Wagombea urais Zanzibar, waeleze kwa Wananchi vipi watamaliz

Written by  //  03/09/2010  //  Makala/Tahariri  //  3 Comments

Na.B.OLE,

Huu ni wakati muafaka kwa wagombea Urais Zanzibar kujinadi kwa sera na itikadi zao za chama bila kusahau jambo moja la muhimu kwa Wananchi ambalo limekuwa ni gumzo la muda mrefu sasa, vipi wao kama wagombea watamaliza mzozo wa Muungano uliodumu kwa muda mrefu sasa.

Wazanzibar walio wengi wanahamu na shauku ya kuwasikia wagombea wakitoa mikakati yao juu ya mustakabali mzima wa suala la Muungano kwani kila kukicha hali inazidi kuwa mbaya baada ya kupatikana suluhisho la kudumu kumaliza mzozo huo, matatizo ndio yanaongezeka.

Muungano ndio maradhi ya Zanzibar na Wazanzibar kwa jumla, kwa maana hiyo kinga na matibabu ya kuponya ugonjwa huu yanahitajika kwa haraka sana iwezekenavyo kinyume chake kuna uwezekano mkubwa wa Zanzibar kama nchi kupoteza uhai wake.

Dawa na kinga zinahitaji Daktari mahiri na mwenye uwezo wa kuelewa aina hii ya ugonjwa katika nchi za kiangazi ambako joto la matatizo huwa ni kubwa mithili ya mvuke wa tanuri unaokoka mikate.

Jambo ambalo linanisumbua ni kuona hadi leo sijasikia kauli mzito kuhusu tatizo hili ambalo ndilo linaloleta matatizo yote Zanzibar.Ugomvi wote na ukosefu wa maendeleo umesababishwa na Muungano huu hewa, kwani hapo zamani wazee wetu waliishi bila Muungano na hapakuwa na matatizo kama haya ya leo, jee wao walikuwa wajinga au walikosa akili au pengine walikuwa hawajui faida za Muungano wakati huo ?

Nimemsikia Mgombea mmoja akizungumza kwa ufupi kuhusu kadhia hii kwa kusema nitadumisha Muungano, sasa mimi kidogo sijafahamu vizuri kuhusu hili, huo Muungano utakao dumishwa ni upi, ule wa zamani au kuna mwengine unaandaliwa sisi Wananchi hatujui ?.

Ikiwa kuna Muungano mwengine zaidi ya huu ambao wengi wetu tunaufahamu basi inawezekana ikawa sawa lakini ikiwa Mgombea huyu anazungumzia Muungano huu uliopo sasa ambao umejaa mizengwe ya kuliua Taifa la Zanzibar basi atakuwa amechelewa hilo kwa Wazanzibar halitowezekana abadan.

Wazanzibar wamesha erevuka kwa sasa, ule wakati ambao tulionekana madhoba, malofa, wajinga na wapuuzi umeshapitiwa na wakati, leo hii Zanzibar na kizazi kipya ndicho kinachotarajiwa kuchukua jukumu la kuingoza Nchi kuelekea kwenye nuru yenye maendeleo ya kiuchumi na tekinolojia ya kisasa.

Kuukumbatia Muungano huu usio tija yeyote kwa Wazanzibar ni sawa na kijitia kitanzi na kujinyonga wenyewe kitendo ambacho ni dhambi kubwa kwa Mwanaadam kukifanya.Ikiwa lengo na madhumuni ya wenzetu ni hayo basi Wazanzibar hawako tayari kuona Zanzibar inapotea katika anga la Dunia.

Natoa changa moto kwa Wagombea kuliona suala hili na pili wale wenye msimamo wa kudumisha Muungano pindipo wakichaguliwa basi watueleze kinaga ubaga ni zipi faida za Muungano tokea kuasisiwa kwake na pia kama wao hawazijui hasara zake basi tuko tayari kuwaeleza moja baada ya mengine matatizo ambayo Wazanzibar wameyapata na wanayoendelea kuyapata hadi leo hii kupita Muungano huu wa madhabe.

Ukweli ni kwamba hawana hoja madhubuti, wanachofanya ni kuwababaisha Wazanzibar kwa hoja dhaifu eti faida kubwa utasikia Muungano umeleta amani na utulivu, hivi kweli huko nyuma Zanzibar ilikuwa haina amani na utulivu au wao ndio walioleta fujo na balaa zote hizi, hivi sasa wanajifanya mamba wanatung’ata huku machozi yanawabubujika, huu ni uongo na uzandiki hawa wanamalengo yao juu ya Zanzibar.

Wazanzibar tumechoka kuburuzwa na kudanganywa kila siku kwa faida ya wachache,tunasema kwa kauli moja kwamba hakuna lenye mwanzo lisilokuwa na mwisho na kwa hali ambayo inakwenda hivi sasa basi naona kama vile mwisho uko karibu.Wakati umefika wa kila mmoja kubeba mzigo wake mwenyewe. Kwenye dhiki, njaa, maradhi na ukosefu wa haki basi hapo kuna amani na utulivu huo utakuwa usanii wa kisiasa ambao ujanja wake sasa unafikia kikomo na kilele chake.

3 Comments on "Wagombea urais Zanzibar, waeleze kwa Wananchi vipi watamaliz"

  1. mrfroasty 03/09/2010 kwa 9:07 um ·

    @B.Ole,

    Nadhani daktari hujakusudia Dr.Shein….just to make things clear you know!

  2. Ghalib 04/09/2010 kwa 1:00 um ·

    Hata mimi nashangaa sana kuona viongozi wanalinyazia kimya suala hili sijui wanaogopa,nashindwa kujua vipi watalichukulia,kubwa wanachosema wataudumisha muungano kama unasema muandishi.

    Sasa kuudumishwa kwa muungano huo ni vipi ? nikuwayazia kimya na kuyafumbia macho mauvu ya muunga au vipi ? masuala ni mengi ya kujiulizakatika muungano kuna masuala ambayo yanaturejesha nyuma kiuchumi,pia katika uwongozi,zanzibar katika serikali ya muungano tumepewa nafasi moja tu ya uwongozi tukitoa wabunge,na ndio inayowafanya hawa jamaa watupeleke peleke katika masuala ya muungano.

    Viongozi wote wazanzibar ni wakati wao kwa pamoja kutoa ufafanuzi vipi watamaliza na hawa wahalifu au wahaini wa muungano,kwani muungano uliopo sasa sio ule uliofanywa na waasisi wetu wawili,ikiwa viongozi wetu wanalifumbia macho hili na hawataki kulieleza haina haja ya kuwateuwa,kwani kazi ndo ile ile,tukiachana na siasa zetu hapa znz lakini muungano ndio chanzo kikubwa kinachosababisha turudi nyuma.

    Ikiwa viongozi hawataki kutuleza basi hawa ni waroho wa madaraka tu,sio wale viongozi wanaotaka kutuletea maendeleo na kudai haki zetu.

  3. kitamli 04/09/2010 kwa 5:09 um ·

    ahlan B.ole habar za masiku kitambo sikuingia katika ukumbi unajua harakati katika mwezi huu zimekuwa nyingi anyway habar uliozungumza ni muhimu sana kwa hakika kwani kuna kero nyingi katika muungano huu ambazo zinahitaji kuzungumzwa na ni vipi tutaweza kuondokana na kero hizo hapa kunataka uangalifu wa hali ya juu kuweza kumpata kiongozi ambaye sera zake zitakuwa na maslahi zaidi kwa zanzibar na wanachi wake.
    Hatukatai wageni kuja zanzibar lakini sio namna kama hii wanakuja watu bila ya mpangilio maalum, zanzibar imekuwa haitoshi wauza njugu mitaani wamekuwa wengi na hawafahamiki wapi wanakaa na ndo hao hao wanawavizia watu mitaani kuwakaba na kuwaibia vitu vyao nyakati za usiku hayo yashatokezea yote ni athar ya muungano hapakuwa na vitendo kama hivyo kabla na kuna mambo kadhaa wa kadhaa ambayo yanahitaji kutizamwa upya na ikibidi kerejeshwa pass za kusafiria na zirudishwe.

Comments are now closed for this article.