Login



Fotos

Get the Flash Player to see the slideshow.

Migawanyo

Kumbukumbu

Sauti:Harambee:Mchango wa wazanzibar walio nje (Wazanje)

Update:

Tumepokea ujumbe kutoka kwa Mwenyekit wa MUWAZA kutakuwa na sala na dua siku ya Ijumaa katika viwanja vya Lumumba.Fuatilia maoni ya mwisho mwisho katika chapisho hili kupata habari kamili.

Sikiliza tangazo hilo:
 

Tafadhali andika alama ya NDIO unapotoa mchango wako, shukurani

MUWAZA-COMMUNITY-ACCOUNT
HSBC BANK,
23,RIPPLE ROAD
BARKING-ESSEX-IG11-7NW.

ACCT   :      71691759
S/CODE:      40-09-06

INTERNATIONAL BANK-ACCOUNT-NAMBER: GB27MIDL 40090671691759.

BRANCH IDENTIFIER CODE:MIDLGB2102F

Tangazo:

Kuna maoni hapa tumeyapokea ya watu kuchangia kampeni maalum ya NDIO – Kura ya maoni.Mchakato huo ni kusponsor program ya TV/Radio ambayo watu wapo nyumbani watashiriki kufanya kampeni hio, na mwisho kutakuwa na maelezo kuwa kampeni hio imedhaminiwa na wazanzibari walio nje.

Waandishi ambao tunatarajia kushiriki katika programu hio ni kama Shk Ally na wengine.Hivyo tunaomba michango ya wazalendo kufanikisha kampeni hio na kudhamini programu hio.Anaetaka kutabaruk inshallah amtumie Shk Ally mchango wake.

Nukuu:
Nadhani wazanzibari wengi wanazo njia zao muafaka za kutuma michango yao Zanzibar.Hii inakuja kutokana kuwa hatuna bank account ya kupokea michango ya aina yoyote ile kutokana na ukiritimba uliopo kwenye masuala ya mabenki.Tunayo PayPal account kwa watakao weza kutumia, nayo imesajiliwa kwa email ya admin@mzalendo.net.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na uongozi wa mzalendo.

Nukuu:(Orodha hii iko kwenye matengenezo, kama jina lako halipo tafadhali tutumie barua-e)

Orodha ya waliochangia au kuahidi:

  • Zamko amechangia £25
  • Sharif ” ” £20
  • Ashakh……….£20
  • Kuna $500 kutoka Denmark.
  • Mrfroasty – 25E
  • B.Ole – 25 GBP
  • Nad Mbarak – 10GBP

Uongozi wa MZALENDO

Share and Enjoy:
  • Facebook
  • Twitter
  • Digg
  • MySpace
  • del.icio.us

65 maoni Sauti:Harambee:Mchango wa wazanzibar walio nje (Wazanje)

  • ashakh

    Shukran

    Nakumbuka tulizungumza kuanzisha hawa mawakala kwa kila nchi. Kwamchango huo tungefanya kama ni majaribio.

    Hivyo tunawaomba kutoka kila nchi mmoja wao ajitokeza ili kuwapa bank details baadae wale wazalendo waliopo nchi hapo waweze kuingiza hizo pesa kwenye account yake.

    Au kunamashauri gani.

    Mwisho mchango wangu uko tayari, natafuta wa kumkabidhi.

  • Assalamu alaykum,

    Kwa wale ambao watapenda kutuma michango yao kwa paypal tupo mbioni kuweka account ya mzalendo ya paypal, ila kwa wale walio na uzoefu wa kutumia paypal wanaweza kutumia njia njii hii:

    Nenda kwenye account yako ya paypal kisha bonyeza SEND MONEY, weka email hii admin@mzalendo.net
    chini yake andika kima cha fedha ulizojaaliwa kuchangia. na chini baada ya hapo kuna tabs mbili ambayo moja ni purchase na moja ni personal, chagua utakayoiona wewe inakufaa, ikiwa ni purchase paypal watakata cent kdg kwa zile zile pesa ulizotoa na kama ukichagua personal basi utalipa cent za ziada.

    Shukran,

    Mzalendo.net

  • mrfroasty

    @Ashakh,

    Kuna changamoto nyingi kwenye masuala ya kutumia bank account.Its not that simple, hususan kama pesa zinatoka nje ya nchi.Benk nyingi zina algorithm ya kudetect na inaweza hata kupelekea account ya mtu kuwa blocked for security checkup.

    Hivyo nashauri watu watumie Western, Said Makka n.k kumtumia Shk Ally Zanzibar.Hii ndio njia pekee ambayo ni sahihi na rahisi.


    PayPal nadhani ndio njia rahisi ya kuchangishana online.Lakini kama tujuavyo si wengi wenye kutumia huduma hii.Licha ya hivyo, inshallah nikipata muda nitaandika kidogo kuhusiana PayPal ni nini na jinsi gani unaweza itumia katika maisha ya kila siku ukiwa kwenye Internet.

  • ashakh

    Western Union simshauri mtu yeyote kutumia. Hiini njia mbaya sana. Binafsi wamenitesa na kutaka mapassport na madriving license mpaka nikawa tayari pesa kuziacha. Tena basi hilo jina la huyo anayechukua si miongoni mwa majina yetu.

    Nilichokiona kutmia saidi mmaka, kwa sh Ally saleh itakuwa usumbufu jaalia watu 20 kutoka UK, kila mmoja kamtumia kiasi chake, ni vigumu kwake kukumbuka. Pia ikiwa pesa zinatoka UK kila mmoja atachajiwa £2. Jee hizo 2×20 = £40. Pesa nyingi hizo.

    Iwapo mtu mmoja hapo UK atazipokea pesa za watu 20 hawa kubwa atatumia £2 tu kutuma, tutakuwa tumesave £38.

    Halkadhalika walioko Denmak watatafuta mtu wao, Canada pia watatafuta mtu wao, na nyenginezo. Baadae huyo ndie atakaye ziwasilisha kwa Sh Ally.

  • zamko

    Saalam ndugu wachangiaji, mawazo sio mabaya lakini nina suala. Hii nikutokana na ufanyaji kazi wangu. Nina hulka zile zile za my X employer UNDP. Inapotoa michango ya project nilazima ipatiwe feedback. Samahanini kama nitawakera.

    Q:Nakumbuka mwezi uiopita hivi,tulichangia pesa za stationary/lengo lilikua kuchapishwa kwa ujumbe wa Kura Ya Maoni ya Ndio. Ili usambazwe kwa wale wananchi wote wa Unguja na Pemba wasiokua na ACCESS ya INTERNET.

    Sasa kazi hii ilifanyika? Na matokeo yake yalikuaje? Mbona hatukupata maeelezo yoyote? Au nyinyi wezangu mulisikia NDUMU…NDUMU? Na kama ilifanyika mbona sh.Ally au B.Ole hawakutuletea feedback yoyote ile.

    Nataka nduguzangu munielewe kama kuchangia sio jambo baya, na wala sikatai. Lakini naona tunapochangia kitu nilazima tufuaatilie kwanza matunda ya michango yetu tuliyotoa mwanzo. Yalilenga kwa yale mambo tulioyakusudia? Ikiwa ujumbe ule umesambazwa kwawananchi ni sawa kabisa.

    Kwavile sikupata feedback yoyote ya mchango wa mwanzo, naomba mwenye habari hizo anieleze kidogo.Au tufuatilieni kwani siku za kura ya Maoni zimekaribia. Hapo ndipo nitakua na motisha wa kumtumia tena Sh.Ally mchango wangu.

