliochangia ambao mna TONGO za MUUNGANO, huu Muungano ambao mnasema kuuvunja itatuletea matatizo makubwa, jee hamuoni hivi kuwanao ni matatizo makubwa zaidi!? jee mnajua makubaliano ya muungano? au ni siri kali? Kama ni siri utafanyaje kitu bila ya kujua malengo? au lengo ni ile sera ya CCM ya kuifuta ZANZIBAR katika map ya dunia?

    Kama wewe ni Mzanzibari ujuwe hii ni nchi yako na ni haki yako kukilinda chako na Mwenyezimungu ametwambia TUSIDHULUMU WALA TUSIDHULUMIWE.
    Naam nafikiri kinachotendeka kwenye unaoitwa muungano sote tunafahamu. kwazi kwenu (kwetu)

    @ frosty, nakubaliana na hoja zako isipokuwa moja tu kuhusu suala la afya, hili bado liendelee kuwa jukumu la Serikali kwani nnaamini iwapo yatatekelezwa hayo mengine ulioyataja basi Serikali itakuwa na uwezo mkubwa wa kulishughulikia hili na mengine kwani itakuwa na fedha za kutosha, nategemea hata jirani zetu Tanganyika wakija kuomba msaada tunaweza tukawafikiria baadhi ya wakati , pengine itamsaidia pia Kikwete kwenda kuomba Marekani akaja kuomba ZANZIBAR.

  • muhimu

    hahhaa huu mfumo haufai ata kuongoza shehia moja si kwambii nchi basi raha ingekuwa kuandika mambo kumi tuu ushakuwa na maendelo sahauni mushapata sera ya sefu nyie siku 100 mara ohh mambo kumi but hakuna hata mtu mmoja anayefanya uchunguzi in detail akataupa data vipi utafanikiwa hayo mambo yako
    kama ivoo na mie nitakuj anitandika ooh tufanye hivi tufanye vile but kwa mdomo tuu without feasibility study ?tupe uchunguzi wa kina vipi mambo haya yatawezekana

  • shamuhuna

    Wazungu huwa wanasema”its easier said than done”…ni rahisi sana ukakaa kwenye kiti na kuandika huo utumbo ulooandika hapo,ila hakuna mtu yeyote atakae kabidhiwa dhamana ya nchi na kufanya utumbo huo!!..

    Wewe(mrfroasty)umetoa mapendekezo yako hayo jee umeangalia apande wa pili wa hayo mapendekezo,umeangalia ni jinsi gani tutatengeneza hizo nafasi za ajira na kuleta maendeleo..Kuna vitu mtu anapokuwa rais anatakiwa kuvitizama ma macho saba na hayo uliyosema ndio moja wapo!!yawezekana ikawa hayo ni mawazo mazuri..ila me bado sijaona suluhisho na wala sifikirii kama atatokea rais yeyote atakae yafanya hayo bila ya kuwa na suluhisho!!..

    Ushauri wangu kwako mtoa mada..isome jamii ya wazanzibar,yatafakari maisha ya zanzibar na itafakari zanzibar na mipaka yake,kisha fikiria tena hayo uliyo yafirikia..mimi nina uhakika kuwa wewe hauna elimu ya kutafakari uendeshaji wa kitu(management)hususan jamii..so bora waachie wenye uelewa tuu!!..anyways..mawazo ni mawazo..yanaheshimiwa ila hayafuatwi!!

