Wako wapi 114,630 wasipige kura
Written by Mrfroasty (Ufundi) // 21/08/2010 // Makala/Tahariri // 33 Comments
Na Jabir Idrissa,
TAKWIMU za matokeo ya kura ya maoni iliyofanyika Zanzibar tarehe 31 Julai 2010 zinaonyesha kwamba watu 114,630 hwakujitokeza vituoni.
Hawa ni watu waliofika vituoni wakati wa kuandikisha wapiga kura kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura (DKWK) la Zanzibar, lakini ilipofika siku ya kutumia haki yao ya kikatiba kuchagua, wakakaa nje ya uchaguzi.
Takwimu hizo zimepatikana kutokana na matokeo yaliyotangazwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Khatibu Mwinchande Agosti mosi.
Ni idadi kubwa isiyotarajiwa kwa kuzingatia uzoefu wa uchaguzi Zanzibar. Inashitua maana haijawahi kutokea watu wengi hivyo waamue kutopiga kura katika siku ambayo haikuwa na kikwazo chochote.
Tume ilipokamilisha uandikishaji wapiga kura kwenye daftari, ilisema imeandikisha watu 407,669 katika majimbo 50 ya uchaguzi, Unguja na Pemba.
Kwa hivyo, katika orodha hiyo ya ZEC, ndipo wanapopatikana watu 14,630 walioshindwa kujitokeza kupiga kura. Ni takwimu nzito na zinahitaji ufafanuzi kuzikubali.
Wapo wanaosema kwa kuangalia mazingira na uzoefu wa uchaguzi Zanzibar, ni vigumu kuamini watu hao wasipige kura.
Mazingira ya kuitishwa kura ya maoni hayakuwa na utata. Suala hilo liliridhiwa na Baraza la Wawakilishi lenye wajumbe kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF).
Hivi ndio vyama pekee vinavyoshindana kwa nguvu kubwa katika udhibiti wa siasa Zanzibar.
Baada ya mwakilishi wa CUF, Abubakar Khamis Bakary, kuwasilisha hoja binafsi barazani, iliungwa mkono na wajumbe na hatimaye ikapitishwa kwa kauli moja na baraza hilo.
Hapo ikawa ni jukumu la serikali kuandaa muswada wa sheria wa kuwezesha kura kuitishwa ili kufanyia kazi mabadiliko yanayotakiwa.
Muswada ulipowasilishwa barazani ulipitishwa kwa kauli moja na wajumbe wote CCM na CUF.
Kura ya maoni iliitishwa katika msisitizo wa umuhimu wa suala la mabadiliko ya mfumo wa utawala wa nchi kuamuliwa na wananchi – kikatiba wananchi ndio wenye mamlaka ya kuendesha nchi yao.
Katika hali kama hiyo, haikutarajiwa watokee watu wengi kiasi hicho wasipige kura. Hivi ni kwanini wakae nje?
Hata kama kulikuwa na baadhi ya viongozi waandamizi wa CCM waliipinga, kura ya maoni ilikuwa ni tunu kubwa kwa watu.
Haijawahi kupigwa Zanzibar. Si kabla ya uhuru wala baada ya hapo.
Kura ya maoni haijawahi kupigwa Zanzibar licha ya mambo mengi na makubwa kufanywa baada ya mapinduzi ya 12 Januari 1964.
Dola ya Zanzibar iliyokuwa ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, iliunganishwa na iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika tarehe 26 Aprili 1964. Wananchi hawakushirikishwa.
Kabla ya hapo, mara tu ilipoundwa serikali, baada ya mapinduzi, Zanzibar iliendeshwa kwa sheria za amri (Decree) badala ya kuongozwa kwa katiba rasmi. Wananchi hawakushirikishwa.
Uongozi ulikiunganisha Chama cha Afro-Shirazi (ASP) kilichosimamia mapinduzi, na Tanganyika African National Union (TANU) na kuzaliwa CCM tarehe 5 Februari 1977. Wananchi hawakushirikishwa.
Kura ya maoni imekuja kuwa moja ya mambo shauku miongoni mwa watu kwa kuwa mbele yao kuna jambo muhimu linalowagusa kuhusu mustakbali wa maisha yao. Watakataaje kushiriki?
Pamoja na hayo, kibinadamu isingewezekana kila mtu atumie fursa siku ilipofika. Dharura ni jambo la kawaida kwa binadamu.
Wapo waliokosa kupiga kura kwa sababu walidharurika. Wapo waliokufa tayari. Labda mtu alikuwa mgonjwa; alikuwa safarini.
Watakuwepo waliokataa kwa kuamua tu wenyewe kutotumia haki ya kikatiba kuchagua. Bali makundi yote hayo, yasingeweza kufikisha idadi ya watu 114,630.
Hiyo ni idadi kubwa katika hali ya kawaida. Hapa itakuwa kuna tatizo limejificha. Ni tatizo linalohitaji majibu muafaka maana ni kubwa kiuendeshaji mambo.
Nitoe mifano michache ya kura za kushitua: Jimbo la Chake Chake waliandikishwa watu 8,195 lakini waliojitokeza kupiga kura ni 6,314. Watu 1,881 hawakupiga kura zao.
Jimbo la Wawi (yote ni majimbo ya kisiwani Pemba) waliandikishwa watu 9,355 lakini waliojitokeza kupiga kura ni 7,100. Watu 2,255 hawakupiga kura zao.
Jimbo la Donge waliandikishwa watu 7,872 lakini waliojitokeza kupiga kura ni 4,645. Watu 3,227 hawakupiga kura. Jimbo la Kitope walijiandikisha watu 7,737 lakini waliojitokeza kupiga kura ni 4,723. Watu 3,014 hawakupiga kura zao.
Jimbo la Koani walijiandikisha watu 12,034 lakini waliojitokeza kupiga kura ni 7,898. Watu 4,136 hawakupiga kura zao.
Jimbo la Uzini waliandikishwa watu 8,743 lakini 5,902 ndio waliopiga kura. Watu 2,841 hawakupiga kura zao.
Jimbo la Dimani walijiandikisha watu 12,813 lakini waliojitokeza kupiga kura ni 8,959. Watu 3,854 hawakupiga kura zao na jimbo la Fuoni waliandikishwa watu 10,884 lakini waliopiga kura ni 6,560. Watu 4,324 hawakupiga kura zao.
Vipi mtu anayefikiri vizuri asishituke kwa takwimu hizi katika nchi ambayo suala la kura ni miongoni mwa mambo muhimu mno kwa watu wake.
Wako wapi watu wote hawa 114,630? Wakuu wa tume hawajaona hili ni tatizo? Kama hawajaona hivyo, watu wanaoipenda nchi yao wanauliza “watu hawa wamejificha wapi wasipige kura zao.”