    Kwa wale waliokua ready kuchangia nawakumbusha, si Saidi MMmaka tu anaetoa pesa. Kuna ndugu mwengine anaitwa Abdalla Mrusi (pale Darajani makontena). Nayeye anatoa pesa, akipelekewa. Mtu wakumpelekea pesa hizo ni Sh. Abdallah Khalid wa Reading in UK.

    Kwahiyo watu wanaweza wakafanya hivo kutokana na urahisi wao.
    Msaaalam.

    • mrfroasty

      Fuatilia chapisho lenye kichwa cha habari “Update:fotokopi project”, maelezo yafuatayo yamechapishwa kama ni feedback:

      salaam,

      wana ukumbi zanzibar imepokea fedha za machapisho ya kizalendo mara mbili.

      moja ilikuwa ni makala ya ally salehna ile ya bole. kulitoleshwa
      nakala 300 na zaidi.

      hizi zilisambazwa unguja zaidi lakini pia pemba. kopi zilikuwa
      zimebaki na hivi karibuni zilitumika katika semina ya vijana kuhusu
      civic education.

      pia kulitolewa pesa za kuchapisha KWA NINI UPIGE NDIO. tulichapisha
      kopi zaidi ya 3,000 na hizi zilisambazwa unguja na pemba. kopi hizo
      ziliibua msisimko mkubwa juu ya suala la kura ya maoni.

      wengine bado wanafikiri kuwa kama kuna harakati zilianza kuhusu kura
      ya maoni…hasa zile hoja 10 zilizokuwa zimetolewa.

      kama kuna wana mtandao wowote ambao hawakuwa wamepata feedback basi
      hali ilkuwa ni hiyo.

      ally saleh

  • ole

    Kwa Wazalendo wote.

    Kwa kweli ni idea nzuri sana na naamini huu ni wakati mzuri kwa wazalendo kuungana pamoja kufanikisha hili.

    Naamini kwa yeyote yule atakae changia basi hatopeza bali atakuwa amejenga na kuwasaidia wengi. Nasema huu ndio wakati pekee wa kuonesha ushirikiano wa hali ya juu, na mfano mzuri wa kuonesha ni jinsi gani tunavyojali maendeleo na maslahi ya visiwa vyetu.

    Kwa wale ambao wako nje na hawatopata nafasi ya kupiga kura basi hii ni njia pekee ya kuonesha kuungana mkono kwao, na ni njia nzuri ya kushiriki kwao kikamilifu katika zoezi hili lenye maslahi kwa dola yetu.

    Na wale waliopo Zanzibar ambao watawawakilisha wenzao walikuwa hawapo basi watafarijika kuona wenzao walioko nje wanajali maslahi ya nyumbani kwa kuchangia kampeni hizo.

    Ombi langu kwa wahusika ni kutaka kujua ni kiasi gani kinakadiriwa ili kuweza kufanikisha zoezi hilo ?.

  • Mkavirondo

    Ni wajibu wa kila mpenda Zanzibar
    Ndugu Wazanzibari majuto mjukuu. Maji yakisha mwagika hayazoleki.

    Mdharau mwiba humchoma. Hizi zote ni hadhari tunazopewa pale ambapo

    hufanya mapuuzi, hasa pale kila mmoja kumtegemea mwenziwe atafanya.

    Tabia hii tujaribu kuiepuka, kwani hili ni lettu sote na la wanetu na Wazazi

    wetu au wa wenzetu. Ni wajib wetu sote tukaamka kutoka kwenye

    usingizi mzito na tuanze mchakato wa kulipigia debe kwa wote tunao

    wafahamu wenye nia njema na Zanzibar watowe michango ya hali na

    mali katika kampeni ya NDIO kwenye Kura ya Maoni. Tuna siku 10

    ambazo tunatakiwa kuzifanyia kazi usiku na mchana mpaka tufikie

    lengo letu. Inshaallaa. Usitosheke na mchango wako pekee washajiishe

    wote uwajuao WACHANGIE.

  • Banda

    jamani eee haina haja kuchangia bureeeeeee kwahili halisaidii chohote kile, musitake tuibia bueeee .kama munge anzisha michango ya watoto yatima na wasio jiweza mie naona hhiichi ndo chakufanya kitamsaidia mtu hapa duniani na huko twendako sio hili , amkenii nduguzangu maisha mafupi anzisheni vitu vya maana hasa vya hukoooo kwetu akheraa bana, nyie vipii lakini mupo hapa duniani, hamuyasikii haya matangazo yakifo kla leoo hujui nawewe karibu lako latatolewa jee umeazisha nini hapa duniaani kitakacho kusaidia hiyo safari yako huko ? au unachangia watu wakarape kura yamaoni nakwaya wakaimbee sio , namgoma jamanii hiyari yenu atakaetoa pesazaee nayeye yumooo mdundo ukipigwaa kule achukuwa zake nawewe ulotoa dola yk wachukua zako dahambii, najua mutasema sio ngoma ila hilo ndo kubwa litakalo fanywaa huko kuimarisha watu wapige kuraaa , twawajuwa watu wetu kama hawajapigiwa ngomaa basia hawsikiichochoooooooote kile

  • zamko

    @.Mfroasty ahsante kwa barua ya shekh Ally Saleh, ni vizuri umeileta kwenye jukwaa na watu wataiyona faida ya michango yao. Barua kama hizi za feedback nimuhimu zipelekwe jukwaani kwa mtandao mara zinapopatikana. Shukran.

    @banda: Naona unazungumza kama vile uko-usingizini, kuanzisha mambo yatakayotufaa akhera. Hunahaja ya kungojea watu wa-anzishe, ungefanya hivo wewe mwenyewe kwanza, silazima uwe na project kubwa . Unaweza kusaidia individual farmily kama wanavofanya watu wengine. Hapakwenye mtandao unajua kunawatu wengi wanaproject zakuwasomesha watoto masikini wa visiwa hivi?Wanaweza kuwa wanafanya hivo individual, kwani sadaka kama hiz hazitangaziwi.

    Huku niliko mimi kuna watu wawili wao ni Convarted Danish muslim wanasafiri kila mwaka wekenda Zanzibar.Mmoja anaitwa Sh.Abdulwahid Petersen na mmoja Mohammed, wanaproject zao na wanawasaidia watoto wa skuli za Unguja na Pemba.Mfano skuli ya Shengejuu, maziwa ngombe na Wambaa.

    Sasa kama wewe hutaki kuibiwa kwa mchango huuu nenda kwenye http://www.abdulwahed.dk or google na search jinahili la Abduwahed utapata information na number za simu. Naunaweza ukawasiliana nae. Kama unataka kuwasaidia watoto maytima utamuuliza ni vipi utasaidia.

    Nahisi utaupata ujumbe wangu: USITULETEE DOMO KAYA SHANUO MTOTO WA DIFU.

  • Salmin Kiluwa

    MUWAZA ina account UK naomba viongozi wa MUWAZA muwape watu account yenu ili tupate michango ya UK na kama ilivyoshauriwa munaweza kupeleka as one lot na gharama za kupeleka huko Znz zikawa ndogo
    Kiluwa

  • ashakh

    wewe umejiita BANDA jina limekusibu, kumbe BANDA kweli. Zanzibar watu hawataki tena mabanda, wanajenga majumba ya kifakhari, na yule aliyekuwa hana uwezo hutia bati. Mpaka leo bado unamawazo mgondo kama hayo. Tunadhani umetembea utakuwa umestaarabika, bako ukombali.

