Zama za Maalim Seif hazijakoma!
Written by amini // 11/01/2012 // Makala/Tahariri // 42 Comments
muhariri Absalom Kibanda
TAIFA linao viongozi wawili tu maarufu zaidi ambao majina yao halisi yameunganishwa na uasilia wao wa kitaaluma na kikazi waliokuwa nao kabla hawajaingia katika ulimwengu wa siasa.
Viongozi hao wawili si wengine bali ni Baba wa Taifa ‘Mwalimu’ Julius Kambarage Nyerere na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), ‘Maalim’ Seif Sharif Hamad.
Ni jambo la bahati tu kwamba, viongozi hao wawili wa kisiasa walio na ushawishi mkubwa na ambao wamefanikiwa kuishi na sifa yao ya kitaaluma ya ‘Mwalimu’ (Maalim) kabla ya kuingia katika siasa walikuwa ni walimu.
Ingawa kifalsafa, kiuongozi na hata kimaono wanasiasa hawa wawili hawawezi kufananishwa achilia mbali kulinganishwa, bado ukweli unabaki pale pale kwamba, kazi walizofanya zimeweka alama ya kudumu katika maisha ya watu waliopata kuwaongoza.
Ukimwacha Baba wa Taifa ambaye wasifu wake unafahamika miongoni mwa Watanzania walio wengi, Maalim Seif anabakia kuwa mmoja wa wanasiasa adhimu ambao Zanzibar imepata kuwa nao tangu mapinduzi ya visiwa hivyo, Aprili mwaka 1964.
Alama alizoweka katika medani ya siasa na uongozi, tangu akiwa Waziri wa Elimu Zanzibar na baadaye Waziri Kiongozi miaka ya 1970 na 1980, kabla hajalazimishwa kuingia katika vuguvugu la siasa za upinzani mwanzoni mwa miaka ya 1990 kwa kiwango kikubwa ndizo ambazo zinamweka katika daraja la juu la kiuongozi katika taifa hili kwa kiwango ambacho hakijapata kufikiwa na mwanasiasa mwingine yeyote ukiwaacha waasisi wawili wa taifa hili, Nyerere na Abeid Amani Karume.
Viatu vya kisiasa na kuongozi anavyovaa au alivyopata kuvivaa mwanasiasa huyo kwa namna yoyote ile vinawapwaya makumi ya viongozi wa kisiasa waliopata kutokea katika visiwa vya Zanzibar, achilia mbali wale wa Tanzania Bara.
Kwa miaka mingi, Maalim Seif, amekuwa ndiye rais aliyekuwa ndani ya mioyo ya Wazanzibari walio wengi tangu aliponyimwa fursa hiyo kimizengwe mwanzoni mwa miaka 1980 na nafasi yake ikachukuliwa na marehemu, Abdul Wakil Nombe.
Ingawa ndani CCM na hata akiwa CUF hajapata kutawazwa kuwa Rais wa Zanzibar kwa sababu za kufitiniwa kisiasa, Maalim Seif ameendelea kuwa mwanasiasa mwenye mvuto mkubwa na wa kipekee kisiasa na kiuongozi ndani na nje ya visiwa hivyo.
Heshima aliyojijengea kama kiongozi wa watu aliye na ushawishi na nguvu kubwa kwanza katika kisiwa cha Pemba na kisha Unguja ndiyo ambayo kwa upande mwingine imemfanya ajikute akizalisha maadui wengi wa kisiasa.
Uadilifu wake kifikra na kimaisha, uchapaji kazi wake usiomithilika, utu wake uliotukuka na mapenzi yake ya kweli kwa watu anaowaongoza, mbali ya kumjengea sifa na heshima vimemjengea maadui wa kila namna katika maisha yake ya kisiasa.
Jina jipya lililoingia katika orodha ya maadui wa kisiasa wa Maalim Seif ambaye sina shaka hata kidogo kusema kwamba naye amenaswa katika mtego ule ule uliowanasa wanasiasa wengine kabla yake ni Hamad Rashid Mohammed mmoja wa wanasiasa wenye majina makubwa hapa nchini.
Katika mazingira ambayo si rahisi kuyaeleza kwa ufasaha, Hamad Rashid kwa matendo na maneno alijiweka katika mtego wa kutimuliwa ndani ya CUF tangu siku alipopata ujasiri wa kuamua kukabiliana na Maalim Seif ana kwa ana na nje ya vikao rasmi vya chama hicho.
Ingawa katika fikra za wadadisi wa masuala ya siasa, wakiwamo wanasiasa wa ndani na nje ya CUF, wanazuoni na wanahabari, Hamad Rashid alionekana akifanya jambo sahihi lililomfanya aonekane kuwa shujaa wa kisiasa ndani ya moyo wa chama hicho, kile alichokifanya kilibeba taswira moja kubwa; usaliti.
Mara moja, mwanasiasa huyo ambaye alijipatia umaarufu mkubwa Tanzania Bara pengine kuliko ilivyokuwa kwa mwanasiasa mwingine yeyote ukimwacha Maalim Seif mwenyewe kwa namna ambayo hakutarajia akashangaa akijikuta akibaki mpweke ndani ya chama chake kadri siku zilivyokuwa zikisonga mbele.
Yale yaliyotokea ndani ya kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la CUF siku ajenda yake ilipokuwa ikijadiliwa, yalitosha kumfanya Hamad Rashid abaini haraka haraka kwamba, wabunge wenzake na baadhi ya watu aliokuwa akiamini kwamba walikuwa upande wake wa pili na si kwake.
Ni jambo la kutatiza sana kwamba, Hamad Rashid aliingia katika mapambano hayo akisahau kwamba, Maalim Seif ndani na nje ya CUF ana nguvu za kitaasisi zaidi pengine kuliko walizonazo au walizopata kuwa nazo wanasiasa wengi wengine ndani na nje ya chama hicho.
Matamshi ya Hamad Rashid na yale yaliyokuwa yakitoka vinywani mwa wafuasi wake kabla ya vikao vya kumjadili yalimfanya yeyé na wenzake wengi kuamini kwa dhati kwamba kwa mara ya kwanza walikuwa wamepata mbinu ya kumbwaga kutoka katika kiringe cha siasa jabali la siasa za Zanzibar, Maalim Seif.
Hamad Rashid alifanya hivyo akisahau kwamba, Maalim Seif aliyekuwa akijaribu kupimana naye nguvu ndiye mwanasiasa pekee aliyepata kukabiliana na Baba wa Taifa na akaendelea kubakia na heshima ya kipekee kwa watu wake.
Mbunge huyo wa Wawi alionekana dhahiri akisahau ukweli kwamba, Maalim Seif ndiye mwanasiasa pekee anayeishi leo aliyepata kukabiliana na ‘maguvu’ ya CCM na dola tangu mwaka 1980 na akaendelea kudumu na kubakia na ushujaa alionao leo pasipo kutetereka.
Kama hiyo haitoshi, Hamad Rashid na mashabiki zake waliingia katika vita hiyo wakisahau kwamba ajenda ya mabadiliko ya kisiasa Zanzibar yaliyoilainisha CCM haiwezi kufanikiwa pasipo kuunganishwa na jina la Maalim Seif.
Wapinzani hao wa Maalim Sef walisahau kwamba kile ambacho Hamad Rashid alikiita ‘CCM B’ akinaswa na mtego wa hoja za washindani wao, CHADEMA kwa wana CUF wenzake na hususan viongozi wa chama hicho walio ndani ya serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar ni mtaji wa ushindi mkubwa siku zijazo.
Hamad Rashid aliingia katika vita hivi huku akisahau kwamba alikuwa akipambana huku akisahau historia ya yeye mwenyewe kupata kukaribia kukataliwa katika mchakato wa kusaka mgombea mbunge wa Wawi kwa tiketi ya CUF kabla ya jina lake kurejeshwa na Maalim Seif yule yule aliyedhani angeweza akamkabili na kumshinda pasipo kwanza kupata baraka za wapigakura wake.
Pengine kikubwa ambacho, Hamad Rashid na wenzake walikisahau wakati wakipambana ni kosa lao la kushindwa kumtambua adui wa kweli wa CUF ambaye, yumkini siyo Maalim Seif ambaye walimlenga na kumshambulia.
Ni jambo lisiloingia akilini hata kidogo kwa wanasiasa makini wa aina ya Hamad Rashid kumtwisha mzigo wote wa lawama Maalim Seif za kukwama kwa chama hicho kupenya ngome ya kisiasa ya upande wa pili wa muungano.
Zile lawama walizokuwa wakivurumisha kwa Katibu Mkuu wao kwamba alikuwa ameshindwa kuchukua hatua zozote za maana kukijenga chama chao Tanzania Bara wakati wenyewe wakijua fika kwamba jukumu hilo ni la viongozi wote wa chama hicho akiwamo mwenyekiti wao, Profesa Ibrahim Lipumba, japo zilionekana kuungwa mkono na wapambe wengi bado zilikuwa hazitoshi kuwafanya wakabaki salama.
Katika mazingira ambayo nguvu ya kipekee na ya kihistoria ya jina la Maalim Seif iliyokijengea uhalali chama hicho kwanza Pemba na kisha Zanzibar nzima, yalitosha kabisa kuwaadabisha na kuendelea kuwaumiza mbele ya safari Hamad Rashid na wafuasi wake ambao ama wamesahau walikotoka au hawajui nini wanakitafuta Wazanzibari na wapenda mageuzi huko tuendako.
Kushindwa kwao kuutambua ukweli huo, ndiko kulikowafanya waonekane haraka haraka kuwa mawakala watu wasioitakia mema Zanzibar na mamluki waliotumwa kuiua CUF badala ya kuijenga kama ambavyo wao walitaka waonekane kuwa.