  • Mohammed Maalim

    Big Boss Assalaam alaikum,

    nataka niweke sawa kuwa mie sina tongo za muungano hata kidogo lakini najaribu kuliangalia suala hili kwa upana wake ndio nikasema nakubaliana na Mrforsty lakini kuvunja muungano “rakadha” yaani kwa kishindo itatuletea tatizo. naomba nawe ufikirie hilo kwa upana kidogo. suala la kuwa hati ya muungano au makubaliano hilo kwa hoja hii halina uzito maana muungano huu upo na unaendelea kuimaliza zanzibar. nilipotoa mfano wa serikali tatu maanaake zanzibar ipate mamlaka zaidi na hata kama hilo litapelekea kudhoofika na kisha kufa kwa muungano itakuwa njia salama ya kuirejeshea zanzibar hadhi na haki yake. hilo linawezakana kama zanzibar tutakuwa na serikali madhubuti ya kuwaunganisha watu tukadai haki zetu kwa mfano hili la mafuta, elimu ya juu. fedha, kodi nk na hatimae ukapatikana muundo wa serikali tatu mbona itakuwa tumekwenda kwa mwendo mdundo. Wakati unafikiria kuwa ni rahisi kusema zanzibar tuvunje muungano fikiria zaidi kuwa huu muungano unatambulikana kimataifa ni halali hivyo jaribio la kuuvunja waziwazi litapingwa hasa kwa kuzingatia historia ya zanzibar. kumbuka kuwa hata muungano wenyewe ulikuwa na mkono wa mataifa makubwa kama marekani na uingereza hivyo inabidi tuwe makini na mambo yaende kimkakati. nakubaliana na hoja kuwa zanzibar ikipata uhuru wa kujipangia na kujiamulia pamoja na kusimamia mambo yake bila kuingiliwa na tanganyika itaendelea sana hata ndani ya siku mia. hivyo vitu kama maji, afya, elimu, nyumba na maisha kwa ujumla yatakuwa mazuri mno na nchi yetu itakuwa ya kupigiwa mfano katika ukanda huu. lakini waswahili walisema vishindo vingi havifanyi jambo. nadhani nitakuwa nimeeleweka nilichokua nakikusidia kukieleza

    mungu ibariki zanzibar
    shukran

  • Ghalib

    KAZI KWELI KWELI
    Ndugu muandishi nakubaliana na wewe ila na mimi nitarekebisha kitu kimoja.
    Badala ya kusema mapinduzi tuseme wananchi ( serikali ya wananchi wa zanzibar) tukiwa na bendera yetu na na uwakilishaji wetu kwa utaifa wetu passport.

    mimi naweza kusema ili zanzibar kuwe na maendeleo kwanza kuvunjike muungano hewa,japokuwa utatuathiri kiasi kikubwa naambini wazanzibari wako taya kuvumilia kwani wamechoshwa na muungano huu hewa,pia utakapo vunjika muungano itachukua muda kuwa katika hali ya standard kwa zanzibar kama huduma za umeme tutakuwa hatuna kwa umeme ni kutoka bara,na mambo mengine madogo madogo.

    Pia ipo haja ya kuwatoa viongozi wote hawa kwani wameshakuwa walemavu wa akili na wameshindwa kutuletea maendeleo kwa kipindi kikubwa sasa,kwani hata hao cuf mwanzoe walikua ccm,sasa tunahitaji viongozi wapya wenye elimu na busara na wenye confident ili waweze kutuongoza,pia katika suala la maendeleo hapo yatafutalia taratibu huku tukijipanga kama ni serikali mpya kwani maendeleo hayaji kwa haraka.

    Tuondoe hawa walemavu wakaili kwanza katika madaraka wasio kuwa na imani na zanzibar,tuingie wenyewe vijana tusonge jahazi au vipi wenzangu ?????????????????

  • mpigaduri

    Kupunguza idadi ya wafanya kazi wa Serekali ya Zanzibar,hahah so ikisha uwapeleke wapi,wawe majambazi au ?nchi yenyewe haina viwanda,au jku wazidi kupiga w2 makwaju..hlf Kupunguza majukumu ya Afya kwa serekali, badala yake kuacha sekta ya Afya kuendeshwa na makampuni ya bima.zanzibar si uingereza sheikh,hicho kitu utawaua w2 bure kwanza idadi kubwa ya w2 ni maskini maskini wanategemea jembe km hujui usione w2 town wanaishi frsh wakafikr w2 wanalingana,m2 anaishi kwa alfu mia tano hlf umwambie ajilipie bima ya afya,nenda katembe vijijini uone w2 wanavyoishi.

  • Big Boss

    @Ghalib
    Huo umeme hao Tanganyika hawatugaii bure, tunanunua tena si kwa bei ya udugu wala kwa bei ya ujirani, wanatuuzia kwa bei ya kukandamiza!! (mukome!)