    Ndio nyie munaodhani mutaingia peponi kwa sababu munaswali tu. M/Mungu hatizami hilo tu anatizama mtiririko wa matendo yako uliyoyafanya wakati uko duniani. Soma aya 80 Surat Baqarah utawaona ninani watakao ingia peponi.

    Banda kama wewe akuibie nani, na hasa kwa kipi ulichonacho. Umetangaziwa michango mingapi hapa mzalendo na ni upi umechangia. Jee umezuiliwa usisome? Huu mtandao unagharama zake hata kusema ngoja nionyeshe ihsani angalau nisaidia hizi gharama kwani hichi kitu kina faida, hufanyi. Jee huo si ni ukafiri?

  • ashakh

    @ Salmin Kiluwa

    Wazo lako mujarab, niko njiani likokwenye fikra zangu.

    Na ndio hilo nimekimbilia kuandika lakini nimepata kichefuchefu baada ya kusoma maoni ya BANDA.

    MUWAZA inayo account yake tena MUWAZA ni jumiya kwenye katiba yake inaklusanya member dunia nzima. Hivyo kuitumia account yake hakuna tatizo. Kwa vile wako mstari wa mbele kuipigia debe kura ya maoni na hili sidhani kama watasita kuwa ruhusuwatu kutumia.

    Hii itakuwa rahisi sana na kwa vile iko UK.

  • zenjiboy

    @ Banada,
    Ukitaka kujua kama hili la kura ya maoni ni katika mambo ya kukuingiza peponi soma hotuba ya kufungia kongamano amabayo aliitoa Maalim Seif Sharif hapo Zanzibar. Kuna aya nyingi na hadithi ambazo zinaonesha umuhimu wake. Na kila atakaechangia basi yuko katika kheri inshaAllah.

  • zenjiboy

    sorry si banada ni BANDA

  • Addil

    NAHISI HAPA ANATAKA KUTIWA MTU CHANGA LA MACHO.TUSICHANGIE CHOCHOTE MPAKA KUWE NA UTARATIBU MAALUM AMBAO TUTAKUA NA UHAKIKA KITAKACHOPATIKANA KITAKWENDA KULIKO KUSUDIWA.

  • ole

    Shukurani za dhati kwa Banda na Addil.

    Wazalendo hamna budi kuwapa mgongo watu wa aina hii, kwani ni watu ambao hawajui wanachokisema na wala wao wenyewe hawajijui.

    Mimi ningependa kuwafamisha kwamba ikiwa hawana cha kusema basi wanyamaze kimya, hilo litakuwa ni jambo zuri kwao kuliko kuropokwa na kuwaonesha watu kwamba wao ni wamuumini wa kweli.

    Banda mtu hajisifu katika kufanya mema, kuna mambo ukiyapigania basi ni sadakatuljaria hata ukifa basi utafaidika.

    Banda wewe ni mtu ambae ukitoa moja basi dunia mzima itapata habari kwa maana hiyo ni sawa na zero kwani sadaka na mambo mema hufanywa kwa siri. Sasa wewe unajionesha kwa watu ili tukujuwe kwamba ni mtu wa dini, jambo ambalo katika dini yetu haliruhusiki kujionesha kwa watu.

    Leo hii Wazalendo wanapigania kuondosha dhulma na kuwasaidia walio wengi, jambo hili likifanikiwa basi kuna fungu kubwa kwa mola kwa wale wote waliohusika.

    Wewe unawakatisha watu tamaa Mola atakulipa kwa hilo, kwani unafurahia kuona dhulma inadumu Zanzibar.

    PIA NAKUMBUSHA TENA KWA WAHUSIKA KUTUPA IDEA NI KIASAI GANI AMBACHO KINAHITAJIKA KUFANIKISHA ZOEZI HILO ?

  • mrfroasty

    @Banda && Adil,

    Mnadhani watu wizi hapa sio ? Hapa takriban kila kiongozi wa mzalendo ni mtu na heshima yake, msituletee mambo ya kihuni.Kama mtu hataki kuchangia akae kimya, awaache wengine.

    @Kiluwa na wote
    Shukurani ni mawazo mazuri uliyoyaleta, na kheri MUWAZA washatupatia details za account yao nitafanya update hapo juu ya chapisho hili.


    Watu kama Banda && Adil ni wa kupuuzwa tuu, obviously they dont know what they are talking about.

    Maasalaam,
    mrfroasty

    • muhimu

      mimi mrforasty nimefurahi kuanzishwa kwa harambee hii mwenye alikuwa nacho atowee alokuwa hana japo duwa japo letu lifanyike kwa salama Mtume (SAW ) ANASEMA KILA JAMBO ZURII SADAKA na mie naimi hii jambo zuri kwa hiyoo hii ni sadaka
      na vile vile Mtume SAW pia anasema MANENO MAZURI SADAKA sasa unapoongea maneno mazurii poa ni sadaka sasa wewe kuwa umeanzisha mtandao hauna sababu kila anayekupinga wewe au kuwa na maoni tofauti na wewe ukamtoleaa ujauri na kiburi cha hali ya juu jishundishe kuongeaa na watu vizuri sio kila mtu umfookee tuu na kumpuuza huo ukmbushoo tuu wangu kama muislam mwenzangu

      • mrfroasty

        Well, shukurani kwa maneno mazuri nitajaribu inshallah ….

        P:S
        **Lakini tukumbuke isije kuwa unatumia hicho kipengele cha kuwa nimeshiriki kwenye mtandao ikawa sababu ya kunifumba mdomo :D

        Anyways, pia tumefundishwa katika dini yetu kuwa usichopenda wewe kufanyiwa…basi usimfanyie mwenzio.Sasa ikiwa watu wanafanya jitihada kama hizi.Anaibuka mtu kama Banda na maoni ya kipuuzi unataka afanywe nini?Tusherekee?

  • mrfroasty

    Info au ushauri tuliopokea kutoka MUWAZA ni kutumia njia ya Radio, sababu ya msingi ni kuwa Radio inafika wengi zaidi hususan mashamba wengi hawana TV.

    Maasalaam,
    mrfroasty

  • ashakh

    Mrforasty, Inshaallahkeshonitaweka zangu. Kiasi nitakachotowa ni GBP (£20).

    Tuyaache hayo mabandayasubiri kuchomwa moto kama mwakakwogwa kule kaye

  • mrfroasty

    @Ashakh na wote,

    Kama umefanikiwa kuchangia naomba utupe feedback , mimi nimeshindwa system ya bank yangu inasema BIC/Swift code has to be 8-11 characters.

    Nimeshamtumia email Mwenyekiti wa MUWAZA Dr.Yussuf kupata verifications na double checkups, inshallah nitatoa feedback nikifanikiwa kutumia account hio.

    Maasalaam,
    mrfroasty

  • ashakh

    Loo nikweli lazima itakuletea mashaka.
    Hizi information ni kwa locals tu,kwani ni bank account pamoja na sortcode yake.

    Kwa matumizi ya International nilazima ipatikane hiyo swift code amabayo long numbar ikichanginyika na herufi.

