KUWEKEZA KWENY MRADI WA KUNUNUA MELI

Written by  //  08/02/2012  //  Matangazo  //  9 Comments

KUNA RAFIKI YANGU AMEAMUA KUWEKEZA KWENYE SEKTA YA USAFIRI WA BAHARINI, KWA KUTAKA KUNUNUA MELI YENYE UWEZO WA KUBEBA ABIRIA 1000 NA MAGARI YASIYOPUNGUA 56 AMBAYO ITAFANYA AFARI ZAKE KATI YA UNGUJA, PEMBA NA DAR. TAYARI AMESHACHUKUWA MKOPO KWENYE BANK MOJA HAPA NCHINI KIASI CHA TZS 2.5 BILIOINI. ANATAFUTA MTU AU WATU WATAKOKUWA TAYARI KUWA PAMOJA NAE KWENYE KITEGA UCHUMI HICHO KWA KUCHANGIA MTAJI WA TZS 500 MILIONI, YUKO TAYARI KUTOA ASILIMIA 30% YA UMILIKI KWA WATAKAO CHANGIA KIWANGO HICHO, PIA WATAKUWA NI SEHEMU YA UONGOZI WA COMPANY HIYO. KAMA UNAYE MTU/WATU AU WW MWENYEWE WAKO/UKO TAYARI NAOMBA TUWASILIANE KUPITIA NAMBA HII 0773190110.

9 Comments on "KUWEKEZA KWENY MRADI WA KUNUNUA MELI"

  1. kassem 09/02/2012 kwa 10:48 mu ·

    Ni wazo zuri ambalo mimi siku nyingi nimekuwa nikiwafahaisha watu. Lakini swahiba wako inaonekana hayupo serious na hili jambo. Unapofanya jambo kama hili inatakiwa uwe na matanganzo rasmi na ujulikane wapi unapatikana.

    Lakini kinacho nipa wasi wasi kuhusu hicho kima cha pesa ambacho chote amekipata kwa mkopo, mkopo ambao hautokosa kuwa na riba yake. Mathalani ningesikia Baharesa ameleta boti nyengine mpya na ametanganza kuuza hisa hapo kidogo ningekuwa na moyo wa kuamini.

    Hata hivyo mimi nahisi wazo ni zuri sana sana na hizi ndizo njia ambazo wenzetu wanatumia. Kwa hiyo tunaomba kujuwa hizo hisa ziko vipi? unaweza kununuwa kuanzia kiasi gani?

    ahsante

  2. Ashakh (Kiongozi) 10/02/2012 kwa 6:54 mu ·

    Mimi sina wasiwasi nalo ni sawa kabisa na niko tayari. Hii initial pale tutakapokutana tunaweza tukachangia mengi pengine hata uongozi unaweza kcuhukuliwa.

    Suala la riba halina mashaka kwa benk muhimu ni kuwa taratibu za kuanza kujipanga na kuitangaza.

    Wazo halianzi na watu wengi, siku zote huanza na mtu mmoja. Baadae ni watu kulichukuwa na kuliendelea.

    Nitapiga hiyo namba ya simu, halafu Bw Makame Ame nitakuletea hizo taarifa. Unakumbuka tuliwahi kuzungumza suala hili.

  3. abu 10/02/2012 kwa 12:52 um ·

    kassem@
    nimeweka namba yangu ya simu kwa makusudi ili mtu ambae anataka kujua zaidi tuwasiliane na mm niko tayari kumuunganisha kwa huyo mtu a kumpa kila aina ya taarifa anazozitaka. Huwezi kutoa kila kitu hapa ndio maaa nataka mtu tufaye mawasilaio ili kuwepo kuaminiana maana hizo pesa sio kidogo.

    Unaweza kuniandikia kwenye sirabm@yahoo.com mimi nitawaunganisha kwa huyo muhusika mwenye mali hasaa.

  4. Rocket 11/02/2012 kwa 3:17 mu ·

    Ni mpango mzuri na itakuwa vizuri kama kutakuwa na uwezekano kupatikana hisa ndogo ndogo za kiasi cha alau dola 5,000 ili wengi waweze kuekeza, lakiniwawe Wazanzibari tu ambao ni pamoja na Zanzibar Diaspora.

