MSAADA WA HARAKA KWA NDUGU YETU
Written by Junius // 10/08/2010 // Matangazo // 2 Comments
Wadau nimeikuta hii kwa Mapara naomba kuiwasilisha…anayempenda Mungu na Mtume msaada tafadhali.
Karibuni tumepokea ombi kutoka Hospitali ya Mnazimmoja na Afisa wa huduma za ustawi wa jamii, Bi Salama kwamba kuna mtoto mmoja mwenye umri wa miaka mitano kutoka Micheweni Pemba ambae ana matatizo ya ugonjwa wa macho.
Mtoto alifikishwa Hospitali ya rufaa Mnazimmoja kutoka Pemba na ametazamwa na Madaktari, Mnazimmoja na kuamua kumpeleka Muhimbili kwa matibabu zaidi kwa sababu amepata uvimbe kwenye jicho lake la kushoto – left eye tumour.
Kwa bahati mbaya familia yake haina uwezo wa kugharamia gharama za safari, matibabu pamoja na kujikimu kwa kipindi watachokuwepo Dar kwa matibabu.
Zanzibar Outreach Program baada ya kupata taaarifa hizi imewasiliana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ambao wamo katika utaratibu wa kumsaidida mtoto huyu. Hata hivyo ZOP tumeona kwamba tunalo jukumu la kusaidia familia na kwa hivyo imejitolea kuchangia Shilingi Laki mbili ukijumlisha na msaada ambao utatolewa na Wizara na kwa ujumbe huu tunakuomba ujumuike nasi katika kumchangia mtoto huyu kwa kuwasiliana na
Dr Naufal Kassim 0773047979,
Dr Kassim Faki 0777416945
Afisi za ZOP +255245500711)
BANK DETAILS
JINA LA AKAUNTI: ZANZIBAR OUTREACH PROGRAM
AKAUNTI NO. : 021108 01008
JINA LA BENKI: PEOPLES BANK OF ZANZIBAR
TAWI : MALINDI
SWIFT CODE: PBZATZTZ
Kwa maelezo zaidi kuhusiana na ZOP ingia kwenye tovuti zanzibaroutreach.com
Dr Naufal Kassim Mohammed
ENT, HEAD & NECK SURGEON
ZOP EXECUTIVE SECRETARY





2 Comments on "MSAADA WA HARAKA KWA NDUGU YETU"
A/a
Tafadhali mtoa mada angebainisha wazi diagnosis ya huyo mgojwa kwa ridhaa ya wazazi wake kwa vile hiyo ni siri yao na daktari wake.
Kwa kuchangia ikiwa hiyo eye tumuor ni retinoblastoma ambayo ni common kwa watoto basi haina haja ya kupelekwa muhimbili wala kungojea huo mchango maana kila dakika hiyo tumour inazidi kuspread na kupitia optic nerve itaishia kwenye ubongo na hapo matatizo zaidi yatajitokeza na mwisho wake uhai unapotea.
msaada wa haraka ni kusave life kwa hiyo uwamuzi mzito inabidi uchukuliwe na wazee na kupewa ushauri nasaha ili wakubali jicho hilo liondolew kwa kufanyiwa operation ya enucleation ambayo inaweza kufanyika hapohapo pemba{ikiwa dr iddi bado yuko pemba}hoyo itamsaidia mtoto kuishi na kuweza kuendelea na maisha yake na jicho moja na kupatiwa prosthesis
Kwa kuchelewa kufanya hiyo procedure tunaweza kumpotezea maisha yake huyo mtoto
Bahati mbaya kwa mazingira ya kwetu mtoto anapokuja na matatizo hayo mara nyingi uvimbe unakuwa umeshaspread na inabidi ushauri nasaha na maamuzi ya haraka kuchukuliwa kusave life
Kwa nchi zilizoendelea excision ya tumuor ihafanyika na kufuatiwa na cytotoxic drugs na kuweza kusave jicho na life pia .Wenzetu wanawahi kumpeleka mtoto mapema kwa daktari wakiiona mboni inaanza kuwa nyeupe kwa uchuguzi wa haraka na matibabu
WAZO ZURI JALUO
LAKINI NADHANI WAHUSIKA WALISHAPATA RIDHAA KUTOKA KWA WAZEE NA KAMA HAWAJAPATA BASI WACHUKUWE WAZO LAKO.
NIA NJEMA HUJENGA.