  • Banda

    msikasrike jamnii hayo yalikuwa ni maonai yangu ,sasa nyinyi nataka niwaulize huu mtandao unaendeshwa KIDIKTETA ? tu, hapa mtu akitoa maoni tofauti kidogo tu mwakasirika hivoo, nawashukuru wote walionni beza na kunizarau na ndomana kule kwetu mpaka leo hatuendelei kwahili , mtu mmoja kujiona yeye bora kuliko mwangine , mimi nimetoa maoni yangu kama mwanawamtandao mwengie yoyote yule, ila tafauti yangu sikukubaliana nahilo je nimefanya dhambi? sasa hiyo deokrasia mnayo ipigani iko wapi? kama hapa tuu ukitoa maoni kinyume na viongozi munkuwa wakali kiasi hicho , jee hayo mengine mutayawezaa? mtu akitoa maoni tofauti hiyo ndo challenge nzuri kwenu kujua munaendesha vipi huu mtandao sio kukasirika mambo madogo tu haya yanakushindeni, je hiyo serikali mukipewa simutauwana nyie ? simtapasuka mashavuu kwa kununa nyie? kuweni wastaarabu wa kujibu hoja

    • mrfroasty

      Acha kutupambaza, kwanza fanya utafiti ujue nini demokrasia halafu ujiulize haya maoni yako yanaingia kuhesabiwa kuwa ni sehemu ya demokrasia?

      P:S
      Ukimaliza utafiti tuletee hapa tuone kama unafahamu nini maana ya demokrasia.

      Apart from that, ignored….

    • ashakh

      BANDA, jaalia nimekutukana jee hayo utayaita maoni?

      Pale ulipofika kuwaita watu wizi, unataka tuyapokee kuwa ni maoni pia?

      kumbuka ZAMKO aligusua zuala hilohilo la kutofahamu nini kilitokea kwa pesa zilizochangishwa, lakini hakuthubutu kuwaita watu wizi. Yale ndiomaoni.

      Kiasi watu wavimbe mashavu, kama mabunju, kwani umewakashifu.

  • mrfroasty

    Update:
    Kufuatia suala la B.Ole hapo juu kuhusiana na gharama nimepata jibu kutoka kwa Shk Ally ni kama ifuatavyo:

    salaam,

    tunataraji kutumia kama radio tatu:

    Sauti ya Tanzania Zanzibar ( government)

    Zenj FM

    Hits FM

    Wallahi si rahisi kusema kiasi gani kwa sababu inategemea tunataka
    kufanya matangazo mangapi kwa maana ya wingi au mara nyingi ya
    kutangazwa.

    lakini tuseme tuikipata 1.8shs kwa hali ya sasa vyombo vya habari
    vyenyewe kulipenda suala hili tunaweza kupata matangazo mengi. 1.5
    tutawalipa wenye radio kama fedha ya huduma ya kutangaza na hiyo
    200,000 ni ya kutengeza tangazo lenyewe

    nitajua matangazo mengi kiasi gani baada ya kukaa nao…na kuengeneza
    tangazo ambalo litakuwa na urefu kama dakika 1 mpaka dakika moja na
    sekunde 30.

    kama nikipewa nguvu…tangazo litaanza kutoka jumatatu mpaka jumamosi.

    ally


    P:S
    **Naomba tusiwe wenye kuuliza masuala mingi na kuwa vizingiti, badala yake tukubali kuaminiana juu ya masuala kama haya.Maana down side ya kumuuliza mtu sana, ni kueka dhana kuwa actually hamuna imani nae…nadhani ntafahamika hio ni logics au discrete math kwa wanaopenda.
    **Zingatieni pia kuwa muda ni mdogo, na suala hili ni nyeti

  • ashakh

    Nadhani hapa point ni moja.

    Linapokuja pendekezo kama hili nilazima liwe limekamilika huku likiwa na taarifa za kutosha. Hapo tutaondoa mwanya kina BANDA kuanza kujipenyeza.

    Information hizi ni kama hivi, kila kutuo cha habari kina utaratibu wa kucharge gharama za tangazo. Mfano;
    inaweza kila dakika moja inagharimu TSh 50k (50,000). Pia wanaweza kukwambia kutokana na time slot kwa siku tutakupa slots 5 au kilingana na uwezo wao.

    Mwanzo wa hesabu ni moja. Tunachotaka kujuwa ni tangazo moja linagharimu kiasi gani, basi? Tukizijuwa taarifa kama hizi sisi wenyewe tutaweza kutathmini kwa mfuko wetu tufanye matangazo mangapi. Hata iwe elfumoja itapatikanakwa kufanya hesabu tu.

    Ukianza kunitajia pesa kabla ya kunipa hizi infomration hapo nitaanza kukutilia wasiwasi kuwa hii kazi huiwezi. Kwani nitakuuliza jee nikikupa 10 million utaniletea matangazo mangapi. Jibu likiwa “ngoja nikaulize”. Basi mojakwamoja project nzima na scrape. Hutoweza kuitekeleza.

    Plan mwanzo, ndio ulete wazo. Fanya research kabla ya kueleza kile unachotaka kufanya.

  • kayson

    musishambuliyane ndugu zangu wa kislam. sote ni ndugu na sote hapa lengo letu ni moja ila kila mmoja na mtazamo wake tuungane pamoja ili tutimize zamira yetu. akasae hakuna budi kumkosowa ila tumkosowe wa maandiko mazuri sio kaandika ushafu na wewe unamjibu uchafu hapa tutakuwa tumekoseya ndungu zangu huo ni mtazamo wangu WABILAHI TAUFIQ

  • Banda

    Wewe ashakh naona unajizonga tuu , naona sasa umekubaliana na mimi kuhusu mchnago huutaki tena sio, hapo mwanzo ulikubali sasa unaanza kutilia mashaka ya nini? si utoe tuu wewe lijigamaba utatoa kesho sasa tena kipi kimezidi ushashtuka sasa eeeh, Mrfoasty mimi sikusoma kama wewe lakini huu wenu ni UDIKTETA, demokras ni mtu kuwa huru kusema analoliona yeye kwake sawa hiyo ndo demokrs shehe , sasa km wewe unayako maana nipee
    kuweni fair musikasirike na mambo madogo kama haya , pesa kupatikana kwake ni ngumu nakatoka vile vile ngumu sio easy tu km unavo fikiria ukisema tu changieni tuchngie lazima tu ku challenge kwanza na musha feli kwahili manke huyo aly saleh mwenyewe mushamsikia hata bei ya tangazo hajalijua mpaleo nahuo muda wenyewe ushakwisha musichngaye wtu bora mujiandae najenginee sio hili ushauri waburee huu chukuwa mrfoasty MUJUE JINSI YAKUJIPANGA KWA MAMBO YENU VIZURI

  • kayson

    mbona mimi nikiangaliya naona kama hamufahamiani wakati wa maelewano umefika KUBALI MATOKEYO SOTE NI WAMOJA . MARIDHIANO NDIO PEPO YETU

  • ashakh

    @BANDA ingekuwa tokea mwanzo umetowa maoni kama haya, ningekuwa nawe popote pale kukutetea.

    Lakini unaponambia, nakariri maoni yako:
    “jamani eee haina haja kuchangia bureeeeeee kwahili halisaidii chohote kile, musitake tuibia bueeee.”
    Nikufahamu vipi?

    Pia nakuomba ufahamu, kuna kukataa kuchangia na kuna kuboresha mchango. Maoni yangu hapo juu hayakatai kuchangia, yanachokataa ni infromation. Na hii ni kutaka tujiweke sawa, na kuwajenda imani watu kama nyie.Kwamba hichi tunacofanya ni cha uhakika. Na usionekwamba tunalengo la kukuibia.

    Ikiwa nimeweza kuchallenge hapa nadhani utaona kweli kuwa hapa haibiwi mtu, hasa maskini kama wewe,si wa pesa bali fikra na upeo wa kuonambali.