  5. sinalawy 15/02/2012 kwa 9:24 mu ·

    Invyotakiwa ni kuonesha portfolio ya hiyo biashara, total capital kiasi gani, makadirio ya matumizi ya kawaida kila mwezi kiasi gani, makadirio ya mauzo ya kila mwezi na pia makadirio ya kukuwa kwa biashara angalau kwa kila mwaka au miaka fulani n.k. ni mfano wa information kama hizi ndio zitozoleta mvutio wa mwenye kutaka ku-invest.

  6. abu 16/02/2012 kwa 6:40 mu ·

    Sinaalawy@ kwenye hii post imewekwa namba ya simu kwa lego la kwamba kwa yule ambae yuko interested basi tuwasiliane ili aweze kuonyesha kila kitu, kwa vile hii io PUBLIC COMPANY huwezi kuweka kila jambo hapa. Nimeweka email na namba ya simu ili tuwasiliane tupeane tarifa za ndani zaidi za hii project.

    Kwa yyte yule ambae yuko tayari tafadhal;li tuwasiliane kwa namba iliyopo hapo juu au kwa email iliyoweka hapo.

  7. Rocket 16/02/2012 kwa 7:45 um ·

    Ni sawa maneno yako. Kama unataka kujua zaidi basi wasiliana nao wahusika. Mimi nimewasiliana na brother wangu kama yuko interested basi atakuwa ameshawasiliana nao huko Zenji.

  8. aslam 20/02/2012 kwa 11:54 um ·

    salamu wazanzibar, kwa kweli ni wazo zuri lakini lisifanyike kiholela holela , nakumbuka ile mali iliyo dhama baada ya matatizo mwisho wamiliki wakaanza kugombana walioshiriki wote wanasema mie siyo meli yangu na huyu siyo yangu na huyu siyo yangu mwisho wote wameshtakiwa na kama munavyojuwa nyumbani bado hatujajirekebisha kwa yote yaliyo tufika bado bandarini kuna matatizo wanaweza watu wakafanya uzembe ikabidi wawezekaji wa meli mukawekwa ndani kwa uzembe wa watu wengine , na vile vile ikuwepo uchunguzi wa kutosha wa hiyo meli itakayo nunuliwa kwa sababu upo udanganyifu mwingi tu wa kuwapashika meli isiyo faa hasa wageriki sio waaminifu wanaficha ukweli , kwa hivyo ninamuomba muhisika atuwekee maelezo kamili hapa kwenye mtandao tuutasmini na tuangalie tuone vipi tutaweza kuchangia na kuwa ni mmoja wa wamiliki , na hisi kukikuwepo watu wakachangia na kama watapata asillimia 50 na alie chukuwa mkopa 50 itakuwa uzuri dhaidi kwa sababu kutakuwa na wamiliki wengi italeta kupunguwa uzembe , ni wazo zuri lakini linataka umakini kamili isije ikageuka mie sie mie sie .

  9. Embesakua 21/02/2012 kwa 4:24 um ·

    Wazalendo me nadhani hapa home saiv biashara ya meli ni nzuri lakini tuangalie kwa upande mwengine demand kubwa saiv sio meli jamani. pesa hizo mlonazo nnaweza kuweka hata viwanda vidogo vidogo, pia mnaweza kuweka zizi kubwa la wanyama kama ngombe na wakaproduce maziwa mengi sna na yakatumika km yogurt na matumizi mengine mengi sna.

    Tatizo kubwa hapa kwetu sio meli ni chakula, kwa hio tuwekeze kwenye vyakula vitu km vinywaji pia ni big deal, kwenye biashara ya meli naona wapo wazalendo ambao wameshajitahid kwa upande wao
    Pia mnaweza kuwekeza kwenye retails ya super-market kubwa kubwa na baade biashara ikikua mnaweza kudiverisify kwenye business nyengine.

    Wazalendo tuangalieni mahitaji ya jamii ni lipi la muhim kula au kusafiri na lipi linauzito?

    @ Sinaalawy
    Umeongea kitaalam zaidi mchango wako unapaswa kufanyiwa kazi. na wala sidhani kwa kuweka numba ya simu unaweza kutosheka na majibu utakayoyapa.

    Nausia tu kwamba biashara isifanye borrowing nyingi kuliko capital na asset zake, More borrowing more risk

    @Ashak (Kiongozi)
    Sijakufaham unaposema riba haina ttzo, ukipata muda nieleze kwa uhalisia wake.

Comments are now closed for this article.