Katika mazingira ambayo nguvu na historia ya mtu mmoja anayeungwa mkono na kulindwa na rekodi ya fikra, maamuzi na matendo yake kama alivyo Maalim Seif, kujitokeza na kuamua kumkabili kwa namna walivyofanya kina Hamad Rashid ni kujitakia kifo cha kudumu cha kisiasa.
Ingawa ni kweli kama kiongozi na mwanasiasa, Maalim Seif anayo mapungufu mengi, Hamad Rashid na wenzake walipaswa kulijua hili mapema kwamba, si jambo rahisi hata kidogo ukamshinda kwa namna ya kumuumbua mtu ambaye mnajua fika kwamba taswira anayoibeba ina sura ya kitaasisi zaidi kuliko alivyo mtu binafsi.
chanzo tanzania daima





42 Comments on "Zama za Maalim Seif hazijakoma!"
Ndugu kibanda umenena, ahsante.
YAHE,KIBANDA UMESEMA MANENO MAZIMA MNO HUJAACHA KITU,KILA KONA KUN -ZUNGUUKA HWEACHA JAMBO,
AMMA KAMA NNAPIKA,PILAU LEO NINGEKUKARIBISHA, ELA NYAMA UNGENIACHIA NILE MWENYEWE EHEEEEE
MWAMBIEN UYO HR ASOME HII MAKALA ,KAMA MTU KWELI MTUME ITAMTOA MACHOZI NA KUMTIA AIBU,
MH HAYA KWAHERINI MIE,
KISAKUNDE BIN MTI MKAVU
Mada ipo wazi na nzuri sana, ahsante mwandishi ingawa wapo watakao………………………………………….., ila umemaliza kila kitu.
Samahani wazalendo ipo nje ya Mada
..Scotland’s First Minister Alex Salmond fuelled a tense constitutional clash with the government on Wednesday, insisting that his government can organise its own independence referendum in 2014.
Prime Minister David Cameron announced on Tuesday he would give Edinburgh legal powers to hold a vote on a break-up of the 300-year-old union, but said it will be unlawful unless done with London’s approval of the timescale and conditions.
But Salmond, a nationalist who is widely regarded as one of the sharpest political operators in the British Isles, has announced plans for Scotland to hold its own referendum in the autumn of 2014, on its own terms.
The issue could now end up at the United Kingdom’s Supreme Court.
Salmond, whose Scottish National Party last year won the first majority in the Edinburgh assembly since it opened in 1999, said there was a “mandate for the Scottish parliament to organise and hold the referendum” on its own.
“It must be a referendum built in Scotland and decided by the Scottish people,” Salmond told BBC radio.
Polls currently show a lack of support for independence among Scots.
But Salmond is seeking to capitalise on nationalist sentiment as 2014 is the 700th anniversary of the Battle of Bannockburn, a famous Scottish victory over the English.
In the same year, Scotland also hosts the Commonwealth Games in its biggest city Glasgow and golf’s Ryder Cup.
Cameron’s coalition government wants the vote to be held as soon as possible and on its own terms, in a bid to keep the United Kingdom together.
In its statement on Tuesday it did not set out the conditions it wanted but reports say it would seek a simple yes/no question on independence, whereas Salmond is thought to prefer a third “independence-lite” option.
A row is also brewing over the voting age for the proposed referendum. The SNP wants 16 and 17-year-olds to be involved but London believes it should only be those aged 18 or above, in line with Britain’s general election.
Cameron said at the weekend that uncertainty over the issue was harming the Scottish economy.
But Salmond accused Cameron of being “almost Thatcher-esque” by trying to set conditions for Scotland, referring to the former Conservative premier Margaret Thatcher played by Meryl Streep in new film “The Iron Lady.
He indicated however that he was ready to strike a deal if London recognised it was lawful for the Scottish government to hold the referendum.
Former finance minister Alistair Darling, himself a Scot, said he believed the pro-union campaign would win if his Labour party worked with the Conservative-Liberal Democrat coalition.
“The only reason we have been put off until 2014 is because Alex Salmond doesn’t think he can win just now and he is playing for time,” he told the BBC.
In Scotland, newspaper The Scotsman ran the front-page headline “1,000 days to decide our future”.
It also ran a piece by an expert on referendums, Matt Qvortrup, saying that Salmond’s arguments were correct, citing the examples of Montenegro’s secession from Serbia in 2006 and Estonia’s independence from the Soviet Union in 1990.
“The basic principle in international law is that the seceding country (in this case Scotland) decides whether it wants to become independent,” he said.
A survey by British Future, an independent think-tank, said Monday that 54 percent of Scots wanted Scotland to remain part of the United Kingdom, compared to 29 percent in favour of independence. It polled 497 people last month.
The Scottish parliament currently has power on matters such as education, health, the environment and justice. Key areas including foreign affairs and defence are still controlled by the British government in London.
A break-up would involve thorny economic issues such as North Sea oil and gas. Scotland has long complained that tax revenues from the industry — £8.8 billion ($14.4 billion, 9.9 billion euros) last year — go direct to London.
But there is also the issue of a currency, with Salmond refusing to say whether an independent Scotland would join the struggling euro.
…
@Kibanda
Ahsante sana
@ Embesakua
Hizo ndo mada kaka za kuweka, nakushauri mara nyengine ieke kwa kiswahili ili na wazalendo wengine wajue nini kipo, na si vibaya ukiiweka kama mada ikaonekana na watu wakapata kuisoma, humu kwenye comment si wote watakaofaidika.
Soon Zanzibar nayo tutaamua hayo hayo na tumo katika harakati za kujikomboa inshaallah Mwenyezi Mungu tupe uhuru wa nchi yetu ya Zanzibar nasi tujitawale tusitawaliwe.
Kila la kheri Zanzibar,
Umoja, mshikamano, Uhuru.
Absalom Kibanda
Ama kweli kumbe bado wapo wasomi wanaojua na kutumia elimu zao na nafasi zao kwa umakini. nilidhani watu wa bara hawaelewi mambo ya ndani ya zanzibar na juu ya suala linaloendelea la hamad rashid. Nimekuwa nikimfuatilia Absalom Kibanda kupitia gazeti la tanzania daima bila shaka amesema kweli na hilo ndilo ambalo viongozi na waandishi wengi wa bara wanalolificha.
kutokana na umahiri na umakini wa kibanda ndio maana serikali ya muungano imekuwa ikimtisha na kumnyanyasa kila siku ili asiandike na kuruhusu ukweli katika gazeti lake.
tunajua wote kuwa gazeti analoliongoza ama kwa upande mmoja baadhi ya habari au waandishi wake wamekuwa wakilishabikia suala la hamad rashid lakini kutokana na makala yako kibanda imeonesha dhahiri kuwa wewe uko makini na unafuatilia kwa makini kila kinachotokea iwe zanzibar au bara.
hongera kwa makalayako na usikubali kuburuzwa kuongea ukweli hata kama unakera baadhi ya watu. hawa ndio wahariri inaowahitaji watanzania na tanzania ya sasa tuliyonayo.
biguuuuuuuuuuuuup KIBANDA.
salamu wazanzibar, @ EMBESAKUWA, mimi sitowacha kukuandama mada inasema nini na wewe unasema nini wewe inaonyesha limbukeni kama humpendi seif hiyo ni broblems zako kama huwapendi cuf huo uhuru wako lakini kwanini hujibu mada siku zote najaribu kukutasmini mtu wewe lakini kila nikukustasmini naona najipotezea wakati wangu kwa mtu juha kalulu, hapo kazungumzwa sifa za seif kama unazihisi sivyo lete zilizo sawa ili wapambe kama mie tuelimike au tukuelimishe , lakini wewe siku zote uko mpande mwengine unapinga lakini hutoi hoja , umekuwa unaruka kama sungura hutulii sehemu hoja iko wazi anae zungumziwa hapo ni mr sif sharif hamad mzanzibar, na sio hao ulio wataja, alex and cameron, usikasirike mimi kukwita mbumbumbu hii imetokana na wewe mwenyewe kuwa hujui unafanya nini , muhimu usitoke nje ya huja .
@ Aslam
mimi siku zote namwambia Embesakua huwa haangalii mada inasemaje yeye huwa anaenda upande mwengine, na wakati hii comment yake ni mada nzima bora angeitafsiri akaiweka kama madanyengine.
@ Embesakua
Jirekebishe, na halafu pia uwapende watetezi wa Zanzibar usiwachukie akiwemo huyu Maalim Seif, ukifanya hivyo kaka ni vizuri, huwo ni ushauri wangu kwako.
ama kweli, ndugu zangu leo mumeniwacha hoi, kwa sababu huyo kabunda kamponda HR basi kila mtu anasema ndio, wengine wanasema kamaliza kila kitu, jamani hemu someni vizuri, HR mulimtukana kuwa anamsifu nyerere, leo katokea mtu anamtukana HR, then anamsifu Seif na Nyerere, kawa mtu wa maana, wengine wanasema ni watu wanotumnia elimu zao hao, hee kumbe nyerere nae mtu? mie nilikuwa sijui mpaka leo, anasema nyerere kawacha athari kubwa kwa watu alowatawala (nakumbuka kama Nyerere alikuwa rais wa jamhuri ya Muungano, maana tanganyika nz znz) na munasema kweli kabisa, umemaliza kila kitu kabunda, leo mtanganyika anomfananisha seif na nyerere kawa mwema? mtumeeeee, mungu atawasaidia.