  • Banda

    asante sana ashkh kwa kunifahamu nia namdhumuni ya maoni yangu naomba uwafahamishe hao mtajiri wenzio wa fikra na upeo wakuona mbali labda wewe watakufahamu tajiri mwenzao , wewe umefahamu nini maana ya demokras sio lazima ukubaliane nahoja,
    shukran
    BANDA

  • kitamli

    ahlan wasahlan wanaukumbi nimejaribu kutizama maoni ya wenzangu na nimeona maswala haya ya kuchangia hayana tofauti na michango mengine katika community za kiswahili yanakua na uzito sana na mpaka kusababisha baadhi ya watu kufarikiana jambo linaweza likawa kwa nia nzuri lakini kama ashakh alivyosema wakati mwengine unapoleta jambo hili uwe umejipanga na ujue watu nini cha kuwajibu kwa sababu mtu ukianza oh!manake unampa mtu wasi. na mie nadhani nia nzuri ipo lakini nafikiri hili jambo halikufanyiwa matayarisho ya kutosha.

  • ole

    @wANAUKUMBI WOTE.

    Kwanza kabisa nawapongeza wote wale waliochangia katika hoja hii. Mawazo yao ni mazuri na hatuna budi kushukuru kwa hilo. Hii ni kuonesha ni jinsi gani mtandao unavyokuwa siku hadi siku.

    Kimtazamo wangu mimi nimeridhika na hatua ya uongozi wanazochukua katika kuongoza mtandao huu. Naamini wanafanyakazi usiku na mchana kupigania maslahi ya Wazanzibar.

    Pia nampongeza kwa dhati, MRFROASTY kwa jitihada zake binafsi mimi kaka yetu namwita mpiganaji asieogopa vita. Na tunaona ni jinsi gani utendaji wake ulivyomakini, mimi nasema hatuna budi kuiga mfano wake.

    Mrfroarty kumbuka kwamba kuna watu wanaumwa sana kuona huu mtandao unafanya kazi nzuri ya kuwaelimisha wazanzibar, usifikirie kwamba kuna watu wanapenda hili liendelee.

    Inashangaza atokee mtu tena Mzanzibar , akurupuke tu na maneno ovyo huku wenzake wanatoa nguvu zao zote kufanikisha jambo jema, halafu asingizie demokrasia. What kind of democracy,they are talking about ?

    Mr. BANDA Hii yako sio Demokrasia bali nikaraha, matusi, kejeli na kuwarudisha nyuma wana ukombozi . Kama unaweza changia huwezi basi kaa kimya.

    Mtandao huu ulipoanzishwa hatukutakiwa fedha bali wenye uchungu na nchi yao walijitolea. Kumbuka kwamba wako wengi waliokuwa wakitoa maneno mabaya na ya kukashifu kama ya kwako lakini leo hii hatuwaoni humu kwenye mtandao, lakini bado mtandao unaendelea na kazi zake bila kutetereka.

    Unapoleta hoja kwamba tunataka kuibiwa, huku ni kuvuuka mipaka na kupayuka kuonesha kwamba una chuki fulani zidi ya wahusika.

    Tunakumbuka mara moja kulikuwa na vifaa vya hospitali ambavyo paliombwa michango yenu, mbona hukutoa hata shilingi na ile ilikuwa ni sadaka kubwa .

    Kuonesha kwamba watu wanauchungu na Wazanzibar vifaa vile watu walijitolea from Finland to Zanzibar, sasa unapokuja ukapayuka kwamba tunataka kuibiwa, mbona vifaa vilipofika hamkusema kitu, jee pale hamukuibiwa ?

    Wacheni kuwakatisha watu tamaa, kumbukeni mulikotoka ndio baadae mufanye kiburi na kuwakejeli wengine wakati uwezo wa kulifanya wewe huna na hata ukiwa nao basi huna moyo.

    Nimekuwa nikitembelea mitandao mbali mbali yenye lengo na hisia kama Mzalendo, lakini sijawahi kuona watu wenye mawazo mgando kiasi hichi, hivi kweli hapa Wazanzibar walipofikishwa leo, halafu wakatokea watu kama akina BANDA na wenzake tuwafahamu vipi ?

    Kuna haja ya kuheshimiana kumwita mtu mwizi ni tusi kubwa wakati kuna watu wanajulikana wanatuibia mamilioni ya pesa na tunashindwa hata kunyanyua mdomo.We need 2 be fair kama Wazanzibar.

    KAMA NIMEKOSEA NAWAOMBENI RADHI, KWANI NDIO UUNGWANA.

    MWISHO KWAKO MFROASTY, kwa kipindi hichi kifupi nipo hapa u.k ingawa niko busy sana kufanikisha mambo fulani, kwa maana hiyo nitaweka kiwango cha £25/= kesho ijumaa kama ni mchango wangu juu ya hili kwa kutumia ACCOUNT HIYO HAPO JUU.

    • mrfroasty

      @B.Ole

      Shukurani, tuko pamoja inshallah…mie mchango wangu nishatoa leo inshallah kheri.

      mrfroasty

  • Banda

    usiwe mkali ole mambo mazuri hayataki haraka, jazba haijengi inabomoaa sasa wewe ukipandisha na mimi nikipandisha hatuto fahamina, tumia busara nahekma ulizo jaliwa kutufahamisha mambo hasira hasara cool down pengine nilikuwa sijafamu lakini ukiwamakali nitazidi kuwa sifahamu taratiiiiiibu mzee olee sawa?

    • zenjiboy

      Tabaan, Mh. Banda sasa unaonekana kufahamu. jamani muachieni tena :) Natarajia na wengine wamefahamu nia njema za wenzetu.

  • Banda

    sio taabani wala nini zenjiboy tatizo hapa wewe usipinge kituu wewe ukubali tuuuu hata kiwe ndicho kiswe hatufiki hivoo

  • ole

    Asante sana Banda.

    Inaonekana kwamba kidogo Mr Banda ni mtu ambae anafahamu vizuri lakini wakati mwengine unapenda kuwachangamsha vijana.

    Naamini pia huna lengo baya, kwani fikiria hatua ambayo tumefikia leo hii Zanzibar, zamani ukiwa na mawazo tofauti na Serikali ulikuwa Adui, lakini leo hii wenzetu wengine wameelewa kwamba fikra tofauti sio ugomvi wala chuki bali kwa wanaojua hutumia fikra hizo na mawazo hayo kujenga pale palipoharibika.

    Wazanzibar ni watu wanaopenda matani sana lakini wakati mwengine unaweza hata kulia. Wazalendo tukumbuke kwamba wakati mwengine mzaha au matani yanaweza kuleta balaa na tafrani kubwa kwa wahusika.

    Mr.Banda wakati nikiwa mwanafunzi wa darasa la tatu, nilikuwa na mtido mimi na wanafunzi wenzangu, tukikaribia nyumbani kutoka skuli, tulikuwa na bokora mikononi, basi hapa tulikuwa tuna act kama Mwalimu na Mwanafunzi mtoro.

    Tulikuwa tunauuliza mnazi kwa nini jana hukuja skuli, Mnazi unajibu eti nilikuwa naumwa . Unacho cheti ? Mnazi unajibu sina. Basi wewe muongo ulikuwa huumwi isipokuwa wako ni utoro tu, kwani mtu akiumwa huenda hospitalini kutibiwa.

    Kinachofuatia hapo ziliuwa ni bakora tu huku sisi wenyewe tukipiga mayowe makubwa sana na vilio vya kwikwi, ilikuwa ni utani lakini wazee wetu hawakupenda utani ule, kwa sababu walikuwa wanakuja mbio kutuangalia wanaposikia mayowe yetu, kwa hofu kwamba tumefikwa na tatizo, lakini wakifika sisi tulikuwa tunangua vicheko.