Tume yenye watendaji wanaofikiri mara mbili kwa maslahi ya nchi, ingekwishatoa tamko kuhusiana na watu hawa. Ni vigumu kuamini hii tuliyonayo watendaji wake hawajaguswa kabisa.
Mtu akisema daftari la wapiga kura ni chafu atakosea? Je tume inaweza kujitoa hapo ikaamua kuliweka daftari hadharani? Kwanini ikatae kuyafunua mambo? Inayaficha kwa faida ya nani?
Hakuna msingi kusema haishurutishwi na sheria kulitoa daftari. Mbona Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imefanya hivyo mara nyingi? Ilitangaza daftari wakati wa uchaguzi mdogo Tarime, Busanda na Biharamulo.
Daftari ni nyenzo ya kiutendaji isiyopaswa kuwa siri kwani inahusu orodha ya wapiga kura wanaoshiriki uchaguzi kuamua viongozi wanaowataka.
Vyama vinavyoshiriki uchaguzi vina haki ya kulikagua kabla ya upigaji kura kufika. Kuna suala la kujiridhisha liko sahihi.
La kama bado Tume ya Uchaguzi Zanzibar haijaona hilo kama ni muhimu, watu wana haki ya kujenga mashaka kwamba labda kuna jambo linalofichwa.
Tume itakuwa inadanganya watu inapojitia kuridhia itifaki za maadili ya uchaguzi kwa Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) wakati haizingatii misingi yake. Ni uhuni kusaini makubaliano ambayo mtu ameshaamua asiyafuate.
Yawezekana daftari ni chafu kweli. Mwaka 2005 tume ilitangaza kugundua watu 3,000 na ushei waliojiandikisha zaidi ya mara moja. Hawakushitakiwa maana ilipeleka tu majina bila ya vielelezo vya namna ya kuwapata.
Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) wa Zanzibar alishindwa kufungua kesi maana ni uwendawazimu kumshitaki mtu usiyemfahamu alipo.
Uwazi katika kusimamia uchaguzi ni jambo jema sana. Hapo tume inajiweka pazuri katika kupata vigezo vya kuwa imeendesha uchaguzi huru na wa haki. Vinginevyo, basi hatujaamua sawasawa kuchagua maridhiano.
Chanzo:mwanahalisi
Unaamini kuwa ZEC inatumikia wazanzibari kwa uandilifu?
- Hapana (76%, 1.019 Votes)
- Ndio (24%, 326 Votes)
Total Voters: 1.345





33 Comments on "Wako wapi 114,630 wasipige kura"
hiyo idadi yote ambayo haijapiga kura ndo watu wa kupandikizwa hao wanasubir 31october watuibie tena ni kweli idadi ni kubwa sana na kama hatujaangalia yatakuwa yale yale kwani kwa hakika daftar ni chafu sana la kuandikishwa wapiga kura chukua chako mapema ni wajanja sana hawa ila m mungu yupo kwa wanzanzibar safar hii kuikomboa nchi yetu.
Watu wasiojitokeza katika kura ya maoni ni kwa hakika niwengi nafikiria kua wengi wao ni ambao watu wasiokua na haki yakupiga kura lakini wamepwa vitambulisho hivo vya kura ili wapate kupiga kura zao wakati wa Ucguguzi wa Oktober kwa kuipa ushindi CCM.kwani ninamini hao wengi wao ni waupande wa bara na ndio maana hawakuja katika kura ya maoni,vile hao watajitokeza kwa kupiga kura ya mwezi wa oktober ili kuipa ushindi CCM,kwani hizo ndio mbinu za CCm ili wapate wajumbe wengi katika serikali ya umoja
a/a hapasasa nikuwamakini ukweli hawa niwalewatu waliyopandikizwa chakufanya hapa kwamaoniyangu kila mtu awe askari wajiraniyake sikuikifika kuanziya kufunguliwakwa vituwo hadi kufungwa vituwo lazima tujuwane wapi mtuanakwenda na asiye husika tusimpe nafasi yakwenda kupiga kura na mawakala lazima wajuwe kwanza watu watakao kuja vituwoni na majina idadiyake kwenye madaftari yavituwoni hapa lazima tuchungane maana ukimwachiya mtu sikumoja maanayake ni mazonge ya miyaka 10 sasa fikiri ukimjuwa hana haki usimpe nafasi ukimjuwa kapiga kura tayari usimpe nafasi waznz tunajuwana hataiweje tusikubali mateso ya maisha
Bwana hapa hapataki tochi, hiyo takriban asilimia 25 ya watu wote walioandikishwa na ambao hawakupiga kura, miongoni mwao wamo wabara na wazanzibar ambao wanavitambulisho zaidi ya kimoja, na ni mamluki wa makusudi ili kuipa ushindi CCM chini ya uongozi wa tume yao wenyewe.
Wenzetu hawa pamoja na jitihada zote zinazochukuliwa kuhakikisha nchi inakuwa salama lakini kabisa wana udhalimu wa ndani kabisa, na nakuhakikishieni ndugu zangu wameshajiwekea wachukue hio 25% wajumlishe na asilia 45 walionayo halafu wajipangie matokeo ya 70%, na kama hamusadiki tutakujaelezana. Na wala tusijidanganye kusema tutalinda visanduku au kuwaangalia watu wanaopiga, mtu akionyesha kitambulisho alichopewa na tume ni ithibati ya kupewa haki ya kupiga kura na wala hutoweza kumzuwia kwani mtutu utatumika hapo ndugu zangu, tutaonyeshwa watu wakiletwa kwa magari kama huko nyuma, wageni kutoka bara ambao hata siku moja hawajawahi kuonekana hata mitaani seuze kukaa katika majimbo watayopigia kura, wataingia na kupiga kura halafu hao wajiondokee zao wakiwaacha wazanzibar na hasa macuf walitoa macho tu na kulalamika, kelele za mlango tu hizo.
Mtego mwengine ni pale ilipoandikwa kwenye katika kuwa ndani ya siku saba raisi ataetangazwa achague makamo wake wawili na kama chama cha pili yaani cha upinzani kikikataa basi nafasi itabaki vacant yaani tupu, maana yake ni kuwa hata mukisuta hamutawazuwia wao kujiundia serikali yao na kuendeleza mipango yao ya kidhalimu.
Hebu tulijulize, katika sehemu ambayo kuna upinzani mkubwa ni Pemba,ile ni ngome ya CUF, si CCM, wala vyama vyengine vya siasa, kamuulizeni Mbatia na Mrema halafu uambiwe ati jimbo moja tu la Chake Chake lina watu zaidi ya 1000 hawakupiga kura, hicho si kiini macho ni nini?.
