Visiwa virudishe asili yake, silka na utamaduni wetu.

Written by  //  09/09/2010  //  Makala/Tahariri  //  5 Comments

Na.B.OLE,

Kila jamii ina asili na hulka yake na mara nyingi hufatana na mila, desturi na silka za watu wake katika jamii inayohusika. Asili huandamana na haiba na mapenzi ambayo hujenga udugu na upendo miongoni mwa wahusika, pia huwa ni itikadi yenye kuonesha asili au chimbuko lake katika maisha ya kila siku.

Ikiwa itikadi hiyo itafuatwa ipaswavyo,bila shaka hapo ndipo utapoikuta jamii ile inaishi kwa furaha na faraja,Wanajamii wakifurahia matunda mazuri yenye baraka, upendo na ufanisi, kinyume chake ikiwa jamii hiyo hiyo itapuuza na kuiga mambo ambayo hayakuzoeleka na wala hayana faida na wao, basi ni dhahiri jamii hii itaharibika nakupoteza mwenendo mzima wa maisha yao.

Wazanzibar hatuna budi kujiuliza ile fahari yetu ya visiwa, asili, haiba,desturi na silka zetu visiwani zimeenda wapi ? Leo hii haiba ya Visiwa vyetu imepotea, tumeacha yale ya kwetu tumevamia na kuvaa majoho ya wenzetu kwa kuacha mila na desturi zetu jambo ambalo kama hatukuliangalia kwa undani tutakuja kupoteza ile fahari yetu kwa vizazi vyetu.

Sote tunaelewa kwamba hali zetu ni ngumu, lakini haihalalishi kuacha yale yetu ambayo ni mazuri na kuiga ya wengine kwa sababu tu tunataka kwenda na wakati, au pengine kutaka kujipatia kipato zaidi kwa maana hiyo takapuuza mila na asili zetu.

Leo hii Visiwa vimegeuka ni sehemu ya kuuzia Masanam lakini wanaojifanya wajanja wamegeuza miondoka wanaiita ni vinyago kwa ajili ya watalii, lakini wenye akili na Elimu zao za dini wanaelewa kwamba sanamu ni sanamu tu hata ukilita kinyago haliwezi kubadilisha dhana hiyo na wala dhambi zake haziwezi kupungua au kuepukika kwa kubadilisha usanii wa jina.Na wala Utalii hauwezi kuchukuliwa kuwa ni kigezo cha kuhalalisha hayo. Vinyago sio asili yetu wala na wala haviendani na mila na desturi zetu za dini hapa Zanzibar.

Hivi kweli Visiwa vyetu hakuna mambo ya kujivunia mpaka tuchonge Vinyago ? Zile nakshi nzuri za milango na viungo vyenye harufu nzuri, matunda na mandhari nzuri haiwezi tosha kuwa ni vivutio vya Watalii ? au ndio ule msemo wa kale, unaosema ukikaa ma muwaridi basi na wewe huachi kunukia ? Sasa mimi naona hatunukii na badala yake Zanzibar inanuka.

Sio ubaguzi lakini naona sio asili yetu , itakapotokea kumuona mtoto wa Kinzanzibar akiacha kuvaa kanzu yake ya darzi, makubazi na kofia ya msikitini na badala ukamuona kajifunga Rubega na mishale kama vile tuko mawindoni tunawinda paa, litakuwa ni jambo la kushangaza sana kwani hio sio asili yetu, na huku ndiko Zanzibar inakoelekee kwa sasa. Kisingizio utaambiwa tunatafuta meandeleo na vivutio vya Watalii.

Lakini pia madanguro na mabaa yamekuwa ni sehemu nyeti na Biashara kubwa visiwani ambayo inashamiri kila kona,inasikitisha na kutia huzuni na aibu kuona Zanzibar imekuwa ni kituo cha Wanawake kuja kujiuza (changu doa) na sehemu ya unywaji wa pombe kali za kila aina, jamani hii ndio ile Zanzibar yetu tulioizoea na mila zetu na asili yetu ndio hii.

Naelewa kuna wengine hawatapenda lakini hii ndio hali ilivyo, na Wahusika tumetia pamba masikioni hatutaki kulizungumzia hili matokeo yake tunaona ni fahari kwa Zanzibar kutangiziwa kama ni Kisiwa cha Maraha . Nasema huu ni upotofu na upotevu wa mila na desturi zetu na sijambo la kujifaharishia nalo. Tukumbuke tunachokipanda ndicho tutakachokuja kuvuna, jamii ya Kizanzibar inapotea kukumbusha ni wajibu.

Imekuwa ni jambo la kawaida kwa sasa hata maamkizi yetu tuliozoea Visiwani yanapotea na badala yake utasikia lugha za ajabu ajabu, vipi kaka mambo ! inakuwaje kaka ! badala ya subal kheri na Assallam Alleikum maamkizi yenye unyenyekevu na heshima kubwa kwetu.