    Wazee wakasema kwamba huo sio mchezo mwema, wala utani mzuri, kwani kuna siku utakuja kufikwa na matatizo basi watu wafikirie ni kawaida yako.

    Ama kweli iko siku nilipigwa na ngombe jike karibu na nyumbani nikapiga mayowe sana lakini Wazee wakasema kwamba hiyo ndio kawaida yao.

    Rafiki yangu Banda bado kidogo nipoteze maisha kama sio huruma za Bibi kwa Mjukuu wake basi hii leo nisengekuwa naandika makala haya.

    Kwani baada ya makele ya muda mrefu, roho haikumpa akaona hata, bora niende nikamtazame, kufika hakuamini macho yake, nililazwa hospitali karibu miezi miwili hivi.

    Hadithi hii ni ndefu lakini ninachojaribu kukizungumzia hapa ni kwamba huu wakati tulionao sio wakati wa wa mas-hara tunahitaji kushirikiana kwa pamoja kufanikisha haya yanayotukabili hivi sasa.

    Usione hivi sisi wengine hatulali usiku wala mchana, lengo na madhumuni ni kuitakia kheri nchi yetu na Wananchi wake.Wala usifikirie kwamba labda tunalipwa, la hasha tunajitolea kwa moyo safi.

    Ni imani yangu kwamba mimi na wewe tunapenda kuona Amani, Utulivu na Usalama unapatikana na pia maendeleo ndio kilio chetu, lazima tukumbuke kwamba matatizo yetu yatakuwa solved na sisi wenyewe, ikiwa tutakuwa na moyo wa kujitolea.

    Naamini michango yetu itasaidia kufika kule tulikokusudia japi kama ni peni tu uliochangia, kumbuka sote sisi ni Wazanzibar na tutaendelea kuwa Wazanzibar licha tofauti zetu kimawazo na fikra.

    Nafarijika kwa kunielewa pia nakupongeza kwa nasaha zako nzuri, nimategemeo yangu utakuwa Mwalimu mzuri baadae, na sisi tutakusikiliza kwa makini.

    Asante.

  • Ally Saleh

    salaam,

    nimeona mtu anauliza na anataka kujua juu ya bei na time slots. ni hoja nzuri.

    lakini tukitaka kufanya njia hiyo hatutaweza kupata matangazo ya kutosha. kwa maana bei hazitalingana na uwezo wetu tulionao. au fedha nilizopendekeza kwa haraka ya wakati zipatikane.

    katika hili kuna uwezekano wa ku ride on the wave. fikra zangu ni kuwa kila kituo tunakipa 500,000 ndio zile 1.5 shs halafu wana run matangazo hayo hata mara au kiasi cha 10 times a day na tena kwa muda
    wa siku tano pengine kuanzia monday mpaka friday.

    sasa kuna ile raghba ya vituo na watu kufurahia jambo hili na we need to catch up on this mood.vituo vingi 500,000 ni nyingi na ni mishahara ya watu wengi.

    hio ndio dhana yangu na kama alivyosema mmoja kuwa kila tukichelewa basi tuna miss ile fursa ya kupata matangazo mengi na kwa hivyo tunakosa kufanya reach out kwa wananchi.

    ally saleh

  • mrfroasty

    Tumefanya update hapo kuhusiana na international bank account details

    Maasalaam,

  • ashakh

    Hata na mie sirudi tena nyuma baada ya kumuona ndugu yetu Banda anataka kufahamu.

    BANDA nakukumbusha kidogo, mwaka 2008 jumiya ya MUWAZA ilifanya kongamano ndani ya LONDON. Pesa zile ni Wazanzibar wenyewe waliopo kila pembe ya duniandio waliochangia. Hakuna hata mmoja aliyekhofia kuwa pesazake zitaibiwa.

    Kwa taarifa yako, mafanikio ya kongamano hili, lilifungua kufuli za milingo hii itakayofunguliwa hivi sasa (kura ya maoni).

    Katika kongamano hil walialikwa wageni kutoka ndani ya Zanzibar, tena basi ni watu na hadhi zao. Ni MUWAZA yenyewe iliyogharamia.

    Juzi umesikia kumefanyika kongamano jenginendani ya Zanzibar, MUWAZA ndio wadhamini wa kongamano lile. Gharama zake zinatoka mifukoni mwa MUWAZA. Hebu niambie kwa tathmini yako makongamano haya mawili unakisia yamegharimukiasi gani. Nataka uone uthabiti wanajumiya zetu wanavyokuwa wakweli kwenye michango.

    BANDA pamoja na wazalendo wengine, hizi ni taarifa kwenu:
    Zamko amechangia £25
    Sharif ” ” £20
    ashakh……….£20
    Kuna $500 kutoka Denmark.
    Mwenyekiti wa MUWAZA ameihadi sijajuwa kiasi gani. Inshaalah nikipata taarifa nitawarifu.

    @mrfroasty
    Tunataka haya majina uyaweke kwenye list,ili iwe ni rahisi kwa yule anayataka kujuwani watu wangapi wamechangia aweze kuona kiurahisi.

    Pia tunamuomba mtu yeyote atakayechangia ajulisha akijumuisha kima alichotoa.

  • kitamli

    addil keshafahamu na yeye? hakuwa banda peke yake alokuwa na mtazamo tofauti au jina la banda ndo limependwa? anyway mie naunga mkono fikra hii kwa hiyo shime wazanje tujitahid na inshallah kheri itapatikana.

  • Banda

    Naam kumbe busara nahekma mukitaka munakuwa nazoo , hivo ndio dini ya uislamu inavotaka sio mtu akipinga auliwe, afahamishwee ” mtoto akijinyelea husafishwa na si kukatwa mkono”asante sna mzeee olee nimekufahamu vizuri, kam unge itoa toka mwanzo busara hii basi tusnge fika huko , na mimi kama binaadam nilikosea kidogo ulimi hauna mfupa NAOMBA NJIRUDI KWA MAKOSA YANGU nilitumia kauli sinzuri nakubali hilo , kwawale wote nilio wakera naomba wanisamehe , nawale wote walio nikera, kunidharau, kunikashifu nishawasamehe fil dunia wal akhera nafikiri challenge yangu imeleta kijapo kidogo faida ila kidogo kama binaadamu hatukujua kuileta lakini akina mzeee ole, ashkh, mr foast na wengineo wamemenifahu nini leongo langu
    SHUKRAN ASANTEN SANA
    TUKO PAMOJA
    KOSA SIO KOSA….
    MR BANDA WENYEWE

  • ashakh

    Banda shukran, unajuwa jina lako zuri sana. Ulikuwa rais wa maisha kule Malawi. Tukiambiwa kuwa alikuwa Dr mkubwa na alikuja kumtibu Qeen.

    Kwa vile umetufahamu sasa tunataka mchango wako kwa vitendo. Huyu katoa 25, yule katoa 20, wewe tunataka utowe kwa uwezo wako.

  • ole

    @ASHAKH & MRFROASTY.

    Nimefanikiwa kuweka £25/-muda si mrefu.
    Kama kuna la ziada basi tuko pamoja.
    Ahsanteni,kidogo kidogo tutafika Wazalendo.

  • Addil

    KITAMLI KAKA@ NA MIMI NIKO PAMOJA NA WAZALENDO WENZANGU.

    MIMI SIPINGI TUSICHANGIE BALI NAOMBA KUWE NA UTARATIBU MZURI NA WA UHAKIKA ILI KITAKACHOPATIKANA KIFIKE KULIKO KUSUDIWA.

