YA WANA CCM PEMBA AMA KWELI NGOMA INOGILE’

Written by  //  05/09/2010  //  Makala/Tahariri  //  7 Comments

  • WAWEKWE KATIKA KUNDI LA WATU WENYE MAHITAJI MAALUM{People with special needs}
  • Waraka huu wapelekewe Maalim Seif na Dr Shein

By Zdaima.

Katika maisha ya mwanadamu inapofika wakati mtu ikawa tabia na matendo yake hayaeleweki jamii huingiwa na wasiwasi,ukoo wake na hasa familia yake na mawazo ya kutafuta ushauri wa kidaktari huanzia hapo, Yawezekana ndugu zetu wana CCM Pemba wanaumwa tena kwa mda mrefu sasa na wanahitaji kutafutiwa tiba ingawa gonjwa lao linaonekana ni sugu{samahani hapa}

Katika muktadha huu naomba nifahamike kwamba lengo ni kukusudia wasaidiwe  wana CCM wa Pemba yaonesha wana matatizo hasa.

Msururu wa matukio ya wanachama hawa unatia shaka kwa matendo yao hasa katika kipindi kilichopita cha ”Gharka ya siasa mbaya hapa Zanzibar”  mpaka kuja kwa kura ya maoni na ndio msingi wa hoja yangu hii ulipoanzia kuelekea katika Mfumo mpya wa serikali ya maridhiano.

Tokea kuja kwa mfumo wa vyama vingi kuna vioja vingi sana vimetokea .Tazama kule pemba tokea asili kunajulikana ni ng’ome ya ya CUF hili wanalijua .Miaka ile  ya 1995 baada ya kuzuka zile siasa za uhasama jamaa hawa walitumika Kama mawakala wa vitimbwi vya serikali kwa wapinzani.Masheha walitumika kuhujumu na kuwatenga watu katika ajira,kutoa huduma,kutia fitna watu wafukuzwe kazi n.k  wote hawa wakiwa ni majirani zao na ndugu zao .Tuseme hapa siasa za vyama vingi zilikuwa ngeni wakidhani kwamba labda hivyo ndio wanawapiku wapinzani bila kujua kwamba siasa za vyama vingi ni kupata mbadala wa kupata chama cha kuleta maendeleo, ustawi na umoja katika jamii. Kwa Pemba hawa walipaswa kuangalia hatma ya maendeleo yao kwa ujumla wao kwanza  katika kisiwa sio hujma  za kivyama .Hapa sisemi kwamba nao wana CUF ilikuwa hawana hujuma hapana lakini katika hali ya kutengwa kulikokuwepo wakati ule katika maendeleo,madaraka,elimu,kubaguliwa  n.k wana CCM wengepaswa kufikiri mara mbilimbili hayo wayofanya ni kwa faida ya nani na ndio maana hata wana CUF waliwaona wenzao wa CCM kama masaliti.

Ni nani asiejua  kwamba katika utawala ule uhasama ulikuwa ni wa kivisiwa zaidi kuliko chama?

Kwani hata hao mana CCM walifaidika na lipi na waliepuka vipi kunyanyaswa kwa kebehi,maudhi,kutengwa na kuaibishwa kama walivyofanyiwa wengine kwa sababu ya ukada wao tu?

Jee ilikuwa hawaoni kwamba awamu zote tatu za vyama vingi kuanzia uongozi wa juu mpaka chini hawakuwa na uwakilishi wowote wa maana katika serikali.Wana CCM wa Pemba hawakuwa na sifa za kuwa wakuu wa wilaya,mikoa, makamishna,wakurugenzi, mawaziri,mabalozi kwazile nafasi angalau mbili za Zanzibar walizokuwa wakipewa, Uwakilishi wa kuteuliwa na Chama chao .Uwaziri kiongozi au hata uraisi? kilichokuwa kinafanywa ni ubabaishaji tu kuletewa meli ya Mv Mapinduzi {marehemu sasa} kwa ajili ya sherehe hujazana na wakifika Unguja huambulia zile kejeli nilizozitaja. Wanaweza wakaleta ubishi kwa kuangalia maslahi ya mtu binafsi kwa sababu wengine walipewa pipi na kupewa zile fedha mikononi mwao kwa ajili ya kufanikisha hujma za kuandaliwa kule pemba ,wanaweza wakatafsiri huku ni kuenziwa. Hapa kwa upande mmoja ni kuonesha uaminifu kwa chama chao lkn ni uaminifu uliochupa mipaka ya hadhi ya mwanadamu yoyote duniani.Kwani  lugha hizi hawakuzisikia?