Nawaomba wanamtandao huu ushauri tuwafikishie TUME na viongozi wa vyama vya siasa hususan CUF kuwa tunacheza kamari, na kama hatujakuwa serious, wakweli basi haakuna haaja ya kuutangazia ulimwengu kuwa tunataka kufungua ukurasa mpya wa haki na usawa, tunataka daftari lianikwe hadharani na kama kweli tunatakaa kufanya uchaguzi wa haki basi lazima tuunde mikakati STRATEGIES maalum zaa kuwatoa hofu wananchi, vinginevyo tujiandae na adhabu kali ya moto wa jahannam kwa kuendeleza UNAFIK.
TUWE WAKWELI, TUJIJUE KUWA DUNIA NI MAPITO TU, NA ADHULMA LA YADUMU, NA PIA CHOCHOTE UTAKAACHOKITANGGULIZA MBELE YAA MOLA WAKO BASI UTAKIKUTA NA UTAULIZWA SIKU YA MAJUTO.
Nakuusieni pamoja na kuiusia nafsi yangu kuwa tunapofunga na kuswali haitoshi kutuokoa na adhabu kali ya Mungu siku ambayo hautomfaa mtu ufalme, ukubwa wala mali yake ikiwa tutakuwa tunaendeleza udhalimu.
naheshimu mawazo ila na mimi natowa mawazo kulingana na ninavyohisi.
ni kwamba hiyo asilimia ni sawa na ni kubwa hata mm binafsi nimo kwenye hiyo asilimia kwa sababu ninazozijua mimi lakini cha msingi ilikuwa ni kutowa maoni na sauti ya wengi imesikika na inafurahisha hata hao walokataa wameonekana kuridhika kwani hakuna kelele kama tulivyozoea kwa chaguzi zinazopita,vinginevyo ni kusema kuwa wasopiga kura ya maoni ndio walopandikizwa ili waje kupiga kura wakati wa uchaguzi mkuu kwa hili mimi naona si wakati wa kulipigia debe kwani kwa muda tulonao tuangalie mbele na kuzidi kuwa pamoja tusijenge visingizo vya kuturudisha kule kwenye malalamiko pindi mmoja ataposhindwa na nasema hivi kwa sababu sisi ni wapiga kura na tuna viongozi wetu na ni makini kwa hayo, sasa ningeomba hata kama tuna shaka tuulize kwao ili watufafanulie kulikoni kila mmoja kupeleka kwa jamii lile analohisi yeye ingawaje ni maoni lakini ni yenye kugusa wengi.hivyo hivyo kulinganisha na idadi ya wasopiga kura kufikia asimia 25%hebu tutizame wenzetu kenya ambacho tulichofanya ndio walichofanya, waloandikishwa kupiga kura walikuwa 12,656,416 walopiga kura 8,641,960 sasa angalia percent ngapi haikupiga kura jee wao walipandikizwa?
kiufupi maoni yangu muda huu tusijenge viulizo badala yake kila mmoja ajipange kwa uchaguzi kwa takwimu iliopo na tuaminiane tufanye uchaguzi na tukubaliane na matokeo ili tuzidi kujadili zanzibar moja baada ya uchaguzi.
ni maoni yangu si lazima ukubaliane nayo.
Takwimu za kenya tusizifananishe na zanzibar kwa sababu kama alizozitoa ndugu jabir.
Mimi labda kwa kuweza kunipunguzia wasiwasi na wala si kuutoa wote wasiwasi wangu dhidi ya hii tume ya zec basi ningeomba nipatiwe takwimu za waliojiandikisha mwaka 1995 na niwangapi hawakupiga kura ili tulinganishe na hizi za maoni.
Salaam ndugu mtoa mada na wachangia mada zenu zote.
Mimi kwaupande wangu jana jioni nilizingalia data hizi za kura ya Maoni na nikazungumza na ndugu (ASHEKH) juu ya wasi-wasi wangu. kwani kama alivosema muandishi kwamba asilimia ya watu wasiopiga kura ni kubwa kulingana na lengo halisi ya kura ya Maoni. kwamba:
Hili lilikua ni jambo geni, wazanzibari hawajawahipo kushirikishwa kidemocrasia kutoa maoni yao katika matukio mengi ya mabadiliko ya “KISIASA” visiwani kama ndungu Muundishi alivotoa mifano yake tofauti.
Licha ya hivyo kuna watu hawa 114,630 hawakujitokeza ni kwanini? Tusikae tukatoa mifano ya Kenya na tukajifananisha na sisi na ikawa ndio kielelezo.Na wala tusianzekujenga chuki za wenyewe kwa wenyewe. Lakini kutokana na mazungumzo yangu hivi leo na mtu nyeti ( CUF statitisian). Amenambia mpaka sasa hivi Zanzibar kuna makundi makundi yaliojitokeza na tunatakiwa tuwemakini sana na tusiregee -regee.
kwasababu ya kura ya MAONI imepita na ikawa kigezo cha kuaona Wazanzibari ni wamoja /tumeshikana ila kuna haya makundi mapya:Mfano
1.Kundi la Makunduchi wao wanasema hawataki Raisi awe MPEMBA that is black & witte. Hata akiwa CCM lakni asiwe Mpemba.
2.kundi la Bilali, ambalo linajulikana wazi kwamba wao ndio hivo tena.
3.Kundi jengine nilile la watu wa visiwani amba wao wanaona wana danganywa tu nakufanywa victim wa matatizo.
Sasa nakuja kwa ndugu yangu Bosco mimi sina ujuzi wa mathmatics. Lakinikutokana na data ilizoletewa na Ashekh nitakuandikia hapa idadi yote ya wapiga kura ya 2005 na 2010. Wewe utazifanyia kazi.
nawasilisha
@bosco:Analysis ya kura
:::::2005———2010—tofauti–CUF—05—-CCM05——ndio1020/hapana2010.
Pe:138074…….128959.=9115……=115693…=23346…….88153/11660
Ug:430022…….407669.=25634…..=198816…=232205……186669/95324.
Kwaufupi kama utakua hujafahamu ni Waliojiandikisha 2005 Pmb ni 138,074 na unguja =430022.Na 2010 Pmb =128,959,Unguja ni 407,669.Tofauti yao Pmb ni 9115 na unguja ni 25,634.
Kura za CUF 2005: Pmb was 115,693 na Ungja was 198816, kur za CCM Pmb was 23,346 na Unguja was 232,205. Sasa kutokanana kura za Ndio 2010 Pmb ni 88,153 na Unguja ni 186,669. Nakura za Hapana Pmb ni 11,660 na Unguja ni 95,324.
Sasa hapa tunatakiwa majibu “BUSCO” kaziyako na others “Methmetisians”.
Lakini wazanzibari tunatakiwa tujuwe wazi CCM Tanganyika wamemleta Sheni kwa mipango yao.na hawatokua wajinga Visiwa kuviachia ni jambo la gharamu kwao. Na tujue hawa watu wasiopiga kura ni akina nani? Kazi po wala sio ndogo.