    ISIJE IKAWA YULE JAMAA ALIEPITISHA KOFIA MSIKITIINI KUCHANGISHA HALAFU AKAJIFANYA ANAKWENDA KUTIA UDHU,PESA AKAONDOKA NAZO.

    MIMI NIPO ENGLAND,NAUNGA MKONO SANA JAMBO NA ISHALLAH KWA UWEZO WA ALLAH ATAKACHOJAALIA NITACHANGIA.

    TUNAJUA HALI YA NYUMBANI ZANZIBAR SIO NZURI ,DHULMA IMETAWALA KILA KONA ,KWA HIO TUNATAKA KUIONDOA DHULMA HII ILIODUMU ZAIDI YA MIAKA 40.

    NAWAOMBENI WASIMAMIZI WA MICHANGO HII,MJITAHIDI SANA MUWE WAANGALIFU ,PESA INA IBILISI MBAYA.

    TUNAOMBA, WAHUSIKA TU NDIO WASHUGHULIKIE JAMBO HILI NA WAO NDIO WAZIFIKISHE PESA ZOTE KUNAKO HUSIKA NA SIO KUPITISHWA KWA WATU WENGINE.

    ISHALLAH ,MUNGU ATUJAALIE HUU NDIO MWANZO WA KUIJENGA UPYA ZANZIBAR YETU-AMEEN.

  • kitamli

    poa basi addil tupo pamoja letu sote hili.

  • mpapani

    Sisi sote tunaosoma hii mitandao, huwa tunajuwa lipi jema na lipi sizuri kwa jamii yetu. suala la kuchangia michango ni katika masuala ya hiari halazimishwi mtu ni moyo wa imani ya kutowa ndio muhimu.
    Mimi naona kila mtu akisha soma akafikiri kidogo anajuwa kwamba hili ni jambo jema haina haja ya kuchukua muda mrefu kuliwaza ama kuhoji kama hizi fedha vipi ama vipi, muhimu kuwa na moyo wa kuwaamini wezako tu.
    Mrfrost umeandika jambo la muhimu sana, juu yakutuma fedha kwa njia ya international bank, hii inamashaka kidogo kwa hilo nakuunga mkono bila shaka yeyote kwa maoni yako.
    lakini hili la Western Union nalo linamatatizo kama alivosema Ashkh ni kweli kabisa maneno yake yapo juu ya mstari hakukosea kabisa.
    Hebu tuangalie suala la Said Makka. hili halina dosari yeyote ile kama mtu atapenda kutumia kwa hiari yake, suala la harama isiwe kikwazo ni bora hizo fedha zimetumwa kwa wakati muafaka,tukiangalia hizi harama utaona kwa wale wanaoishi nchi za ngambo, mara nyengine ni vigumu kwa wao kwenda bank lakini Said unainuwa simu na kumpigia wakala wake kwa hivo hizo harama zinafidia nauli ya bus fare na wakati.
    tusifanye hesabu ya madole sana, tukaharibikiwa na hapo hapo kuna faida nyingi kwa mmakka hata kama huna nafasi ya kwenda bank upo mbali, ukimwambia anaweza kutuma (advance)kwa hivyo tusindike hasara tu za mmakka pia tuandike faida ya kutumia kwa mmakka.
    kwa kuwa 2+2+2 zitakuwa nyigi, hio ni biashara. kwetu muhimu njia ipi ya urahisi na ipi mtu atapenda kutunia, ili zifike kwa walengwa,kama njia hio haitokuwa na matatizo kwa mwezetu kutumia katika kutuma fedha isiwe kikwanzo.

  • mrfroasty

    @Addil,

    Honestly, mimi ni mtu wa sayansi naweza kwambia kuwa risk iliopo ni reasonable.Kwa maana ya kuwa jambo unalochangia lina uzito zaidi, kuliko mchangiaji kupoteza mchango wake.Kwa maana ya kupoteza 25gps huwezi kuanguka kimaisha au akafa njaa.Wakati kutokuchangia maana yake ni kuwaacha watu wa mashamba kutofikiwa na habari nyeti ya suala hili.

    Kwa kweli kueka khofu ya kuibiwa 25pnds ni kujichanganya na kuturudisha nyuma.Hakuna shaka kuchangia kitu kuna risk ya kuwa mchango unaweza usifike, hii inafahamika.Lakini tujiulize…MUWAZA wameshatekeleza makongamano mingi tuu ambayo matunda yake sote tunayajua, na hii ya SUK ilikuwa huwezi kuepuka.Kufanikisha mema yote yanayosimamiwa na MUWAZA, ni wazi kuna gharama hapo na walipaji ni wenyewe wazanzibari na wazalendo wa visiwa.

    Kila zuri lina gharama zake, kutengeneza matangazo ya radio haiwezi kuwa ni bure.Hivyo nashauri tukaendelea kuhamasisha kuchangia na kujadili mafanikio mara tuu mchakato huu utapomaliza.Kuliko kudili na khofu za kupotea mchango.

    Mwisho kwa kumalizia, mimi pia personally nimechangia kama mzalendo mwengine yoyote kwa kupitia data hizo hapo juu.Na wala sina hofu yoyote, pengine hii hofu ni kitu personal.Nashauri ukawasiliana na uongozi wa MUWAZA, au ukatuma barua kwenye inbox ya Administration mjadala huu wa khofu yako na uaminifu wako juu ya michango….you never know.


    @Wote
    Kutakuwa na feedback baadae juu ya suala hili lilivyokwenda, mp3 ya tangazo hilo liko swafi kabisa tumeshatumiwa sample ambayo iko kwenye matengenezo ikimaliza itawekwa hapa kwenye mtandao.

  • ashakh

    Ninawazo moja wazalendo.

    Ikifika kesho,Inshaallah, ikiwa wale wazalendo vindakindaki hatuja wasikia, napendekeza tutaje majina. Hii ni kutokana na umuhimu wa suala lenyewe.Kwani siku zinasogea. Hichi ndio kipindi mnasaba kabisa.

    @Adil
    Pendekezo nikuwa mzalendo washirikiane na MUWAZA kulidhamini hilo tangazo. Hapo tutaweza kujenga imani kwa vile MUWAZA wameshafanya mambomengi ya kifedha. Ndio ukaona account inayotumika ni ya MUWAZA.

  • kitamli

    kwani vipi tena jamani haya mambo?watu si washafahamiana kilichobakia ni kwenda kutuma hizo fedha kwenye account ilotolewa hapo juu,naona kama tunarudi tena kwenye mjadala wa mwanzo.
    mie binafsi bado sijatoa nilikuwa nimepanga kesho inshallah nende town nikaziingize ndo nafasi yangu.naona tusiwaconfuse watu kama account ishatolewa haina haja ya kwenda kwa said mmaka ninavyohisi mie,halafu tena zitolewe kwa pamoja zitumwe kwa huyo mmaka at once au mnaonaje? atakaepata wasaa kesho inshallah akatume na atakaekuwa hajapata mda amjaribu hata rafiki yake.kwani hao walotangulia kutoa wametumia njia gani? pia napenda kujua kwa ndugu zetu walokuwapo canada,states n.k ambao wangependa pia kutabaruk wao watatumia njia gani? na ni wazanje wenzetu.

  • Administrator


    Tangazo inshallah litaanza kurushwa kuanzia Monday na tangazo litaendelea kutolewa kwenye radio hadi mchakato wa kura umalizike.

    Shukurani kwa michango yenu.

  • ashakh

    @Kitamli

    Waliopo UK wao watatumia hiyo account number na sort code yake.