“Disemba naja Januari narudi” “kumpa mkono mpemba ni kujinajisi”"mpemba hatawali” Mpemba kuingia ikulu ni sawa na Kelbu {nimeficha kidogo} nk  haya yote hawakuyasikia. lkn kadri siku zilivyokwenda walizidisha uaminifu wao ingawa huwakuweza kufua dafu kuwapiku wapinzani wao.

Pengine ni kutokana na vile walivofinyangwa na viongozi wao na athari za ule mzimu wa siasa za chuki zilizoletwa na watawala. Pengine walifika wakati wakahisi ni bora kunyanyaswa,kujipendekeza bila kujaliwa,kutumiwa na kudhalilishwa,walihisi haya ndio majaliwa yao na kwamba mabadiliko kwao wao ni ndoto iwe iwavyo.Walizugwa kwa ule msamiati “daima”na wakazugika kiaasi cha kushindwa kujifahamu hata majaaliwa ya ubinadamu wao,hili ndilo gonnjwa hatari.

Tazama basi hata ule mchakato wa kumpata Dr SHein kama mgombea Mwana CCM kutoka Pemba jinsi walivyovurugwa na walisikika wakitoa kauli za kutoridhika lkn ikawa tena lisilo budi hutendwa .Hawa ndio wana CCM wa Pemba

Lengine la aibu ,hata kura ya maoni walivurugwa na kuweka hapana wakati ilikuwa ndio nusura ya watu hawa .Ama kweli ngoma inogile .Inapofikia hatua hii watu hawa wanahitaji msaada na tunapaswa tuwasaidie wanaumwa hawa.

Kwa maana hii watu hawa waingizwe katika kundi la watu wenye mahitaji maalumu maana hawasikii,hawaoni,hawafahamu hata kwa vitendo na nadhani pengine hata hawana hisia{waepushe ya Allah}wanahitaji malezi maalum.

Naam kwa mantiki  hii na matarajio ya serikali mpya  ya Maridhiano baada ya uchaguzi naogopa wasije wakatutoka{kufa kihoro kwa fedheha} gonjwa lao ni gumu sana  wawekwe sawa kabla hatujakamilisha hilo kwa sababu likitokea hilo na ule uaminifu waliokuwa nao siku nyingi juu  ya “Kudumu”wanaweza wakapoteza fahamu na ikawa sababu ya kututoka.

Mwisho niwaombe radhi kwa kila atakaekereka.Mwenyezimungu waongowe watu hawa na wajirudi ktk kujumuika na wenzao kuijenga nchi yao na kuondoa mifarakano iliyodumu kwa kitambo sasa.

7 Comments on "YA WANA CCM PEMBA AMA KWELI NGOMA INOGILE’"

  1. Elbattawi. 05/09/2010 kwa 12:49 um ·

    La kusudi haliambiwi pole – huo ni uamuzi wao, akili yao inavyowatuma. Ila tunaweza kuwaambia kuwa Mwenyezi Mungu ni mkubwa. Zaidi ya hayo watajijuu….

  2. sale 05/09/2010 kwa 1:05 um ·

    Ndugu yangu unayosema ni kweli na mimi mwenyewe nimeyaona kwa macho yangu,,,Mimi ni mpemba niliezaliwa na kuishi maisha yangu Unguja lakini nilikwenda Pemba mara kwa mara kujuwa na kuwatembelea wajomba na mashangazi,Mimi wazee wangu wametokea Mjimbini na babu yangu katika uhai wake alikuwa mtu maarufu klwajina Saleh Kombo (makesi)
    Lililonishangaza mimi kuwa watu wengi walikuwa wakiishi katika hali duni, nchi haijajengwa serikali haijapeleka maendeleo yoyote muhimu kama vile mawasiliano, hakukuwa na barabara, maji safi, umeme nk,
    Ni kweli niliona kuna watu wamevalia nguo za kijani nyumba zao wamepaka rangi za kijani na njano, baadhi yao wamepewa vi ciao na vespa wakajiona kama wanaishi peponi kumbe wanashi katika shimo la moto,
    Walipeleka fitina kwa mapolisi juu ya wale wenzao walio wengi ambao walikuwa hawakubaliani na mfumo au matendo ya serikari juu ya Pemba na kizazi kijacho,,Chakushangaza nilizungumza na hao hao makada alijizalillisha baada ya kunambia Mpemba hatawali haliyakuwa yeye mwenyewe ni mpemba na ana watoto wakipemba wanakwenda skuli nawatoto hao ni miongoni ya wenye ndoto za kuwa viongozi wa visiwa hivyo baadae, Alinisikitisha sana na sikuweza kumfahamu,,,
    Sasa Ndugu mwandishi ni kweli unavyosema kuna gonjwa tena gonjwa lenyewe sugu na halina dawa, lakini ndio hivyo “MVUA IKINYESHA, HAIMNYESHEI MMOJA”
    Mimi jina langu Saleh Abdullatif Ahmed Mohammed Haji Mjimbini