Tena tizameni anavowatukana halafu nyie munamsifu (ama kweli waznz kwa fikra hizi tumeumia) baada kumsifu nyerere na kumfananisha nyerere na Seif anasema hivi na nanukuu
”Ukimwacha Baba wa Taifa ambaye wasifu wake unafahamika miongoni mwa Watanzania walio wengi, Maalim Seif anabakia kuwa mmoja wa wanasiasa adhimu ambao Zanzibar imepata kuwa nao tangu mapinduzi ya visiwa hivyo, Aprili mwaka 1964”
hivi jamani kumbe mapinduzi ya zanzibar yametokea april 64? mie nilifikiri hio ni tarehe ya muungano, nilifikir mapinduzi yalikuwa January 1964? lakini madhali kasifiwa seif hapo, nakwambia hata aseme muungano ulikuwa 2011 basi watamsifu tu madhali kasifiwa Seif. tena yale matusi ya waznz kuwa nyerere ni baba wa taifa wa Tanganyika si Tanzania leo yameenda wapi? yaani ukitaka kuwapumbaza wapenzi wa Seif kwanza msifu Seif Sharif then hata ukiwatukania mama zao, madhali umemsifu Seif basi haya tu.
Mhhh!!!! yangu macho na mapenzi yenu ya halal badri hayo
ss jamani embesakua si kaomba radhi kwanza, lakini mbona hatuna stahamala, ss kama ana kazi muhimu jee hawezi kuifanya hivyo munavyotaka nyie lakini kaona faida isikosekane kabisa kahisi aiweke hapo tu kwani kuna ubaya gani? mbona tunakosa hekima jamani?
ss kama ww unahisi hio mada ingetafsirwa kwanza then ikawekwa hapo si uitafsiri ww then uieke kama makala, then uandike tu imetolewa na embesakua, imetafsiriwa ueke jina lako, sidhani kama embesakua atanuna kwa hilo, tuwe tunasaidiana jamani tusiwe mabingwa wa kulalamika tu
@ MZANZIBAR HALISI, sikiliza ndugu yangu huyu kazowea sio leo tu hii ni tabia yake hukurupika tu sio leo hii ni tabia yake sisi tunataka tumrekebishe , sasa yeye ikiwa anajua kuwa anatoka ndani ya mada na akaendelea hu hisi hapa amefanya makusudi , kwa upande wangu mie inanisubua sana inabidi nitoke ndani ya mada, na nianze kusoma jambo ambalo sio pahala pake , hio ndio tatizo na mara nyingi hajibu hoja huvurumisha mabomu kesha hukimbia watu wakianza kumjibu anabadilisha hadith kwa kweli haeleweki , kama kesi mahakamani basi gaji kesi yake ataitupa inatoka nje ya mada .
@ aslam
sawa ndugu yangu hakuna mkamilifu kati yetu, hewallah atajirekebisha insha Allah kishawasikia lakini sote hatuijui hii embesakua ndo ipi pengine ina kazi nyingi hii embesakua tuwe wavumilivu ndo mtandao wa jamii unavokuwa, embesakua vijana wanalalamika unakimbia mijadala, jitahd usikimbie kama ni kweli waelimishe kwa unachokiamini na kama tumefika mahala tunahisi mpinzani wangu ktk mjadala yuko right naomba tukubali kwamba naam mm nilikuwa siko sahihi hilo ndo lengo la kutumia muda wetu kuelimishana hapa. pole aslam
@ Aslam
Mwanaadam haachi kukosea
Tatitzo nini kama mada imekuchanganya nlitanguliza samahani kwanza au hujaiona?
Kama ttzo ni kukimbia mjadala sio kweli ttzo lako unatanguliza matusi na unatuma deadly comment kwa hio unavunja taratibu za mijadala ,kama kweli unataka kufaham kitu jaribu kutumia lugha ya kutaka kufaham.
Juzi juzi ulitoa comment yako ukasema HR akija znz auliwe nikakukataza bali ulishikilia msimamo ule ule. Kweli sio kweli? sasa kama wewe kama inakujia ktk akili yako Muislam mwenzako auliwe au apate tabu yeyote ile kwa mambo ya kisiasa mi sipo pamoja na wewe. na itabidi uombe msamaha kwa Mola wako unless uwe Kuffar
Hio ndo fumolar ya Dini yetu kwamba kama unataka mjadala basi tumia lugha ya mjadala kama ukija na lugha zako za madharau au matusi au inciting violence mimi sina muda wa kupoteza.
Falsafa hizi zitakusaidia ktk maisha yako.
Mkere mwalim ubaki na ujinga wako
Mkere daktar ubaki na ugonjwa wako.
@ Said- Said
Sikua na muda wa kutafsir hio mada na hio habar imepatikana BBC ndio nikaona kwa njia moja au nyengine ina faida.
Katika comment zangu mujue kwamba mimi sio cuf wala ccm kwa hivyo musinilazimishe kuwapenda wanasiasa, na kama mnavyosema narusha mabom kisha nakimbia basi ndo mujue mimi sina cuf wala ccm bali ni muislam tu aliye dhaifu na wala sio maridadi au handsome au tajir fulani au msomi no. Na ukweli hayo sio mabom huo ni ukweli na uhalisia.
Mtandao huu nnavyojua ni wakizalendo si wa cuf wala ccm unless nipate maelezo zaid.
@ Mzanzibar original
Ushauri wako lazma ufanyiwe kazi kwa njia moja au nyengine
Wasia ni kwamba
Watu wasimdharauliane wao kwa wao kwa sbb anayedharauliwa huenda akawa bora kuliko anaedharau.
Natanguliza Shukrani
@ embesakua
pole ndugu yangu ndo mambo muhimu kusameheana tu, hakuna mkamilifu
Ama kweli mwandishi unaonekana umekula biriani leo kwa vile unawasifu
viongozi ambao kwa kiasi fulani ndio wametufikisha hapa tulipo.
Tukianza na huyo Nyerere,yeye ndio kiongozi mbaya kuliko wote Tanzania iliowahi
kuwa nao,kwani yeye alikuwa anajiamulia mambo atakavyo na kutuendesha kama
atakavyo ,kutunyonya, kutubinya na hata kutuondolea Rais wetu wa Zanzibar na
sijuwi katiba ile kaitowa wapi wakati nchi hizi kila moja ina mamlaka yake sasa
sifa gani alizokuwa nazo Nyerere?.
Tuje kwa huyo Maalim mwengine Seif Shariff yeye ndie mmoja aliemfanya rafiki
yake huyo Nyerere na hadi akampelekea kumpa siri za Aboud Jumbe za kutaka
kuuvunja muungano sasa mbona hayo hukuyatia?.
Tuache mambo ya kusifu kwa kumpenda mtu japo katenda makosa makubwa
ambayo katu hatutosahau kwani tungekuwa mbali hivi sasa.
Huyo Nyerere tunamjuwa kuwa ndie adui yetu mkubwa na ndiye aliekuwa
akifanya juu chini kuikandamiza Zanzibar kwa hali na mali, na tunakuomba
mwandishi siku nyengine ukishiba biriani zako basi bora lala mpaka itoke
na usituchenguwe kwa kutuletea utumbo wa habari kama huu.
ZANZIBAR ITAKOMBOLEWA NA WANANCHI HAPO TUTAPOAMUA .
@Embesakua
Mara nyengine usipachike makala kwenye ukumbi wa maoni ambayo haifanani na mada kuu.Pia ni upuuzi kusema samahani kwanza huku ukijuwa kwamba unataka kufanya kosa.Makala hii inafaa kusomwa na Wazanzibari kujiongezea elimu ya kujikomboa lakini hapa si mahala pake.
@ HALIKUNIKI @ Mzanzibari Orignal @ Embesakua
Mada ipo wazi, mtoa mada hakumsifu Nyerere bali kafananisha upevu wa kisiasa wa Maalim Seif ambao nyie nyote mwaujuwa ila munapinga bure.
Kama mtu kala biriani ni yake mwenyewe jamani, na hakuna mtu anaezuiliwa kutunga mada akaleta hapa, sasa naomba tutungieni mada kama hiyo inayohusiana na Hamad Rashid????????
Pili, lile kundi linalotumiwa kuuparaganyisha umoja wa wazanzibari hizo mara nyingi ndio huwa hadithi zao, Maalim Seif hakumfitinisha Jumbe, Jumbe mwenyewe hakua na nia njema na Zanzibar mpaka maji yalipoanza kumfunika akaona anazama.
Kaunganisha vyama na kuiuwa ASP jambo ambalo kwa urahisi lingeikomboa Zanzibar kwakua na mamlaka yake, halafu anakuja Nyerere namwambia jiuzulu naye anajiuzulu huwo si upumbavuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu????????????/
Raisi wa nchi anaambiwa ajiuzulu naye anajiuzulu bila ya hata kuwa na upeo wowote??? kwani angekataa ingekuajeeeeeeeeeee??????????? Leteni ushahidi wa hiyo kauli yenu ya kwamba seif sharif kafanya hivyo halafu na mimi nitakuja na wangu wa kuthibitisha, hamna mpya hiyo ndo hadithi ya wengi wasiompenda Maalim Seif.