    Walio nje ya UK wao watatumia swift code(internationa bank). Hapana cha kujichanganya.

    Tunaomba wazalendo waharakishe kutoa hicho walicho jaaliwa. Si lazima kiwe cha maelfu au mamia, hata cha makumi kitatusaidia. Na kwa yule mwenye wasiwasi, nimepata ahadi kuwa hata kesho akhera atakwenda kikuta kile alichochangia.

    @mrforasty
    Ahsante kwa kuivisha mambo. Najuwa kuna wengine wanasubiri waje wapakuwe. Wakati hakuna anayetaka kupakuliwa, kila mtu kaingia jikoni mwenyewe. Huo ndio uzalendo,ushirikiano ndio silaha pekee.

    Wawekee wazalendo uhondo wauone.

  • ole

    SHUKURANI.
    Ahsanteni sana wachangiaji wote ambao mumechangia japo kwa mawazo kulifanikisha hili. Sote tunaelewa kwamba mwanzo siku zote ni mgumu lakini baadae matunda yake yataonekana.

    Naamini kuna wengine watakuja kujuta na kujiuliza kwa nini hawakuchangia jambo zuri kama hili ? Inshallah mola atatupa ufahamu ili tujuwe umuhimu wa hili.

    Nasema bado wakati tunao, tuwatie moyo Wazanzibar wenzetu ili waone kwamba hata wale wasio kuwepo nyumbani basi roho zao na mioyo yao bado ipo Zanzibar.

    Tuelewe kwamba michango yetu haitopotea ovyo, bali itajenga yale tuliokusudia kwa Nchi yetu na watu wetu.

    Hatuna budi kusimama kifua mbele na kujilabu kama sisi ni Taifa la Kizanzibar. Mimi binafsi nafarijika sana nikiitwa Mzanzibar.

    Mwisho nawapapa hongera za dhati kwa uongozi wa Mzalendo, kwa kweli jina limesibu. Naomba alopendekeza jina hili basi anahitaji pongezi na zawadi kwa hilo.

    Nimategemeo yangu kuna siku nitajikumbushia ule wakati niliokuweko shule kwa kulihakiki hili jina la MZALENDO ili tupate kuona ni jinsi gani jina hili lilivyofanikiwa. Kwa wale wanafasihi, watanifahamu niko na maana gani.

    Samahanini najua humu kwenye mtandao wamo watu wa fasihi, lakini mimi nitajikumbushia licha ya kwamba nimeihama kwenye fani hiyo, lakini kujikumbusha sio mbaya, kwani mazoea yana tabu sana.

  • Salmin Kiluwa

    Kwanza huu ni ugomvi wa ndugu sina tabu nao. La pili nashauri kwamba ili kuweka transparency ni uzuri MUWAZA UK kila wiki ikatoa hesabu ya huu mchango ulipofikia
    Ahsanteni
    Kiluwa.

  • abu

    Mie nadhani kuwepo watu kama BANDA ni muhimu sana ktk kuleta changa moto za kutekeleza mambo ambayo MUWAZA wanakusudia kuyafanya, viongozi wa mzalendo hakuna haja ya jazba nadhani hekima itumike zaidi ktk kuwaelimisha watu pale wanapokuwa na mashaka au wasiwasi juu ya jambo llte. Baadhi ya wakati mtu sio kwamba hakuamini anapohoji bali huwa anataka kujiridhisha nafsi yake juu ya kile anachokichangia.

    Mimi kwa upande wangu na unga mkono idea na tuko pamoja ktk hili. Allah akinijaalia natarajia kwenda unguja siku ya tarehe 31/07/2010 kwa ajili ya kusema NDIO.
    Wahusika wa hii michango nigeomba maelzo kuna utaratibu gani kwa wale waliopo hapa nchini ikiwa wanataka kuchangia au hii ni kwa ajili ya walio nje peke yake, maana na sisi wengine tungependa tuwe ni sehemu ya kusaidia kujenga Znz mpya.

    • mrfroasty

      Kama uko Zanzibar wasiliana na Shk Ally huko nyumbani.Ni wazi kutuma pesa kutoka Zanzibar kuzipeleka UK, halafu ukazirudisha tena sauti ya radia Zanzibar haingii akilini…and very expensive too.

      Inshallah tangazo litaanza kurushwa leo, na mp3 final version nitaiomba na kuiweka usiku wa leo inshallah…

      Maasalaam,
      mrfroasty

  • mrfroasty

    Tangazo hilo inshallah litaanza kurushwa leo…update na mambo mengine yote yatafuatia baadae inshallah.

    Maasalaam,
    mrfroasty

  • Update kutoka Zanzibar

    Tangazo limeanza kutoka hits fm na zenj fm.Kesho litaanza kutoka radio istiqama, pemba.

    ally

    • Sala na Dua - Lumumba

      Asalaam aleykum

      Ijumaa ijayo tarehe 30/7 Jumuia za Kiislaam zitajumuisha Wazanzibari kwenye kiwanja cha Lumumba kwa sala na dua kuiombea Zanzibar kheri, fanaka na mafanikio ya kuwa ya maoni na SUK.

      Jumuia hizo safari hii zimeshindwa kutumia viwanja vya Maisara kwa sababu ya gharama kubwa. Lakini hata huko Lumumba nako kunahitajika msaada wa Kiredha kwa hivyo wale wenye uwezo wanaombwa watabaruk kwa haraka iwezekanavyo.

      Wasalaam
      Yussuf

      • Update ya Harambee

        Update:
        ASA

        Katika acc. ya MUWAZA zimetolewa leo £135 lakini wameahidi watazijaliza zifike angalau £ 200 na watampelekea Ally Saleh.

        WSL
        Yussuf

  • ashakh

    Hongera kwa MUWAZA na WAZANJE nimesikia tangazo lenu.

    Sasa ukweli ukidhihiri uongo hujitenga. Number one Saleh Ramadhani Ferouz. Number two Juma Duni Haji. Number three MUWAZA na number four WAZANJE. Serikali ya umoja tayari imeundwa.

    Penye nia ipo njia, na hakuna lisilo wezekana. Mchango umefanyika, tangazo limetoka. Aliyekuwa hakuchangia pia kasikia. Hata hivyo ikiwa wako waliobakia, wasione wamechelewa kutoa michango yao. Account ipo pesa zitahifadhiwa. Huu ni mwanzo tu, MUWAZA ina mengi ya kufanya baada ya kura ya maoni kufanyika.

    Miongoni mwao ni kusimamia uundwaji wa serikali yenyewe, kutoa elimu kwa viongozi na wananchi juu ya uendeshaji wa serikali ya umoja, kukinga kurudi tuliko toka hasa kipindi cha uchaguzi mkuu, kama ilivyopendekezwa na wasomi wengi tunahitaji 3rd party, hivyo MUWAZA inastahiki kuwa THIRD PARTY katika serikali ya umoja.

    Shukran Sh Yussuf kwa usimamizi na mchango wako wa kutupatia ujumbe huu. Pia hapo uliposema, nakariri:
    ” Katika acc. ya MUWAZA zimetolewa leo £135 lakini wameahidi watazijaliza zifike angalau £ 200 na watampelekea Ally Saleh.”

    Sasa wale waliokuwa na wasiwasi wa michango watajiuliza ninani hao watakao jaliza? Pia unaweza kuingia vichwani mwao zimeingia £135 zimetoka £200, jee MUWAZA inafanya biasharagani hata ikapata faida kiasi hichi. Yaani pesa imeingia wiki moja tu inatoa faida ya 50%!!!

    Mwisho namuomba MUHIMU & Co walete mchango wao.