  3. muhimu 05/09/2010 kwa 1:28 um ·

    hii mada mbaya imejaa pumbaa na uchochezi katik akipindi hichi cha maridhiano haifaaii
    siasa ni chaguo la mtu akitaka kuwa ccm au cuf au chochote iyoni imani yake mwenyewe imefika wakati tunachukiana kwa chama kuliko hata kafiri kwa muislam znz km leo atakuj akiongozi wa chama akiwa mkiristo utamsikiliza kuliko musilam mwenizo wa chama tofauti
    imefika wakati tujuwe kuwa siasa znz tuliipokeya vibaya ccm na cuf sote tuliopokeya vibaya watu tumeithamini kuliko dini ilifika wakati mtu ana mwacha mkewe kisa tuu mkewe ccm or cuf kuna watu walikuwa maduka yao yamesusiwaa tuu kisa ya ccm or cuf imefika wakati tukubali sote tulikuwa tuna makosa sasa ukikaa ukatonesha ndona ati alitumiwa kuleta askari or alifanya nini hii haijengi na ccm pemba still wana haki ya kuwa wanacham wa ccm chama sio dini sasa kejeli zako ulozikumbusha “december twaja ” namengine nadhani kwa usahuri wangu hayana mana kwani tunasonga mbele we dont care past

  4. salix2020 05/09/2010 kwa 2:08 um ·

    mimi nakubaliana na mtoa mada mia kwa mia na wala (muhimu) usikatae ukweli uliozungumzwa hapo ila kwa kuongezea niwape siri ya ccm wa pemba kuwa hivyo walivyo ni kwamba baada ya uchaguzi wa mwaka 1995 ccm walipoona wamepoteza viti vyote wakahofia chama chao kufa sasa nini cha kufanya kwa hao wanachama waliobakia ilikuwa ni kuwalisha yamini kwamba hawatokwenda kinyume na maagizo ya chama na wakubwa wao kwa namna yoyte ile ilimradi wainusuru ccm isije ikafa kabisa pemba na kwa ushahidi huo mimi binafsi ni mtu wa mkoani pemba kwenye ccm wakorofi kuliko wote kulikuwa na mzee mmoja wa kitumbatu kaishi pemba miaka mingi sana na alikuwa ccm gogo lakini kutokana na hali yamambo ilivyokuwa ikienda na asili ya watumbatu wengi ni cuf na alikuwa anaumia na ile hali lakini kutokana na shindikizo la ccm ikawa anaiunga mkono iyo basi tu maana uchaguzi wa mwa 2000 hakuweza kustahamili ilipofika zamu yake kupiga kura tupo kwenye msongo akamwita mmoja katika vijana tuliokuwa pamoja na alijua hakika huyu kijana ni cuf akamwita akamwambia njoo unipigie kura maan alikuwa haoni vizuri wallahi akasema apigiwe kura yake kwa wagombea wa cuf lakini cha kushangaza ccm wenziwe walipogundua walimtenga ama akaingia kama kihoro hakupata uzima wake mpaka akafa allah amsamehe na amridhie kwa hiyo ccm wapemba wamelishwa yamini na pia wamekunywa maji ya bendera ukiwapasua watoka damu ya kijani wao ilimradi ipepee tu hata kama ale dongo

  5. sale 05/09/2010 kwa 2:22 um ·

    hiyo ni kweli Salix2020..
    Lakini ukizungumvia ukweli watu huumia na kusema”WE DONT CARE THE PAST” Lakini mi naona watu “THEY ARE LEARN FROM THE PAST”
    Alafu mi naona Siasa ni sera za maendeleo, sasa kama kuna Chama kina sera ambazo hazileti maendeleo sehemu fulani, Watu wafanyeje kukihama chama au kukiunga mkono hicho chama? kama walivyofanya huko pemba?

