Zanzibar ni haki yetu ya asili na sio jimbo linalotaka kujit
Written by Hassan10 // 04/09/2010 // Makala/Tahariri // 4 Comments
Taifa la watu wa Zanzibar na kuona viongozi wao wa smz wako weak. Mungu ibariki Zanzibar na watu wake wote.
Nilazima ndugu zetu waweze kutufahamu kuwa Zanzibar ni nchi tokea enzi na ina watu wake wazanzibar na utamatuni wake wa asili. Hakuna Mzanzibar hata mmoja alakuwa tayari kupoteza utaifa wake,utamaduni wake na asili yake kwa sababu tu ya Muungano.
Hofu na wasi wasi miongani mwa Wazanzibari nikuhishi mfumo wa Muungano ni kupoteza utaifa wa Ki-Zanzibar na Nchi kuwa mkoa. Kuna dalili na mambo mengi yanayo wafanya Wazanzibar kuona kuwa Zanzibar Muungano hau it-(Treat) Zanzibar kama ni Nchi ilio ungana na Tanganyika, inaonekana na wenzetu kuwa Zanzibar ni sehemu ya Tanganyika na ni mkoa mdogo wa Pwani.
Na mifano hii ipo mingi hata viongozi wahusika wamesha sikilikana mara nyingi katika meadia wakitamka kauli za zarau na kuigebehi Zanzibar na wazanzchi wake. hali hii ndio chachu cha kuleta kero za Muungano na Wazanzibar kuhisi Muungano ni mzigo na ujanja wa kulifu







4 Comments on "Zanzibar ni haki yetu ya asili na sio jimbo linalotaka kujit"
maskini zanzibar ni nini kilicho kufika hata ukawa hivyo ulivyo ulikuwa una kila kitu cha kujivunia na kuheshimiwa leo jirani kajifanya mjanja eti anakuonea huruma na wewe kwa upole wako ukamuamini mumiani ukamuachia kila kitu chako chakwako leo ndio anajifanya chake leo inafikia unamuomba kitu chako mwenyewe ulompa kwa ridhaa yako anakwambia huna haki ya kitu chako chako wewe zanzibar ni chake yeye chake yeye ni chake pekeyake masikini zanzibar hali hiyo itakuwa hadi lini watoto wako leo hawana haki katika nyumba yako ambao ndio watoto wako wa kukurith leo wanaambiwa hawana haki na watoto wa nyumba ya pili ndio wenye haki ambao wewe mwenyewe hukuwazaa wala huwajui maskini zanzibar ni visiwa viwili vikiwa nje ya bara la africa yote yamekufika kwajili ya jirani yako alie na husda mungu atakusaidia zanzibar urudi hali yako kama zamani ameen ndio mtihani umeshamjua nani adui yako hutorejea tena makosa yako mungu wabariki watoto yatima wa zanzibar mungu ibariki maskini zanzibar
DAH hizi history zilikuwa wapi ? kati kutusomesha vita vya manyema na majimaji,tumechoshwa na uwongo wa chama tawala,siko tayari kumpeleka mtoto wangu shule za serikali kwani wanachosoma ni uwongo mtupu.
Kwanza natoa shukurani kwa kutuletea history hii,na ningeomba wazalendo wakusanye history za ukweli wazichapishe na viuzwe au vitolewe bure,najua ni gharama,lakini ikiwa tutafanya hivyo tutaamshana na kuelezana ule ukweli halisi,na kufichua maovu,mi siko tayari kuuza utaifa wangu kabisa.
zanzibar ilikuwa ina hadhi yale wakati ilipokuwa iko chini ya utawala wa ki SULTAN ukitamazama picha utajua hayo
Rafiki yangu Al Kiyumi sasa kama Zanzibar ilikuwa hivyo hao Warabu waliondoka na Utaifa wa Zanzibar na kuiwacha Zanzibar mikononi mwa Mwalimu Nyerere. Mimi ninahisi Ukweli utabaki kuwa ukweli Zanzibar ilikuwa nchi kamili hata historia inaonyesha kuwa Afrika Mashariki ilikuwa na nchi nne ambzo zilisomeka kuwa ni Tanganyika, Kenya, Uganda na Zanzibar. Hivyo kila nchi ilishiriki kwenye umoja huo kwa hadhi ya nchi na utaifa wake kamili, wakati huo Zanzibar ilikuwa na hadhi sawa kama ilivyokuwa kwa Uganda, Kenya na Tanganyika. Cha kujiuliza wanaoikataa Tanganyika kuwa si nchi kwa sasa kwa madai kuwa imepoteza utaifa wake wanamaana gani kufanya sherehe za 9 December Tanganyika ipo bali wameilazimisha kuiita Tanzania lakini si kweli Tanganyika sio Tanzania hebu fikiria watu wanasherehekea sherehe tatu ndani ya taifa moja kweli? kuna 12 January Mapinduzi ya Zanzibar, 9 December Uhuru wa Tanganyika na 26 April Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa hali hii ni wazi kuwa kuna serekali tatu tofauti. Tukae tena tuufikirie Muungano wetu, hapa sipo kisiasa bali nipo kiutaifa zaidi tuyarejeshe mataifa hayo tuondoshe kuoneana na kunyanyasana kisaikolojia. Hongera Mheshimiwa Rais wa Serikali ya Jamuhuri ya Zanzibar kwa kutusainia sheria itakayofufua utaifa wetu uliopotea, M/mungu akulipe kila lenye kheri na wewe, akutakabalie swaumu zako, akupe akili na maarifa zaidi kwa kushirikiana na viongozi wenzako na kila anayeipenda Zanzibar juu ya kuikomboa Zanzibar yetu. Bado tunaweza na tunayo nafasi