Wito kila Mzanzibari aw ni mlinzi wa Mwenziwe, tukiikosa Serikali mwaka huu basi tumekwisha. Na hawa wanatuka ktuibia kwa number mara hii.
Nawasilisha
kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho.hao watu laki wamewekwa maalum na c c m.kwa ajili ya kura ya urais ili c u f washindwe.hizo ndio akili zao lakini msemo nimekuambieni iko siku hawa watu itafikia kikomo chao angalia u s a wamekimbia mpaka leo inaongozwa na mtu mweusi.na sio hilo tu nakuhakikishieni pia kiko chama cha 3 zanzibar kitaingizwa kwa makusudi kwenye baraza la wawakilishi kwa nguvu ya c c m yote hio nikuogopewa c u f.lakini hilo sio tatizo mwaka huu itakuwa kugawana mbao.chamuhimu serikali3 tuzidi kuzidai kwanjia yoyote ikiwezekana watumalize wote maisara. gombani
Maelezo yafuatayo tuliwahi kupatiwa kutoka tume ya uchaguzi ZEC kupitia afisa wake.
Kwa ufupi hapa MZALENDO hatuna taarifa yoyote ya kama zoezi la kubandikwa majina limefanyika au ndio maelezo hayo ya ZEC hayakuwa sahihi.
Vyovyote iwavyo kama yalivyo maelezo hayo ZEC inawajibika kisheria kulitoa daftari.Ni wajibu wa wadau wa siasa za Zanzibar kulihakiki daftari hilo na kutuondoshea mazingaombwe yoyote yaliomo ndani yake.
@mfroasty: ZEC mpaka sasa haijaliweka wazi daftari hilo na wakati ndio unakwenda.Hii nikumaanisha kwamba kuna uhaini ndani yake. sisi wanamzalendo ndio tunatakiwa tutoe changamoto kwa wenzetu waandishi wa habari zanzibar na hata kupitia wananchi wenyewe.
Hii n kazi yetu na la leo hufanywa leo tunatakiwa tu-ipresure ZEC right now before dome (0ctober). kupitia viongozi hawa wa Siasa na wana media kama vile akina Ali Batho, Salma saidin.k na hata VOA.
Kama kuna wenzangu wana mawazo mengine zaidi ya haya nawaomba wayatoe hapa,ili tuyajadili na tuwe na solution kwani litakapo tota sila mmoja.
Kwa kweli idadi ya watu [114,630] ambao hawakujitokeza kupiga kura ya maoni ni kubwa sana na inatushituwa sana kwa uchaguzi ujao.Bila shaka na ikiwa nikweli wanavyo sema watowaji maoni kuwa hawa ni watu wa kupandikizwa, basi inabidi tujuwe kwamba kura imeshapigwa, sasa tungojee
kutangaziwa tuuuu.
Hatuna elimul-ghaib walahatujuwi nini kimetokea, fikra ni nyingi na kila mtu anahisia yake kwa mambo yanavyo kwenda hapa zanzibar; khususan kwa zile chaguzi zilizopita.Kwa kweli idadi kubwa ya watu wa ZANZIBAR, wameshavunjika moyo na kuchoshwa na matokeo ya chaguzi hizi.Sihasha kuweza kusema kwamba mimi nikipiga kura au nisipopiga kura, natija ni ile ile haigeuki wala sipati faida yeyot; isipokuwa kuadhibika tangu asubuhi mpaka usiku, kusukumana na pengine hata kutokea kupigwa na kurejea nyumbani na majarah.Hapo humjia akilini; na akasema nibora nichukuwe hili JEMBE LANGU NENDE SHAMBANI NIKALIME MUHUGO,VIAZI AU MPUNGA.Riziki kwa mungu, nitapata faida ya mavuno na kunisaidaia mimi na watoto wangu.
Sihasha kuwa ikawa idadi hii [114,630] niwale waliochoshwa, kuvunjika moyo na hata kukata tamaa na kusema sinaimani na chaguzi hizi[KHALLI WALLI] Litakalokuwa liwe.
Ikiwa dhana hii ni sahih, basi hatuna budi illa kuwaombea dua hawa wenzetu M\Mungu awape imani warejee kama walivyo kuwa zamani. AMEEN.
NAWASILISHA
Mimi kwa maoni yangu Uchaguzi CCM tayari wameshamaliza imebakia Formalities ifike siku ja Uchaguzi wamueke mtu. Na ndio maana ikaitwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Na ndio maana japo kuwa Bara walipata uhuru kwa njia ya Mazungumzo lakini chama Kiliitwa chama cha Mapinduzi. Aliyeyafanya hayo ni Nyerere na alikuwa hajalewa wala hakugonjwa wendawazimu. Aliyafanya hayo kwa maana yake. Jambo la muhimu kwetu sisi wazalendo kujitokeza kwa wingi kupiga kura na tusijetukavunjika moyo tukasema hatujitokezi. La pili nafikiri imefika wakati kwa wananchi wa chini ambao tunahamu ya Mabadiliko kuanza Kampeni ya mtu kwa mtu, nyumba kwa nyumba, kwani sisi ndio tunaowajua majimboni kwetu ni watu gani bado ni masugu na wamekunjwa maji ya Bendera. Tukiwaachia viongozi wa juu kupiga kampeni basi Vita hivi tutashindwa. Tukishindwa mara hii basi jamaa wa bara watatumaliza.
@ zamko shukran kwa takwimu. Lkn kabla ya kuzungumzia hizo takwimu ningependa niongezee kundi la 4 ktk yale makundi 3 yaliyopo znz hivi sasa kama alivokutajia huyo kiongozi wa cuf. Naongeza kundi la 4 la dr shein ambae anataka urais wa znz.
Nionavyo mimi makundi yote haya ispokua hili la 4 yanamuongezea maalim seif ushindi kwani kama ni hivyo ni wazi kua kundi la wamakunduchi either hawatopiga kura au hawatompigia dr shein, pia halkadhalika kundi la dr bilal. Sasa hizi nyingi zao ilikua ziwe ni kura za ccm lkn watazikosa inshallah.
Hapa utaona kua kura zilizopungua ni za dr shein lkn kura za maalim seif zipo palepale hazijapungua bali zinaongezeka kutokana na makundi haya (amin).
Lkn na mimi nawatahadharisha wazanzibari wenzangu kua tusibweteke na haya wala kura ya ndio kwani wana ccm hawategemei kura ktk kushika madaraka hata ukiangalia kauli za viongozi wao wakubwa kama vile rais kikwete aliposema hategemei kura za wafanyakazi, pius msekwa aliposema atakae kuhama ccm kwenda upinzani na aende na akitaka wanaweza kumsindikiza kwenda upinzani,dr shein aliposema kua ushindi kwa ccm ni lazima na viongozi wengine.
Kuhusu takwimu. Naona zinatafautiana na hizi nilizonazo mimi ambazo nlizipata hapa mzalendo.
Takwimu nlizonazo mimi 2010 ni waliojiandikisha unguja na pemba jumla ni 407739 waliopigakura jumla unguja na pemba ni 293039 wasiopiga kura jumla ni 114700 kura za ndio jumla unguja na pemb ni 188705 na kura zote za hapana unguja na pemba ni 95613.
Sasa kwa mujibu wa takwimu zako ndugu zamko ni kua 2010 waliojiandikisha pemba ni 128959 unguja ni 407669 na ukijumlisha zote utapata jumla 536628 hii ni zaidi ya ile takwimu ya jumla ninayoijua mimi ya 407739 ya hapa mzalendo.
Sijui kua mimi mahesabu yamenicheza au vipi?
Lkn kwa ujumla ni kua mimi nataka takwimu za uchaguzi za mwaka 1995 na si za 2005 kwani uchaguzi huu wa mwaka 1995 mimi sikusikia habari za ulalamishi ktk daftari lkn ktk chaguzi za 2000 na 2005 daftari limeharibiwa kwahivyo sipendi kutumia hizi takwimu za kupanga. Mimi naziamini takwimu za 1995 zaid kwani ktk uchaguzi ule mambo yote yalikwenda vizuri ispokua matokeo tu ndio yaliyopikwa na zec kumuweka dr salmin madarakani.
Mimi nataka takwimu za mwaka 1995 ili niweze kujua ni % ngapi hawakupiga kura ili nilinganishe na hii 25% .
hilo swala la turnout mimi sioni kama geni kwasbabu .uchaguzi wa marekani 2008 ulikuwa na 61% turn out 39% hawakwenda.uchaguzi wa uk 2010 ulikuwa na 65.1% turn out wakati huo huo nothern ireland peke yake walikuwa na 56.9% voter turn out.
swala la kupiga kura ni la hiari si lazima.watu wana mazonge yao tele ya maisha.vile vile zile siasa za miaka ya nyuma naona zimepungua sana zanzibar .watu wako busy kutafuta maisha.there is a life rather than politics.hao watu waliokuwa hawajenda mimi siwalaumu wala sishangai.who give a damn anyway its just a politics.
@Muunguja,
Kwanza karibu tena MZALENDO maana ni muda nilikuwa sijaona maoni yako.Pili naona hii hoja yako ya kuwa watu wengi wako bizzi na maisha haingii akilini mwangu.
Ikiwa mtu hakutaka kupiga kura ni uwezekano mkubwa pia hatokwenda kujiandikisha.Hakuna mtu hapa aliepandwa na wazimu anaedai kuwa turn out ya Zanzibar iwe 100%.Hoja ilioko mbele yetu ni kuwa takwimu zimebadilika ghafla kwa muda mfupi.
Hio mifano yako ya UK, US nadhani turn out yao mara zote ni hio around 60′s.Sasa ikija mwaka wakapata turn out ya 25%, nadhani kunahitajika uchunguzi hapo!Hii ndio hoja yetu, kuwa Zanzibar miaka yote turn out ni kubwa lakini kwenye kura ya maoni ni ndogo mno.
Ni hayo tuu kwa sasa….
1995:
Avarage turnout: = 95.7%
2000:
Avarage turnout: = Not available ??
2005:
Avarage turnout: = 90.8%
2010: Referundum
Avarage turnout = 71.30%
Details on Referundum:
Total Voters=407669
Spoiled Ballots=8677
Valid Votes=281993
Total Votes Cast=290670
Polling Stations published=1286 of 1292
REF:
1.1995 Election report http://www.eisa.org.za/WEP/zan1995results2.htm
2.2005 Election report http://www.scribd.com/doc/27189767/Zanzibar-Election-Report-2005#fullscreen:on
3.All Zanzibar Election data http://africanelections.tripod.com/zanzibar.html
@mrfroasty
kwanza ukumbuke general election na referundum na vitu viwili tafauti.kwahiyo usitegemee kupata turnout iliyofanana katika upigaji kura.naamini general election ya october turn itakuwa kubwa kidogo lakini sidhani kama itafika 80%.
vile vile kura za urais safari hii nyingi zitaharibika.haya ninayokwambia hapa trust me yatatokea.
@Muunguja,
Nafahamu kama uchaguzi na referundum ni vitu tofauti, lakini kwa Zanzibar hivi vitu vilikuwa na upinzani takriban sawa.Nilitarajia turn-out ya ~90%, badala yake tumepata 70%.
Halafu kwenye uchaguzi mkuu turn-out iwe 90%, kuna kipi kitachotuzuia kusema kuwa hii 20% ndio wale wa kuletwa na mameli na kurandishwa na magari (tunazo hadi video hapa MZALENDO wapiga kura wakipelekwa kwa magari wakapige kura).
Anyways, nataka nikuamini hayo usemayo kuwa lakini nashindwa kupata background info.Kwanini kura za rais ziharibike, kuna kipi kinachopikwa huko na ZEC ? Tunafahamu vizuri kuwa ZEC haifuati kura, bali hujifungia pale Hoteli ya Bwawani na kumchagua wao rais wamtakae (mara nyingi kutoka CCM).
Safari hii wazanzibari wengi tuko macho kufuatilia, uongozi kwani tunaamini kuwa khatma ya taifa la Zanzibar imo mikononi mwa rais anaefuata.Tusije yakatukuta kama yaliowakuta wenzetu wa Mombasa.Sasa wamebakia kulia tuu, tayari washageuzwa mkoa wa Pwani.Leo tunawaona ndugu zetu wanahajir kuhamia Zanzibar.
Hivyo uchaguzi wa mwaka huu lazima machachari kuhakikisha haki inatendeka.Na ZEC wanaogopa nini kulitoa Daftari hadi leo ??? Au ndio daftari lina madhambi mengi!
cha muhimu hapa majina ya walopiga kura za maoni yapo .kwahiyo hawa ndio wanatakiwa wapige kura ya oktober.hii ndiyo suluhisho.nani alowaambiya wasende kupiga kwahiyo washapoteza haki zao wenyewe kazi kwao
Thank u mrfroasty kwa turnout ya 1995. Hii inaonesha wazi kua huu mtandao una viongozi makini na wakujitolea na wanasadifiana na jina la huu mtandao ie mzalendo. Lkn musije kugeuka mgema!.
Kwa maana hiyo ikiwa turnout ya 1995 ni 95.7% na ya referendum ni 71.3% hapa ndipo ninapothibitisha kua hawa watu 114630 ambao hawakupiga kura ya maoni kua wengi wao ndio hao mapandikizi kutoka bara na wengine waliondikishwa zaidi ya mara moja.
Kimsingi hii idadi imezidi kwa upande wa unguja kuliko pemba kwani pemba kufanya hujma inakua ngumu kidogo.
