Tunakusanya Computer zisizotumika

Written by  //  20/08/2010  //  Matangazo  //  12 Comments

Salam

Tumeanzisha mpango wa kukusanya computer ambazo hazitumiki tena. Lengo ni kuwasaidia ndugu zetu huko nyumbani.

Hivyo kwa yule mwenye nayo na ikawa yuko radhi kutupatia, basi tunaomba afanye hivyokwa kutujulisha kupitia namba hizo hapo chini.

Wenyewe binafsi tutafanya juhudi ya kuzipitia na kuzikusanya na mwisho kuzifanyia matengenezo na kuzituma huko nyumbani.

Tunaomba ushirikiano wenu.

Wasiliana nasi kwa namba hizi za simu:

07508016265, 07957654192, au 07535656346

12 Comments on "Tunakusanya Computer zisizotumika"

  1. Ghalib 20/08/2010 kwa 11:34 um ·

    A.laikum
    Computer hizo munasaidia kivipi ? Munazigawa tu mitaani au munapeleka mashuleni,au hospitalini au katika idara fulani ? elezea muhusika ili watu waweze kusaidia,

  2. mohamed soud 21/08/2010 kwa 12:07 mu ·

    A. alaykum,
    Ama baada ya salamu mtoa mada ningependekeza uweke nyinyi wakusanyaji muko nchi gani ili wazalendo waweze kuwapata kwa urahisi kupitia hizi namba zenu za simu pamoja na majina yenu pia.
    ahsante

  3. mseto 21/08/2010 kwa 4:32 mu ·

    Mnaweza kutujulisha nyinyi ni nani na ni nini lengo na azma ya mradi huo?
    Shukran

  4. ashakh 21/08/2010 kwa 5:44 mu ·

    Hawa jamaa ni waokotaji takataka. Musishtuke kusikia zikitajwa hizo computer, ndionaona kila mtu karuka zitafanya nini na maswali mengine kibao.

    Nilivyofahamu ni computer ambazo hazitumiki, naziita “takataka”. Badala ya kuzitia kwenye bin ni just kuwajulisha tu. Sio muanze kuuliza zitapelkwa wapi, atasaidiawanani na masuala mengine.

    Hizi namba ni namba za wakaazi wa UK.

  5. Kimewaka 22/08/2010 kwa 1:22 mu ·

    Ndugu zangu nawaomba kama mnakusanya computer mbovu!huko ulaya, kusanyeni mzisage halafu muziuze kwa company za recycle huko huko itakua ni jambo zuri sana. kwani nyumbani znz kuna taka taka za kupita mpaka na za kutosha hasa makomputer mabovu hata vya kuyafanya hatuna ni uchafu umetapakaa katika visiwa vya zanzibar hata pakutupa hatuna? kwa maana hio tunaomba msaaada wenu na nguvu zenu za hali ya juu kabisa kwani makorokoro ya friji,maredio,macroweve makomputer umejaa hatari kwa mazingira na kwa usalama wa kiafya. nadhani mwisho wake yatadhuru wanannchi wote wa znz.

    Lengo ni kuijenga znz kiserikali,kimazingira na kiafya sio kufanya jaaa la kila aina ya uchafu ulimwenguni.

    Nawasilisha

  6. Wamtambwe 22/08/2010 kwa 6:32 um ·

    Asalam Aleykum wazalendo,
    Mimi niku Ujerumani na nilikuwa na Mpango kama huo kuwasaidia baadhi ya Shule kule Pemba. Niliwahi kuzungumza na Kampuni ninayofanya kazi waliniahidi kunipatia komputa 30- 50 (Pentium IV). Baadae Kampuni ya Semens wakazichukuwa hizo komputa na wakanikatalia mimi. Kwa vile nimeshaahidi bado niko njiani kutafuta na huwa nanunua mojamoja nikikusanya. Tatizo kubwa hapa ujerumani niko peke yangu na sina mtu wa kushirikiana naye kwa hiyo tatizo kubwa litakuwa ni usafiri. Niliwahi kuzungumza na Mtanzania mmoja akanieleza niwasiliane na nyinyi. Jee jamani munamipango gani kuhusu Usafiri? Mimi mwenyewe ni nina hobie ya kuunda na Kutengeneza Kompyuta, Pendekezo langu jengine tunaweza kukusanya Parts za kompyuta halafu nyumbani tukaunda modei tunaouhitaji
    Kuhusu maneno ya Kimewaka sikubaliani nayo . Kweli kuna makrokoro mengi Zanzibar. Lakini jee ni nani anayefikiria kuzisaidia Skuli za Mashamba. Au ni skuli ngapi za mashamba ambazo zinamiliki angalau Komputa mmoja.

  7. Kimewaka 23/08/2010 kwa 1:19 mu ·

    @ Wantambwe
    Msimamo wako sikatai ni mzuri sana lakini kama wewe unaweza kufanya masuala ya kiufundi wa makomputa mabovu mimi naweza nikakupatia hata 500 huko huko zanzibar uzifanyie ukarabati ili ziweze kufanya kazi halafu uzipeleke huko mashamba na maskuli ya vijijini unguja na pemba kwa mujibu wa maneno yako kuliko kutuongezea mazagazaga na uchafu visiwani znz.

