Login



Fotos

Get the Flash Player to see the slideshow.

Migawanyo

Kumbukumbu

Sauti:Sikiliza mahojiano baina ya DW na Bakari Shamte.

  • Nani atakuwa mtetezi wa CCM kwa urais wa Zanzibar?
  • Shein, Bilal, Nahodha au Shamhuna, mtetezi wa CCM kwa urais wa Zanzibar?

Wakati huo huo, washabiki wa watetezi wanaowania kupata kibali cha uongozi wa chama tawala cha CCM kuwania nafasi ya urais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu wamefika mjini Dodoma kuwapigia debe watu wanaowaona wanafaa kukamata nafasi hiyo. Watu wanaotajwa na kuzungumziwa sana kuwa huenda wakachomoza kushinda, kati ya majina 11 yaliowasilishwa kwa kamati kuu ya chama cha CCM, ni Dr. Ali Shein, makamo wa sasa wa rais wa Jamhuri ya Muungano; Dr. Gharib Bilal, aliywahi kuwa waziri kiongozi wa Zanzibar; waziri kiongozi wa sasa wa Zanzibar, Shamsu Vuai Nahodha; na naibu wa waziri kiongozi wa sasa wa Visiwani Zanzibar, Ali Juma Shamhuna.

Othman Miraji alizungumza punde hivi na mmoja wa makada wa CCM kutoka Zanzibar waliofika Dodoma kushawishi wajumbe wa Halmashauri kuu ya taifa wamuunge mkono mtu wao: Naye ni Bakari Shamte…

 
Share and Enjoy:
  • Facebook
  • Twitter
  • Digg
  • MySpace
  • del.icio.us

13 maoni Sauti:Sikiliza mahojiano baina ya DW na Bakari Shamte.

  • muarab

    A a,naona baraka shamte amekuwa msemaji wa wazanzibari wote,hapanaona amechanganyikiwa gharib bilali ,sikuwa anatakiwa na wanzanzibari wote; bilali unamtaka wewe shamte pamoja namakada wa kisonge na baadhi ya wana ccm ,bilali sichaguo la wanzanzibar,kwani kama utafanya kura asilimia ngapi wana ccm ,na wasiokuwa ccm utaona ccm nirobo ya wazanzibar,sikosa wewe kumpigia debe bilali lakiniusiseme ni chaguo la wazanzibar hilo nikosa, nakutowa wasiwasi shamte mkwala wa bilali umemsaidia,huenda lolote likatokea, INSHALLAH TUSUBIRI KESHO, TUNAKUOMBA ALLAH UTUPE KIONGOZI MWENYE GHERI NASIE AMIN

  • spark

    muarab
    kusikia ni kitu kimoja na kuelewa ni jambo jengine sio wote wanomsikiliza mwalimu wanaelewa. mimi nimemsikia akisema 75% ya wanachama wa chama cha mapinduzi (CCM) wanamtaka Dr Bilal na sio Wazanzibari wote kama ulivyosema vinginevyo uwe uliweka utashi wako wa kisiasa. nibora umsikilize tena ili ujisahihishe.

  • kijini

    mimi naamini ukisomaaaaaaaaa ukiwa daktariiiiiiiiii kama hawa madaktari CCM wako wengisana hawa wengine wameishia humu humu wanaita fom 3 kujiendeleza sikweli hamna utasikia tu ametunukiwa shahada ya DR wa ZNZ wapo tu wanatowa macho kama dagaa lililokosa bizari Baraka Shamata jina lakwa wazee wake la mjini Bakari Shamte sawa mambohaya ya majina ya kujipiga ZNZ tumeyazoweya lakini kama hatakikujuwa sawa yeye na ndumila kama yeye watalia siku moja kama SALIMINI kwani sasa ndio anajuwa na anona kama ndani ya CCM hakuna anaye faa kwa ZNZ asante sana

  • Gumegume

    Muarab na spark; Huyu Baraka Shamte analilia njaa, bado ana mawazo ya kule nyuma kamando na ufujaji wa fedha. Katika kipindi cha Rais Amani hakuwa na kete…kwa hiyo mtazameni analilia njaa, ndio hawa wanaouza utu kwa kuganga njaa, hata hivyo anajihangaisha ataendelea na njaa yake mpaka hivyo hivyo, kutokana na kukosa shukurani na unafiki. Hata utaona amejifanya msemaji wa Wazanzibari. Ebu tumulize hao wazanzibari 75% wanaomtaka Bilal wako wapi? Wamemtuma lini? Au ndio kusema njaa yake imenchanganya? Sasa wanamzalendo ninaanza kupata picha kuwa hili kundi la akina Bilal ni kundi baya sana na ndio wanaotaka kuvizisha maridhiano. Tukumbuke tuwa Bilal nchi ya Kamando wametumisha ubaguzi mpaka na kuwafanya wazanzibari (Unguja na Pemba) wajione kama maadui kila mmoja kwa mwenzake.