Nawambia ndugu zangu hasa wa unguja musimruhusu mtu kupiga kura mara 2 wala mtanganyika asipige kura hata akawa na vitambulisho mia 1. Mawakala inabidi wawe makini kuangalia vidole kwa anaekuja kupiga kura na pia wahakikishe kila anaepiga kura ameweka dole ktk wino na pia waangalie wino usije ukawa feki na hata hizo kura zisije zikawa ni za mchina. Ndugu zetu wa unguja mara nyingi ndio wanaotuacha mkono wenzao kutoka pemba mbona ngangari au unguja urojo mwingi? Am sorry sikusudii kubagua upemba na uunguja hapa mimi nawasilisha mawazo yangu.
@Mrfroasty mimi nimemfahamu kidogo muunguja aliposema kua mara hii kura za urais nyingi zitaharibika. Nafikiri hawa ndio wale ambao hawakuridhishwa kwa kuteuliwa kwa dr shein. Sasa wanataka kutoa ujumbe fulani ili waonekane kama na wao wapo. Wanaweza kutumia kama zile kura za CUF za maruhani mwaka 2000
Ndio maana nikamwambia zamko kua makundi yote 3 yale yanamuongezea ushindi maalim seif. Ama kweli siku ya kufa nyani miti yote huteleza na huu ndio mwisho wa CCM october 31. Kwa uwezo wa allah.
asalam alaikum kwa upande wangu mimi kuhusu hiyo idadi kubwa ya watu wasio kwenda kupiga kura ya maoni kwa mimi upande wangu hainitishi sana wasiwasi najua ndio akili ili ujiweke tayari ikiwa kupandikiza watu kwani wameanza leo au jana kuna watu hupiga kura zaidi ya mara tano vituo tofauti ni mtu mmoja huyohuyo na huwa wengi na matokeo yake huwa vipi hupelekwa na magari ya plice na yote hayo pia hushindwa kwa idadi ya kura na maalim seif hushinda ila hatangazwi tu hutangaza wanae mtaka na tukumbuke pia hao walio tia kura ya hapana ndio kweli hatotokea mtu kubadilika lazima watatokea wenye kubadilika tukumbuke tu alipangalo mungu binaadam hana uwezo wa kulifuta ni nani iliyo mpitia kama seif na karume watakutana na kupeyana mikono hata huyo seif na karume hilo walikuwa hawalijui ila mungu kataka liwe na limekuwa kila jambo mungu huweka na wakati wake wa kwisha ikifika litakwisha ni kweli ccm tanganyika hawapendi litokee hilo la z’bar upinzani ushinde lakini mungu yupo na wanao dai haki yao utakuja kushangaa watakuja tiwa mtihani ccm tanganyika wasiweze kuleta watu huku kwasababu na wao wanataka watu wakuwapigia kura kwa maana hali kwao imeshaanza kuwa ngumu kwa ccm tanhanyika watu hutoka kwa makundi wataweza kuwashuhulikia hawa si kila mtu atatapia roho yake mwenyezi mungu huzibadilisha nyoyo za watu kwa anavyo taka yeye wakumtegemea ni mungu na si watu
sisi binaadam tunatakiwa tuwe tunafikiria mambo mazuri na sio kufikiria mambo mabaya na dalili nzuri au mbaya huonekana mapema na kila kibaya kitakuwa kina uzuri wake hii yote mungu aliwafedhehi hiyo tume ya uchaguzi zec kwani walivyo panga wao sivyo alivyo panga mungu walianza kuandikisha watu na kuwapandikiza kabla ya haya makubaliano na kutoa hizo card kabla kwasababu hawana elmu ya khaib hawakujua kama yatatokea haya yalio tokea sasa wao walitarajia kwa imani zao mtu wao gharib atapitishwa kinyume chake katokea mtu mwengine bila ya kutarajia sasa inafaa tujiulize ni ? nani hasa mpangaji ya yote hayo jibu kila mmoja atajijibu mwenyewe kwasababu yote hayo wao hawana elmu ya khaib na kama wangelijua mapema kuwa ni dr shein ndie atagombea na kura ya maoni itapingwa basi wasengelifanya aibu hii lakini yote haya mungu alipenda awafedhehe hapa duniani na kesho akhera wataulizwa ikiwa mungu yeye husimamia haki kwa viumbe vyake je wao wamesimamia haki juu ya viumbe wenziwao naamini na nitaendelea kuamini kuwa hao walio pandikizwa hiyo siku ambayo ya kupiga kura kwa uweze wake yule ambae atakalo huwa na kuwa basi hata hata robo yake ya hao walio pandikizwa hawatokwenda kupiga kura nina sababu 2 kuu kwanza walio mtarajia kuwa atagombea huyo walio mtaka awe mgombea wao sie na sivyo matarajio yao walivyo zani na wala hawakutarajia kama itatokea siku moja kura ya maoni kupingwa nakuombeni msije kunifikiria vibaya wana ukumbi na wala kufikiriwa ni mbaguzi ok mlitarajia nini zec iseme na idadi ya watu wameshasema kabla kuwa tumeandikisha watu idadi fulani kabla ya hata hiyo kura ya maoni idadi ya watu watakao piga kura hiyo siku ya asomwana aelekee tanganyika itakuwa ni idadi ya watu wale walio piga kura ya maoni ikiwa kuongezeka basi ni kidogo sana kwa hiyo nirudi suala la juu ya yote hayo mungu alivyo wafedhehi punda ni punda tu hageuki lakini penye kundi la watoto hupigwa mawe na kukimbia japo kidogo narudi pale kwenye sehemu yangu ya 2 ya sababu gani kidogo inayo nitoa wasiwasi mimi ninao na sio kama sina ila kwenye vita lazima uweke nitashinda na sio kushindwa tuache hilo shein ni mpemba na seif ni mpemba sasa hapo pana mtihani mwenyezi mungu kapaficha sote hatujui ila khof kubwa ipo kwa tume ambayo mungu ameshawatia kwanza hawajui wafanye nini na amani karume anataka nini kwasababu yote hayo amani karume yuko kwa seif aman karume ni yeye ndie alomtaka shein kwa upande wake kama angemuachia gharib ingekuwa ni hatari kwake naomba muwe na tafakari sana fikiria vizuri utapata jibu
Muunguja, usishangae niko nawe bega kwa bega juu ya maoni yako.
Kuna factor nyingi tumeshindwa kuziangalia kwenye hii kura ya maoni tukilinganisha na uchaguzi mkuu. Hapa nitaleta chache tu.
Moja muda wa kutangazwa kura ya maoni ulikuwa mfupi.
Pili kampeni ilikuwa kwa kipindi kifupi sana.
Tatu nakumbuka hata Sh Ally saleh alikuwa akizungumza hakuna elimu ya kupiga kura iliyotolewa, mpaka dakiika za mwisho.
