Mkono wa Pole kutoka ZAWA UK
Written by Stonetown (Kiongozi) // 05/02/2012 // Kitaifa, Matangazo // 9 Comments
Assalamu alaykum,
Kwa niaba ya uongozi, wanachama na wazanzibari kwa ujumla, Jumuiya ya Zanzibar Welfare Association UK, inatoa mkono wa pole kwa aliekuwa mwenyekiti wa ZAWA UK na pia ni mlezi wa jumuiya hiyo kwa kwa sasa maalim Abdallah Ali na kifo cha baba yake mzazi Maalim Ali Juma, marehemu atazikwa leo huko Zanzibar.
Twamuomba Mola amughufirie madhambi yake mja wake huyo na amuingize katika pepo zake Inshaallah. Vile viletunamuomba Allah awape subra wafiwa wote katika kipindi hiki kigumu cha msiba huu.
Mwenyekiti ZAWA UK
Hassan M Khamis







9 Comments on "Mkono wa Pole kutoka ZAWA UK"
INNAA LILLAAHI WA INNAA ILAYHI RAAJI’UN
TUNAMUOMBA ALLAH AMGHUFIRIE MAREHEMU NA AMREHEMU NA AMPE KAULI THABIT NA AMPE MAKAAZI MEMA PEPONI, NA AWAPE SUBRA WAFIWA WOTE…AMIN.
Inna Lillah Wainna Illayhi Rajioun
Nachukua fursa hii pamoja na familia yangu kutoa mkono wa pole kwa Wafiwa wote na hasa Mzee wetu Maalim Abdalla.
Tunamuombea marehemu alazwe peponi – Ameen
Pia, tunawaombea Wafiwa wawe na subra katika kipindi hichi kigumu cha masiba/
INNAA LILLAHI WAINNAA ILAYHI RAAJIUUN
TUNAMUOMBA MWENYE EZIMNGU AMUEKE BABA YETU MAALIM ALI PAHALI PEMA
PEPONI, AAMMIN
NA NAWAOMBEA SUBRA JAMII YA MAALIM ABDULLAH.
INALILLAHI WAINA ILAHI RAJEEOUN NASI TUNATOWA MKONO WETU KWA WAFIWA.
WAKATI HUWO HUO TUNAOMBA PANAPOTANGANZWA MSIBA UELEZWE KIDOGO
KAMA VILE MHR MAALIM ABDULLA AKIKAA MTAA FULANI AU KASOMESHA SKULI FULANI KWENYE MIAKA FULANI, PENGINE TUNAMJUWA KWANI WAZANZIBARI SASA TUMETAWANYIKA KILA PEMBE YA ULIMWENGU TUPO.
NATANGULIZA MSAMAHA IWAPO NIMEKOSEA .
INALILLAH WAINNA ILAYHI RAJIUUN
TUNATOA MKONO WA POLE KWA WAFIWA, MOLA AMUHIFADHI KWENYE
MOJA YA JANNAT ZAKE AMIN.
MAALIM ALI ALIKUWA NI MTU MTARATIBU SANA KWENYE UHAI WAKE, ALIKUWA
AKIISHI WETE, SELEM MPAKA KWENYE MIAKA YA 1975/78 NADHANI
BAADA HAPO ALIHAMIA UNGUJA KWENYE IDARA YA MICHEZO [MENEJA WA UWANJA WA
AMANI] ……………………………………………………..
INNA LILAAHI WA INNAA ILAYHI RAJIUUN.
Allahumma ja’alhu fida’a lahu mina nnar. x 3
allahumma ja’alhu fakaaka lahu mina nnar.x3
Wa min adhabil qabri wa min ahwaali yawmil qiyaamati, waghfri lahum warham wajma’a3naa maahum fi-daari karaamatik wamustaqar rahmatika ma’a e3baadika assalihyna wa hizbikal muflihyna.
Allahumma dkhilhul jannat ma’al anbiya’a walmuralyn.
Poleni nyote muliohusika na msiba huu, M/mungu atawapa subra wa selwan.
AMEEN
MCHONGOMA
nami sina budi kutoa mkono wangu wa pole kwa mfiwa. Sifa za Maalim Abdallah zimeenea jiji zima la London kutokana na malezi mazuri aliyopata. Bila ya shaka hili litakuwa pengo kubwa katika maisha yake.
Hivyo ni kuhimisha ustahamilivu, na kushukuru M/Mungu tukijuwa kuwa ni kifo ni moja kati yanguzo za maisha. Tunamtakia Maiti huyu khatma njema.
Ina lillah waina ilaihi rajiun,tunatoa mkono wa pole nami pia,M/Mungu amlaze mahali pema baba yetu ameen.
Sk. Abdulla tustahamile msiba Mungu amlaze pema mzee wetu, Amin.
- Master-