  • Ghalib

    @big boss
    Tambua kwanza huu umeme tunanua na tena kwa kukomolewa,ngalia sasa tuna muungano hewa huu wanatukomoa,je tukivunja itakuwaje,serikali itashindwa kuendelea umeme huu,kitakachofuata ni kutafuta vyanzo vipya vya umeme,kabla ya mapinduzi zanzibar ilikuwa inajitegemea kwa umeme wake,na waliuwondo hawa walemavu wa akili ili tuwategemee bara kwa kila kitu,na ndipo pia wakaiyuwa tanyanyika,ni taratibu zao na ujanjwa wao kutumaliza na sasa tunaelekea ukingoni kuwa mkowa.

    big boss hatuna umeme,umeme wenyewe wa mgao.

  • kindy

    Mafrost maneno ulosema ni sawsaw japo tunapingana kwa baadhi ya point basic turejeshewe nchi yetu tuliambiwa hatutolazimishwa sasa na tuulizwe wangapi tunautaka na wangapi hatuutaki hilo labda watalifanya baada idadi yao kutuzidi hio ndio njama kwa mwendo tunakwenda hivi sasa hatutofika kila miaka 5 tungojee hayoo ya mwisho wa mwezi tujue wapi tupo

  • kibakora jaz

    Nakubaliana na wewe mia kwa mia na naamini hayo yanawezekana ikiwa atapatikana kiongozi alie na uchungu na nchi yake,pia awe na vission ya kuona mbali na hiyo ndiyokazi ya kiongozi kwa nchi kama znzibar.

    Nchi yetu ya znzibar inahitaji mtu alie na uwezo wa ku create mambo ambayo yataliongezea taifa pato pia kupatikana kwa ajira kwa vijana ,ama tukisema haiwezekani,serikali pesa itapata wapi hayo ndiyo hayo tulionayo sasa hivi yanayoitwa mawazo mgando.

    Kuhsu muungano hewa uliopo mimi nadhani ni kuuvunja bila kufikiria chochote,kwasababu hawa jamaa zetu hawana nia njema kabisaa kwa zanzibarna kila anaekuja anafikiria vipi aimalize sio kuiendeleza.

    Tatizo tulilonalo la muungano huu ni kwamba hauko wazi kila mmoja akajuwa tumeungana vipi?Ni siri inayoendelezwa bado iwe siri,swali ni kwamba jee siri hii mpaka lini?kwanini Wazanzibari tunaruhusu ujinga kama huu uendelee?

    Napenda kuwakumbusha kitu kimoja tukubaliane kwamba huu muungano uliopo ni LAANA na laana hii haiondoki ikiwa sisi wenyewe tunaishabikia,miongoni mwetu tunao wanaoshabikia laana hii kwanza kabisa ni wale wanaosema wataendeleza mapinduzi.

    Hivi niwaulize hayo mapinduzi yalikuwa ni kitu kizuri kiasi kwamba mtu anajigamba kwamba atayaendeleza?

  • ukwelituu

    Nakataa kwa yoyote anae sema mungano hauna faida.muungano unaleta faida nyingi sana.Nitazitaja kwa ufupu hizo faida yakwanza ni mungano unamaliza uisilamu znz.mungano ni batili.mungano unajaza majambazi.mungano unaharibu vijana wa tifa la leo. mungano haramu.mungano umetuwondoleya paspoti.mungano unatuleteya ukimwi.mungano umetulaza miezi 3 bila ya umeme. mungano umetulisha mchele mbovu mungano unataka kufuta ramani ya znz.mungano umefanya vijana mashabab mpaka sasa hivi hawana hata uwezo wa kuwoa mke kwa sababu ya hamna ajira. mungano unataka kuiba mafuta yetu.mungano umewafanya viongozi wetu wawe mashwain

    kuhusu mapinduzi.hawo wote waliyoyafanya hayo mapinduzi filnari jahanama.

