TAARIFA YA MAHOJIANO KATIKA (VOA)
Asalamu Alaykum.
Napenda kutoa hii taarifa kwenu kwamba Dk Harith Ghassany amefanya mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya Voice of America (VOA) na mtangazaji Abdul-Shakour Aboud pamoja na Professa Alwiya Omar na Dkt. John Mtembezi Innis kuhusu namna ya kuandika kitabu.
Lakini pia amefanya tena mahojiano menginge juu ya kitabu kilichotungwa na Dk Harith kiitwacho Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru! Kwa hivyo tunaomba msikose kusiliza matangazo hayo ambayo yatarushwa hewani siku ya JUMAPILI inshaallah saa 1:30 usiku saa za Afrika Mashariki au mwa maneno mengine saa za kwetu.
Kwa taarifa zaidi kwa wale walio ndnai ya nchi yetu ya Tanzania muungano wa nchi mbili huru yaani Tanganyika na Zanzibar tunapenda kuwajuulisha kwamba matangazo hayo wanaweza kuyapata kupitia Radio Free Africa ya Tanzania bara na Coconut FM ya Zanzibar ambazo hujiunga moja kwa moja.
Naomba kuwasilisha taarifa hii na pia napenda kutoa shukurani kwa Dk Harith kwa na wenzake wote walioshiriki kwa njia moja au nyengine kuandaa kipindi hiki ambacho ni muhimu kwetu na taifa letu.
Salma Said.





One Comment on "TAARIFA YA MAHOJIANO KATIKA (VOA)"
Shukurani Bi.Salma tutayafutilia kwa karibu katika VOA ili kupata yaliyojiri.
mrfroasty