    Sasa Baraka Samtee chukua ujumbe huu, InsaAllah Mwenyezi Mungu tunamuomba asiwe pamoja na nyinyi wa wenzenu kam nyinyi wanataka kuendelea ubaguzi na ufisadi miongoni wa jamii.Na wewe utaendelea na porojo tu huna lako; kwa sababu Mwenyezi Mungu ametakaza sana mambo hayo ya fitna, ubaguzi na kujifanya wewe ni bora. Ndugu yangu bado jembe unaliweza japo kulima mchicha wacha kusubiri kutia fitna kwa ajili ya kuganga njaa; kama umri ulifikia bado hujawahi kula ukashiba; Allah Alam. Wacha fitna zako na tafuta vitabu uhudhurie darsa, InshaAllah Mwenyezi Mungu akakutanabahisha ukaachana na fitna na ufisadi. Mungu itarini Zanzibar na Wazanzibari. Pia tunakumba uwatanabahishe wale wote wenye kiburi na chuki za kuendeleza fitna na ubaguzi miongoni mwa Wazanzibari

  • tahti zamba

    Ama kweli watu wanakuwa na ubongo kwenye vichwa vyao lakini huyu Baraka Shamte naona ana matope kichwani kwake.

    Anatwambia ikiwa mgombea wao hatachaguliwa basi kasi ya maendeleo itapungua. Kwani kuna maendeleo gani ya kujisifia Zanzibar ambayo yameletwa na Salmin au huyo Bilali badala ya kutia fitna, chokochoko zisizo na faida yoyote.

    Baraka Shamte funga mdomo huna mpya maana Dr. Bilali hatakusaidia chochote kama hao waliopita

  • Junius

    WAZALENDO KABLA SIJAMSIKILIZA KADA BARAKA MOHAMED SHAMTE NATAKA NIWADOKEZE ZA DODOMA ASUBUHI HII KUNA HABARI KUWA DR.SHENI AMEJIONDOA KATIKA KINYAN’GANYIRO CHA URAIS BAADA YA MASHAURIANO NA BOSI WAKE KIKWETE NA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI.
    HABARI ZAIDI NAULIZIA WATU WA JIKONI AU MPAKA KUCHE.
    J

  • depsis

    Ewe Mola wetu mtie nakama na kitahanani, umpeperushe nchi yetu aione paa tu na usimrudishe kutoka Dodoma yeyote ambaye ameweka nia ya kuifarakanisha Zanzibar yetu (AMEN)

  • sarhan salim

    salaam wazanzibar, junius washa utani ikiwa kweli hayo unayo yasema , na mafisadi kina salmin watarudi serkalini, zanzibar kutawaka moto , jamani hatari hiyo inatukabili yarabi kheri.

  • Big Boss

    Asalm alykum

    Huyu Baraka anachozungumza yeye ni kuwa Bilali anauwezo mkubwa wa kukiongoza Chama, kwa hiyo Wazanzibari tuamke huyo mpiga debe mkuwa aliekwenga kumpigia debe bilali ansema hivyo, kwa maana hiyo tukubali yeye aongoze chama lakini hana uwezo wa kuongoza nchi, anaeweza kuongoza yupo KURA ZOOTE KWA MAALIM SEFU

    Hakiiiiii

  • kassim

    Naona kila mmoja anasema vyake kuhusu Dr Shein. Mwanzoni tukiambiwa Kikwete ndiye aliyemshauri agombaniye na ndiye chaguo la Bara na baadaye tukasikia Aman Karume anapendelea Dr Shein awe ni mrithi wake kwa vile hana magurupu na ni mtu ambaye ataweza kuendeleza haya yaitwayo maridhiano.

    Leo tunasikia eti kajitowa baada ya kupata ushauri wa Kikwete na mwanasheria Mkuu! Inawezekana kikwete, lakini mwanasheria mkuu kwani ni mtu wa chama?

  • mtumbatu

    baada ya muda si mrefu wakucheka atacheka na wakulia atalia.hata awekwe nani ni walewale tu mafisidi na wanaotumalizia nchi yetu. mungu awalani

  • Abuu Said

    Asalam alaykuma ndugu zanguni,
    Nimefurahishwa sana kuona vijana wote mlotoa maoni yenu kua mnajua Rais wa Zanzibar ni yule atakaeteuliwa na CCM sio vyenginevyo na ndio maana nnaomba chama cha CUF kifungwe (niulizeni kwanini? muda mwengine).
    Kwa kweli inahudhunisha kuwaona watu wanampaka matope DR Salmin Amour na kumsifu Masharabu, hebu nikuulizeni kwani masharubu alikua hayumo kwenye serikali ya awamu ya tano? Jibu alikuwemo sasa huyu bwana(Masharubu) kafanya yale yote na kuiba kila pembe ya fukwe za Wazanzibar na bado mnamsifu achene hayo msiwe madumla kwa kumkubalia huyu masharubu na muafaka wake fake ( ule ni mtego…)
    Haya mimi nikikwambieni mnaniona Kada hilo, laa , bwana hawa watu wote hawatufai . Zanzibar intaka vijana wampya wasiokua na chuki wala majungu.
    Ahsanteni

  • virus99

    Baraka Shamte anachopigania kupata kiongozi wa kukijenga chama chao!! kwa sababu kimevunjika!!Sasa haki hio anayo, mwachieni apiganie kiongozi bora ili ajenge chama !! kwake chama ni bora kuliko nchi au mkowa!!sasa dogo hilooooooooooo ???