  • mrfroasty

    @ Abuu Said, muhimu , shamuhuna

    Nimetoa maoni yangu sijatoa amri uwezo huo sina, wala sijasema kuwa mimi nataka kugombea urais.Hio niliotoa hapo ni step-wise plan ambayo ni maoni yangu binafsi.Plan hio haina ugumu wowote ni maamuzi tuu ya wazanzibari wakiamua leo kesho linakuwa.

    Hoja nambari 1 ni kuchachamaa kwa wananchi na kudai kilicho chao.

    **Tumeona nchi nyingi tuu zikiwemo Ukraine watu walivyo chachamaa na kupinga matokeo ya uchaguzi.
    **Tumeona Eritrea watu walivyopoteza uhai kutetea haki yao.
    **Kenya
    **Kwa Mugabe etc…

    Hivyo hili linawezekana sana kuhakikisha matokeo ya uchaguzi yanaheshimiwa.Kwa mujibu wa takwimu za International Observers CUF hushinda chaguzi zote Zanzibar, na badala yake matokeo kupangwa Hoteli ya Bwawani kwa kushirikisha vyombo vya Usalama na majeshi mengine ya Tanganyika.

    Sasa wananchi wanatakiwa wadai haki yao, wamechagua serekali wasimamie kidete kuhakikisha wanaipata serekali waliochagua na si vyenginevyo!Hili si jukumu la Seif, ni jukumu la wazanzibari kuhakikisha wanapata walichokichagua!

    Nukuu:
    **Kwa ufupi step-wise plan hio inatekelezeka na wala haijazungumza vitu vya maajabu.Sekta ya Afya kuachiwa makampuni ya Bima ndio njia sahihi nchi zote zilizoendelea zinafuata mfumo huo.Hapo kama kutakuwa na wananchi hawana uwezo ni kulipwa posho ya bima ili waweze kumiliki bima ya afya.

    Maasalaam,
    mrfroasty

  • muunguja

    @mrfroasty
    unaongea vitu lakini huna data ya kusuport point zako.typical like african politician kwamfano umesema sekta ya afya kuachiwa makampuni ya bima sasa hebu elezea vipi hiyo process inavyokwenda.ninavyoelewa mimi hii system ambayo wewe unaitaka sasa hivi obama anaipiga vita kwasababu watu wamerikani million 50 hawana bima ya afya.sasa hao ni matajiri sembuse sisi mburu matari,asilimia ya watu wengi znz ni masikini na hawana kazi sasa niambie kampuni gani ya bima itakupa health insurence kama huna kazi.
    mfumo amabo mimi naona unafaa kuhusu afya ni ule kama wa uk,canada,france n.k
    health services is free for anyone but kuna mkato wa kila mfanyakazi na makampuni amabo unaitwa national insurence or social security.sasa pesa inayopatikana inakwenda kwenye huduma za afya direct not makampuni ya bima.uzuri wa mfumo huu ni kwamba kwa yule amabaye hafanyi kazi still anafaidika na huduma ya afya na vile kama una earn mkia wa mbuzi basi rate yako ni ndogo vile vile.kumbuka makato hayo ni tafauti na income tax.sasa tuchukulie wafanyakazi znz ni laki 4.sasa ikiwa kama kila mmoja atachangia tzs2000 kwa mwezi basi mapato yatakuwa 800 million sh per month.sasa hesabu ya haraka haraka uki convert na dollar ni kama $600,000.
    sasa huo ni mfano lakini naamini mkato uwe more than 2000 basi tutakuwa mbali kwa huduma za afya .maji n.k
    kwa kuongezea naona wakati umefika kwa watu kuchangia huduma za maji .makato yawe reasonable lets say 500tz sh for every household each month or year.hii itasaidia uendeshaji wa mashine za maji na miundo mbinu pamoja vitendea kazi kwenda smooth ili kuondoa tatizo sugu la maji.

    • mrfroasty

      Marekani wana matatizo na mfumo wao wa afya, sina uhakika tatizo nini lakini mfumo wao ni mbovu kwa kulinganisha na EU.

