TANGAZO LA KIFO
Written by salma // 27/08/2010 // Vifo // 5 Comments
HAKIKA SOTE NI WA ALLAH (S.W) NA MAREJEO YETU NI KWAKE.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia kwamba Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Harith Bin Khelef ametutoka leo majira ya alfajili huko nchini India alipokwenda kwa matibabu kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa ndugu yake ambaye tumezungumza naye amethibitisha habari hiyo lakini hadi sasa serikali haijatoa tangazo bado lakini bila ya shaka watatoa watakapokamilisha utaratibu khasa kwa kuwa suala hili linakhusu zaidi familia yake.
Mwenyeenzi Mungu amfutie dhambi zake na amuweka pahala pema inshallah.
Kufuatia kifo cha Mufti wetu hapa Zanzibar siku ya Jumanne gazeti la Annur tutatoa chapisho maalumu kwa kifo cha Sheikh wetu na kiongozi wetu huyo kwa hivyo kila mwenye mchango wake wa maelezo anavyomfahamu Mufti anaweza kuniandikia katika email yangu binafsi iitwayo muftiiy@yahoo.com na tutachapisha ikiwa ataweka jina lake au atataka jina lake lihifadhiwe tutaheshimu bila ya shaka.
kwa niaba yangu na familia yangu ya Al-Ghaithiy tunatoa mkono wa pole kwa wazanzibari wote kwa kuondokewa na kiongozi wetu na zaidi kwa familia ya Al marhum.
Naomba kuwasilisha
Salma Hamoud Said Al-Ghaithiy




5 Comments on "TANGAZO LA KIFO"
Innalilahi wainna ilayhi raajiuun… ALLAH amlaze mahali pema ndugu yetu ktk imani na mufti wetu wa znz.. ni msiba mkubwa kwa waznz…
ALLAH AMLAZE MAHALI PEMA PEPONI …AMIN
بسم الله الرحمن الرحيم
( يا ايتها النفس المطمئنة ارجعي الى ربك راضية مرضية فادخلي في عبادي وادخلي جنتي )
((صدق الله العظيم))
بقلوب مؤمنة بقضاء الله وقدره
نتقدم بخالص العزاء وصادق المواساة الى
أسرة الفقيد
لوفاة المغفور له بإذن الله تعالى
الشيخ حارث بن خلف
(كبير المفتيين في زنجبار)
تغمد الله الفقيد بواسع رحمته وأسكنه فسيح جناته
((إنا لله وإنا إليه راجعون))
Tunamuomba Mwenyezimuungu
Tunamuomba Mwenyezimuungu amsamehe makosa yake na ampumzishe pahali pema Amin.