  6. chachandu 05/09/2010 kwa 3:48 um ·

    ramazani njema kwa wote. inashangaza kuona mada kama hii ikiandikwa katika ukumbi kwani imejaa majungu na uchochezi..yawezekana hayo aloandika yametokea sikatatai kwani binadamu tuko hulka nyingi lakini sio vyema kwa wakati huu hasa tukiwa katika maridhiano kuanza kutonisha madonda .sina haja ya kuleta utashi wa kisiasa wala malumbano ya aina yeyote lakini ni vyema wazanzibar tukaanza na tabia chokochoko na kuangalia zaidi mustakabali mwema wa vizazi vyetu.tukianza na kusema ahh waunguja walikua hivi na hivi jee inamaana sasa wapemba nao kwa vile ndio wameshika hatami za uongoza nao wafanye kama walivyofanyiwa?yawezekana hayo makubaliano ya seif na karume ni ya wao wawili tu na wengi bado wanavundu katika nyoyo zao na wanasubiri wakati muafaka tu waanze vioja vya visasi..Nyimbo mbaya haichuchiwi mtoto.

  7. Junius 05/09/2010 kwa 3:57 um ·

    I’m sick of this U-unguja and U-Pemba nonesenses, tatizo la CCM wa Pemba ni tatizo la CCM wengi kama si wote Zanzibar. Unapo li-specialize ni sawa na kuishadidia ile dhana ya ubaguzi wa kieneo wa Unguja na Pemba,ambayo ilishabikiwa sana na Nyerere kutugawa, Hii si sawa hata kidogo.this is Mapurism!!

    Zanzibar imekuwa na chungu tele ya matatizo,sote tunayajuwa. Wengi tulitaka Mungu atusaidie kupata dawa ya matatizo yetu, wapo watu licha ya matatizo haya yote walitamani hali ibakie hivi hivi.

    Hawa hawakuwa Pemba tu, walikuwa Makunduchi, Donge, Dole, Kwahani,Chaani, Muyuni n.k wengi wao ni wana CCM, wafurukutwa wakubwa ambao hawakujali umasikini, ziki, shida n.k zinazovipata visiwa hivi kwa kukumbatia siasa za mifarakano. Wote hawa walikuwa wanahitaji msaada maalumu kama wenzao wa Pemba na kwengine kote Zanzibar.

    Shida za Zanzibar hazikuwa kwa wpemba tu, maeneo chungu nzima yalikuwa na yana shida zile zile…Watumbatu wana shida zao kuliko za Pemba, kadhalika na Uzi, Unguja Ukuu, Shangani-pitanazako n.k kote kulikuwa na makada wa CCM waliokuwa hata hawahisi shida hizi kuliko ukerekweta wao au walikuwa wanahisi ila kasumba walizolishwa ziliwazidi nguvu hata kufikiri mabadiliko yanahitajika,ilikuwa kazi pevu kwao.

    Ni hao hao yalipokuja mabadiliko ya muundo wa serikali, waliyapinga kwa nguvu zote na maeneo yao yaliongoza kwa wingi wa kura za hapana, tena afadhali ya Pemba hoja inaweza kujengwa kuwa mwitiko wa mabadiliko ulikuwa mkubwa, pengine hata CCM wa Pemba waliyaridhia.

    Zaidi tunaweza hata kusema kuwa, CCM wa Pemba walijitokeza wazi kuunga mkono mabadiliko hayo. Sote tunamkumbuka Salim Juma Othman na nasaha zake, nikikumbuka maneno yake akisema “Kamba hiyo tumerushiwa kazi kwetu…”. Sahibu yangu naye Issa Ahmed Othman, kada mkubwa wa CCM kutoka Pemba, ndiye aliyengoza kampeni za Dr.Sheni kutoka Pemba.

    Hivyo, kwa CCM wa Pemba ni wazi kuwa walishachoka na kuburuzwa buruzwa, hawakuwa na la kufanya tu hapo kabla, lilipotekea walishukuru na kuunga mkono bila vikwazo, mifano nimetowa hapo juu.

    Kazi kwa CCM wa Unguja ambao kampeni zao na matendo yao yanaakisi kabisa na makala ya mwandishi, ni sawa mtu kusema Maalim atangazwe leo kuwa rais, basi maiti za watakaokufa kihoro, tutakazookota Makunduchi, Donge, Chaani, Dole, Kwahani n.k zitakuwa nyingi sana kuliko za Mkoani, Chake na Wete.

    Wapemba, na ukaidi wao wote sifa yao kubwa ni waelewa, tumeona siku moja baada ya Maalim kuzomewa Unguja kwa kumtambuwa Karume, siku iliyofuata haikuwa hivyo kwa Pemba. Walitulia wakatafakari na kumuelewa na kutokana na wao hali ikabadilika.

    Kwa hiyo madai ya mwandishi hayana usahihi sana kuwa CCM wa Pemba wanahitaji msaada maalumu wakati kwao wao hayo yote ni ahuweni na wanamshukuru Mungu, ALHAMDULLILLAH!
    MUNGU IBARIKI NCHI YA ZANZIBAR
    J

Comments are now closed for this article.