      EU ndio mfumo bora na ndio unaotumika na nchi takriban zote za bara hilo.Kinachofanyika kwa wasio na kazi hupewa posho ambayo ndio hio nadhani unayoita Social.Hii posho ndani yake kuna budjet kamili ya kula, kuvaa na kulipa bima.

      Bado napingana na wewe kuwa UK huduma za Afya ni bure au zinaendeshwa na serekali.Kinachofanyika ndio hicho ninachokizungumza mimi kupunguza majukumu kwa serekali na kuongeza ufanisi.Sina uhakika sana UK kwani kidogo naamini wako nyuma kwa miaka kadhaa ya maendeleo kulinganisha na nchi zengine za EU (fact hio sio pumba).

      Lakini nina uhakika nchi zengine za EU kila mtu analizimika kukata bima ya afya.Hii ni lazima kwa katiba zao kila raia awe na bima, na ukiwa huna unaweza pandishwa mahakamani kwa kuvunja sheria.

      Sasa hapa nadhani mfumo ndio ule ule huduma ya afya kwa kila mtu hata masikini asie na kazi.Nasema kuwa ni sawa kwa vile huduma itapatikana kwa kila mtu, na wasio na uwezo watapatiwa Social au posho kwa ajili ya kulipia huduma hio.

      Kilichopatikana ni huduma bora kwa kuongeza ushindani wa mahospitali.Na zaidi ya huduma bora, pia jukumu la kuendesha sekta ya afya linakuwa limeondoka kwa serekali.

      Maasalaam,

  • Ghalib

    @mrfroasty
    kuna watu wapo ulaya hapa lakini hawajui hata ile pesa inayo mtibu inapatikana wapi,wako tu kama madudu,mfuko wa kukusanya insurance si upo lakini kule bara wanaita NSSF ( NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND) na hapa zanzibar unaitwa ZANZIBAR SOCIAL SECURITY FUND(ZSSF) Jee sector hii ni ya nini,na wafanyakazi wanalipia,lakini wanaolipa ni wachache wanaonekana

    hii inahitajika kwa kila anafanya kazi yoyote ile alipe,hata uburuze rikwama,uchangie ufuko huu,sasa sijui bima gani munayooiyongea nyie hebu nifahamisheni,nilipokuwa tanzania nalipa kwa mwezi mimi elfu 20,000 hapo bara,na lazima ulipe, jee zanzibar munalipa mfuko huu kila mtu ? kila mkaazi wa zanzibar anatakiwa awe anayo number yake katika mfuko huu,achangie kila mwezi inategemea na kipato chake.

    suala la muungano,marekebisho ya muungano,kwanza irudishwe TANGANYIKA,kuwe na serikali 3
    tanganyika ,zanzibar na tanzania,sio kutugeuzia tanganyika ikawa tanzania,mukae vikao elfu kumi tatizo halimali,na hakutokuwa na fair,this unfair dismisal.

  • mrfroasty

    Nilichokusudia mimi hapo juu ni bima ya afya, yaani Health Insurance.Hii inalipa malipo kwa hospitali kila mteja wa insurance anapoumwa au kutumia huduma za afya.

    Nimejaribu kueka sawa kidogo, maana inaonekana kuja kuchanganyika na Social Security Funds.Social Security Funds kwa mfumo wa Tanzania, ni pesa za Pension nilivyofahamu mimi.Kiilivyo naona vijana wengi hukimbia kukatwa mishahara yao kwa ajili ya matumizi ya uzeeni.

    Hizi NSSF na ZSSF zinahusika na hio kwa kiswahili inayoitwa pensheni, malipo unapoacha kazi.Vijana musikimbie kuilipa hii, ni muhimu kuna siku utazeeka!