Kura ya maoni haina umuhimu wowote ndio maana wengi hawakwenda. Siasa ni mambo ya kigeugeu, leo CUF wataka nseto kesho wata kunde. Ndio maana USA na UK wapigakura wengi ni wazee, vijana hawana wakati wa kulumbana na siasa. Rais ata awe Bahamadi umasikini ni ule ule tu, Bahamadi atawapa ulaji wanawe na shemeji zake, mlobaki jua kali kama kawa. Jaribuni kujitafutia maendeleo yako mwenyewe binafsi.
Mangala hapa unaonyesha mawazo mgando.
katika maisha yako huwezi kuikwepa siasa. Ukiniuliza kwanini napenda siasa, nitakujibu kuwa ndio inayonipangia maisha yangu kila leo. Hivyo kwanini niwaache watu wanipangie, sasa nataka nijipangie mwenyewe.
Nimesema huwezi kuikwepa siasa,kwanini?
ushuru unaolipa unapangwa na wanasiasa. Wapi uende na kwa sheria zipi ni wanasiasa. Passport wanaotoa ni wanasiasa. Wakitaka mule mseto ni wanasiasa. Wakitaka mule sembe la yanga ni wanasiasa. Hebu nambie nikitu gani unachokifanya ikawa hakiko chini ya dhamana ya wanasiasa.
hayo yako ni mawazo mgando yakitiliwa bashrafu kidogo na chuki ya fulani.
@ashakh
ahsante sana kutumia utalaamu wako kwa kuelezea hizo factor.kwanini watu wachache wamejitokeza kwenda kupiga kura, angalau hukutaka kuingia kwenye conspiracy theories kama wengi wao hapa.
@mrfroasty
niliwahi kusema hapo nyuma kwamba ushindi ni ushindi tu hata kama wa goli moja kura ya maoni imepita kwa asilimia nyingi tuu lakini bado hamjaridhika mnataka asilimia 90.binadamu wametafautiana kimawazo jamani mambo ya kuburudhani yashapitwa na wakati au unataka turudi enzi za asilimia 99.999999? kama ccm wanataka kufanya wizi mimi naona wangeanzia kwenye hiyo kura ya maoni.
niliposema kura nyingi za raisi zitaharibika nilimaanisha kutoka upande wa ccm sio za cuf.ccm kuna makundi na moto unafukuta chini kwa chini.wengi wao watachafua kura za uraisi lakini za ubunge na uwakilishi zitakuwa za kawaida.kwa ufupi maalim atashinda safari hii lakini ccm watakuwa na viti vingi vya uwakilishi.
sasa hiyo ni prediction yangu can be right or wrong .but I believe 90% might happen.
JAMANI KWA NYOTE WENYE MAPENZI NA ZANZIBAR NA WAZANZIBAR BAADA YA KUSOMA MADA HII NA KUWASILIANA NA KIGOGO MMOJA WA JUU KATIKA SERIKALI HII ILIYOPO AMENIELEZA KUWA HUYU MWENYEKITI WAMEMUWEKA WAO KWA HIVYO NI LAZIMA ALIELEWE HILO NDO MAANA HUU NDO MTEGO WALOUPANGA KUWAZIDI MBINU WAPINZANI WOTE ILI KUWA WAONEKANE UCHAGUZI ULIKUWA HURU NA WA HAKI NA AMENIHAKIKISHIA KUWA RAIS ATATOKA CHAMA CHA CCM.
JAMANI NATOA NASAHA KWA WAZANZIBAR KULIELEWA HILI HILI PIA NAMUOMBA MWENYEKITI WA TUME YA ZEC AONYESHE MFANO WA KUIGWA KWA KUHIMIZA UCHAGUZIN SALAMA NA WA UKWELI SIO HUU ULIOPANGWA TO PRETEND LIKE FREE N FAIR ONE.
KILA LA\ KHAERI ZNZ NA WAZANZIBAR WOTE.
@ ashakh sababu ulizozitoa zinaweza zikafanya kazi kwa upande wa tanganyika au nchi nyengine ambozo elimu ya democrasia kwao ni ngeni au hata elimu kwa ujumla. Lkn kwa upande wa zanzibar sababu zako mimi siziungi mkono kwani wazanzibari wanaelimu ya democrasia ya kurithishana tokea miaka ya 50.
Leo nataka uitishe uchaguzi bila ya kapeni basi watu watajitokeza wengi kupiga kura.
Hebu ulizia mwaka 2005 CUF ilifanya mikutano mingapi pemba ya hadhara?
Ulizia pia CCM walifanya mikutano mingapi ya hadhara unguja na pemba?
Halafu utapata jibu kisha linganisha na turnout ya over 90% iliopiga kura.
Unahisi ni kipi kilichowapa wanasia wa zanzibar ujasiri wa kuupisha mwezi mtukufu wa ramadhani?
Kwa mawazo yangu wameupisha huu mwezi kwa kujiamini kua siku chache tu zinawatosha ktk kampeni.
Ramadhan kareem!
@Muunguja,
Naona kama maada sio kujadili ushindi wa kura ya maoni, bali ni creditability ya ZEC.Tunachojadili mbona takwimu zimeruka na kuwa tofauti na mazoea ?Kuna nini hapa ?
Zanzibar tumezoea turn out ya 90%, sasa na hii kura ya maoni ilikuwa na changa moto sawa na chaguzi nyengine.Isipokuwa kwa upande wa CCM hawakuwa na haja ya kufanya ulalamishi na vile vile muda ni mfupi kupandikiza wapiga kura.Hii ndio theory iliopo kichwani mwangu….
Sasa tutarajie nini uchaguzi mkuu turn-out ya 90%, yaani hio 20% kutoka Tanganyika kuja kupiga kura visiwani mwetu ?
Nadhani sasa utakuwa umenifahamu, sijadili ushindi wa NDIO – HAPANA.Hilo lishapita wala haliwezi badilika, bali nina mashaka na takwimu…nadhani na mwandishi Jabir pamoja na maada ni hio i.e “Wako wapi 114,630 wasipige kura”.
@Muunguja: Well came back.kwani nduguyetu ulipotea kwenye matandao huu kama ndugu (Mfroasty) alivosema.Mimi nakubaliana na mawazo yako kwamba ushindi ni ushindi tu, hata uwe wa goli moja. Lakini naona mada haikua kwamba watu wamelalamika juu ya ushindi wa kura ya Maoni. Bali watu wanalolijadili nakututia hadach ni hiyo turn-out ya vorters.
Kama sisi ni wazalendo na tunavipnda visiwa Vyetunilazima tulijadili jambo hili. Kufanya hivyo ndio kunatupa confidance na mwanya wakuwatia mortisha Wazanzibari watakao piga kura.Na siokama tulitaka tuwaburuze watu na kila mtu akatie kura ya Ndio hilo sio lengo la mtandao huu wala mada hii. Katika kuchangia madahii tumeshaona kwamba kulikua na factors tafauti zilizoshindikiza kuwa na watu 114.636. hawakjitokeza kupiga kura.