Maalim Seif na chama chake wanapigania hayo mnayosema aliyataka Jumbe sasa sijui ipo wapi hiyo hoja yenu?????/
Kila la kheri Zanzibar
Umoja, mshikamano, uhuru
@ said-said
mimi nakushangaa sana ndugu yangu, hoja hii uashawahi kuileta na nikakujibu ukaingia mitini, leo unaileta tena? nakuuliza tena ww umeona upumbavu sana Jumbe kujiuzulu kwa sababu alikuwa rais, lakini mbona huoni upumbavu Seif kukubali kushindwa wakati kashinda? na huo si upumbavu? utafutie jina kama si upumbavu, au kunya anye kuku tuu ……. na kwani Seif angekataa matokeo nae ingekuaje? na kama ni hivyo unavyosema ww nilikwambia kuwa kama kaunganisha vyama sawa ni kosa lakini alipojua kuwa kishafanya kosa si kataka kulirekebisha au vp? au tuseme nyie ss hv munaichukia CCM, kama CCM imeizamisha znz na seif sharif si alikuwa huko huko? basi na yy achukue fungu lake la lawama. isitoshe nakushangaeni munasema kuwa HR kafukuzwa na CUF na si Seif lakini munasahau kuwa Jumbe alilipeleka jambo hili la kuunganisha vyama tokea ngazi za matawi ya ASP, basi si Jumbe alounganisha ASP na TANU, semeni ni wanaASP wenyewe akiwemo huyo Seif Sharif.na isitoshe Jumbe kalazimishwa ajiuzulu na kamati za Chama ambacho kilikuwa kinamdhamini na nyerere ni too powerful katika vikao vile, ss ww unategemea nn?na wznz wenzake kina Seif wamekaa kimya na kujitia kwenye kwapa ya nyerere?
jengine ndugu yangu ukicomment kuwa specific uzijaze majina juu kama utungo wa chaza then ukatoa maneno ambayo hatujui unamjibu nani
jengine ni kuwa mm nilikwambia kuwa wakati nyerere anamtoa Jumbe znz atahakikisha kuwa anawaweka watu ambao anahisi si kitisho kwa CCM, muungano au ukoloni wa Tanganyika, ss ww mbona hujajibu hilo, kama kapeleka au hajapeleka yy ila lazima ukubali kuwa nyerere alimuona Seif si adui wa maslahi ya Tanganyika, yy na Mwinyi na ndo maana mmoja akawa Rais mwengine waziri kiongozi, au unafikiria nyerere mjinga sana amuondoe adui wa muungano awaweke maadui wengine wa muungano? haya hukujibu ukaingia mitini, na kama CUF wanapigania hayo si tatizo, lakini tunachosema ni kuwa Seif kwa hili alimsaliti mwenzake japo kwa kutokumtetea tu kule Dodoma.
na na nilisema kuwa ww madhali unaujua huo ukweli, basi si uwaambie watu hapa kwani unaogopa nn? useme huo ukweli tuuchambue na huo mtego wa panya munaohubiri, ss unaogopa nn kusema ukweli kama kuna mtu kamshutumu Seif kuwa kaupeleka mswada ule yy, basi na ww ulikuwa ukatae kwa kuweka hoja zako na si kutoa psychological threat za kuwa toeni nitoe, ww madhali unao utoe, mm nimetilia nguvu kwa kukuwekea hoja ambayo inaweza kussuport theory (wanaforensic wanuita circumstantial evidence) ya kuwa Seif kamsaliti Jumbe hio hapo juu, ijibu na ueke huo ushahidi wako tuuchambue usitoe empty threats
kila la kheri
na jengine ndugu yangu nafikiri mumekuwa munafikiriwa na kutiliwa mawazo, hivi kwani kumkosoa Seif ndo kuchukia umoja wa waznz? kwani yy hakosei? na kama kakosea pakisemwa isiwe kuwa unachukia umoja wa znz kwa kuwa umemkosoa Seif, acheni utumwa wa kifikra huo na ndo hayo mukaambiwa HR anatumiwa na kuuvuruga maridhiano kwa kuwa kamkosoa Seif basi na nyie mukarukia tu ila naahidi kuandika makala nzima kuhusu haya maridhiano Isha Allah na nione mwenye nguvu ya hoja aijibu
Mimi nimekuwa nikifuatilia sana maneno ya mzanzibari original kama ni mzanzibari kweli. Ninachona mimi huyu bwana haelewi historia ya kabla wala baada ya Karume (post karume Zanzibar). Anapokea madarasa ya itikadi yatlewayo na baadhi ya vyama vya siasa vinavyopambana na Maalim Seif.
Mimi nakushauri sana soma makala yangu haa ukumbini yenye kichwa cha habari “KUMBUKUMBU YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR 8″ ujifunze jap kwa ufupi yaliyojiri katika utawala wa Maalim Aboud Jumbe ili na wewe usherehekee vyema kama mimi miaka 48 ya mapinduzi.
Ahsante
@Said said
Wewe kama wataka msifu huyo Seif wako msifu mpaka umalize kurasa zote
sisi hapa hatumsifu mtu kwa jambo asilolifanya au hastahiki na wala sio
kama tunamchukia la hasha.
Sisi yeyote atakaefanya utumbo wake tutausema na sio wewe usiojuwa chochote
na yeye mwenyewe Seif ukimuuliza juu ya hilo na umshikishe msahafu basi katu
hatolificha hilo na atakuambia.
Sasa Said Said unaweza kuniambia Jumbe na wenziwe kina Ramadhani Haji
Faki wamefukuzwa kwa sababu gani maana mimi sijuwi chochote,naomba unipe
jawabu mtaalamu wa siasa na mkweli.
@Said Said
Sasa unataka tuandike mada za huyo Hamad Rashid zitatusaidia nini ktk
ukombozi wa Zanzibar?, kwani kama kufukuzwa chama keshafukuzwa na
yameshakwisha sasa wewe ndio kwanza wasema kama tunataka tulete
mada zetu za Huyo Hamad Rashid huo ni utoto habari hizo kwa hizo.
@Said Said
Nangoja jibu naona kimya basi nakuongeza jengine, kama ulivyosema kwenye
kipande chako kimoja hapo juu kwamba Jumbe hakuwa na nia njema na Z,bar
mpaka alipoona maji yamemfunika akaona anazama ni sadakta kabisa na
sisemi huyo Jumbe labda hakuharibu no,yeye pia ndie mmoja alieimaliza Z,bar
baada ya kuunganisha chama cha ASP na hiyo TANU na hilo ndilo lilikuwa kosa
kubwa la Aboud Jumbe ambalo katu hatolisahau.
Na Aboud Jumbe Alifanya hivyo baada ya kuahidiwa atapewa urais wa muungano
lakini wapi, na alipogutuka ndipo alipoanza kutaka kupapatuwa na yote hiyo ni
uroho wa viongozi wetu wapate madaraka.
Na huyo Seif Sharif nae vilevile alimzamisha Jumbe na bahshish yake akapewa
uwaziri kiongozi, kwani Nyerere hakuwa mjinga, na Seif ndipo na yeye akaona maji
ya shingo yashamfika baada ya kufukuzwa ndipo na yeye akaanza kutaka kupiga
mbizi ajikwamuwe na kuanza kudai serikali tatu na hii yote ni uroho wa madaraka
wa viongozi wetu na sio uchungu wa nchi yetu.
@Said said
Nakuomba usome hapa hapa kwenye mzalendo net mada isemayo
kumbukumbu ya mapinduzi ya Zanzibar 8.
@ Mzanzibari Orignal
Kwanza naomba sorry kidogo kwa kuchelewa kukujibu wewe na wenzako, chuo kilinibana tunakaribbia exams, okay nije kwenye hoja yako, hakuna siku hata moja ambayo sikumjibu hoja yake nikakimbia hilo ni uwongo usizue, ninavyojua mimi siku zote huwa najibu hoja na watu mwisho hubakia kimya hao kina Embesakua na wapinge hilo tuzitafute mada tuone nani anakimbia hoja, kuhusu Maalim seif na jumbe umeshindwa kuleta hoja ya kuthibitisha umeendelea na porojo, na nikwambie hizo ni hadithi za paukwa pakawa, ninavyojuwa mimi kama unampinga mtu kidhati haiji tena weye weye upiganie kilekile ulichompinga mwenzako hapo inaonesha hujampinga ni kumuunga mkono, Maalim hakufanya lolote huwo ni uzushi, na hilo la kufukuzwa abudu jumbe ndio chanzo cha mgogoro wa maalim seif na nyerere, wakati huo maalim seif alikua ni waziri wa elimu hakuwa na authority ya kufanya lolote ishu imefanywa na usalama wa taifa. na ikiwa hilo kosa limefanywa nataka ujibu yafuatayo
a) Nini lilikua azimio la Jumbe? b) Seif anapigania nini sasa? c) Jee unadhani nini kifanyike tuikoe zanzibar? d) Maalim Seif analolitetea ni sahihi ama si sahihi?
Halafu hoja ya kwamba Maalim kakubali matokeo ipo wazi mawakala walishindwa kupeleka uthibitisho ulitaka apinge kwa kutumi ushahidi gani???? na mantiki kuu ya kukubali matokeo ni kuubakisha umoja wa wazanzibari ambao vyenginevyo ingekua haupo kwa sasa.
@ Halikuniki
Tuseme hayo yapo sawa unayodai, sasa ni nini kifanyike mtu anapokosea aendeleze makosa au afanye juhudi kurekebisha makosa???/
Hizo history zina vary kila mtu anakuja na zake kwa jinsi alivyozipata, sikuambii uamini ninavyoamini mimi ila ujue tunachokitaka ni Zanzibar kwaiyo hadithi za nini kimefanywa nyuma zitabakia historia tu, tunataka impact ya mtu katika zanzibar ya sasa, hoja hii nimeshaijibu zaidi ya mara 5 kwa hawa kina Embesakua na wenzake, ila inaonekana badala ya hoja hii hawana jengine na nia yao ni kuwaonesha watu kwamba Seif mbaya ilhali ndie mtu pekee kwa sasa anayesimama kuitetea zanzibar yeye na chama chake.
@ Wazalendo
Tulete hoja za kuitetea Zanzibar, mapungufu ya viongozi hayasaidii kitu kwa sasa, kama watu wamekerwa na uamuzi wa kufukuzwa HR basi wamezee mte jamaa hana mpya na hana hoja na nia ya dhati kwa zanzibar mungu amsaidie.
Kila la kheri zanzibar,
umoja, mshikamano, uhuru.
Mimi nimekuwa nikifuatilia sana maneno ya mzanzibari original kama ni mzanzibari kweli. Ninachoona mimi huyu bwana haielewi historia ya kabla wala baada ya Karume (post karume Zanzibar). Anapokea madarasa ya itikadi yatolewayo na baadhi ya vyama vya siasa vinavyopambana na Maalim Seif.
Mimi nakushauri sana soma makala yangu hapa ukumbini yenye kichwa cha habari “KUMBUKUMBU YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR 8″ ujifunze japo kwa ufupi yaliyojiri katika utawala wa Maalim Aboud Jumbe ili na wewe usherehekee vyema kama mimi miaka 48 ya mapinduzi.