  • Ghalib

    Ni kweli mrfroasty hata mimi nikiumwa basi ndio nilikuwa natibiwa kwa hiyo number yangu na tena,na bila ya kuwa na number hii gharama juu yako,lakini mimi naweza kusema wengi wetu hatujui nini maana na ZSSF,na vipi itatusaidia,kwa kweli mimi nilikuja kujua wakati nipoanza kazi,tena katika company kubwa nikilipa nikikatwa pesa hizo,ndio nikavuta picha kutoka nchi za njee

    ZSSF kila mzanzibari lazima ajiunge na kila mtoto akizaliwa apatiwe number ya kutoka idara hii ZSSF, na pia kila mzanzibar achangie,kwa kila mzanzibari lazima mfuko huu,tukitoa mbao ya tax,ili tuweze kusaidia taifa,isiwe tu kwa mtu fulani,pia kitengo Cha ZSSF kiahamasishe watu nakieleze faida ya kuwa na zssf na pia iwalazimishe,hata unapompeleka mtoto skuli lazima awe nayo hii number ni muhimu sana,

    MR afroasty nakuomba tuletee mada hii ya afya ni muhimu sana tuichambue zaidi,tupige kampeni ya afya,hapa znz ili iweze kuwasadia kwa wale wasiokuwa na uwezo.

    ZSSF ni muhimu sana kwa kila mtu kuchangia,tusiwe wagumu jamani,serikali ina majukumu ya kulazimisha hasa naona mimi.

    leteni mawazoo au nipo wrong jamani

  • mkarafuu

    Salam.

    Mimi kwenye mada hii sitachangia kwa vile uwezo wangu ni mdogo kwenye haya, lakini pia mambo haya yanayohusu hatma ya nchi yanahitaji muda wakufikiria na umakini wa hali ya juu ili kutoa mchango unaofaa.

    Nitaendelea kua msomaji wa maoni ya watu hadi pale nitakapo pata mawazo na mimi ya kuchangia ndio nitafanya hivyo,na hili nawaomba wenzangu wafanye kama mimi kama hawana chakusema wanyamaze sio lazima wachangie,ni bora kua msomaji tu.

    Mtu angalijifunza hicho kilicho andikwa, hadi akipata mawazo na yeye atoe mchango wake ,kuliko kukosoa maoni ya mwenzako na kuyakejeli na kuonyesha dharau na kuishia hapo, bila ya kuonyesha nini kilicho bora zaidi yakile alichokifikiria mwenzako.

    Nachukua nafasi hii kwa kumpongeza sana MUUNGUJA pamoja na kua tunaelewa kua anaipenda CCM sana,lakini uzalendo pia anauonyesha kwa kuchangia mambo mengi yanayohusu Zanzibar,pamoja na kupingana na mawazo ya baadhi ya wachangiaji lakini hukosoa na kutuonyesha suluhisho kwa kile anacho amini yeye kua ndichokitakacho faa kwa mtazamo wake.

    Huu ni mfano wa kuigwa kwa wachangiaji humu mzalendo.net na hapo ndio tutafika kule tunakotaka kuenda.

    Hakuna haja ya kudharau mawazo ya mwenzako,bora kuyapinga kwa kutoa yako unayoyaamini nibora,huenda kwa kufanya hivyo tukapata kitu kizuri zaidi na tukaishawishi serekali au viongozi kutumia mawazo yatokayo humu kuendeshea sekta fulani ambayo imejadiliwa na tukaona yatafaa mawazo hayo kwa maslahi ya Zanzibar tuipendayo.

    AHSANTENI.

  • zamko

    Sinabudi ilakutoa shukrani zangu kwa ndugu Mfroasty kutuletea MAONI yake na kuwapongeza nduguzangu wengine ambao wamechangia mada hii. Eitherway, wengi wa wachangaji walikua wamebanwa na wasiwasi wa ushindaniau kutaka kujua ufafanuzi wa vipengele vya mada hii. Kama vile Bima ya Afya (Health Insuarance Tax). Sina budi kuungana na ndugu yetu MUUNGUJA kwa maazo yake ya Bima ya Afya, kwamba kuna nchi kama Uk, France, Canada na hata hapa Scandernevian countries wanatoa matibabu ya afya kuwa ni ya Free.

    Lakini kuna mchango ambao unatolea na kila mtu mwenye kufanya kazi anachangia kwamujibu wa income yake. However kuna NHS (Natinal Health Service)kwa kule UK Canada,France Danmark n.k Hizi NHS ziawatibu hata mtu akiwa mgeni, kama kaumwa na kapelekwa hospital basi anatibiwa. Lakni mgeni huyu hapati farcilities zote kama vile mwenyeji /mtu anayelipa Bima.