    Nawasilisha

  8. Wamtambwe 23/08/2010 kwa 12:01 um ·

    @Kimewaka
    Kama kweli unazo Hizo kompyuta tuekeane Ahadi ili mimi nije Zanzibe kwa ajili ya kuzitengeneza na kuzisambaza Maskulini. Lakini inabidi unieleze mapema ni Komputa zenye uwezo gani na Window gani inaweza kufanya kazi kwa ufanisi zaidi. Vile vile ningependa kujua ya kwamba jee zinazo modem au Network card kwa ajili ya kuunga kwenye Internet?. Lengo langu ni kuwa kila skuli tutakayowapatia iwe tumewaungungia atleast kwenye Local Network . Nijuilishe Sparepart gani nichukue
    Nasubiri jibu kutoka kwako
    Ramadhani njema

  9. zamko 23/08/2010 kwa 12:59 um ·

    wamtambwe mawazo yako ni mazuri sana, lakini hili tangazo la ukusanyaji wa hizi comp. jaribu kuwasiliana na ashekh,taymia. humu kwenye mzalendo admin.address zao zipo hapo juu mkono wa kulia au ashekh@mzalendo.net atakupa majibu

  10. scaba scuba 23/08/2010 kwa 7:37 um ·

    @@@wamtambwe@@@
    Nadhani fikra zako safi sana na kuhusiana na usafiri inategemea wapi unaishi hapo germany kwani mimi huwa napakia mzigo mara nyengine huko na kama unavyosema nikuwasaidia ndugu zetu kule nyumbani mimi nakuafiki zaidi …nijulishe mji ulio na tunaweza kuwasiliana kwenye e mail yangu z.nz@hotmail.com shukran sana

  11. Kimewaka 26/08/2010 kwa 1:27 mu ·

    @wantambwe
    kwa kweli hayo makomputer yalioko hapo znz ni kama nilivokueleza ni mabovu hayana window,card na hata kuwaka hayawaki ni ya kusagwa na kupelekwa ricycle, mana yamepigwa na mvua mpaka yameota mwani. zinafika computer 500.

    ndio maana nikasema musilete uchafu mwengine zaid mana hizi hatuna vya kuzifanya na hazifanyi kazi sasa kama wewe utaweza kuzitengeza hizi itakua ni jambo la busara muheshimiwa wantambweeeeeeeee.

    Nawasilisha

  12. Wamtambwe 27/08/2010 kwa 10:41 um ·

    Asalam Aleykum,
    Nafikiria katika mazungumzo yetu hatukufahamiana. Katika hilo tangazo hapo juu paliandikwa ” Tunakusanya Computer zisizotumika”. Pengine kutikana na kwamba muda mrefu niko nje Kiswahili kilinipiga chenga Kidogo. Mimi nilifahamu ya Kwamba ni Komputer ambazo Zinafanya kazi lakini mtu Haitumii pengine amenunua nyengine mpya na hii kongwe kidogo kaiweka. Computer kama hizi hapa Ujerumani Kuna siku Maalum huwa zinawekwa Uwanjani kama mtu unazihitaji unachukua wela mtu hakuulizi. Baada ya Siku mbili yale mabaki ndio linakujaMagari maalum ya Kuzoa mataka kuyaondoa. Mimi naweza kutengeneza Komputa lakini sio kuchokonoa. Mimi nachukua likizo wiki mbili au tatu nataka wiki moja kutengeneza hizo Computer, yaani kubadilisha part Zilizoharibika kuweka mpya, kuweka Software na wiki ya pili kuzisambaza hizo Cumputer wenyewe. Mimi naweza kutengeneza lakini siwezi kufanya miujiza, kama Computer imekaa mvuani mwaka mzima hata ukiirejesha kiwandani haifanyi kazi tena, hizo labda ufanye mabox ya kufugia Kuku. Mimi nakusudia Computer ambayo angalau unaweza kuweka Window XP. Chini ya hapo labda tuzigawe kwa chekechea. Ndio maana nilisema Kampuni yangu ninayofanya mwaka huu walibadilisha Computer 7,000 na waliniahia mwanzoni ya kwamba watanipatia angalau 30-50. Tatizo ni kwamba wao wana mkataba na Siemens, kila baada ya miaka 4 wanawafungia mpya na kongwe wanachukua wenyewe, sasa siemens ndio walionikatalia. Computer ninazotaka mimi iwe sio chini ya Pentium IV au uwepo uwezekano wa Ku upgrade kufikia Pentium IV
    Maoni yangu kwa wale wote ambao wanataka kweli kuwasaidia ndugu zao kule Zanzibar, Kuna muingereza mmoja aliwahi kusomesha Pemba kwa muda wa miaka, hivi sasa anakaa hapa Ujerumani na ameanzisha NGO maalum kwa ajili ya kusaidia maskuli kule Pemba na Unguja. Mkutano wa mwanzo utakuwa Hamburg kunako October mwaka huu. Baada ya mkutano huo nitatoa Tangazo tena kwenye ntandao huu kwa wale wenye hamu ya kusaidia na sio kufanya Biashara

Comments are now closed for this article.