Ahsante
@ said-said
ndugu yangu pole na exams wala hakuna haja ya kuomba sorry kwa upande wangu mm, lakini umesema nimekuzulia, kwanza naomba kukuomba radhi ndugu yangu nilivofatilia makala za nyuma sie ww, ulokimbia kwa hio nisamehe sana ndugu yangu, nilichanganya majina kutokana na kufanana sana hoja zenu. nisamehe sana.
ss tuje kwenye hoja zako, kwanza nashangaa sana kuwa mwanafunzi wa chuo kikuu nampa ushahidi wa kiakili, then kwa kuwa hana la kujibu anasema ni porojo, nasikitika sana, mm sikutoa hadithi kabisa mm nilichosema ni kuwa baada ya Jumbe kuvuliwa madaraka znz na nyerere, basi nyerere atahakikisha kuwa anamuweka mtu ambae si hatari kwa maslahi ya Tanganyika, ndo kwa maana akawachangua Mwinyi na Seif, na nikasema kuwa Nyerere si mpumbavu kumuondoa adui wa muungano halafu amuweke adui mwengine wa muungano, kwa kuwa huwezi kuijibu hoja hio ww na wenzako, basi mumekuwa munaikimbia hoja hio, nataka muijibu. lakini eti umedai ugomvi wa nyerere na Seif ni Jumbe si kweli hata kidogo huku ni kuopotosha ukweli kwa makusudi, hivi unataka kunambia kuwa baada ya Seif kukosa urais ndo akajua kuwa nyerere mbaya? na kama ni hivyo, mbona hatumsikii kabisa kumtetea mzee Jumbe kama anavotetea maslahi yake, tushamsikia sana akimtukana nyerere, mbona hatujamsikia akimsifu kwa Jumbe kwa uamuzi wake? halafu eti unasema Seif hakuwa na nguvu kwa sababu alikuwa ni waziri wa elimu tu, kwanza naomba ujue kuwa kuwa kwake waziri elimu, maana yake yy ni member wa Baraza La Mapinduzi, ss kwa nn asimtetee rais wake? isitoshe jee alisema Dodoma kuwa nyerere unavyofanya sivyo? so hakusema hivyo kwa sababu alijua ndo ungekuwa mwisho wake kama Jumbe, lakini alichofanya ni kujitia kwenye kwaoa ya nyerere, akazawadiwa uwaziri kiongozi kwa kukaa kimya kwake, na huo ni usaliti tu, ss ninachosema ni kuwa hata kama leo sikatai yy ndo anotetea maslahi ya znz kuliko kiongozi mwengine yoyote, lakini pia tukubali kuwa aliwahi kuisaliti znz kipindi cha nyuma, na hapo ndo ninasema kuwa akikosea pasemwe na akifanya vizuri pasemwe pia.
nije kwa maswala yako sasa, tizama ninavyojibu masuala yako then nataka na ww ujibu hoja zangu kama hivyo na si kusema porojo ukiwa huna la kujibu (hoja yangu hio imewatia mitini wengi kabla yako)
(a) azma ya Jumbe ni kuirejeshea znz mamlaka yake baada kuhisi kuwa amefanya kosa katika kuunganisha vyama na kufanya kila liwezekanalo kuizamisha znz kwa kutegema Urais wa Muungano lakini alipotanabahi kuwa kakosea, akataka kusahihisha kosa lake. (wengine wanasema kwa maslahi yake binafsi: itakavyokuwa lakini kama lile lingefanikiwa sasa hivi tungekuwa na Serikali yetu huru irrespective ya motives zake za kufanya hivyo)
(b) swala hilo nikuulize ww mfuasi wake, na sio uniulize mie, lakini kama ilivyokuwa kwa Jumbe , yako mambo Seif nafikiri anawapigania waznz na yapo mengine anapigania maslahi yake binafsi, kwa hio sijui kama ni kweli anawapigania waznz au anajificha chini ya maslahi ya znz kuendeleza ajenda zake.
(c) tuungane waznz kwa sote kuhakikisha tunaikomboa nchi yetu, tuipende nchi yetu zaidi ya maslahi yetu binafsi na elimu ya kutosha itolewe kwa wananchi hasa vijijini kuwaambia hasa ni nn kinaendelea, tuondoe woga kabisa. tuhakikishe tunakuwa na serikali mbili tu, moja ya znz na moja ya Tanganyika, halafu kuweko na kikamati kidogo tu kitakachoshughulikia mambo ya muungano na sio serikali ya muungano kama wengi wenu munavyotaka maana kuirejesha serikali ya Tanganyika peke yake hakutasaidia sana. tutangaze kuwa mambo yote ambayo yameingizwa kuwa mambo ya muungano kinyume na katiba na kinyume na mkataba wa muungano kuwa ni void,.
(d) sina hakika na motive yake kwa hio siwezi kusema moja kwa moja kuwa sahihi au si sahihi, lakini kwangu mie kama nitahisi ktk jambo fulani anatetea maslahi ya znz au wananchi wake, mm nitakuwa pamoja nae, na sii yy tu hata kama atakuwa mwengine yoyote na ndo maana hapa namtetea Jumbe kwa suala hili kwa kuwa nahisi alikuwa anaelekea kuipa uhuru wake znz.
naomba ukijibu hoja uwe unajibu namna hio, ww ni mwanafunzi wa chuo kikuu bwana, kwa hio kuwa kama msomi tafadhali.
lakini tuje katika kukubali kwake matokeo, ss kama kakubali matokeo kwa sababu mawakala hawakukusanya matokeo, nakumbuka blueguard walikuwa wanapita mitaani kuwaambia watu kuwa wanaambiwa na Seif wende bwawani, ss kinachonishangaza mie, kwa vile Seif alikuwa anajua kuwa hata matokeo hawajakusanya kwa nn awaite watu pale kuraise issue za kijinga? huku si kutumia influence yake vibaya, yy hata ushahidi kuwa kashinda hana, ss kwa nn awaite watu bwawani? isitoshe mm najua kuwa kuna macommissioner wawili wa CUF ndani ya tume, na wako pale kuhakikisha chama chao hakiibiwi, na wao wana haki kuona karatasi za matokeo, na wao walikuwa wapi? isitoshe na kama hana ushahidi kuwa kashinda uchaguzi kama unavosema basi kutambua matokeo haikuwa kwa sababu ya umoja wa waznz, ilikuwa kwa sababu hana la kufanya, na angekataa matokeo angeulizwa atoe ushahidi, ambao hana. Na kama utaendelea kutetea uamuzi wake huo basi kwa vile tume ya Uchaguzi znz imemchinja tena kama ilivyomchinja miaka yote na mara hii kakubali matokeo kwa sababu ya umoja wa waznz, nashawishika kusema kuwa matatizo yote ya znz basi yalikuwa yanasababishwa na CUF kwa sababu ya kukataaa matokeo, kama umoja wa znz maana yake ukibiwa ukubali, basi 1995, 2000 na 2005 nawalaumu CUF kwa kuwanyima waznz umoja wao
naomba ujibu hoja kwa hoja
@ ahmed O. Khamis
nije kwako ss ndugu yangu, hio imekuwa kawaida ya waznz, ukiwaambia ukweli, hukurukia kuwa si mznz na hasa hasa ukimkosoa Seif basi kama hawakujui watakwambia kuwa ww si mznz na kama wanakujua watasema unatumiwa na watanganyika, tuache kasumba za kipuuzi, kama umeshindwa kujibu hoja sema sina la kusema, sina jibu kwa sasa au nakubaliana na ww na sio kumvua uznz mwenzako, yaani nyinyi munaweza kumjua mtu kuwa si mznz kwa hoja zake tu? heeeee, taire jamani. na hapo ndo muone kwa mtindo gani munafikiri (yyte asokubaliana na nyie au Seif basi huwa si mznz). na ndugu yangu hio makala yako nimeisoma mm na ahsante nimejifunza mengi ila sikutaka kuingia deep katika makala yako, lakini ukumbuke kuwa pia nimeisoma makala yako inosema Siri ya HR kuivuruga CUF yafichuka na nikakuuliza maswala yangu kule hujajibu hata moja umeingia mitini, leo unazuka na kunambia kuwa si mznz, na wala usipate tabu nakuekea link yake hapa na wazalendo wengine waone kuwa hukunijibu masuala yangu hata moja ( http://www.mzalendo.net/makala/siri-ya-hamad-rashid-kuivuruga-cuf-sasa-kufichuka ) lakini kwa faida ya wengine nitaeka comment zangu tena hapa watu wazione halafu uzijibu nione
ndugu mwandishi mm nimekuwa siku zote nakuheshimu kutokana na mawazo yako na kueleza kwako ukweli lakini sote sisi ni binaadam kama wengine wowote na sote tuna mapungufu yetu. nilipoona hii mada umeiandikia ww kwa kweli nilijishajihisha sana kuisoma kwa kufikiri kuwa kwa mara ya kwanza nitapata ukweli wa nn kinaendelea kwa sababu hakuna sababu ambayo imetolewa kumfukuza Hamad rashid ambayo mm japo si mpenzi wa CUF lakini nimeiona ya maana. naona zote ni sababu za kisiasa tu na kuexploit watu. mm mpaka ss hv namchukulia Hamad Rashid kama victim except atokee mtu na solid facts na kunishawishi kama ni mpotevu. nitaleza sababu ambazo zimetolewa na watu mbali mbali hapa chini.
(a) Anatumiwa na Pinda:wapo wanosema hivi akiwemo Jussa, wengine wanasema kuwa kapewa pesa, wengine wanasema kuwa kaahidiwa urais wa znz/umakamu wa rais wa Muungano. tusemeni ukweli kwa mwanasiasa mzoefu kama Hamad Rashid kuamini haya si rahisi, hizi ni propaganda tu. la kupewa pesa kwa ukweli hakuna anaeweza kujua hilo na kulithibitisha yote nafikiri ni propaganda za Seif na wenziwe tu. tukumbuke kuwa moja ya shitaka alosomewa Hamad Rashid ni kuwa kapiga picha na Pinda bungeni. hivi kwani alimtuma mpiga picha apige picha? na kwani pale yy si mbunge na pinda ni waziri mkuu? na isitoshe kwani hao viongozi wa CUF hawapigi picha na akina Pinda na Seif? au tuseme Seif alipokwenda kwenye sherehe za Uhuru hakupeana mkono na Pinda? au kama yupo mtu alopata kupiga picha wakati wanapeana mkono jee nalo ni kosa? nafikiri tungeacha mawazo kwamba kama kafanya Seif si kosa (ni uana siasa na ukomavu wa siasa) lakini kama kafanya mwengine ni kosa. jambo ambalo kwa kusoma makala zako mwandishi nimeona nawe umo katika mawazo hayo( with all due respect to you) nitathibitisha hili katika kipengele (b) baadae.
(b) eti hakupendelea maridhiano ya waznz: mm nimekuwa mgumu kuamini hili kwa sababu najua kuwa Hamad rashid kajitolea mara nyingi tu kwa maslahi ya znz. kwa mfano yy alifukuzwa na seif sharif CCM pamoja na katika mahojiano uloyaquote ya Star tv anasema kwamba baada ya kufukuzwa Seif alimuuliza utaenda kwa Nyerere akasema hapana sitoenda na ushahidi katoa wa watu walotaka kwenda kumuombea kwa nyerere lakini akakataa, hili nalo tusilisahau pia (give the devil his due : mnyonge mnyongeni haki yake mpeni). kufungwa kwake kwa kesi ya uhaini pia. lakini ndugu mwandishi kilonishangaza ni ww kusema kwamba alitegemea uwaziri kama sifa hasi kwake? kwani seif hakutegemea urais? au kosa yy kutegemea uwaziri lakini si kosa seif kutegemea urais? na hii ni propaganda ambayo inapigwa ili kuiexploit popular idea (maridhiano) kuwa ni silaha ya kumuaa Hamad rashid kisiasa, hivi kwani CCM si walisema kuwa CUF wanapinga mapinduzi ili kuifutia uhalali wa kuongoza ZNZ? kama CCM walivotumia propaganda za mapinduzi ndo hivo hivo leo CUF wanatumia maridhiano na maslahi ya waznz kumvuruga yyte anaempinga Seif Sharif. zamani ilikuwa ni kutumiwa na CCM amabyo mpaka ss inatumika lakini imepikuliwa na maridhiano kwa ss.
(c) anataka kuivuruga CUF kwa kutaka Seif ajiuzulu: mm nimeufatilia kwa kiasi huu mgogoro ila sijawahi kumsikia HR ananukuliwa hivyo. nilivyomsikia mm anasema kuwa yy katangaza kama Atagombania Ukatibu mkuu mwaka 2014. jee hilo ni kosa? kwani seif sharif aliposema kuwa tagombania urais znz mpaka chama kitakaposema basi halikuwa kosa? kama kutangaza nia ni kosa basi na seif nae ana kosa vile vile (sikiliza mahojiano ya Hamad rashid na DW ktk facebook wall ya Salma Said) na katika mahojiano hayo anakataa kabisa kuwa yy hakusema Seif ajiuzulu alichosema yy atagombania mwaka 2014. na isitoshe HR katika hayo mahojiano ya star TV anasema kuwa seif nae alisema atagombania na kumshinda, ss kama kosa wamefanya wote. na wengine wanasema yyana wivu na seif, ama kweli ss hv hamad ni mtu wa kujifundishia kutukana. kila mwenye lake haya
(d) hakuna alowafanyia watu wa Wawi: ama kweli akutukanae hakuchagulii tusi. hivi kutumikia miaka mitano ndo imekuwa hajafanya kitu, sikatai hajafanya kitu lakini kuna mbunge gani au mwakilishi gani znz anofanya ya maana jimboni kwake? hemu nipeni mfano wa huyo mbunge yyt pemba alofanya la maana PBA, yupi na lipi? kura za maoni alishindwa kwa sababu tu alikwisha chukiza CUF kwa sababu ya kitabu chake cha YALIOJIRI hakuna chengine na Seif kuingilia kati ni kwa maslahi ya CUF tu bara na si vyenginevyo. lakini once aliposema anataka utume wa ukatibu mkuu tu 2014, wee hapo kivumbi.
(e) anataka kuizamisha znz katika muungano (hoja ya mwandishi): ah ndugu yangu weee. unamshambulia eti kwa kuwa kasema umoja ni nguvu na watu wanakwenda freely znz na bara. angesema seif haya maneno wallahi ingekuwa si kosa. hivi kwanza nasikitika sana kwa mtu ninaemheshimu kama mwandisi kumquote Hamad out of context kwa makusudi kabisa. mm ilibidi niyasikilize tena haya mahojiano kuthibitisha alichosema mwandishi. tusemeni ukweli kwanza kusema muungano hauna faida hata moja si kweli, kwani CUF wanapinga muungano? CUF wanapinga mfumo wa Muungano, si Muungano wenyewe, kwa sababu wanajua kama sio kama hakuna faida kabisa. lakini hata kama hivyo ulivyomuonyesha ww kuwa anataka kupingana na seif wakati seif anataka kuikomboa znz, hv ndugu yangu umesahau kama umeandika katika makala yako ilopewa namba 8kuhusu mapinduzi kuwa Seif ndo alouchukua mswada wa serikali tatu wa Jumbe akaupeleka kwa Nyerere? eti maslahi ya znz yalikuwa kuwa na serikali zile zile mbili kwa kuwa wahafidhina walitaka kuendelea na maovu yao znz? kwa kweli sikutegemea kama ww utatoa hoja hii, lakini hili ndo lile lile akifanya Seif ni sawa tu, kwanza uliandika kuwa mzee Jumbe aliwaweka mbali wahafidhina na kuwaruhusu wasomi na hilo halikuwapendeza wahafidhina, halafu eti unataka tukuamini kuwa seif alifanya hayo kwa kuwa aliwakhofia wahafidhina znz? si ulishasema kuwa Jumbe alikuwa hawaivi na wahafidhina? tena ilikuwaje hao wahafidhina wawe wasiri wa Jumbe kuwe na serikali tatu? na eti jumbe alitaka serikali tatu kwa maslahi binafsi? sikuelewwi kabisa ndugu yangu Jumbe kutaka serikali 3 ubinafsi lakini seif kupeleka siri ya serikali ya znz kwa nyerere ni ushujaa na uzalendo? si kweli ni usaliti hata kama wapenzi wake watakataa. lakini jengine ni hivi kwani wahafidhina walikuwa na matatizo na mfumo ulokuwepo katika kufanya unyama wao? walifanya mbele ya nyerere na nyerere akitaka kumtia mtu adabu si alimleta znz (mfano bibi Titi Mohammed)? unyama wa wahafidhina znz haukutegemea kabisa muungano wakitaka walifanya tu. nikuonyeshe ulipomquote HR out of context, HR kasema
”umoja ni nguvu ….,lakini nadhani muungano unatakiwa KUTIZAMWA KATIKA PANDE ZAKE ZOTE MBILI kwa upana zaidi…..lakini tukizungumzia kama taasisi YAPO MAPUNGUFU, na lazima MAPUNGUFU hayo tuyakabili…….. nilimuuliza Waioba huoni kuwa haya MAPUNGUFU……. KWA MFANO (naomba nirejeshe tena hili, KWA MFANO) tume ya Fedha ya pamoja, mpaka leo formula yake haijapatikana….”
ss kuurukia mfano kama ndo hoja yake nzima ni kumuonea kwa makusudi. si haki kabisa ndugu yangu
lakini mm binafsi ningependa mtu anipe hoja ya maana ya HR kufukuzwa na si propaganda au politics tu. na yyte anaetaka kunipinga kama HR si victim naomba anipe majibu ya baadhi ya mabaya ambayo HR kayazusha kuhusu CUF.
(a) kwanza anasema kuwa kuna watu wanateuliwa bila kuidhinishwa na baraza kuu la Taifa la CUF kinyume na katiba inavosema, mfano ni Jussa alipoteuliwa kuwa mkuu wa Blue guard, au kuna kamati ambayo wajumbe wake wanatakiwa kuidhinishwa na baraza kuu lakini wajumbe wote wanakaimu nafasi zao, kwa hio wajumbe wa kamati nzima hawakuidhinishwa na Baraza kuu la Taifa.