    Kwa wale masikini wasiokua na kazi au lower Income Nchi kama za EU wanawapatia Raiya wao hiyo Social Benefits ambayo inalipia mambo mengi kama mfroasty alivoeleza na hata hiyo Bima. Sasa kwa upande wetu Wazanzibari/Zanzibar hili nijambo moja kubwa lilikuwako kwenye Manufestor ya chama cha CUF:

    CUF wakipata serikali, walikua na nia ya kuanzisha hizo National Insuarance Cards (kama hawajabadlisha manufestor yao).Hii nikua Wananchi wote wataweza kuchangia direct au indirect. Na wataweza kunufaika na huduma za Afya.Sasa kama kunamtu anataka luctiory na anapesa atakua na fursa yakwenda kwenye Private Hospital. Na pangu pakavu kama mimi, huyu atatibiwa bure kwenye General Hospital

    OOOPS ….Sorry MUUNGUJA, najua utanambia mimi naipenda CUF::::: Lakini nibora niseme kile nilichokiona, Sasa ikiwa kweli tutapata seikali mpya.Na hawa CUF watakua niwatendaji au watapewa Serikali basi. Wazanzibari tusubiri tuwaone kama nawao watatuletea mabadiliko au watakua nikama hawa waliopita.

    Mawazo yangu:

    Kuhusu Elimu ya Bima na ulipaji wa maji,umeme,kodi ni kitu muhimu sana kupatiwa wananchi elimu hiyo. Hiiitawafanya waelewe FAida na Hasara za ulipaji Bima, tax n.k.Kwani sasa hivi wananchi wanapiga kelele yakulipa maji na kodi ya kichwa. Hii nikwasababu hawazioni faida zake. Mbona sisi tulioko Uhaibuni hatupigi kelele tena?
    Kwasababu tunaaona manufaa yakulipa Tax. Japokua mtu aikiita ambulace saa nyengine inachukua muda wakuja hasa wakiona kama mtu hana jina la kizungu. Lakini tunapata huduma hizo.

    Elimu ya huduma za jamii haiwezi kupatikana ikia tutakua na uongozi wenye mawazo Mgando. Kama huu tulionao sasa hivi, kila kitu mtu anachokibuni anaambiwa anataka kuvunja muungano au ni adui wa Mapinduzi. huduma hizi zitapatkana pale ambapo tutakua na Serikali mpya, na sera mpya za Siasa ambazo zinatambua haki na maendeleo ya jamii.

    Kuhusu Muungano unaweza kuvunjwa lakini sikwapupa kama watoa mada wengine wanavofikria. Tukae tufikirie kwamba sisi hatuna Jeshi wala bahari yetu haina ulinzi wowote ule. Tutakapo vunja muungano kwa ghafla ghafla tunaweza tukavamiwa na hata hao mataifa ya nje. Ambayo wanatuona sisi tunataka kurudia kwnye cominist au Uislamu. Mimi naungana na mawazo yakudai serikali Tatu.

    wananchi watakao piga kura wasilale tuuwakasubiri bwawani iwabadilishie mtokeo.Kama haki haikutendeka mara hii Maandamano na solidarity ya wazanzibari wote wa nje na ndani ndio itatuletea mabadiliko zanzibar. Tusiwaachie ndugu zetu wa Unguja na Pemba kuandamana pekeyao. hata walioko nje wanatakiwa wafanye hivo. Najua kunawatu watanicritisise kwamba niko nje ndio nachochea. Lakini waangalieni Wa-Georgean, Wa-Bosnia,Wa-Ukranian, Wa-Checkslovakian,Wa-kenya n.k

    Lakumalizia Umoja ni nguvu na ushikamano ndio ngao yetu wazanzibari, kwanini tugombane na tukejeliane kwenye mtandao. Kwa wale waliokua hawana mawazo ya kuchangia nawajisomee na wakae kimya badala ya kukjli-kejeli.

    Idumu Zanzbar na watu wake