Makala/Tahariri

Zanzibar ccm imebaki jina.

Naomba mniazime masikio yenu leo kidogo nimekuja kwa heshima tupu zilizojaa taadhima kuwafahamisha ndugu zangu wana ccm visiwani unguja na Pemba pamoja na vile visiwa vidogo vidogo vyengine vyote vinavyounda Zanzibar kwa pamoja kuwa kama desturi ya kiumbe kuonja mauti ni wajibu hata uwe muungwana vipi au jahili wa kupigiwa mfano hakuna njia wala uwezo wa kukwepa kuufunga ukurasa wa pumzi ulizoazimwa na mola kwa muda uliopangiwa siku ikifika,sisemi haya kwa kiburi wala kejeli bali huu ni ukweli ulio wazi kwa sasa visiwani kwetu kwa sababu kwa makusudi tumejiingiza kwenye mtego uliotayarishwa na Tanganyika kwenye hii katiba pendekezwa bila woga wala uzalendo kwa visiwa hivi tumelazimishwa kutii utaifa au uzalendo wa Tanzania kwanza kwa gharama ya kuitokomeza Zanzibar.

Umasikini sio wimbo wala kabila hapa kwetu hii ni dhiki inayomfanya mwanadamu wakati mwingine atamani mauti ili hali bado mzima wa akili lakini afya huwa imesha ondoka kwa kuwa bila lishe yenye virutubisho vyote vinayotakiwa mwilini mwili huwa kama gamba la muhogo peke yake lililokosa muhogo ndani huwa linaning’inia tu,halijaufaa kwa kuusitiri muhogo pia nalo peke yake halipikiki kumsitiri mnunuzi au mkulima mwenyewe,akili kwa kukosa virutubisho hivyo {vitamins,proteins etc}kufanya kazi kwa ufanisi sio jambo la kutarajiwa,sasa linalo niumiza kichwa mimi kwa nini viongozi wa ccm hapa kwetu wamefikia kufanya maamuzi ya kukimaliza chama cha ccm kwa makusudi huku wakiwa hawana njaa kwa sababu shibe waliyo nayo haiwazuwii kufikiri kwa kina na kitaalamu kuyajua haya waliyoyatenda kwa kuikanidhi nchi ya Zanzibar kwa Tanganyika kwa kisingizio cha muungano bila kura ya maoni kuwauliza wananchi kama wanataka muungano upi sio katiba ipi au serikali ngapi huko ni kuzungushana tu.

inawezekana pia unapo shiba bila kujua dhiki au umasikini wa walio kuzunguka akili ya mwanadamu huwa inaona miujiza mitupu wakati mwingine wasi wasi wangu waheshimiwa wetu wa ccm hapa Zanzibar wanaona miujiza kwa karibu miaka zaidi ya hamsini sasa bado hawaoni wala hawajui kula mlo mmoja tena haujatimia umekaa vipi,juzi nimeongea na mdogo wangu kwa kuwa bado sijarudi nyumbani baada ya matibabu bado nipo india kwa masikitiko makubwa na uchungu mtupu huku machozi yakinitoka alinijulisha kuwa siku hiyo alipata chakula cha jioni na haikuwa chakula bali alikunywa chakula cha jioni kwa kuwa alipata uji mtupu wa kunde hakuwa na senti ya kuweza kutayarisha mlo mwingine wa aina yoyote pia hana ajira miaka zaidi ya mitano sasa,mimi kama desturi yangu sikukosa kumtania kwa kumwambia asisikitike sana inshaalh baada ya Zanzibar kuwa mkoa tutaweza kupata na mahindi kwa wingi achanganyanye na huo mseto wake kwa ajili ya kupata makande kabisa tukaangua kicheko.

Ndugu zanguni wazanzibari bila kujali tuko chama gani kwa sasa hatuna budi kumgeukia sultani mpya wa Tanganyika kwa sauti moja tukakataa ushirika nae ambao hauna tija kwetu wala hautokuwa na tija Abadan ikiwa tunao watuma kwenda kutuwakilisha kwenye mapatanao hayo ni hawa wajumbe wa baraza la wawakilishi na wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano pamoja na wale wote ambao bado wanaota kuwa udugu wetu ndio silaha yetu hapana udugu wetu ndio mauti yetu kwa miaka mingi hili tunalijua lakini hatukuwa na sauti ya kukataa mifumo tuliyotoka nayo huko nyuma haikuturuhusu kukataa amri za wakubwa bila kujitakia maafa,bado mashujaa wengi wa visiwa hivi walithubutu kuhoji na kutafuta uwiano unaofaa kwa sote lakini wengi walifukuzwa makazini na wengine kutafutiwa kesi la kushangaza itakuwaje nchi iliyo huru inawadhibiti wananchi wake na kuwapa adhabu za kila aina wanapo dai haki na nchi yao ikiwa huku si kutawaliwa ni nini? sasa ikiwa jawabu ni ndio sasa kwa nini tunageuzwa sote taahira kwa kutakiwa tuamini sisi ni watu huru na tuna kula matunda ya usawa,amani na haki kama watu wengine wowote wale ulimwenguni?