(b) katika uchaguzi uliopita CUF mpaka leo hawajakusanya matokeo ya uchaguzi katika majimbo 5 ya Unguja, na hakuna aloulizwa. (maneno yangu: kuipoteza golden chance walokuwa nayo mwaka jana ni upuuzi)
(c) Seif hakwenda kabisa katika kampeni za bara mwaka 2010, kutilia nguvu
(d) fedha za mikoani katika ofisi za chama hazikupelekwa kwa muda mrefu sasa
naomba tuache kumsifu Seif hata kama kakosea, yy ni binadam kama wengine, naye ana tamaa kama wengine, mapungufu kama wengine, ubinafsi kama wengine, in short ni binaadam na kwa hivyo anaweza kukosea na akikosea wapenzi wake mukubali (japo mutanitukana).
na kama kweli mwandishi ulosema basi seif kawasaliti waznz na yy ni mmoja wa chanzo cha matatizo ya znz, tafadhali naomba unielimishe na usiniletee siasa, propaganda au yale Seif kafukuzwa lailatul Qadr (lol) na HR basi kafukuzwa lailatul Qadr ktk CCM vile vile. au yy ilikuwa lailatul Qadr ishapita (lol)
mm nimejaribu sana kufanya utafiti ni nani alopeleka siri ile baada kusoma ktk makala ya Joseph Mihangwa kuwa Seif ndo kapeleka ule mswada, lakini nilivofatilia kwa CUF wakabisha katu katu kuwa si yy, japo walishindwa kujibu masula yangu. lakini nilivofatilia zaid nikaja kugundua kuwa the main suspect si Seif ni mtu mwengine kabisa na alipoulizwa kama ni yy na mtu ninaemuamini, hakutoa jibu la maana kwa hivyo nikawachikulia waote wawili, lakini kama seif kweli kawasaliti znz kwa kisinizio eti haikuwa ni kwa maslahi ya znz si kweli, kama kawasaliti waznz basi kawasaliti tu na si vyenginevyo, tuache politics mapenzi ya halal badr, kama kweli kafanya hivyo basi ni wa kunyongwa kabisa, si mtu mzuri hata kidogo na yy pia ni maslahi yake tu anayazingatia na si mwengine (ila hii ni mada mbali pia), tusiwe kama wabara ambao hata kama baya kama kafanya nyerere basi huwa ni zuri, CUF wana ba seif wao nao hawasikii hawaoni hata kama ni baya litafinyangwa mpaka liwe zuri
naomba ndugu Ahmed O. Khamis unijibu usiingie tena mitini, na nataka pia kuelimishwa kuhusu hayo madai alotoa HR dhidi ya CUF
@Mzanzibar original
Endelea kuelimisha watakuelewa tu ila sidhani kama hoja hizi wataweza kuzijibu. na kusema ukweli idadi kubwa ya wazalendo wapo na mtazamo huo mbovu.
Huu mtandao umevamiwa na watu wa cuf na kujaribu kutuchafulia direction zetu na kuzileta zile za cuf ila tukiendelea na kuelimishana huenda kheri ikapatikana.
Endelea kuelimisha watakuelewa tu.
Hizo hoja hata Maalim Seif hawezi kuzijibu na ukimuuliza mara anajitia kulia upumbavu sasa sijui anamlilia nani huyo Seif.
@ Mzanzibari Orignal
Umeshindwa kuproove but see tour answer hili
a) azma ya Jumbe ni kuirejeshea znz mamlaka yake baada kuhisi kuwa amefanya kosa katika kuunganisha vyama na kufanya kila liwezekanalo kuizamisha znz kwa kutegema Urais wa Muungano lakini alipotanabahi kuwa kakosea, akataka kusahihisha kosa lake. (wengine wanasema kwa maslahi yake binafsi: itakavyokuwa lakini kama lile lingefanikiwa sasa hivi tungekuwa na Serikali yetu huru irrespective ya motives zake za kufanya hivyo)
Naomba nikufahamishe kwamba ikiwa Jumbe kakosea na alikua right baada ya kutaka kuitetea Zanzibar kwa mujibu wa maelezo yako Maalim Seif naye atakua yupo hivyohivyo kama Jumbe kwamba amekosea na kwa sasa anaendelea na harakati za ukombozi. Hii nakujibu kwa maelezo yako kuhusu vu=iongozi hawa wawili.
Then, kuhusu Hamad Rashid unajipotezea mda, hayo ni mawazo yako tu, nenda WAWI utamjua ni nani HR.
@ embesakuwa, sawa kwa hayo uliyo sema lakini suala langu liko pale pale yeye hamad rashid amemaanisha nini kusema nishakufa nishakufa ? je nimesema mimi au amesema yeye , na vile vile kuhusu usemi wako , mkere mwalimu ubaki na ujinga wako , nimeelewa lakini bora niwe mjinga kuliko nikawa na mwalimu juha kalulu , atoke somo kiswahili akarukie hisabu na ijapokuwa kaomba samahani huhisi huyo mwalimu kizungumkuti , la msingi jibu hoja usiruke ndani ya mada hakuna mkamilifu sdte tunamakosa sio ugomvi , suala liko wazi yeye hamad rashid amemaanisha nini kusema nishakufa. @ mzanzibar original hilo suala jumbe mimi nadhani nalijua udhuri dhaidi na ukweli hasa lakini yaliyo pita yamepita la muhimu wapi tunaelekea , sasa ikiwa seif hafai hebu nitajie nani anae faa manae simuoni hata mmoja tangu yatangazwe maoni ya katiba anae sema kitu ,nimekusudia viongozi lakini seif yeye peke yake awatete wazanzibar hilo ndio suala, hakuna alie mkamilifu ila allah na yeye seif ni binaadamu kama wewe na mimi amefanya makosa ndio ubinaadamu , lakini hebu kaa kwa utulivu wakuu wa kanisa wawe wamekasirishwa sana kwa kufukuzwa hamadi rashid mwisho wanataka hata chama kifutwe ? kwa mtizamo wangu mie hapa pana udini na chuki tu basi na ni sawa sawa kama alivyo sema seif kuwa ndani ya cuf hakuna ugomvi bali choko choko tu , nadhani unajuwa nini maana ya choko choko hizo ndizo zinazo fanyika.
@ said said
umeshindwa kujibu hata hoja moja, ww na wenzako, ukarukia kuniquote, hilo ndo mm nilokuwa nasema kila siku na ninalolipigania, kwamba Seif nae ni binaadam kama wengine, kukosea anakosea kama wengine na ana weakness zake, ss musimfanye kama hakosei na ndo hapo nikasema kuwa hata na yy akisema jambo basi munapswa kufikiri na sio kurukia tu kuwa anayosema yy au anofanya yy ndo sahihi kila siku. na mm nimesema mara nyingi kuwa nikihisi Seif anatetea waznz mm nitaungana na yy, awe yy, awe CCM, awe mwengine yyte madhali anatetea masalhi ya waznz basi nitaungana nae lakini hilo halimaanishi kuwa kwa sababu katika sehemu moja yuko sahihi maana yake yupo sahihi ktk kila jambo. kuhusu HR mm nimeweka madai ya HR dhidi ya CUF mbona hujayajibu? ndo hapo nasema kama Seif, HR, mm, ww na mwengine yyte tuna weakness zetu kila mmoja, kwa hio hata kama HR hapendwi wawi kutokana na mambo yake, haina maana kuwa kila analosema ni uongo au si sahihi, na ndo hapo nikaweka madai yake munisaidie kunipa majibu hakuna hata alojaribu mpaka sasa. na hapo ndo nikasema kuwa hata suala la HR, kwa vile Seif na HR wote wana weakness zao, basi tuchunguzeni kwa makini madai ya wote wawili na sio kurukia kuwa madhali hapendwi Wawi basi anoyasema yote ni uongo na anayosema Seif ni kweli tupu. kwani Seif jamani haiwezekani kusema uongo? therefore ndugu yangu nasema tena na nakubaliana na ww kabisa kuwa kama Jumbe alivyokuwa wrong akataka kusahihisha kosa lake kama na maalim nae anataka kufanya hivyo fine ndo uungwana na ubinaadam lakini haina maana kuwa ndo hakosei tena, naomba unijibu hoja zangu, kama huna majibu sema usiziignore, then ukajitia mitini, jibu hoja tafadhali.
@ aslam
nafikiri kuna mtu hapa mzalendo aliijibu vizuri hio hoja na naomba kuchukua maelezo yake kuwa inawezekana kabisa kuwa HR alikuwa hatumiwi na Bara au kanisa, lakini baada ya kutoswa na hao watu wakamnyooshea mkono basi yy either kwa kujua au kutokujua akakubaliana na msaada wao,akatoa mfano wa Hamas na mm naongezea Muslim Brotherhood pia,( baada kutengwa na masunni wenzao, wakaambatana na mashia, si kwa kuwa wanatumiwa na wao lakini ni kwa kuwa hao ndo pekee walotoa msaada kwao walipotengwa na masunni wenzao) isitoshe hakuna kanisa lilosema hivyo ninanvyojua mm, nakumbuka alosema hivyo ni mwanasheria mkuu, Jaji Werema, baada kusema kuwa kama kweli CUF wamedharau amri ya mahakama, wapo wengi walompinga na mm nakubaliana na wale ambao wamempinga kwa hoja za kisheria na si porojo tu. lakini ss hivi chochote kinokachomtia doa HR mutakitumia then museme munaona? naomba ww ndugu yangu ukae kitako uchambue kila liloendelea na si kutafuta cheap explanations. na kuhusu ukamilifu yes nakubaliana na ww hakuna mkamilifu na ndo nikasema hapo juu kuwa hili la HR na Seif pia tuchunguzeni kwa makini na sio kurukia tu maana hakuna mkamilifu
@ aslam
na anza kwa kutafuta right informations kwanza maana naona kwanza uko misinformed then unatoa decision kwa kutumia hizo misinformations ulizonazo, hapo utapotea tu na itakuwa miujiza kuanza na wrong facts ukamalizia na right decision, kuna mchungaji mmoja tu ndo alisema kuwa walofanya CUF si sahihi, sijamsikia mwengine, kwa hio ndugu yangu juu ya umahiri wako wa kiswahili, lakini tafuta facts kabla kumuhukumu mtu
@ Mzanzibari Orignal
Hemu soma haya maelezo yamewekwa kwenye nakala ya KUMBUKUMBU YA MAPINDUZI 8
((((Mwisho wa utawala wa Jumbe ukawadia. Jumbe alianza kupigwa vita na waasisi katika baraza la mapinduzi kwa kutuhumiwa kuwapendelea washirazi na kuwapuuza wazanzibari wenye asili ya bara. Hivyo basi wanamapinduzi wakahoji inakuweje mamlaka yote ya Zanzibar kuwa chini ya washirazi wakati wapiganaji wa mapinduzi wote walikuwa ni wazanzibari wa asili ya bara. Hata hivyo kilichotia mwisho utawala wa Jumbe hasa ni vile alivykula njama za kutaka kubadili Mfumo wa muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kudai uhuru zaidi kwa Zanzibar kwa shinikizo la wanamapinduzi. Jumbe na wanamapinduzi walikubaliana kuirejeshea Zanzibar uhuru wake kamili wa kimaamuzi kwa kudai serikali tatu katika muungano. Kuthibitisha kwamba alikuwa akiudai uhuru huo kwa maslahi binafsi Jumbe hakutaka kulijadili suala hili na wajumbe wote wa baraza la mapinduzi badala yake alianza pirika za chini kwa chini na usiri mkubwa. Lengo la Jumbe ni kurejesha nguvu za Zanzibar kwa baraza la mapinduzi na waasisi ambao wote au wengi wao ni watu ambao hawakupenda mabadiliko ndani ya Zanzibar. Hivyo basi Jumbe aliandaa kesi kwa kutafuta mwanasheria nje ya nchi na kuandaa documents maalum ilikuishitaki serikali ya Jamhuri ya muungano kuwa imekiuka makubaliano ya muungano. Kwa mujibu wa tafsiri ya makubaliano ya muungano katika kesi ya Jumbe, muundo wa serikali ya muungano ulipaswa kuwa na serikali 3. Hivyo basi Jumbe na sio CUF ndio alikuwa mtu wa mwanzo kudai serikali 3. Baada ya kundi la damu mpya ndani ya baraza la mapinduzi kubaini lengo la Jumbe kudai serikali tatu waliungana pamoja kuupinga mpango huo wakiongozwa na Seif Sharif. Suala la serikali 3 kwa wakati huo lilikuwa na madhara makubwa zaidi kwa mustakbali wa Zanzibar kuiko manufaa.