Muungja: kuhusu kuharibika kwa kua za Uraisi hili linaonekana wazi.CUF wanalijua hasa ukizingatia kwamba bado kuna watu, wana chuki za U-pemba na U-unguja. Na Wanaona chama cha CUF ni cha Kipemba japokua wanakosea.Ukijiuliza chuki hizi chanzo ni nini? watu hawa hawana jibu rasmi ila choyo cha nafsi na hakuna mtu anayeweza akaibadilisha nafsi ya mtu mwengine ila (ASW).
Angalau Wapemba wakia na chuki zao juu ya nduguzao wa Unguja unaweza ukazitia maanani kidoo. Mf: wakati wa utawala wa Mjombaako salimini Amour Wapemba walidhalilishwa sana wamefukuzwa makazi,kuvunjiwa majumba na kusambaratishwa na familia zao. Hatuna haja yakuwatonesha watu vidonda vyao. Hiyo ilikua Ndwele na imeshapita.
Lakini Waulize baadhi ya watu wa Unguja kwanini wanawachukia Wapemba hawana sababu.Kwani wao na watanganyika ndio Waliopindua, ndio wanaowasaliti ndugu zao wa Kipemba na ndio Waliotawala Visiwa tokea 1964. Sasa kuharibika kwa kura za Uraisi itatokana na kuwa haya majimbo 8 yote hawataki Mpemba awe raisi.
Kuhusu CCM kudorminant kura za uwaklishi/ubunge unaweza ukawa umetabiri right/wrong. Nasema hivo kwasababu kama uchaguzi utakuwa wa huru na haki. Upande wa Unguja CCM watayachkua majimbo yote 8 yaliosema hapana: hii ni kutokana na pesa zinazotumiliwa kwa kuwalipa Usalama wa kila jimbo.Ili wafanye kazi ya nyumba kwa nyumba lakini uchaguzi ujao BLW CCM wawe na nguvu. Tusidanganyane wawakilishi/wabunge wote wa CCM wana-mwaga pesa na kuwasaidia vijana wengi ambao hawana uzalekendo wa nchi yao. Na hii inakutokana nakua wana Serikali na pesa za bure.
Kwaupande wa Pemba kama uchaguzi utakua wa haki na huru basi CCM hawana jimbo hata moja watakaloshind. Hii nasema kwauhakika. kwani ndugu zetu wa upande wa pemba wana ari na nchi na sio pesa.
@mahluk: Nduguyangu maelezo yako ni mujarab sana,lakini tafadhali nakuomba ukiandika tena jaribu kuacha (paragraph/ nafasi baina ya sentece). kwani ujumbe wako umepachana sana na ni shida kusomeka.
kwanin nasema maneno yako n mazuri ya kuzingatia ni hili la kuliangalia tume ya uchaguzi. Nakujikumbusha kwamba ZEC walipoanza kuandikisha watu, ilkua hili neno la muafaka wa Maalim Seif na Mh.Amani lilikua na kebehi na kutokuaminika. Sasa wanaweza wakawa kwamba wameandikisha watu hewa kama alivoniambia mtu mmoja nyeti wa CUF ilipozungumza nae kwa simu.
Kwamba kuna majina mengine ndani ya Daftari hilo niyakubuni tu, wala hawa watu hawapo kabisa. Sasa hii ilikua ni njama yao ya makusudi walifikiria Mtu wao Bilal Gharib atapita ili watumie majina haya hewa. Lakini kama alivotupa mawaidha ndugu “Mahluk”. kwamba wewe ukipanga lako na (ASW) anamipango yake.Na ndio mpaka sasa hawajalitangaza daftari hili na wana-adhirika.
Maoni yangu kwa wazanzibari wale ambao wana uchungu wa nchi yao na vizazi vya baadae:
Tusilale na tukabweteka na tukaona opposition wna chance yakushina. No Still there is a lots of work need to be done. Nawakuifanya kazi hiyo nisisi watu walioko Uhaibuni na walioko nyumbani tushirikiane kuwa na umoja.
Uhaibuni: michango yenu pale ambapo inahitajiwa,musiquestion nakusita kufanya hivyo.
Nyumbani: Kampeni za nyumba kwa nyumba ili tuwabadilishe watu wale waliokunywa maji ya bendera, walikata tamaa na waliokua hawajui nini maana ya Nationality.Hawa anataka elimu na msasa.
la mwisho tujue kwmba CCM hawaibii number tu hata maneno yanaweza kuwa wizi kwao na wakamueka mshindi wanaemtaka. Kumbukeni uchaguzi wa 1995, hazikua number zilizotumiwa ila ni ulimi wa mtangazaji wa ZEC ndiyo aliempachika Salimini Amour madaraka haramu akesha akawasulubu Raia wenzake.
nawasiliha.
siasa ni sawa na mchezo wa mpira.hapa ccm wamechezesha kikosi cha pili kwa kuwapima nguvu CUF .Kutokana na mchezo ulivoenda na matokeo yake kocha wa CCM ameshaona ni wapi ataweza kupita kuyafunga magoli kwani wenzake waliingiza full nondo .kwa kilichosalia sasa tusubiri hapo wakati wa final ambapo ccm watachezesha kikosi cha mauaji. tumuombe mola atupe salama ya kudumu
asalam alaikum najua kila mtu ana wasiwasi kuhusiana na hiyo idadi ya watu walio zidishwa au walio pandikizwa kila mtu inampasa awe na wasiwasi lakini vilevile nyimbo mbaya haichombezi mtoto kwani ni sisi sisi wenyewe ndio tunao wambia kama tunawazindia zaidi na kujua linalo takiwa hapa ni kusema tu inshaallah tunashinda hata wafanye vipi ikiwa sasa tunaanza na wasiwasi si ndio tunawapa nguvu zaidi tukiwa tunashikilia tutashinda sasa wao ndio watakuwa na wasiwasi tusijivunje moyo na kusema kuwa matokeo yameshapangwa hapo ndio watu wetu wataona hata haja ya kwenda vituoni kupiga kura haina maana kwasababu mambo yashapangwa tujiepushe na kauli za kuwavunja moyo watu inatakiwa tuwajenge watu wetu na kuwambia tutashinda hata wafanye nini lakini utaona mtu anasema maneno yasio na msingi acheni maneno hayo inshaallah wazanzibar tumeshashinda kwakila dalili inaonyesha ccm hana chake atachukua majimbo yake 10 tu unguja na pemba hana chake inshaallah mtaukumbuka utabiri huu akipenda mungu kwani si chaguzi zote hawa ccm si wanapandikiza watu na wanashindwa iweje leo tuogope masalam