Ukija kwenye mavazi hapa ndio utakuwa umefika mwisho wa maono yako, kwani kinachovaliwa hakijulikani kisingizioo ni” Fashion” tunaenda na wakati lakini jamani haya mambo yanaendana na mila zetu na asili zetu, jee yanakubalika na miongozo ya dini yetu.

Nasema kuna haja ya kurudisha asili pamoja na mila, desturi na silka za Kizanzibar kabla kizazi chetu hakijapotea zaidi,mimi sioni mantiki ya kuiga jamii nyengine ambazo haziendani na hazikubaliki katika maadili ya Wazanzibar. Kuna haja ya kujivunia kizuri chetu ambacho ni asili na mila zetu, hii ndio fahari yetu.

5 Comments on "Visiwa virudishe asili yake, silka na utamaduni wetu."

  1. sauti ya umma 09/09/2010 kwa 8:03 um ·

    wazanzibar wenyewe ndio tuliofikisha hapa hakuna wa kulaumiwa zaidi ya sisi kama wazazi pia kwa vizazi vyetu kuruhusu kutembea uchi na kuvaa nguo zisizoendana na mila zetu na kuhusu hayo mabaa ni wajibu wa serikali kuangaliya sheria inasemaje mimi nashangaa hakuna sheria inaruhusu mabaa kuwepo katikati ya makaazi ya watu na hilo ni kawaida kwa sasa, tunaiomba serikali ijayo itambue kati ya matumaini yetu ni hili moja la kurejeshewa mila na desturi zetu ikibidi kupiga marufuku mabaa yote na kama kuna ulazima kuwepo kwa kisingizio cha mapato basi wayaruhusu yawepo kwenye mahoteli tu..

  2. sale 09/09/2010 kwa 8:35 um ·

    Mi namjua wakulaumiwa…
    Watu wakulaumiwa ni kina Komando Salmin Amour, Dr Bilali, Abdalla Rashid, Waliowahamisha kwa nguvu wazanzibar mji mkongwe na kuwabomolea nyumba wazanzjbar na badala yake wkawakaribisha watanganyika wengi kuja zanzibar na kuwapa ajira na maakazi mji mkongwe na ng=ambo na bila kuzipigia kelele tabia zao na desturi zao,,,,Kisha ati kuna wizara ya mila na utamadu,hivi niuleze waziri wa mila na utamaduni ana asili ya tanganyika ama_

  3. Mandi 09/09/2010 kwa 8:38 um ·

    nikupa big up mwandishi kwa makala yako hyo mzur na yenye kufichua hisia fulani kw wale wenye akili.than namuunga mkono sauti ya umma hasa pale uliposema nisisi wazanzbr wenyewe lkn kwa upande wangu viongoz wanamsukumo mkubwa wanauwezo wakulikataza jambo hata kama me and you tunalikubali.kw mfano.mkuu wa mkoa wa mjini magharibi leo amesema kwamba siruhusa kupigwa madisco viwangani na wala vibali visitolewe na vituo vyote vifungwe saa nne.kwa kweli ni jambo zuri na mm na wewe maswali yetu kaburni ni machache kuliko viongozi.allah tunakuomba utupe viongozi waadilifu amee.eid mubarak

  4. sale 09/09/2010 kwa 11:46 um ·

    hehehehehehe Jamani mnaposema utamaduni, mnanikumbusha mbali kweli..
    Tulikuwa na kawaida baada ya laasiri vijana na wazee hukaa pamoja kuzungumza na kucheza Keram, Nyumba ya pili alikodi mtanganyika akawa anaishi hapo, Kwa utamaduni wetu wa kizanzibar watu wanapo kutana ama kupishana huombeana kheri(kusalimiana) ambapo wengi husalimiana kwa kusema “ASALAM ALEYKUM” Sasa huyu mtanganyika alitoka nje ya nyumba aliyopanga na alitusalimia tulio wengi lakini baada ya kusema “ASALAM-ALAYKUM” Alisema “BISMILAHI APO” KKKKKKKKKKKKKKK lakini tulimjibu WA ALYKUM-MSALAM

  5. Utomvu 15/09/2010 kwa 3:47 um ·

    doooo sale hio kali bt sihaba angalau kutamka maneno ndani
    ya quran,mimi nina amini mazali bado tuna hili zarba lamuungano nakauli mbiu atakae naaje znz ninjema kweli watatumaliza kwakila kona,maana haya mambo yalikua hayapo kabisa but saivi zahir shahir, mungu sw ailinde zanzibar naiokoe namajanga haya yanayoendlea kutusibu amin.

Comments are now closed for this article.