Lengo la wanamainduzi ni kuirudisha Zanzibar katika himaya ya “Karume wadogo” (wanamainduzi) na kuitoa katika mikono ya Nyerere. Hii ni kwa kuwa Nyerere aliwapa fursa wapemba na viongozi vijana kuingia serikalini. Wanamapinduzi hawakulipenda hilo kwani ilikuwa ni kinyume na misingi yao na historia ya mapinduzi, yaani mpemba na mwarabu kuwa kingozi wa serikali ya mapinduzi . Hivyo walidhamiria kuleta serikali 3 ili Zanzibar ijirejeshee mamlaka yake ya kisiasa kama ilivyokuwa wakati wa ASP kabla ya kuja kwa CCM ambapo mamlaka ya siasa Zanzibar yalindoka Kisiwandui kwa Jumbe na kwenda Dodoma kwa Nyerere.
Seif Sharif na wenzake walifahamu kwamba kuunga mkono mpango wa Jumbe ni kuirudisha Zanzibar katika utawala wa Karume wa “Sheria mkononi” kubaguliwa kwa wapemba, kuonewa kwa watu wenye asili ya kiarabu na kikomoro, kuondoshwa madarakani damu mpya, yaani viongozi wote vijana ambao ni chachu ya mabadiliko na wapambanaji dhidi ya unyama kwa raia na hivyo bila shaka ni kuirudisha nyuma Zanzibar kama ilivyokuwa baada ya mapinduzi. Baada ya Jumbe kukamilisha maandalizi ya mpango wake wa siri wa kuing’oa Zanzibar katika mamlaka ya Jamhuri ya muungano, Seif Sharif akishirikiana na wenzake walikula njama kuukabili mango huo na kuusambaratisha. Walifanikisha kwa kuiba dcuments za Jumbe za mpango wake huo na kuzikabidhi kwa siri kwa Nyerere. Mara tu Nyerere akaitisha Kamati kuu ya Chama cha Mapinduzi na agenda ya “machafuko ya hali ya hewa Zanzibar”. Kupitia kikao hicho, Jumbe akashambuliwa mno na kuitwa msaliti. Baada ya kika kujadili kadhia hiyo na Jumbe kupewa nafasi ya kujitetea ambap alisisitiza msimam wake huohuo alitakiwa kujiuzulu na akajiuzulu. Baada ya hapo Seif Sharif akawa kipenzi cha Nyerere.))))
Nia ya maalim seif na wenzake ilikua safi kwa Zanzibar na hakuwa na makosa yeyote kwakua hata Jumbe angefanikiwa angeturudisha kulekule kwenye balaa,
Kuhusu HR hoja takriban zote nimeshazijibu katika makala zilizopita kumjibu Embesakua, nikitulia inshaallah nitakujibu kwakua tena vuta subra kwa leo ila HR mambo yake yako bayana kaka hayataki tochi, kujibizana kuhusu huyu HR ni kupoteza muda tu.
@ Mzanzibari Orignal
Juzi nilikujibu kupitia maelezo yako mwenyewe wala sikukuquote kama unavyosema, ila katika Zanzibar Maalim Seif ana nafasi ya kipekee ndani na nje y serikali kwakua daima amebaki na nia njema na Zanzibar, muadilifu, mchapakazi na mengine mengi kama aliyoyataja mwandishi juu, makosa binaadam wote wanafanya kwaiyo hata na yeye kukosea ni wajibu, ila kuhusu suala hilo unalozungumzia hakufanya makosa, na kuhusu HR uamuzi wa chama upo sahihi Hamad Rashid kavuna alichokipanda.
@ embesakua
mm nafikiri nimeijibu hoja hio katika comment yangu, na nikasema wazi kuwa kwanza ndani ya makala hio uloiquote kuna mkanganyiko wa kimawazo, kwanza munasema Jumbe aliwaweka mbali wahafidhina, halfu eti munataka niamini kuwa Jumbe alikuwa msiri wa wahafidhina? huku si kujikanganya? isitoshe ninasema tena kuwa wanamapinduzi walikuwa hawataki kuwe na mamlaka yao huru ili kufanya unyama wao, kwani hayo walofanya walifanya nje ya Muungano? si waliiyafanya ndani ya Muungano? na eti unataka kunambia kuwa Nyerere alikuwa ni kikwazo kwao? si kweli kwa sababu hayo waliyafanya mbele ya Nyerere bila karipio lolote kutoka kwa nyerere, na hata nyerere mwenyewe kama alitaka kumtia mtu adabu si alimleta znz? mfano nikatoa Bibi Titi Muhamed? hio hoja haina mashiko kuwa Jumbe alitaka hayo kwa sababu ya wahafidhina walitaka kufanya unyama, lakini wacha nikuonyeshe kasoro nyengine ndani ya hio makala, ushahidi anaoutoa kuwa Jumbe hakuwa na nia njema ni kwa kuufanya mpango ule siri, ww unategemea Jumbe angeenda wazi wazi kusema kuwa nataka kuuvunja muungano wakati anajua power za nyerere wakati ule? na ndo maana akataka kutumia nguvu za kisheria kujivua kwa sababu kwa mabavu, asingemuweza nyerere, na lazima jambo lile liwe la siri kwa sababu ingekuwa dhahiri lisingefanikiwa hata kidogo, na mfano ni hapo lilipovuja, athari zake si umeziona, wala usinambie kuwa nyerere aliwapenda waznz saaaaaana, mkoma yule. kwa hio ule mkataba hata mm ningekuwa Jumbe kwa mazingira yale ningeufanya siri, kuwa mkataba umefanywa siri haina maana kuwa Jumbe alikuwa anafanya yale kwa maslahi yake binafsi. kwanza hizo hoja za usiri na ubinafsi hapo hazina mafungamano yoyote. so hizi hoja Ame hakuzijibu na ww naona umeamua kuzunguka in circles tu, naomba ujibu hoja isitoshe kama umemjibu embesakua ulikuwa unambie tu vichwa vya habari vya hizo makala zako mie ningezitafuta, still nitajie majina ya hizo makala zako nizione.
don’t go in circles, kwanza umenambia nimeshindwa kuprove kuwa Seif kapeleka mswada ule then unaniwekea mada inothibitisha kuwa Seif kapeleka, ww unachofanya ss ni kutetea tu itavokuwa baada kunambia nimeshindwa kuprove na kushindwa kujibu hoja zangu now unarukia nia safi alokuwa nayo alipofanya hivyo? jibu hoja don go in circles
@said said
kuhusu HR nasema tena hemu jibuni hoja zake hizo, na sio habari za kuvuna alichokipanda, jibu hoja na si kufuata propaganda za wanasiasa tu, ss kumkosoa Seif adhabu yake kufukuzwa? kama si hivyo basi hemu jibu hizo hoja zake, kwani kuna uzito gani kujibu?
@Mzanzibar Original
@Embesakua
Siamini kuwa yupo anayeweza kuwa na majibu ya hoja zilizowekwa na @Mzanzibar Original.
Majibu yanayotolewa juu ya hoja zako ni ya dhana na hisia tu bila ya kuwa na ushahidi.
Ni vyema pia mkaelewa ni watu wa aina gani mnaojadiliana nao katika ukumbi huu,hilo pia lizswakatishe tamaa na kuwavunja moyo katika kutoa maoni yenu.
Endeleeni kuwaelimisha,na naamini kuwa wapo watakaoelimika,maana wao hawakutawaliwa na kasumba.
Watu wajadili kuhusu Zanzibar maswala ya vyama na HR yashapitwa na wakati, hoja zote za huyo HR binafsi nishazijibu zaidi ya mara 3 na huyo Embesakua nishamjibu mara nyingi ndio maana sioni haja tena ya kuendelea na Hoja hizo, watu wa Wawi ndio wanaopaswa zaid kumtetea HR lakini kinyume chake hatakiwi kaoza ananuka, jifurahisheni tu kwa kusifiana mnaelimisha kwa hapo hamna mnachoelimisha zaidi ya kupoteza mda kumjadili mtu ambae hana mana, nashkuru sasa ivi mada zake zimesita inaonekana amekwishaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaah mana naskia na yeye mwenyewe huingia humu akajitetea.
@ Wazanzibari
Kwa sasa tuweke pembeni siasa tujadili vipi tutaikomboa Nchi yetu na umoja uwe ngao yetu inshaallah Mungu atatuonesha njia.