CCM kwa maoni yangu kwa sasa tumeshika saa mkononi{stop watch} hatuna ubani wala kisomo cha kutunusu na mauti yetu katika visiwa hivi kwa sababu tutakavyofanya kuendelea kutawala au kuongoza nchi hii hatuna budi kutumia nguvu kuanzia alfajiri mpaka magharibi na kukicha itabidi tuongeze nguvu za dola katika kuwadhibiti wananchi wakubaliane na muungano,katiba mpya na kila tunachotaka tukipitishe kwa nguvu za polisi,tume,mahakama,rais,bunge au baraza na kila chombo tunachomiliki kitakuwa ni silaha ya kuwaburuza wananchi kwenye maslahi ya chama cha mapinduzi{fil duniya wal alkhera} sasa hili linawezekana katika karne hii tunayo kwenda nayo? na kama haliwezekani kwa nini tunajiumiza vichwa kulazimisha tusiyoyaweza? ukweli usio pingika kwa sasa huwezi kuwageuza watu kuwa ng’ombe ukawafuga au ukawafanya unavyotaka hata ikiwa una uwezo wa serekali tatu na nguvu zake zote za dola {china, usa, Russia}ikiwa wenye nchi hawataki utatesa, utauwa, utafunga lakini utaondoka na utashindwa.

Ni jambo la kawaida siku zote baadhi yetu kukata tamaa na kudhani msumeno ni ule ule siku zote wananchi watakuwa magogo na serekali kuwa chuma atakae umia hujulikana mapema ndio maana bado siya kustaajabu kusikia kuwa wenye dola kujinadi kwa kifua kipana kuwa bado sherehe iko kwao,sisi sio wengi wepesi kufuatilia siasa kwa kufuata mchezo wa chess wengi hukurupuka kujibu mapigo baada ya mpinzani kumaliza kuzukuma kete yake unapofanya tathmini kwenye siasa hata maisha ya kawaida huwa umesha feli au utashindwa siku zote unachotakiwa kufanya ni lazima uwe mwenye kubuni au kulicheza bao lote la mpinzani wako kabla haja sukuma wala kugusa kete atakapo kimbilia uwe umesha fika ili uwe tayari kumkabili kwa kumdhibiti hata ukijifunza mbinu za kijeshi mfumo ni huo huo,hutakiwi usubiri ushambuliwe kwanza tena ndio ukurupuke kujibu mapigo ndio maana wenzetu hupiganisha vita mezani kwanza (star wars} kabla hawaja mchokoza mtu ili siku ikifika wamesha vipigana hivyo vita siku nyingi kabla,matatizo ya ccm bado tunapigana vita ovyo hatujakaa mezani kukabili upinzani tunatarajia miujiza siku zote na nguvu bila hekima ndio maana tumejiweka katiaka nafasi nzito kisiasa katika nchi hii kwa sasa na si rahisi kujinasua bila kushindwa.

mimi mzanzibari kwanza ccm baadae kwa hapa tulipo fika hakuna sera wala kanuni ya chama hiki itakyo ingia akilini mwangu bila kupingwa labda kwanza iwe na marekebisho kuhusu uhalali wa Zanzibar kama mshirika sawa na Tanganyika sio vinginevyo kwa sababu hapa ndipo walipo wenye visiwa hivi na ni hiari yao hakuna wa kuwalazimisha kukubali
ccm au cuf wanataka nini hivyo ni vyama vya siasa na sisi ni wananchi wenye mali hapa kwetu imegeuzwa mwenye mali amegeuzwa CCM na wananchi wamegeuzwa kuwa kama wapangaji tu katika ardhi hii.

nchi hii nzima ya Tanzania mpaka leo miaka hamsini na kitu zaidi ya nusu ya miaka hiyo ccm ndio mpangaji mkuu wa maendeleo ya taifa hili la kushangaza yale mahitaji muhimu kwa binaadamu ndio adimu Tanzania nzima miaka yote hii,
maji safi,matibabu{afya} pamoja na ajira hakuna kwa vijana wala wazee pia umeme bado tuko nyuma katika sekta hii katika ukanda wa nchi za afrika sasa kwa nini bado imani na cm iwe ya kiwango cha juu hatuhitaji katiba pendekezwa peke yake kuikataa ccm haya ni muhimu pia ikiwa tunataka maendeleo ya kweli sio ya majukwaa ya siasa.ule wakati wa lazima ukisifu chama cha ccm ikiwa wewe ni mwanachama wetu halalihata kama haya yote niliyoanika unayajua umekwisha pitwa na wakati na haurudi tena wananchama wetu wapya na wa zamani ni lazima tuweke uzalendo mbele kwa kuwa mifano ya walio weka chama usoni tunayo ni wale wote walio isaliti Zanzibar Dodoma vipindi tofauti.

Mtanisamehe kama nimewakosea kina mpetehalisi etc pia nawasilimu sana shakush sahib yangu na alhabib pamoja na mmatemwe nashukuru kwa dua zenu na mimi natoa zangu kwa shakush kwa kuuguza,pia siku zote mimi ni mtoa maoni tu leo nimejaribu kuandika kidogo kwa maana hiyo makosa yatakuwa mengi naomba mnifumbie jicho nipite bila kuniona katika upungufu huo lakini pia ikibidi basi nirekebisheni kwa ustaarabu mtupu kwani uungwana wetu usiwe kama mishono inakuja na kuondoka.

asanteni

mzeekondo,India.

Share: